Dr. Mwakyembe, kushidwa kwa ATCL kunatokana na sababu hizi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mwakyembe, kushidwa kwa ATCL kunatokana na sababu hizi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wwww, Jun 16, 2012.

 1. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Kwanza kabisa napenda nikupe pole kwa yoteyaliyokukuta, napenda kukupa moyo wa dhati kwani kila unapotenda mema kwa ajiliya wengi daima Mungu huwepo katikati yake. Wamejaribu wameshindwa nahawatajaribu tena, kwani wanajua Mungu yu katikati yako.

  Vilevile napenda kukupongeza kwa hatua mbalimbaliambazo umekuwa ukizichukua dhidi ya idara, taasisi na wafanyakazi wasio waadilifu katika kusimamia rasilimali za nchi yetu. Ni matumaini yangu kuwakila mpenda maendeleo na mzalendo atakuunga mkono katika juhudi zakounazoendelea nazo kwa sasa.

  SABABUZA KUSHINDWA KWA ATCL

  1. ELIMUBILA UZALENDO
  Watanzania tulio wengi tumekosa uzalendo katika rasilimali za nchi yetu. Kila tunapoamini wana watanzania wenzetu au Serikali kusimamia sehemu au taasisi fulani tunatanguliza maslahi yetu, watoto wetu, wajomba zetu, wapenzi wetu, nyumba ndogo zetu na kusahau UTAIFA WETU.

  Kimsingi tangu 2007 Serikali ilipovunja makataba na Shirika la ndege la Afrikaya Kusini (SAA), ATCL ilikuwa na wataalamu wa Kitanzania wengi tu ambao walisheheni elimu za kutosha ukianzia kwa Mkurugenzi Mtendaji (CEO), lakini alikosa uzalendo na kampuni na nchi yake. Idara ya Fedha ilikuwa na CPA Holders wawiliyaani Acting Director of Finance ndg. Eliasaph Ikomba Mathew na Finance Manager ndg. Prosper Mzee. Hata hivyo Acting Director of Finance alikuwa na Elimu lakini alikosa uzalendo hivyo pamoja na elimu yake nzuri hakuwezi kuisaidia kampuni. Idara ya Ukaguzi wa Ndani ilikuwa na CPA Holder mmoja na ACCA holders wawili, pamoja na elimu hizo, Acting Director of Internal Audit ndg. William Haji alikosa uzalendo.

  Hivyo elimu pekee hazitoshi kuikomboa nchi yetu na taasisi zake bali UZALENDOndiyo liwe jambo la msingi. Katika kikao na wafanyakazi wa ATCL Dkt. Harrison Mwakyembe aliutaka uongozi mpya wa kampuni chini ya kaptani Lazaro Lusajo kujaza nafasi zote zilizoachwa wazi na wafanyakazi waliosimamishwa. Ni matumaini yangu kuwa ATCL itazijaza nafasi hizo either kwa kuzitangaza yenyewe au kwa kutumia SEKRETARIETI YA AJIRA.

  Hata hivyo katika kutangaza nafasi hizo utasikia wakitaja elimu kubwa kubwa na uzoefu mkubwa mkubwa mfano; walipotangaza nafasi ya CHIEF EXECUTIVE OFFICER (CEO) miezi kama mitatu iliyopita walihitaji waombaji wenye sifa kemkem huku wakisahau uzalendo. Najua kwenye nafasi ya Chief Finance Officer (CFO) na Chief Internal Auditor (CIA) nazo watahitaji sifa kama; awe na CPA, ACCA, CIMA, CA, MBA (Finance), au Phd, huku wakitaka mtu huyo awe amesajiriwa na Bodi ya NBAA kama Mhasibu au Mkaguzi wa Hesabu, na awe na uzoefu wa zaidi ya miaka 12 huku wakisahau UZALENDO kuwa ni jambo la msingi sana.

  Napenda watambue kuwa ATCL ilikuwa na watu wenye elimu za kutosha na nzuri na uzoefu wa kutosha sana lakini walikosa uzalendo hawakuisaidia kampuni. Hivyo pamoja na elimu kubwa kubwa mnazozihitaji tafuteni namna ya kupata watu wazalendo ambao wataisadia ATCL na nchi yao, bila kung'ang'ana na elimu kubwa tu. Serikali itumie vyombo vyake kutafuta Watanzania wazalendo ili kuinusuru ATCL.

  2. MENEJIMENTI YA ATCL
  Menejimenti ya ATCL tangu 2007 ikiongozwa na David Mattaka kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa na wafanyakazi na vyombo vya habari lakini mwitikio wa Serikali umekuwa mdogo kufuatilia kwa ukaribu shutuma dhidi yao, hivyo kupelekea mambo kuharibika kabisa ndipo Serikali inaposhtuka.

  Chukulia mfano; Kaimu Mkurugenzi wa Fedha Ndg. Eliasaph Ikomba Mathew na KaimuMkurugenzi wa Idara ya Ukaguzi wa Ndani Ndg. Willliam Haji kuhongwa suti na kampuni ya Mercator jijini Dubai mwaka 2007 walipokwenda kwa ajili kutathimini jinsi ya kuingia mkataba wa kuifanyia ATCL kazi ya mapato (Revenue Accounting). Kama wafanyakazi waliokuwa wanapokea msharaha zaidi ya Tshs. 6,000,000/= (Huu ni mshahara kwa kipindi cha 2007 -2008) kwa mwezi kila mmoja wanafikia hatua ya kuhongwa suti hapa ujue kuna hatari.

  Hata hivyo pamoja na kuhongwa suti mkataba na Marcator ulikwamishwa na wafanyakazi wazalendo ambao baadaye waliondolewa kazini mwaka 2009 kwenye zoezi la kupunguza wafanyakazi. Kama hiyo haitoshi MweziOctoba, 2007 Menejimenti hii ikaigia mkataba mbaya na kampuni ya WALLIS TRADING Inc. ya Lebanon na kukodi ndege chakavu aina ya Air Bus A320 – 214 ambayo iliigharimu ATCL matengenenzo kwa takribani mwaka mmoja (Octoba, 2007 hadi Mai, 2008) nchini Ufaransa na kuisababishia kampuni deni la Tshs. 322 bilioni.

  Mwaka huohuo Menejimenti hiyohiyo ikaamua kukopa pesa kutoka Stanbic Bank takribani Dollar 700,000 kwa ajili ya kununulia magari chakavukutoka AWILI – SHARJAH –Dubai kwa bei ya kutupwa ili kujinufaisha. Hivyo hata mkatabamwingine wa ndege aina ya Boeing 737- 500 kutoka kampuni ya AERO VISTA kutoka Dubai lazimaungechakachuliwa na akina Paul Chizi ,Justus Bashara, Josephat Kagirwa, John Ringo na Amini N. Mziray kwavile waliochakachua ule wa Air Bus A320 – 214 mwaka2007 hawajachukuliwa hatua zozote za kisheria.

  3. KATIBU MKUU (OMAR CHAMBO)
  Katibu mkuu wako amekuwa sehemu ya kushindwa kwaATCL kwa muda mrefu kwa kuitumia menejimenti ya ATCL kujinufaisha binafsi. Nashindwa kuelewa kwanini yeye hajaunganishwa kwenye kesi ya akina David Mattaka, William Haji na Eliasaph Mathew. Hata katika ukodishaji wa ndege ya Air Bus kutoka kampuni ya Wallis Trading Inc. kutoka Lebanon yeye na Mustapha Nyang'anyi walihusika kwa pazia la nyuma.

  Huyu Katibu Mkuu amekuwa mtu wa kukwamisha shirikahili kwa muda mrefu sasa. Hata wakati wa upunguzaji wa wafanyakazi mwaka Desemba,2009 yeye binafsi alikuwa na orodha yake ya aliotaka wapunguzwe hasa wafanyakazi aliowaita wakorofi (waliokuwa wanapaza sauti na kumnyima usingizi) kwa kuharibu mipango/dili zake pale ATCL.

  Ni huyu Katibu Mkuu aliyeamuru wafanyakazi wote wanaojifanya wanaitetea Kampuni wasibaki kwenye zoezi la upunguzaji, ushaidi upona ukitumia kamati yako ya akina Ekingo Magesa, Prosper Tesha na Hashim Butara ikawauliza wafanyakazi pale ATCL watawaambia. Kuna wafanyakazi waliokuwa wazalendo sana na kampuni hii lakini walipunguzwa kwa shinikizo la Omar Chambo, Mustapha Nyang'anyi, William Haji na Eliasaph Ikomba Mathew kwani walikuwa ni kikwazo katika kupanga mipango yao ya ufisadi.

  KIPI KIFANYIKE KUINUSURU ATCL

  1. UZALENDO
  Serikali ijitahidi kwa kila mbinu ikitumia vyombo vyake kutafuta wafanyakazi wenye elimu nzuri bila kusahau uzalendo wao kuongoza taasisi kama ATCL, badala ya kuwapata wafanyakazi kwa kigezo cha kujuana na mtoto wa Fulani. Ifahamike kuwa pale ATCL kuna wafanyakazi hata usaili hawajawahi fanyiwa lakini ni wafanyakazi na hakuna anayewauliza.

  2. MENEJIMENTI
  Juhudi iendelee ya kuisafisha Menejimenti ya ATCL, ili kupata watu ambao watakuwa msaada kwa kampuni na watanzania kwa ujumla. Napendekeza ajira zote za ATCL zifanywe na Sekretarieti ya Ajira au makapuni kama KPMG, ENERST $ YOUNG, PWC au DELOITTE ili kuondokana na watumishi wanaoajiliwa kwa kujuana.

  3. KATIBU MKUU (OMARI CHAMBO)
  Ni lazima huyu bwana aondolewe kwenye Wizara ya Uchukuzi kwa maslahi ya ATCL na Tanzania kwa ujumla. Huyu hana tofauti na alivyofanya Sumaye aliposaini Blank Contract kati ya ATC na SAA na kuwapa SAA kuingiza mambo wayatakayo kwenye mkataba ili kuisaidia Precision Air. Huyu pia ana maslahi makubwa sana pale Precision Air.

  Asipoondolewa huyu bwana juhudi zako zitakuwa sawana kutwanga maji kwenye kinu.

  4. KUIONGEZEA MTAJI ATCL AU KUIVUNJA KABISA
  Serikali ifanye uamuzi wa either kuiongezea mtaji ATCL kwa kuinunulia ndege angalau moja kwa kuanzia na mtaji wa uendeshaji ili kupunguza gharama za kukodi ndege kila mara tena kwa gharama kubwa. Ikishindikana ni bora kuivunja kabisa na kuanza upya (ingawa kuanza upya ni ghali sana). Serikali itafakari kwa kuangalia mfano wa karibu tu UGANDA AIR haina miaka mitano tangu ianze kwa mara nyingine lakini imeweza kufanya safari zaidi ya nchi tano (5) mpaka sasa ukiacha safari za ndani. Huu ni mwanzo mzuri sana kwa Uganda kama nchi na Uganda Air kama Kampuni ya Ndege.

  ''Munguibariki Tanzania, Mungu ibariki Air Tanzania''

  WanaJF naomba tujadili kwa manufaa ya ATCL na nchi yetu.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hivi Uzalendo unapimwaje Wandugu?............
   
 3. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Kwa vitendo, mkuu! Unakuwa kaa vile hujawahi kusikiliza "mazungumzo baada ya habari" kwenye RTD enzi zile za Nyerere miaka ya 80...lol!
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Good question Ogah, kwangu mimi uzalendo ni mtu ambaye yuko tayari kujitolea kutoa huduma bila kufikiria jinsi ya kujaza tumbo lake kwanza. Mtu ambaye yuko tayari kutetea maslahi ya shirika bila kutafuta faida yake kwanza. Mtu ambaye ataona kuwa uamuzi fulani haufai kwa sababu utaliumiza shirika. Watu kama hao hatujawaona miongoni mwa wale walioingia mikataba iliyoiletea ATC hasara kubwa.
   
 5. O

  Ogah JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wee dogo...hujakutana na Wasanii dogo!!.......Juma Ngondaye et al niliwasikiliza sana wakati ule..........lol
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Absolutely........nafikiri "checks and balances" haziko au sio effective.....ndio maana unakuta MIJITU inajiamulia itakavyo.........
  Hebu tuwe wakweli kidogo......package isipokuwa ya kutosha unafikiri uzalendo utadumu kweli.......Nimeshuhudia so called "Wazalendo" wanaacha kazi au hawataki kufanya kazi sehemu muhimu za kuliendeleza Taifa simply kwa sababu hailipi............matokeo yake haya mashirika ya umma yamejaza na yanaongozwa na "Vilaza" na "Wasio-Wazalendo".......

  ......hebu check Bajeti ya Mgimwa.........kuna Uzalendo pale........I mean where are we heading......yaani nilipomaliza kuisoma bajeti ya "mpuuzi" Mgimwa........nikajisemea.......keep calm and move on with business as usual.........
   
 7. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  ATC Kama ilivyo ni shimo lisilo na mbunu (bottomless pit). Kuendelea kumwaga pesa mle ni kufuja raslimali. Kinachotakiwa ni kuifilisi ATCL na kuanzisha kampuni mpya ndogo, hata kama ikianza na ndege ndogo ndogo kama ilivyoanza Precision Air. Pili ni kulitafutia management madhubuti labda kwa kuingia ubia na makampuni makubwa kama walivyofanya Kenya Airways na KLM. Kama si hivyo ikodishwe management company (zipo) yenye utallamu katika usafirishaji wa anga (lakini kwa kuingia mkataba makini si kama ule wa SAA). Hapa ndipo kuna tatizo. Atapatikana wapi wa kuhakikisha kunakuwa na mkataba mzuri? Uzoefu mpaka sasa unaonyesha kuwa kama taifa ni vilaza katika mikataba. Sijui hao wanasheria wanaozalishwa na vyuo vyetu wana kilema gani? Lakini hata kama hatuwezi kuandika wa kwetu tumekosa mahali pengine ambapo tunaweza kunakili (copy and paste) mkataba mzuri? Hapo ndipo linakuja swali, MZALENDO/WAZALENDO wanapatikanaje? Inawezekana kuwa mfumo ndio tatizo, kwamba ukiishaingia ni ama uijivue uzalendo uweze kudumu (ku-survive) au ufanye uamzi mgumu na kuachia ngazi? Na utakuwaje mzalendo ukiwa chini ya Mwenyekiti wa Bodi kama Mustafa Nyang'anyi ambaye ni kama vile yeye binafsi kuwepo ATCL ni swala la kisheria (hagusiki)? Je, ATCL ni taasisi ya kibiashara au ni huduma ya jamii? Kwa nini serikali kama mwanahisa isiachie maswala ya kibiashara yakafanywa na watendaji (kama wana uwezo na uzalendo) badala ya kuingilia kila mara? Waziri au Katibu Mkuu ana utaaalamu gani wa kufanya maamuzi ya kiutendaji katika shirika la ndege?
   
 8. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60


  kuna matatizo mengi ya kiufundi kuhusu ATCL japo mengi huyu JF member kayabainisha tunamshukuru sana musaidia waziri mwakyembe achambue kupata ukweli.Hoja inawezekana vipi kampuni ya mtu ikawa na uwezo kuzidi serikali?Kimsingi haiwezekani.Inakuwaje presecior air iweze na ATCL ishindwe?bado nchia inahitaji kuwa na shirika la ndege lenye uwezo.Kimsingi CHAMBO ni tatizo, aidha anafanya hujuma makusudi au hana uwezo.Sababu anao uwezo wa kutafuta wataalmu mahiri waliobobea wa kuandika mchanganuo mzuri wa uboreshaji ATCL na kuupeleka baraza la mawaziri kwa utekelezaji.lakini kila mara matatizo hayaishi ATCL.nA PIA MBONA serikali haijatoa tamko kuhusu ubia na shirika la ndege la china kama ilivyopendekezwa siku nyingi na kuota mbawa na kubaki wakodishaji ndege?hapa lazima tukubali mkubwa wa nchi ni dhaifu , khali hii haikupashwa kuwepo muda wote huu.hakuna haja ya kuunda shirika lingine ni makosa kama tulivyofanya NBC leo tumewapa ulaji ABSA na kutucheka,hapa ni kusimamia kwa nguvu na uadilifu mkubwa, shirika linaweza kupona.Kulivunja ni gharama kubwa kuliko kuboresha.Pia hivi watu wa usalama wa taifa wako wapi nchi kuharibiwa huku wakiona na kulipwa mishara mizuri ya walipa kodi ?
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Mbona si JAMBO la ajabu.........mbona wapo watu wanaendesha mashirika yao makubwa ya ndege kuliko nchi nyingi tu...............hili jambo si la ajabu............pia binafsi nimeshuhudia moja ya kampuni ya ujenzi worldwide wana kipato kikubwa kuliko pato letu la Taifa........

  Hoja ya msingi kuhusu ATCL ni kwanini hai-perform pamoja na ruzuku nyingi toka kwa wananchi.........simply utagundua kuwa ni UFISADI............hivi unajua kwanini UDA ilikufa?.......hivi unajua wakati ule wa UDA iko sawa among East and Central Africa countries, Tanzania tulikuwa na Public Transport iliyobora zaidi..........vituo, ratiba, ordinary, express services....enzi zile ulikuwa unamuambia mtu nitafika ofisini kwako saa saba mchana....unapanda UDA na unafika on time....! watu tumeshasahau hii......tukadondoka mpaka "Chai maharage"........

  Mimi nina hakika tukitaka kufanya kweli tunaweza.......Dr. Mwakyembe mumseme kwa mambo mengine....lakini jamaa ni Mzalendo kweli kweli.............kwa mara ya kwanza nilimshuhudia akijiuzulu nafasi yake ya Ukurugenzi wa Bodi ya NBC kupinga ubinafsishaji wake uliokuwa umeghubikwa na UFISADI.............vita ya ufisadi Dr. Mwakyembe hakuianzia kwneye Richmond pekee........huyu mkuu amekuwa mwiba kwa watu wengi sana..........you just watch his pace.........na tumpe ushirikiano......he can not fight alone.........
   
 10. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,102
  Likes Received: 1,492
  Trophy Points: 280
  mwenyekiti wa bodi Mustapha Nyang'anyi ambaye kipindi akiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi alihusika kununua pantoni mbovu leo hii ATCL inanunua na kukodisha ndege mbovu sioni sababu ya yeye kubaki hapo nina hakika atakuwa anahusika na madudu ya ATCL kama mtu mwenye maamuzi ya kiuendeshaji
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Tuwasahulifu sana. ATCL imeuliwa na baadhi ya wanasiasa wakubwa na watendaji serikalini. Hizo hoja za kitoto za mleta sredi naona anataka kuwasafisha majambazi na kuwasingizia vibaka! Kikwete alianza na nia ya dhati ya kuifufua ATCL,lakini amekwamishwa na huo mtandao! ATCL haijawahi pewa pesa yoyote ya maana toka serikalini kama ruzuku ama mtaji. Kuna watu serikalini watafanya party ya nguvu wakisikia ATCL imekufa!
   
 12. O

  Ogah JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ...duuhh..........jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza................
   
 13. Sun Tzu

  Sun Tzu Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mimi ninavyoona, ni kuwa Air Tanzania inabidi kufanyiwa facelift na marekebisho makubwa ya nkiutawala na kimfumo. Tukihitaji Air Tanzania iwezekukuwa kiushindani na kuendeshwa kama shirika la ndege tuynahitaji kufnya ayafuatayo:

  1) Kulifanya liwe shirika huru kiutawala na bila kuingiliwa na mamlaka nyingine yeyote
  2) Watafautwe watu wafuatao kuilongoza

  a) Chief Executive Officer Retired kutoka aidha KLM, Swiss Air au British Airways
  b) Chief Operation Officer Retired or experienced from any reputable Airline
  c) Financial Controler Retired from any of the above Airline

  Wapewe Mikataba ya Miaka Mitatu mitatu renewable mara tatu, na wapewe policy space.

  3) Chief Engineer very experienced anaweza kuwa Tanzanian kwani wapo

  4) Policy Space ya kufanya mabadiliko yanayohitajika bila bughudha

  5) Wapewe uweza wa kifedha na serikali,

  6) Shares za ATCL ziwekwe sokoni DSE kukuza na kuongeza mtaji.

  7) Kbuni Routes mpya na kuchukuwa zile za zamani ambazo zilikuwa profitable. Tanzania ina geographical advantage, na ATCL naamini itafanikiwa.
   
 14. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Nakubaliana kuwa jamaa ni Mzalendo lakini akifanya kazi na Omari Chambo atashindwa tu kwani huyu bwana ni tatizo sana na ndiye kikwazo kwa ATCL kufanya vizuri.

  Tambua Serikali inatoa msaada mkubwa sana pale kama ruzuku, lakini kuna mchwa pale ambao umeanzia wizarani aliko Chambo ambao unakula fedha hizo na kushindwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa na Serikali.

  ATCL inaweza kurudi katika enzi zake kama UZALENDO utawekwa mbele kuanzia IKULU hadi kwenye MENEJIMENTI yenyewe, la sivyo itakuwa miujiza kuifufua ATCL.

   
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hivi ATCL ilikufa lini?.....na Eng Chambo amekuwa PS Mawasiliano au PS responsible na ATCL tangu lini?.........mbona walaji wakubwa walioiua ATCL hawapigiwi kelele?..........nafahamu kuwa ni network fulani hivi............lakini haiwezekani Chambo ndio akawa "chambo" responsible wa kuanguka kwa ATCL...........
   
Loading...