Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tk, Mar 15, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. t

  tk JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania Toleo No. 4689 la tarehe 15 Machi 2009 chini ya kichwa cha habari "Dk. Mwakyembe Aumbuliwa" imeripotiwa kuwa Dk. Harrison Mwakyembe ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya kufua umeme na ndio sababu anaipiga vita kampuni ya Dowans ambayo ni mshindani wa kampuni yake. Nukuu ya vipande vya taarifa hiyo ya Mtanzania ni kama ifuatavyo:-

  "SIRI nzito za kimaslahi zinazomhusu Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM, pichani) zimeanza kuibuliwa.

  Imebainika kuwa Mbunge huyo ni miongoni mwa watu tisa wenye hisa katika kampuni binafsi ya kufua umeme kwa kutumia nguvu za upepo.

  Kampuni hiyo inaitwa Powe Pool East Africa Limited. Namba zake za usajili ni 49624. Makao Makuu yapo katika majengo ya Posta ya Zamani jijini Dar es Salaam. Aidha kampuni hiyo imeishapata maeneo ya kuwekeza - Makambako mkoani Iringa na Singida. Maeneo hayo yana upepo mkali amabo ndiyo malighafi muhimu.

  Wachunguzi wa mambo wanaamini kuwa ushujaa wa Dk. Mwakyembe kuishambulia kampuni ya Richmond, na baadaye Dowans, unatokana na mgongano wa kimaslahi.

  Kwa maneno mepesi, wanasema Dk. Mwakyembe na wenzake wanapinga Dowans kununuliwa ili wapate mwanya wa kuuza umeme utakaozalishwa na kampuni yao ya Power Pool East Africa Limited, ingawa nao kwa vyovyote vile utakuwa haujatosheleza mahitaji ya umeme nchini.

  Dk. Mwakyembe na wenzake walianzisha kampuni yao kabla ya ujio wa kampuni iliyozua utata mkubwa wa Richmond. Matarajio yao yalikuwa kwamba wazalishe umeme na kisha waiuzie Tanesco, lakini ujio wa Richmond ulionekana kutaka kuwakwaza. Richmond ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ajiuzulu Februari mwaka jana.

  Akiwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, hakuwahi kutangaza hata mara moja mgongano wa kimaslahi aliokuwa nao kwenye suala hilo.

  Pamoja na Dk. Mwakyembe anayemiliki hisa 1,485 katika kampuni hiyo, wengine wenye hisa katika kampuni hiyo ni Emmanuel Kasyanju (99), Victor Mwambalaswa (99), Mwacha Kagoswe (4,455), Josephine Pina (99), Athumani Ngwilizi (99), Prosper Tesha (99), TBC (199 Limited inayomilikwa na Isaac Mwamango (297) na MECCO Limited, inayomilikwa na Maungo Kwabibi hisa moja.

  Kwa hisa hizo Dk. Mwakyembe ni mtu wa pili kwa maamuzi katika kampuni hiyo, kwani kwa mujibu wa kanuni za makampuni, nguvu na uwezo wa mtu hutokana na hisa zake. Mwenye hisa nyingi ni Machwa Kasogwe.

  Wengine ni Beston Mwakalinga (99) Niels Dahlmann (891) na Leonard Tenende (99).

  Wanahisa wote, isipokuwa watatu, anuani zao zinaonyesha kuwa wako nje ya nchi..........

  Dk. Mwakyembe, akionekana kuwa msitari wa mbele kuhakikisha kuwa mitambo ya kampuni ya Dowans hainunuliwi, anashupalia msimamo huo kutokana na mgongano wa maslahi. Aliwahi kusikika akisema kuwa ni heri nchi iingie gizani , hoja iliyowafanya watu wengine kusema kwama alistahili kukamatwa.

  Katika Power Pool East Africa, Mbunge huyo anamiliki hisa 1,485, lakini anaweza kuwa na hisa nyingine zaidi kupitia kampuni zake mbili tofauti. Kupitia kampuni ya kwanza ya TBC (199 Limited amabyo anamiliki hisa 297 na kampuni nyingine ya MECCO limited ana hisa moja."

  (Taarifa inaendelea lakini ya muhimu kuhusu Dk. ni hayo)

   
  Last edited by a moderator: Mar 19, 2009
 2. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ...i have no idea who to believe, yaani siasa za bongo zina so many twists zisizo na kichwa wala miguu. I hope Dr. ata-clarify this kabla hajaanza kuwa crucified.....du on the other hand it could be the rise of Edward, after all anaweza kuonekana hero who resigned kwa maslahi of the so called Taifa. Tufafika kweli!!!
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Binafsi sioni conflict of interest kwenye hili. Labda tatizo liwe kushindwa kuweka wazi kwamba na yeye ana kampuni kwenye maeneo hayo. Hi ni kampuni ndogo sana hata kuwa na ushindani wa kibiashara na Tanesco. Maeneo yanayosemwa kwa sehemu kubwa hayana umeme wa Tanesco.

  Kama kuna Watanzania wanaanza kuwekeza kwenye umeme ni jambo zuri. Labda muhimu ni kwa serikali kuweka wazi sera ya nishati ili Watanzania wengi zaidi washiriki kuondoa hili tatizo sugu.

  Naona wadau wengi wa Kyela waliko nje ni wabia kwenye kampuni hiyo. Itabidi na wengine tuchangamkie tender kwi kwi kwi!!!

  Ukiona hizo shares zilivyogawiwa (99 kibao) unaona kabisa walio wengi wametoa tu idhini yao kuwemo lakini sidhani kama ni contributors wakubwa. Usajili wa makampuni TZ unaendeshwa kiholela sana, ndio maana hata kwenye EPA kuna watu wamejikuta wako kwenye matatizo bila kujua hata walikuwa shareholders kwenye makampuni yaliyokuwa yanachota mabilioni.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ilianza attack kwa Zitto Kabwe sasa imekuja kwa Mwakyembe, na kuna uwezekano kuwa itaendelea na kuendelea. Hii ni vita dhidi ya ufisadi kila upande unatumia mbinu zake. Bado sitaki kuamini kama Mwakyembe ana kampuni binafsi ya kufua umeme ambayo ingeweza kuwa competitor wa kampuni yoyote ya kuzalisha umeme Tanzania, sounds bollocks to me.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hii si breaking news!!!!!

  Hao mtanzania wasitake kutuchanganya. Mwakyembe kama mtanzania ana haki ya kuwa na kampuni au hisa katika mradi wowote halali. Ishu hapa ni wizi wa hiyo Richmond, Dowans etc. Well hata hii kampuni ya kina Mwakyembe ikifanya wizi tutasema tu.

  Huyu Rostam vp? Mbona anatapatapa sana sasa hivi?????????????
   
 6. 911

  911 Platinum Member

  #6
  Mar 15, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Acha watapetape maana "mwali" ndo amekaribia kutoka.Yaani mtu aliyetoa maoni ya kutonunua mitambo chakavu toka kwa kampuni ya kitapeli pamoja na kutufumbua macho kuhusu kampuni hewa ya Richmond leo hii naambiwa kuwa alifanya hivyo kutokana na mgongano wa kimaslahi....Let it be,he saves us a big deal hadi tumeuvunja mkataba wa Dowans.Lets be sober people,hivi si tumeambiwa kuwa hyo mitambo imewekwa collateral katika mabenki???
  .
   
  Last edited: Mar 15, 2009
 7. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dowans ni kimeo. hata mlete habari gani hapa dowans ni utapeli, wizi, rushwa na uhuni. Tuanze kutumia akili zetu badala ya akili za mafisadi. watataka kuonyesha kila kitu ili tuamini kwamba wanaonewa.

  Wanatumia fedha nyingi kumhonga yeyote hata media yetu imeingiliwa big time. hiyo habari ni ya kipuuzi kwani haijaandika kosa au sababu gani au ni wapi mwingiliano wa kimaslahi wa hizi kampuni mbili.

  ila wote tunajua tulikuwa gizani wakati richmond ikisema inaweza. Tunahitajika kununua mitambo mibovu kwa njia za kifisadi ili kuwaenzi wakoloni weusi dr idrisa na kundi lake.

  sasa kama mwakyembe kuna mahali kalikoroga tuelezwe. kwa hiyo leo mbowe aruhusiwi kuelezea maovu yeyote yanahusu disco kwa sababu ana miliki billicanas???

  sioni kitu hapa. No dowans no lowasa no dr idrisa no Rostam no ngeleja No Zitto.

  Nchi itajengwa na wenye moyo na italiwa na wenye choyo ila kwa miaka hii damu itaamua nyie zikusanyeni tu kwani mtazikimbia siku moja.
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  This is just another idiotic attack from bandido Rostam Azizi.... Ameanza kazi kama alivyoahidi...
  By the way umiliki wake wa hisa una mgongano gani na suala la Dowans...?
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Mar 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ukisoma tanzania daima la leo linasema mwenye dowans ni mtu kutoka oman brigedia huo ni uwongo watoe ushahidi kuonyesha huyo brigedia anavyohusika
   
 10. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu TK heshima mbele, kwanza kabisa napenda kusema hii sio Breaking news, pili sasa hivi watu wanatafuta kwa kuangukia ila naamini hawatoweza. Sio kwamba namtetea Dr Mwakyembe ila kiukweli kwa jinsi ilivyo mafisadi wameumia sana na issue ya Dowans sasa wanafanya any means ya kuwaharibia waliopinga manunuzi haya na watukuja wengine na wengine. Kuhusu Dr Mwakyembe kuwa na hisa kwenye Kampuni sidhani kama kuna tatizo lolote na sidhani kama ana interest yoyote kwenye hiyo nafasi ya Dowans cha msingi hapa ni maslahi ya Taifa ndio maana mambo yanakwenda hivyo. Mnaomchukia mchukie,Mitambo ya Dowans lazima tukubali kwamba ni FAMBA kwa mujibu wa wachunguzi unless bwana Zitto aje atuambie nini kilimgegeda mpk akatoa hoja za kukubaliana na hilo.

  Nafikiri itafikia kipindi itabidi Mhe. Zitto aje jamvi atueleze kinagaubaga kulikoni, mbona hatupo pamoja kwenye hili.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tuko pamoja, hakuna tatizo kwani anayosema kuhusu dowans ni ya kitaifa na pale ambapo kampuni yake itakuwa kwenye questions anatakiwa ku-declare interest. Akiwa kama mbuge wetu ni lazima atetee yanastwisha taifa; na kuhusu huyo rostam... achana na shetani yule utapoteza nywele bure kumfikiria ibilisi aliyeishinda hata system yetu tukufu inayosifika ndani na nje ya nchi
   
 12. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mafisadi ni noma.
  Wameenda kupandikiza kampuni kwa jina la DR.ili watuzuge kwamba maslahi binafsi yanasababisha kudorora kwao.
  Wamekwisha.
  Aliyesoma barua ya ZITTO KWA watanzania naomba anipe dondoo zake
   
 13. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yani matatizo yoote ya Richmond-Dowans kuanzia kwa:

  kutumia hela za wavujajasho kwa LC,
  kuhusishwa na rushwa kubwa ya viongozi,
  kurithishana mikataba hewa baina yao,
  kuwa na ghost owners,
  kutolipa deni letu la 8bn,
  kufungua kesi Paris, na
  kutaka kutuuzia mikangafu ya kufua umeme kwa kucreate artificial crisis.

  Kwa akili yao wa kumlaumu ni Dr Mwakyembe, yeye ndio aliyewatuma mfanye madili machafu?... Kuna kampuni ngapi zimefanya biashara na Tanesco, iweje kila siku panapovunda tena kwa facts ni Dowans. Ama kweli ufisadi unapofua. Wanalaumu walipoangukia badala ya walipojikwaa. Ni wapi imekua dhambi kwa mwananchi kuanzisha kampuni binafsi ya kufua umeme. Na ni wapi imeonekana hiyo kampuni yao ina mkataba wa kuuzia umeme tanesco. Na mnaosema alitakiwa kudeclare mgongano wa maslahi, mgongano upi hapo mnaousema? Mbona hakuna penye mgongano so far. Mafisadi mtahangaika sana mwaka huu, salama yenu mjifunze kuheshimu sheria na taratibu za nchi, si kujifanyia mambo mnavyotaka nyingi, halafu mtegemee kununua vigazeti uchwara na wapambe njaa kuwakingia kifua.
   
 14. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  This is sooooooooo lame
  - hawajatoa indication ya capacity ya hizo windfarm kuonyesha ushindani wake
  - hawajaeleza hii project imefikia wapi na itachukua muda gani (miaka) kuanza kugawa kwenye grid ya Tanesco, tofauti na generators ambazo ni kununua na kuswitch on (process ya miezi)
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi ningependa kufahamu hiyo kampuni imesajiliwa lini? na Dr amekuwa kwenye hiyo kamati ya Bunge toka lini?

  Nikipata haya majibu nafikiri nitapata mwelekeo wa kujadili.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mh... inawezekana mwanyembe na wenzake waliamua kufungua kampuni baada ya kuchoshwa na utumbo wa tanesco, in that way its right move
   
 17. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo zote ni siasa za maji taka ambazo kwa bahati mbaya huku kwetu wote ni wachezaji. Ameendika Johnson Mbwambo kwenye Raia Mwema ya hii kuwa viongozi wa awamu hii kila mtu yuko kwenye malumbano na scheming za ki-mitandao.

  Kwa kweli kitu ambacho JF tunaweza kukifanya ni kupiga kelele na kuhakikisha hawa jamaa 2005 hawaendelei. It is too much kila mtu na kambi yake. Hawakuchaguliwa waunde kambi but for sure it is becoming unbearable.
   
 18. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo zote ni siasa za maji taka ambazo kwa bahati mbaya huku kwetu wote ni wachezaji. Ameendika Johnson Mbwambo kwenye Raia Mwema ya wiki hii kuwa viongozi wa awamu hii kila mtu yuko kwenye malumbano na scheming za ki-mitandao.

  Kwa kweli kitu ambacho JF tunaweza kukifanya ni kupiga kelele na kuhakikisha hawa jamaa 2010 (samahani kwenye post ya kwanza) hawaendelei. It is too much kila mtu na kambi yake. Hawakuchaguliwa waunde kambi but for sure it is becoming unbearable.
   
 19. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Naungana na wewe habari hii ipo SHALLOW SANA...
   
 20. 911

  911 Platinum Member

  #20
  Mar 15, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Mkulu,msaada kidogo...Hapo unaposema ilianza attack kwa Zitto Kabwe.....Nani aliyem-attack ZZK???Yeye alijichanganya mwenyewe na misimamo yake akajikuta anashabikia mitambo ya kifisadi,hakuna aliyem_attack.Wengi walikuwa wakimshtua kuwa kuti alilokaa ni kavu though mwenyewe akaamua kukomaa hivyohivyo!Shame indeed.
  Licha ya hayo siku za hivi karibuni Zitto amekuwa akiappear +vely ktk magazeti ya newhabari corp.Hilo halikushtui??
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...