Dr Mwakyembe hapaswi kuhurumiwa, amevuna alichokipanda

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,506
2,000
Tatizo ugonjwa wa Mwakyembe unatumiwa na kina Sitta na group lao kama mtaji wa kisiasa wa kuwachafua watu fulani. Hata Mwakyembe akigundulika kwamba hajanyweshwa au kupakwa au kutegewa sumu au kufanyiwa foul play yeyote bado wakina Sitta na Mwakyembe hawatakuja kutuambia ukweli.

JIulizeni anayeumwa ni Mwakyembe lakini SItta ndio anabeba bango utafikiri yeye ndio anaumwa!!! Hebu tuache siasa za kijinga. NAsubiri kwa hamu nione Sitta na group lao watakavyoangukia pua!!!
 
Pezzonovante

JF-Expert Member
May 1, 2008
642
0
njia iliyotumika kumnyamazisha iwe sahihi au isiwe sahihi imetokana na mfumo ndani ya chamachetu na utaratibu ndani ya mtandao ambao yeye na wenzake waliubariki kabla ya kujua siku moja wangeasi baada ya kunyimwa uwaziri, mkuu, uspika na uwaziri katika kundi lililokosa kulipwa fadhila ndani ya mtandao. Angalau kuhasimiana kwao kumewafanya warudi kwa wananchi ingawa hiyo si dhamira yao na hili ndilo tatizo, hawana dhamira ya dhati hawa ila tu wanatufanya kimbilio wanapoona wanataka kunyongwa kama wao walivyowanyonga wenzao. Hawana jipya, hakuna haja ya kuwahurumia wala kuwategemea kutatua matatizo yetu.
domo kaya nakusoma dot by dot, line by line wewe unahekima na unakina ebu endelea kuandika ,tatizo la wakombozi wetu hawana udhati huwezi taka fanana na anaye kukukandamiza na ukafaulu kuleta mabadiliko moto wa mabadiloko ya kweli hauwezi zimwa na cheo au nafasi kama nataka mabadiko ya zati hakuna atakaye nisimamisha ,huyu bwana kama angekuwa cjj sasa hayo yasinge mpata,how come una rebuke devil alafu unakaa kuzimu wanahaki ya kumpa sumu ,kumnywesha ,kugusisha ,hata kumwekea kichwani,domo kaya kama mtu wa mapinduzi wa kweli hakuna bei soko itakukunua dr alinunuliwa na system aliyokuwa anatuadaa yuko kinyume nayo je ,unamkumbuka che guavara huyu ni muargentina alikwenda kila sehemu kwenye dhuruma alipigana hadi maisha yake yalipo kwisha alipigana na alikufa kwa kile anacho kiamini, fedel castro alimpa cheo uwaziri pale cuba che ,hakukaa sana akajiuzuru ili anyanye anacho kiamini, domo kaya keeep on pushing keeeep on shinning in your interect and wisdom.
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538

Ukinitajia Che Guevara nywele zinanisimama, ukombozi kwake haukujali mipaka, yeye kila aliyagandamizwa alishirikiana nae kwenda kupigana kusaidia kumkomboa. Leo watu tunapigania makundi na kujifanya washabiki. Muargentina kwenda kumpigania mkongo. Wanatakiwa wakina Che Guevara wengine wengi na si mashabiki na wanafiki
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538
2,000
Anayetufanya sisi wajinga ni wewe na group lako la mafisadi, mtu mzima unakazania tu neno nakumbuka bila kusema unachokumbuka nini, huo ndo UNAFIKI mkubwa, unategemea nani mwenye akili zake timamu ataamini tuhuma ambazo hazijatajwa, mtajitahidi sana kutuharibia nchi, lakini hamtaweza kutudanganya, tuna uwezo wa kufikiria kuliko mnavyodhani, labda mtawadanganya wachache tu.
Kweli wewe una uwezo wa kufikiri kwa kudhani kuwa watu wakilshana sumu halafu wewe ukawahurumia kutabadilisha maisha ya watanzania. Walikuwepo na wamekuwepo siku nyingi, wameifanyia nini nchi mpaka kufikia kulishwa sumu. Si afadhali mama Aninilea NKYA akilishwa sumu ntalia na kulalama kuliko Dr Mwakyembe. Kasoma ripoti mpaka leo umeme hakuna miaka mingapi imepita? Yeye ni mnafiki kama walivyo wanafiki wote wanaojifanya wameifanyia makubwa nchi hii? Wewe mwenye kufikiri vizuri hivi umewahi kujiuliza kama nchi yetu inapiga hatua au inarudi nyuma? Unakujua Ipinda anakotokea Dr Mwakyembe? Wana ardhi inayootesha mpaka COCOA kama miti ya porini, kuna michikichi ya ajabu, kuna mpunga usio kuwa na kifani lakini hata daraja hawana. na Dr Mwakyembe mbunge wao miaka zaidi ya saba. Anafanya nini? Anafanya kazi gani? Kama yey ni mkweli si angerudi kwa wananchi aseme anakwamishwa na nini ili wajue la kufanya. Dr Mwakyembe alikuwa rafiki mkubwa wa mafisadi, wakamfadhili akapata ubunge, akasaliti taaluma, akataka ale peke yake akasahau kuwahudumia watanzania. Kuna wanaofikiri vizuri kama wewe wanasema eti kwa kuacha ualimu na kwenda kuwa mbunge wa afrika mashariki na baadae Kyela amelihudumia taifa vizuri sana. Wanaofikiri vizuri bwana kuna raha kuwajua mawazo yao.
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538
2,000
Dont hit around the bush weka mambo hadharani tujue mabaya ya mwakyembe naona umeongea mambo mengi lakini umeshindwa kuanika uovu wa mwakyembe au umetumwa nini.
Aisee kumbe safari yetu ni ndefu na ngumu kuliko nilivyowahi kufikiri. JF Member tena expert member hajui Dr Mwakyembe alipandaje hapo alipo mpaka akawa mwanasiasa. Nilidhani ni wawili watatu tena waliokuwa hawajazaliwa mwaka 2002 ndio hawajui jamaa alitokea wapi bali wameamua tu kumshabikia, kumbe hata wale ambao leo wanategemewa ndio watoe mawazo na mwelekeo wa wapi tuendako si tu hawakumbuki bali hawajui lolote kuhusu viongozi wao. Ndio maana kumbe hat yule mzee aliyekamatwa na kilo kadhaa za madawa ya kulevya na mizani yake bado aliweza kuwa mmoja wa mameya katika jiji la Dar es salaam.Hata yule mwizi wa meno ya tembo kule Kasulu akawa mkuu wa mkoa na baadae katibu wa chama Taifa. Yote hii kwa sababu hatayaliyoandikwa magazetini nayaliyoripotiwa na polisi watanganyika hatuyakumbuki. Eti hata hatukumbuki Muungano wetu na Zanzibar ulikuwa juu ya nini. Ole wako unayekumbuka, wewe niz mzushi, wewe ni fisadi. Tunaishi kwenda na fasheni na kubaki kuwa washabiki tu wa wanalishana sumu na wanaolishana 'dowans'. Nimehamanika sana.
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538
2,000
Huyu aliyenzisha thread hii ni wale cheap ones wanaondesha maisha yao kwa usuru mdogo wa kulipwa na kina lowassa,days are numbered and what ever goes around comes around my dear either in the same way or otherwise,chain yote waliohusika polisi usalama na vibaraka wengine dhambi hii ya utumishi kwa ujira wataulipa kwani mzimu wa tendo hilo wanatambea hao,hata akifa mwakyembe his spirit will prevail in a good manner siyo ya lowassa

Angalau wewe sio cheap lakini unapenda cheap talks. Hakuna Lowasa anayesifiwa wala kutakiwa hapa, hawa wote ni wamoja wewe unataka kuanzisha group ili watu wafanye ushabiki. Hashabikiwi mwanasiasa hapa wote unawona ndio waliotuleta hapa tulipo, kama wewe una huruma na wagonjwa nenda muhimbili wapo wengi wa kuhurumiwa sio hawa waliojitakia ambao pia waliwafanyia wenzao mabaya
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,845
2,000
Kama yey ni mkweli si angerudi kwa wananchi aseme anakwamishwa na nini ili wajue la kufanya. Dr Mwakyembe alikuwa rafiki mkubwa wa mafisadi, wakamfadhili akapata ubunge, akasaliti taaluma, akataka ale peke yake akasahau kuwahudumia watanzania. Kuna wanaofikiri vizuri kama wewe wanasema eti kwa kuacha ualimu na kwenda kuwa mbunge wa afrika mashariki na baadae Kyela amelihudumia taifa vizuri sana. Wanaofikiri vizuri bwana kuna raha kuwajua mawazo yao.
  • DOMO KAYA SASA UNACHEMSHA NA UNACHEFUA WW WANANCHI WA JIMBO LAKE UNAWAJUA AU WATANZANIA WANAOUMIA NA MGAO WA UMEME UNAWAJUA? HAO MATAJIRI WA TANZANIA 10 AMBAO WAKO KTK weekpedia, weakleaks au google Mwakyembe yumo? mbona unashangilia mtu anayekunya hadharani na kumlaani anayeondoa kinyesi ili pawe safi
  • Mwisho wenu umefika sasa kwa Mafisadi wote hakuna cha urais 2015 wala kupendekezwa na huenda mkaenda jela tutakapokasirika
 
chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,940
2,000
Naamini ni kigeugeu lakini naomba apone ili atafakari zaidi uccm wake. Kwaresma hii ntakuombea
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538
2,000
Mngepata kujua Dini za hao wanaosapoti hoja za mwanzisha hii sred iliyojaa kila aina ya dalili za ujambazi wa kigaidi ndo mngeshangaa na kuamini kuwa hata darasani watu hao wapoje

Ndugu hakuna haja ya kujua dini za wanaosapoti au wasiosapoti ishu hapa ni kuwashughulikia manyanga'u wanaofanya maisha yetu yawe magumu. Bei ya kilo ya sukari haichagui dini. Daraja likivunjika halichagui dini na sumu mtu akilishwa haichagui dini. Kolimba, Malima, Katabaro akina Dr Fupi hawakuulizwa dini zao, waliadhibiwa kwa ukweli wao. Wakati Baraza la mawaziri likiamua kumshughulikia mtu fulani na kazi akapewa Masha, baraza lile lilikuwa na manyang'au wanaokwenda kanisani na msikitini.

Tusikubali hata watugawe kwa misingi ya dini, ukabila ukanda wala ukamanda feki wa ufisadi. Wote ni wamoja, wote ni wezi, wote ni majambazi. Ndio maana nampenda Masilingi, yeye alishughulikia wenzake, aliposhughulikiwa yeye akajua zamu yake imefika. Muulize mzee Kitine aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Imrani Kombe yeye mapema walimpeleka alipowatanguliza wenzake. Fungueni macho ndugu zangu wadanganyika, oh samahani Watanzania, tusipende sana kusahausahau
 
Ngararimu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
285
500
Mbona upangaji wa maneno na taarifa zinazotolewa zinaonyesha wazi kwamba huyu ni E.L naomba asikimbie humu jamvini naondoka ntarudi.
 
patience96

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
1,345
2,000
Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.

Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda

Maneno gani? Unakumbuka nini? Mifumo gani? Alitengeneza sumu gani? Wenzake akina nani? Wamewauwa akina nani?
Kweli wewe domo kaya!

patience96

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
1,345
2,000
Ndugu hakuna haja ya kujua dini za wanaosapoti au wasiosapoti ishu hapa ni kuwashughulikia manyanga'u wanaofanya maisha yetu yawe magumu. Bei ya kilo ya sukari haichagui dini. Daraja likivunjika halichagui dini na sumu mtu akilishwa haichagui dini. Kolimba, Malima, Katabaro akina Dr Fupi hawakuulizwa dini zao, waliadhibiwa kwa ukweli wao. Wakati Baraza la mawaziri likiamua kumshughulikia mtu fulani na kazi akapewa Masha, baraza lile lilikuwa na manyang'au wanaokwenda kanisani na msikitini.

Tusikubali hata watugawe kwa misingi ya dini, ukabila ukanda wala ukamanda feki wa ufisadi. Wote ni wamoja, wote ni wezi, wote ni majambazi. Ndio maana nampenda Masilingi, yeye alishughulikia wenzake, aliposhughulikiwa yeye akajua zamu yake imefika. Muulize mzee Kitine aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa Taifa. Imrani Kombe yeye mapema walimpeleka alipowatanguliza wenzake. Fungueni macho ndugu zangu wadanganyika, oh samahani Watanzania, tusipende sana kusahausahau

... the tongue of a gossip!!!
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,150
2,000
Nilipata kuandika hii kitu miaka hiyo

Ni alasiri nzuri kabisa chini ya jua hili katikati jiji hili la DSM, niko ofisini mwangu kama mwanachama wa JF nasoma na kuchangia maada mbali mbali, mara nasikia hodi ya uwoga inapigwa, nika-respond kuwa ingia, mgeni huyu hakusikia mpaka pale nilipoenda kufungua mwenyewe. Napokewa na sura ya mashaka mashaka na kijana,mwanafunzi wa chuo fulani cha uandishi wa habari jijini. Nasogeza kompyuta yangu pembeni, ili nimsikilize kikamilifu anasemaje, nimeamua namsomesha fani hii.Nimejiajiri kama mhandisi.

Karibu! Nikaanza kusema, asante mzee akaitikia (acha nijitambulishe kama mwanaJF)

Kijana:Shikamoo mzee!
Mwana JF: Marahaba kijana,
Mwana JF: Karibu kijana, masomo yanasemaje??Kijana: naendelea vyema mzee, samahani nimekuja kuchukua muda wako, najua uko bize sana mzee, ndio maana nimeingia kwa woga, secretary sijamuona sio kawaida mzee, is everything ok here??

Mwana JF: Usihofu, nimekuwa nikipumzika, japo ni saa za kazi, umeme umekatika ghafla, sekretari akataka apige simu akagundua nayo imekatwa japo tumelipa bili, kwa hiyo ameenda kufuatilia haya yote, hatuna umeme kabisa, generator nimenunua wiki iliyopita limekufa, linaonekana lilikuwa feki, japo zuri, so unaniona hapa nilikuwa nasoma soma magazeti yetu kutumia umeme wa betri wa kwenye laptop yangu, vipi kuna tatizo.

Kijana: Pole mzee , kilichonileta hapa, da! Kama hali yenyewe ni hii ningejua ningekuja si nyingine, mzee kwa kifupi nimechanganyikiwa, mzee kuna mambo yananiumiza sana, nimeona nije nisikie unasemaje.

Mwana JF: ( najitengeneza vizuri kwenye kochi) endelea kijana usihofu, vipi ni kitu gani hasa, maana sio kawaida hii, I am getting nervous,umeharibu sehemu??

Kijana: hapana!
MwanaJF: Mhh,! Tell me,

Kijana: Mzee pengine, nitakuudhi!, tatizo langu ni kutaka kukuuliza maswali ya kisiasa hapa nchini, hii pia ni sehemu ya project yangu, ywa mwaka huu wa pili. Nimeonelea niulize watu wa kila fani , wakubwa kwa wadogo, nikaona si vibaya nije kwako mzee wangu nikuulize kuhusu mustakabali wa taifa letu, siasa zetu na mambo mengine mengi.

MwanaJF: (Nikaamka kwenda kuchukua vinywaji kwenye kafriji kangu nikazishika shika kungalia ubaridi). Unatumia soda gani?
Kijana: Yoyote mzee,

Mwana JF:afadhali zina ubaridi,karibu pepsi

Kijana: Asante sana!
Mwana JF: Kijana, unataka kuongelea mambo makubwa sana, siasa?? Leta habari unaanzia wapi?? Ni topic pana sana hii kijana wangu! Mh! Uliza maswali yako, naona umeandika kabisa!

Kijana: Ndiyo nimeandika mzee, lakini yanaweza yakabadilika, mzee unaamini ndani ya CCM kuna viongozi wasafi??

Mwana JF: Kijana mpaka unauliza swali hili, kuna maswali unajiuliza,kwa kifupi nakuambia kwa kujiamini kuwa hakuna! Hata mmoja! Hakuna!!

Kijana: (akiniangalia kwa mshangao), mzee maneno mazito haya, kwa nini unafikiria hivi, una proof??

Mwana JF: Kijana nina wasiwasi umechagua topic ngumu sana!
Tumewapa miaka 40 ya kuongoza, kila kukicha afadhali ya jana, CCM hawa ndio walioifikisha Tanzania yetu hapa, tuna watu, tuna maliasili, tuna sheria na katiba, ila mara zote tunakosa viongozi safi, waliojitoa, wanamfikiria mtanzania wa Masaki na yule wa nzega Tabora. Tuna kila sababu ya kuendelea , kila sababu

Kijana: Kwa hiyo? Si…..

Mwana JF: Subiri! Kijana kila kitu kina kipimo chake na muda, huwa tunapewa probation period miezi 3 hili kuwa approved kuendelea na kazi! Kuna contracts na project zote zinaelezea mwanzo wa jambo fulani na mwisho wake,

MwanaJF: what is contract??

Kijana: mhh, is…..

MwanaJF: A contract is an exchange of promises kwa kifupi, kuna contract za aina nyingi, mpaka Oral or unwritten contract. Kijana, unapotoa fedha dukani upate soda how are sure utapewa soda?? Je akikupa kitu kingine utakubali?

Kijana: Hapana

Kijana: Unataka kusema nini??
MwanaJF: Wanakuja kila baada ya miaka 5, wanaomba kura, wanaapa kwa kutumia vitabu vitakatifu, kuilinda katiba, na kutetea wananchi na kusaidia watanzania!
Kijana: Naanza kuelewa kidogo

MwanaJF: wanateuana, wanapeana vyeo, wanakura rushwa, ufisadi kila kona kuanzia ngazi ya kijiji mpaka taifa kwa mkuu wa nchi!, wanalindana, kila kukicha maigizo, CCM hii hii ndiyo imetufanya tuwe maskini, kuna watu wanaishi kama Obama nchi hii, kuna watu wanakosa milo 3 kwa siku! Kuna watu wanasafirisha magari kwa ndege nchi hii, kuna watu wanajifungua njiani kwa kukosa ambulance! Kuna watanzania wanasoma shule za kiingereza tangu utotoni, wakati wko wengine wanasoma shule zisizo na waalimu tangu utotoni!
Kijana: (anashusha pumzi) mzee sasa kwa hiyo unatak..

MwanaJF: Ndiyo , Leo hii kuna watu wanataka watuaminishe kuwa akinawatu kama akina Mwakyembe ni wasafi, akina Kilango ni wasafi na wengine kama hao, kisa kwa sababu wanapinga waziwazi ufisadi, huku wakila na kupanga mipango na hao hao mafisadi,majina yao iliyapite kuchaguliwa yanapitishwa na hao hao mafisadi! wakiomba kura wanataka kupitishwa na mafisadi. CCM imeoza kiasi ambacho mtu yeyote anayeelewa dhana ya usafi hatakiwi kubaki humo! Hata kwa sababu yeyote itakayoonekana ni nzuri! Kwa kifupi hakuna kitu watakachofanya ndani ya CCM kisipitie mikononi mwa mafisadi huu ndio ukweli kijana! Hupo??Kijana: (akiwa mnyonge) nakusikia mzee!

MwanaJF: Najua huna raha, kazi yangu leo ni kukuweka sawa, ili unapoandika article zako ziwe realistic, na zitoke moyoni, lazima uwaze katika big and different directions!

Kijana: endelea mzee;

MwanaJF: CCM haijaanza leo, wabunge machachari hawajaanza leo, kufunguliwa mashtaka viongozi hakujaanza leo, kwa kifupi hamna jipya, watu ni walewale wamekulia kwenye system na sheria zilezile, kubebana kulekule, kuna wabunge walitikisa nchi hii tangua hata wakati baba wa taifa yuko hai! Ulikuwa mtoto pengine!

Kijana: Tutawezaje sasa kuondoa hii CCM??

MwanaJF: Lazima tufuate kanuni za msingi, unapopiga dawa kuua wadudu ndani ya chumba, huchagui wadudu! Unapiga dawa chumba kizima, wadudu walio na nguvu huwa wanaishi, hawa viongozi wa CCM wanaoonekana wasafi hata kama CCM wataondoka kwenye majimbo yao watasimama tu wataishi watakuwa wabunge kwa chama chochote kile!

Kijana: Mzee unataka kusema hawa watu waondoke CCM ili kuthibitisha usafi wao??

MwanaJF: Umenipata haswaa!, maamuzi ya bungeni, hata siku moja huwa hawatofautiani, wanakuwa pamoja, kwa kifupi kuna vyama viwili nchini?

Kijana: vipi hivyo tena?

MwanaJF: CCM A, na CCM B, CCM A-mafisadi, na CCM B, wasio mafisadi.lakini CCM A+CCM B =CCM! Ni walewale! Ebu ona Lowassa baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu CCM ana cheo gani?? Kwa nini?? Au Mwakyemebe lengo la kuacha kufundisha chuo kwenda kwenye siasa lengo ni nini?? Si pesa?? Au?? Funguka macho! Umeshawaona wabunge hawa wasafi wanakataa pesa za posho bungeni, wakati hospitali ya kisarawe na Bumbuli hazina dawa??

Kijana: Interesting!

MwanaJF: Kwa hiyo mijadala ya nchi hii iko ndani ya CCM wasafi na wachafu, lakini jumla yake ni walewale! Vyama vingine vimezikwa hata vile ambavyo wananchi tungepaswa tujitahidi kuviinua tuwape nchi, tuone sera mpya, na nguvu mpya za kweli, lakini vimeuliwa! Hakuna chama cha siasa kitakachoshika nchi hii mbali ya CCM kama vita yetu tutapigana kama sasa hivi!

(Mara mlango unagongwa hodi, ni secretari)

Sekretari:Boss nimerudi, TTCL walikata simu bahati mbaya!

MwanaJF: Na umeme?

Sekretari: Tanesco wamesema hawataleta mpaka keshokutwa,

MwanaJF: haya, tumezoea sasa! Asante, wahi nyumbani sasa, nina mazungumzo mazito

Kijana: kuhusu Rostam unasemaje mzee?

MwanaJF: (akimwangalia kijana usoni kwa makini) naona unataka kufanya kosa la wengi hapa Tanzania.

Kijana: kwa nini

MwanaJF: Ok, kafanya nini??

Kijana: si fisadi??

MwanaJF: kafisadi nini??

Kijana: Kagoda, Richmond, na vitu kibao!

MwanaJF: Kwani yuko jela??
Kijana: Hapana

MwanaJF: Kwa nini? Kama mtu ni fisadi, vithibitishi mnavyo, kwa nini hayuko jela??
Kijana: inabidi uamke, Rostam siyo fisadi kwa lugha ya haraka haraka. Kama angekuwa hivyo angeenda jela tangu tulipoanza kusikia taarifa hizi!

Kijana: unataka ksuema nini tena mzee!

MwanaJF: Kijana katika vita yeyote ile lazima ujue mbinu ya kushinda!, kuandika kwenye magazeti na kumjua kuwa fulani ni fisadi hakuuondoi ufisadi, hata kumpeleka jela kiongozi pasi yeye kuturudishia fedha zetu , hakumsaidii mtanzania wa kawaida! Kusema huyu mtu fisadi, hakutuletei maendeleo wala tija yeyote, nikwambie kitu??

Kijana: sema

MwanaJF: jamii ya Tanzania imekata tamaa, au imeficha uwezo wao kwenye habari za udaku, kwa sababu tumezoea udaku udaku, jamii yeyote maskini huwa inashiba sana taarifa za kusikia au kupewa moyo, kisaikolojia habari ya kuwa Rostam ni fisadi inawafurahisha wengi, japo haiwaondoi katika matatizo yao! Kwa kifupi akili yeyote fupi iliyodumaa ni ile isiyofikiria kiini cha tatizo inafikiria tatizo wanaloliona, unaufahamu mti nadhani, u mgomba

Kijana: Ndiyo;
mwanaJF: Ukikata majani au matawi, hayataota tena??

Kijana: yataota!

MwanaJF hivi hauoni kuwa , Rostam ni katawi kadogo tu kati ya li jimti likubwa linaloitwa CCM ??

Kijana (anacheka)

MwanaJF: Usicheke, havichekeshi hivi vitu, ni miaka sasa tumesikia Rostam fisadi, mahakama, zipo, rais yupo, wabunge na wanasheria wapo, kila sababu ipo! Kwa nini haendi jela??

Kijana: sijui

MwanaJF: Huoni kuongelea kuhusu Rostam ni kupoteza muda?? Kwa nini tusiwabane hawa viongozi watoa hesabu ya uwajibikaji wao katika hili?? Huoni kijana kuwa kumsema Rostam kwenye magazeti ni swa na kumchoma moto kibaka kariakoo?? Kwa nini tunaona ni hatari kuua kwa mawe, na sio kundika kwa peni??

Kijana: sijui!

MwanaJF: Au ni ile akili finyu ya baadhi ya watanzania ya kuwagawa wezi, kuwa mtu wa serikali akiiba hela ya umma elfu 10 ni afadhali kuliko wa milioni moja?? Kwa nini tusikae chini na kuona ufisadi ji janga la kitaifa ?? hatuoni kunogelea kuhusu Rostam ni kulimit mawazo na uwezo wetu?? Kwani akiondoka Rostam mafisadi hawapo tena?? Rostam anafanya ufisadi na nani?? Peke yake?? How?? Kwa nini tusione tunawajibika moja kwamoja kuzuia tatizo kama ili lisitokee tena, tung'oe mzizi huu na mzizi huu ni CCM na serikali yake??

Kijana: kwa hi..

MwanaJF: Umeshawahi kwenda kwa waganga wa kienyeji??

Kijana: huwa nawasikia!

MwanaJF: Basi ,ni sawa na waganga wa kienyeji kutoa shetani mdogo kwenye mwili wa mtu, kwa nguvu ya shetani mkubwa! Ambaye ni hatari mara milioni ya kale kadogo!!! CCM ni shetani likubwa, linajitahidi, liwashtueshtue vishetani vidogo, ambavyo ni fisadi! Ili kuwafurahisha watu, tena mara nyingi , haya majini huwa yanarudia tena mtu yuleyule!!Kijana: Oho!
MwanaJF: Uwezo wetu ni mkubwa kuliko kumsema Rostam au Mwakyembe, uwezo wetu ni mkubwa unatisha, japo watanzania wengi wameprove ni wazuri kuongea na kuandika, uwaambie tuandamane, hawataki, wengine waambie hata kupiga kura hawataki! Nikuchekeshe!

Kijana: Mhh! ( akiwa haandiki tena)

MwanaJF: Viongozi wengi tuliowaita mafisadi, wamachaguliwa na sisi wenyewe akiwamo huyu Rostam! Waliopatikana na hatia, walipokelewa kama mashujaa! Kana kwamba vita hii tunapigana sisi wenyewe! Kuna tatizo sehemu na tusipogundua tutaandika weee mpaka tukome!

Kijana: Nani wa kuwapeleka hawa wachafu jela?? Nani atawashtaki, ni yule mama mjamzito mwenye kipato cha elfu 2 kwa mwezi?? Au ni yule mmachinga anayeuza vitu tandale, nani wa kumpeleka Rostam na wenzake mahakamani??

MwanaJF: Umeuliza swali, juzi Mwakyembe alisema yeye ni mwansheria, mwanahabari, ana makampuni mengi tu, kwa kifupifedha anayo, maana mahakamani huendi bila pesa! Tena akasema Rostam ni mchafu! Kumbe naye anajua, ila naye anamsubiri fulani ampeleke Rostam mahakamani!!! Kama mbunge anaujua uchafu wa mbunge mwenzake basi anaujua kwa mapana kuliko tunavyodhani! Kwa nini asiwe wa kwanza kutushirikisha tupeleke mafisadi mahakamani??

Kijana? Ndani ya CCM kwa taratibu zao sio rahisi mzee!MwanaJF: Good! Then yu are simply saying, tuwaondoea CCM, kama nilivyosema mwanzoni??

Kijana: ndiyo, sasa kwanini alisema vile??

MwanaJF: alikuwa na haki ya kujitetea, kwani hoja za maslahi hapa haziingiliani na swala lake, watu wamechemsha, hoja yangu ni kuwa hakutakiwa kusema Rostan anaoga maji machafu! Kwani yeye ni mchafu , ni sawa na rais kuwapa muda mafisadi wa madawa ya kulevya, bandarini n.k?? kweli umpe mwizi muda?? Mtu aliyeiba fedha za maskini wa nchi hii??
Kijana: duh! Ni kweli

MwanaJF: Kama Rostam anaoga maji machafu Mwakyembe anaishi kwenye dampo!

Kijana: (anachukua peni haraka) mh!, unasemaje mzee??

MwanaJF: Kama Rostam anaoga maji machafu Mwakyembe anaishi kwenye dampo!CCM ni dampo, ni jalala, anayeishi humo hani-convince kuwa naye ni msafi hata kama atasema msafi hata kama nitamwona msafi, lakini yuko sehemu chafu, anakula, anaongea, anapanga mipango na hawa wachafu! Huyu naye by no means ni mchafu!Tusafishe Tanzania

Kijana: Mzee maneno haya siwezi magumu!

MwanJF: Ni kwa sababu mawazo yetu tumeyaweka upande mmoja, mtu yeyote atakayesema kinyume na Mawazo ya wengi ataonekana mbaya, nikimsema vibaya mwakyembe ntapigwa hata mawe hata kama nitasema sahihi! Kila kitu kina mahali pake, siwezi nikacheza mdundiko kanisani wala siwezi kuimba nyimbo za bikira Maria msikitini. Huwezi kuhubiri usafi ndani ya CCM!

Kijana: mzee asante sana, maneno mazito haya

MwanaJF: Unajua hatari ya kuishi dampo?? Taratibu wadudu wataingia mwilini, hata kama utajitahidi kujisafisha na kuwa msafi, why risk?? Kwanini uiishi kabisa sehemu safi ukafanya mambo yako kwa raha? Kuliko kuwa double standard?? Unafikiri kwenye ile press connferene ya Mwakyembe opponent wake angekuwa mweusi angesema maneno yale??? Kwa nini tumuone Rostam ni mwarabu wakati ni raia wa Tanzania na jela imewekwa kwa ajili ya wote wavunjao sheria??

Kijana: mzee inatosha nimeshapata vya kuandika

MwanaJF: habari ndiyo hiyo hata kama utatukanwa!, ila message sent

Kijana: asante sana mzee, neno la mwisho mzee

MwanaJF: Tuko nyuma ya kila anayeitakia mema Tanzania, walio safi ndani ya CCM, waondoke wajaribu Mrema alsihajaribu, tena wakati Nyerere yuko hai miaka 15 iliyopita!!! Kama wasafi na wachapa kazi popote mtakapoenda mtapokewa ! CCM ilishashindwa siku nyingi! Tuone tufanye nini kwa kuwaza mbali na kuwa upeo mkubwa sio kila kukicha kuwasema watu ambao wanatakiwa kuwa jela au wathibitike kuwa sio wachafu!. Vyama vya upinzani vijipange, sio sawa na vinavyofanya sasa! Vibadilike!
Kijana asante sana mzee kwa kuchukua muda wako
MwanaJF: karibu, so title ya project yako itakuwaje??

Kijana: KAMA ROSTAM ANAOGA MAJI TAKA, MWAKYEMBE ANAISHI KWENYE DAMPO!(CCM-A,CCM-B??)

MwanaJF: Mhh, mi simo, je wakipinga watu hiyo title??

Kijana : wakipinga kwa hoja sina tatizo haya ni maelezo na mawazo ya mtu

MwanaJF: Sasa ni saa 11, jioni unaenda wapi, kwako ubungo??
Kijana: ndiyo mzee:

MwanaJF: Itabidi twende wote huwa nakaa mpaka saa 2 usiku kukwepa foleni, leo hata sina umeme hata nikikaa mpaka saa 2 sitakuwa nafanya kitu, twende pamoja

Kijana: kweli foleni inaboa sana!

MwanaJF: Nayo ni Rostam??
Kijana: NO!
(Wote wanacheka na kuondoka)
 
tyadcodar

Senior Member
Aug 16, 2011
170
195
pole sana dr mwakyembe. wewe ni jasiri usiyeogopa fisadi. usingesoma ile ripoti tungejuaje mafisadi wa nchi hii. mungu akuponye wanaochekelea taabu zako washindwe na walegee. endelea kumtegemea muumba wako utapona.

tena wanatapatapa sasa hivi hamupati urais ng'ooooo,yote hayo ni matokeo ya dhambi yao kina manumba na wenzake wanasema hawajaulizwa bado
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,367
2,000
Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.

Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda

Wewe nina mashaka na wewe!!! napita
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,150
2,000
I mean unaweza ukakaa chini na kutengeneza logic na ukagundua tatizo kubwa la Mwakyembe, anawaacha watu njia panda hasa wakati huu.

1. Je kuna watu amewakosea wanalipa kisasi? i.e EL, Rostam, etc

2. anajua siri za mtu fulani na detail zote za richmond na kuna siku atasema?? -Kikwete na Richmond

3. Au je ni akina Sita na ambao watatumia mwanya huo kujinufaisha kisiasa??

In either case unafiki wa mwakyembe umepitiliza na sasa anavuna alichopanda.

angeweka wazi

1. nani anataka kumuua
2. na kwa nini

watam'balali soon na akili zile zile za kitanzania zitaishia kusema lolote lile!
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538
2,000
Mbona upangaji wa maneno na taarifa zinazotolewa zinaonyesha wazi kwamba huyu ni E.L naomba asikimbie humu jamvini naondoka ntarudi.
Hatuwezi kupata jawabu la matatizo yetu kama tunaojidai 'great thinkers' tutakuwa kila inapokuja hoja ambayo moyo wako haupendi kuusikia unakimbilia kufany speculations za kitoto. Lowasa na Mwakyembe ni mama mmoja baba mmoja. Hawana tofauti hata kidogo wale, tofauti yao kubwa angalau msimu wapo katika kambi mbili ambazo kila moja zinutaka urais. Angalau Mwakyembe hafikirii kuwa Rais labda waziri mkuu lakini lengo lao moja kuchukua madaraka ya nchi hjii kuendelea kuwala wajinga. Hivi hatujiulizi hawa walikuwa wapi siku zote hizi na hao ndio tena senior members katika chama chao? EEnnnh jamani ujinga utatuisha lini sisi.

Hakuna hata waziri mmoja wa serikali hii mimi ni mwenzangu, wanaishi maisha kama macelebrities wa huko ulaya katika nchi masikini kama hii ambayo mwananchi wake ana kipato chini ya dola moja halafu unamuona huyo kiongozi mzuri eti tu alisoma ripoti yenye ukweli nusu bungeni na baadae sijui kanyweshwa sumu.

Inawezekana amekula sumu na makahaba ambao viongozi wetu huenda kuwatembelea huko ulaya halafu leo anatibiwa kwa pesa zetu, so what? Tumepata maendeleo?

Wanyweshane sumu, wapakane je kijijini kwangu pale ile jamii yangu itapata maji safi? Kule kwa mtogole ile harufu itaisha, hawa graduates watoto wa mtaani tunajua wanapokwenda baada ya kushinda pale fire kwa miaka kadhaa. Sipendi unafiki wetu, tulifahamu tabia ya EL kabla hajawa waziri mkuu, kuna watu walitoa tahadhari, lakini kama kawaida ya ushabiki wetu tuliwazomea waliotoa tahadhari, leo hata kuja kuwaambia samahani tunashindwa. Angalau Jenerali Ulimwengu na Raia Mwema walipojua makosa waliyoyafanya walimuomba msamaha mzee Mwinyi. Mwakyembe ni muwakilishi tu wa wanafiki na mahayawani waliokimbilia kwenye siasa kujinufaisha kwa gharama ya jasho na damu ya wananchi
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538
2,000
I mean unaweza ukakaa chini na kutengeneza logic na ukagundua tatizo kubwa la Mwakyembe, anawaacha watu njia panda hasa wakati huu.

1. Je kuna watu amewakosea wanalipa kisasi? i.e EL, Rostam, etc

2. anajua siri za mtu fulani na detail zote za richmond na kuna siku atasema?? -Kikwete na Richmond

3. Au je ni akina Sita na ambao watatumia mwanya huo kujinufaisha kisiasa??

In either case unafiki wa mwakyembe umepitiliza na sasa anavuna alichopanda.

angeweka wazi

1. nani anataka kumuua
2. na kwa nini

watam'balali soon na akili zile zile za kitanzania zitaishia kusema lolote lile!

Woooow! Swali la msingi sana. Kwanza ajali. Alisema imepangwa. Pili Alshabab. Alisema wametumwa. Tatu wakampata wamempa sumu. Ni wazi anawajua. Je ni akina nani hao? Je wanataka kumuua kwa sababu gani? Je kuna uhusiano wowote na ile hadithi ya JK ya wanachama wa chama chake kuhasimiiana? Inawezekana hili suala ni la kichama mno kuliko kiserikali. Akiwa bado mwanachama wa chama chake anajua vyema jinsi wanavyofanya kazi, asitupigie sisi kelele wala kutaka huruma zetu, huo ndio utaratibu wao, wacha taratibu zao zichukue mkondo wake
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom