Dr. Mwakyembe: Marufuku TV na Radio kusoma habari za magazetini kwa ujumla wake

Kwa sheria ipi anayoitumia kukataza hayo. This is ultra vires his powers! Mwakyembe should know that powers exercised by him are limited by the constituting or vesting instrument, and any act outside those limitations is ultra vires and may be challenged in the courts of law.
Haya mambo ya kukariri kwa sheria ipi kwa sheria ipi wewe unaona ni sawa. Kila kitu kiandikiwe sheria basi utataka na sheria ya namana ya kula!
 
Wakuu hizi si zama za kubanabana na kufichaficha habari kwa jamii kwa kisingizio chochote kile kutokana na kukua kwa teknolojia za kupashana habari.Hizo redio na tv ziko nyuma sana kuripoti kilichoandikwa magazetini.Magazeti nayo yako nyuma sana kuripoti habari.Mitandao ya kijamii ndiyo iko mbele kufikisha habari kwa jamii.Ni lini utasubiri kesho usikilize kilichoandikwa gazetini kwenye redio wakati unakipata muda huu tena mubashara ? Ndio maana baadhi ya vyombo vya habari vipo sambamba na mitandao ya kijamii kufikisha habari kwa haraka kwa jamii.Sasa ukiwa na simu unapata habari nyingi zingine mubashara hata kabla hazijachapishwa magazetini,unapata habari popote ulipo.Usomaji wa magazeti redioni ungeachwa tu ili habari ziwafikie wananchi wa vijijini ambako magazeti hayafiki na hakuna mitandao ya simu na intenet,tena hata redio inayosikika ni moja au mbili,au hakuna kabisa.Wachapishaji magazeti wao ndiyo wangekataza magazeti yao habari zisomwe zote.Kuna redio moja husoma vichwa vya habari vikubwa tu inatosha.
 
Waziri Mwakyembe apiga marufuku redio, televisheni kusoma habari nzima magazetini, badala yake kusoma vichwa vya habari tu.

Amevizuia kuanzia kesho vyombo vya habari (Tv na Redio) kusoma habari nzima kwenye magazeti, ili magazeti yapate soko.

======

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Televisheni na Redio kuanzia kesho kusoma vichwa vya habari vya magazeti tu ili kuwavutia wasomaji kununua magazeti kwa habari kamili.

Dk Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo pia amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi.

Pamoja na mambo mengine Dk Mwakyembe amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kwa wamiliki wa vyombo vya habari na kwamba ameagiza idara ya mawasiliano kutengeneza mawasiliano ya kudumu na wawe wanakutana angalau mara moja kwa mwezi kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza na kuchukua hatua lengo ni kuwekana sawa.

Chanzo: Mwananchi
Hivi huyu Mwakyembe amekula maharage ya wapi? Na wale wananchi wanaomiliki redio lakini hawana hela ya kununua gazeti watapata wapi habari? Hizi ni njama za makusudi kuwanyima wananchi habari ili wasijue udhalimu na ukandamizaji wa serikali ya CCM.
 
Wadau, sasa ule udikteta aluoonya TL unaanza kujitanua kwa uwazi. Radio na Tv ndio vyombo vinavyowafikia watu wengi zaidi kuliko magazeti yenyewe na kupitia redio ndio wananchi wanajua kilichoandikwa magazetini maana hakuna mwananchi mwenye uwezo wa kununua magazeti yote.

Halafu, wamiliki wa magazeti wamewasilisha malalamiko kuhusu hilo? Mbona wachapaji na wamiliki wa magazeti hawawezi kushindwa kuzitaka TV ba redio kutosoma magazeti bila kupitia kwa Mwakyembe?

Hao wamiliki wa magazeti wakikubali hiyo hoja ya Mwakyembe, basi wajiandae kisu kugeuziwa upande wao punde. Ni suala la muda tu.

Vv
 
Jamani niwaulize: mbona magazeti huwa yanasomwa headlines tu na paragraph moja ya juu tu? Ni lini alisikia redio na TV wanasoma habari nzima? Ama kweli haya maCCM ni misukule wa kutupwa!
 
Kuna baadhi ya redio wakikamata stori, wanapukutisha yote had nukta
 
Mimi mwenyewe CCM mwenzie huwa nategemea Radio free africa na mitandao kama ya Millard ayo etc huwa sinunui gazeti msema kweli mpenzi wa Mungu
Ia print media zinawakati mgumu sana sasa hivi, ili kuziokoa inabidi tu kupiga marufuku magazeti kutokusomwa
 
Jamani niwaulize: mbona magazeti huwa yanasomwa headlines tu na paragraph moja ya juu tu? Ni lini alisikia redio na TV wanasoma habari nzima? Ama kweli haya maCCM ni misukule wa kutupwa!
Radio one ndio ilikuwa ikisoma vichwa tu vya habari wengine wakiwemo wa mitandaoni walikuwa wakimwaga kila kitu kiasi kuwa ukiwasikiliza habari zote wanakuwa wamemaliza huhitaji kununua gazeti kabisa wewe unaonyesha ulikuwa mpenzi wa wachoyo Radio one ungekuwa unasikiliza radio free Africa na mitandao Kama ya Millard ayo usingenunua gazeti hata siku moja. usitukane CCM Kwa usichojua please tuombe samahani kutuita misukule kwani hata gazeti lenu chadema la Tanzania daima lilikuwa halina soko kwa sababu ya hao wasoma magazeti wanaomaliza kusoma kila kitu grow up usipinge tu kila kitu
 
Wabongo taabu kwelikweli, hadi kwenye hili povu litawatoka,

Sasa gazeti zima linauzwa na story 2 au 3 na story zenyewe ndo zinasomwa na redioni au kwenye TV, nan anunue magazeti! Hapa yuko saihi bila chenga tena utakuta wengine wanaibandika story nzima kwenye mitandao ya jamii na matangazo ya gazeti husika yanafichwa yasionekane,

Safi sana, Ingawa wenye magazeti walitakiwa waende mahakaman long time kudai fidia za habari zao, au atleast wawe wanalipwa kiasi flan na hizo radio/TV
Kaka ni sawa,lakini yeye haimuhusu,hiyo ni biashara binafisi,gazeti Lina haki ya kuzuia Kama halipependi kutangaziwa,Ni bongo za samaki tu hizi.kila Analosema waziri ndio sawa uunge mkono tu,hizi vyeti vyake huyu waziri viangaliwe tena,ati daktari wa Sheria,vichekesho,wajifunze kukaa kimya kama hawana la kuelekeza,asimuogope sana bosi wake,hata alete maamuzi ya kushangaza,kwa nini viongozi hawa hawaangalii sheria na haki,halafu wakaropokwa,kuna mambo hawana haki ya kuyasema hadharani.ni maamuzi ya wahusika magazeti sio yeye.
 
Mimi mwenyewe CCM mwenzie huwa nategemea Radio free africa na mitandao kama ya Millard ayo etc huwa sinunui gazeti msema kweli mpenzi wa Mungu
Naogopa sanaaa siku hizi nikisikia sema wakweli mpenzi wa mungu. Wengi ni wanafikiiiiiiiiiiiii
 
Kwa hili namuunga mkono
Wachapishaji wa magazeti wamelakamika kuwa sababu za magazeti kutonunuliwa ni redio na tv? Mbona magazeti ya udaku hayasomwi kwenye tv na redio na bafo yana wateja sana tu, tena yanauzwa bei rahisi tu na bado yanazidi kuongezeka?

Vv
 
Mi naangaliaga sky news yaani wale wanaliscan page nzima wanakata kabisa kipande wanachochambua na wanachambua balaaa sasa sijui lini wenye magazeti wamelalamika maana mi naona ni njia ya kuwatafutia soko(promo)
 
Waziri Mwakyembe apiga marufuku redio, televisheni kusoma habari nzima magazetini, badala yake kusoma vichwa vya habari tu.

Amevizuia kuanzia kesho vyombo vya habari (Tv na Redio) kusoma habari nzima kwenye magazeti, ili magazeti yapate soko.

======

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Televisheni na Redio kuanzia kesho kusoma vichwa vya habari vya magazeti tu ili kuwavutia wasomaji kununua magazeti kwa habari kamili.

Dk Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo pia amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi.

Pamoja na mambo mengine Dk Mwakyembe amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kwa wamiliki wa vyombo vya habari na kwamba ameagiza idara ya mawasiliano kutengeneza mawasiliano ya kudumu na wawe wanakutana angalau mara moja kwa mwezi kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza na kuchukua hatua lengo ni kuwekana sawa.

Chanzo: Mwananchi
Kwahiyo lengo la serikali ni wananchi wasipate habari kamili,hata hivyo sidhani kama habari nzima husomwa.
 
Basi na Taarifa za habari za Radio na TVs zsisomwe ili kulinda biashara kwa wamiliki na ikiwezekana kila mtu awe na Radio station and TV stations zake.
 
Back
Top Bottom