Dr Mwakyembe hapaswi kuhurumiwa, amevuna alichokipanda

Inawezekana niko biased sijui prejudiced. Mara nyingi nimekuwa nikisikia watu wakisema chama si kibaya bali watu ndio wenye matendo mabaya, Nisemehe tu ndugu yangu mimi nimeshindwa kabisa kutofautisha watu na chama. Sifurahii ugonjwa nasisitiza kusema wacha mfumo waliouweka ufanye kazi waliyoitaka hata kama huo mfumo utawaathiri waliouweka. Ingawa haikuwa lengo lao uwaaathiri wenyewe angalau basi wajue ubaya wa mfumo wao kwa wale waliowawekea

waeleze...wataokota kwenye nyavu wenyewe
 
Nashawishika na hoja zako.
 
Nimefanya hivyo makusudi, watanzania tunajifanya tunapenda kusahau sana, wenye kumbukumbu na wenye hamu na ari ya kutaka uchambuzi wa kweli na si kufanya ushabiki watatafuta na kufahamu na katika kutafuta huko kutawafanya wamjue zaidi Dr Mwakyembe na kuwajua zaidi wanasiasa wengine wanafiki ambao hawana lengo lolote la kuwasaidia watanzania bali kuwatumia. Ukiwa makini utataka kujua zaidi kuliko kusubiri kuambiwa. Mangapi umeshaambiwa mengi na umeyasahau hapo hapo bila kuyafanyia kazi? Ukitafuta utakumbuka na utataka kujua zaidi.
uko ni kutegana sasa; weka wazi mambo, mambo yako mengi ya kufanyia utafiti si hilo tu la Mwakyembe, kwa vile wewe umepata kujua kweli mapema hunabudi kusaidia umma kujua hiyo kweli ni ipi si tu kuleta habari zenye mafumbo na utata juu yake.
 
Mkuu wangu meningitis unajua wakati huo Mwl. Nyerere aliposema upinzani wa kweli utatokea pale CCM itakapo gawanyika alikua anadhani kkt CCM kulikua kuna wanachama wasafi ambao wangekataa kuishi na wanachama wachafu,kwa hiyo aidha wasafi wangeamua kujitoa na kuanzisha chama chao ama wangewafukuza wachafu. Hii haikutokea kwasababu karibia wote siyo wasafi na CCM ilikua ni njia ya mkato kupata madaraka na mali. Mleta hoja amemzungumzia Dr. Mwakyembe,lakini kwangu mimi Mwakyembe anawakilisha aina ya viongozi na wanachama ndani ya CCM wanaodanganya watanzania kupigana vita bandia ya ufisadi wakati na wao ni mafisadi wasaka tonge zaidi!
Ndugu yangu kuna sehemu nimesema kuwa Dr ni mfano tu wa wanasiasa ambao wana malengo yao ya kututafuna na kutunyonya, wanapokutana na wanaisiasa wnzao ambao wamewazidi maarifa ndipo hukumbuka kumbe kuna kundi la wajinga ambalo linaweza kutusaidia. Basi wao huchunguza tunataka kusikia nini na wao kufanya kile tunachotaka kusikia na pengine ndio matarajio yetu ndio ajenda yao, lakini bila kuwa na dhamira ya dhati ya kuyatekeleza hayo wamayohubiri. Ndio maana mtu anaweza kujipambanua ni kamanda wa ufisadi kalini anapoambiwa aachane na mkuu wa wilaya ambaye ndio chanzo hasa cha ufisadi hataki kwani anajua mzizi wake utakatwa
 
Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.

Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda
kweli asiejua maana usimpe maana na alalae usimuamshe
 
uko ni kutegana sasa; weka wazi mambo, mambo yako mengi ya kufanyia utafiti si hilo tu la Mwakyembe, kwa vile wewe umepata kujua kweli mapema hunabudi kusaidia umma kujua hiyo kweli ni ipi si tu kuleta habari zenye mafumbo na utata juu yake.
Kupanga ni kuchagua. unayo mambo mengi kweli nakubali. Basi yafanyie hayo mengine na wengine watayafanyia hili kulingana na jinsi wao wanavyoliona umuhimu wake ka,a wewe ambavyo hayo mengine umeyaona umuhimu wake. Imani yangu inaniambia kuwa mtu akifanyia kazi kitu yeye mwenyewe atakithamini na kukipenda. Natamani watu wafanyie kazi hili ili tuweze kuchukua hatua na tusiendelee kusikiliza wengine na kuwaamini hivyo kuendelea kudanganyika. Kama hakusema na mimi ninamzushia tu ni tayari kusutwa na kukosolewa
 
The grain of wheat.

Umenikumbusha Mugo, ni kweli ni kama story ya Ngugi. Najiuliza hivi kama kuna mtu angetokea kipindi kile ambacho Mugo anaaminika na kuheshimika kwelikweli kwa ushujaa ambao hakuufanya akasema aliyemsaliti Kihika ni Mugo watu wamgekubali? Namuheshimu sana Ngugi, ama kweli yeye ni nabii
 
Watu bwana.Utafikiri wewe ni mtakatifu.Mtu akitenda mema 99 na kosa 1 ...hilo kosa litashine kupita mema yote.Inawezekana mwakyembe alikosea lakn kumsulubisha mtu ambaye hata alijitahidi walau kidogo kuweka hadharani yaliyoficha licha ya kuhatarisha uhai wake si haki hata kidogo.Tuwe na huruma wakati mwingine.
 
Mmh Domokaya umejipanga,nakuona unavyozipangua hoja za wanaojaribu kumtetea Dr Mwakyembe.Nimezisoma post zako kwa kina,unaweza kumpoteza mtu hasa kama sio mfuatiliaji wa mambo.We na Dr slaa kuna kitu mnafanana juu ya uwezo wa kubadili fikra za watu na kuwaza yale mnayotaka nyie.Sijui ni Taaluma mmesomea au kipaji toka kwa maulana,ila ni vyema ukaandika mabaya ya Dr Mwakyembe,alifanya nini,alishiriki vifo vya akina nani.Amehujumu vp nchi.Unajua fika kuwa sio rahisi kwetu sie tulio wengi kupata data au taarifa alizowah kuzitoa au maneno ya kashfa aliyowah kunena kipnd anaondoka udsm na kuingia kwny siasa.,tusaidie kwa hilo.Ndo maana utakuta thread nyng watu wanaomba cv ya kiongoz flani kwakuwa hatufaham pa kuzipata.
Tusaidie kwa hilo,nasi tujue nini cha kuamini kuliko kuwa bendera fuata upepo.
Nawasilisha.
 
Pole sana ndugu yangu unafanya speculation sehemu ambayo haihitajiki kabisa. Acha kumshabikia mtu, kuwa objective, umsifie na kumpongeza mtu kwa mazuri anayoyafanya na umkosoe kwa mabaya yake. Tuache ushabiki, tusishabikie tu na wala tusijaribu kuweka kambi kila jambo linalogusa maslahi ya nchi yanapoongelewa. Hebu jiulize swali wewe mwenyewe je unadhani kuna mwanasiasa yeyote mwenye dhamira ya kweli ya lutukomboa wanyonge wa nchi hii tukapata neema? Unamwona yeyote bila kujali anatoka chama gani? Tuache itikadi na ushabiki, kama yupo tummunge mkono na kumpa ajenda zetu, kama hayupo tujiulize tutampata wapi? je nani atamtengeneza? Je tutasubiri azaliwe? Shida hzina vyama, mgomo wa madaktari hauchagui unashabikia upande upi, elimu mbovu inatuathiri sote, kosefu wa madawa mahospitali ni wetu wote, wao wakilishana sumu wanaenda appolo, sisi tukila sumu bahati mbaya tena kwenye uyoga au kasa tunakufa. Tunazikana bila kuulizana wewe chama gani, tunakaa matanga pamoja huku tukitafuta maji na kuni za kupikia wafiwa. Wakija na Ma land Cruiser yao kutupa pole na kilo mbili za sukari wanakaa dakiak tano haooo wanaondoka, wanamikutano muhimu sisi twabaki kushabikia,wamelishana sumu! upuuuzi mtupu.

Duuh mwanzoni nilikuwa napata taabu sana kukusoma... Kweli subira yavuta heri maana niliposoma post yako ya awali na iliyofuatia niliona ni mtu uliyeboreka na kuamua kuandika chochote. Kidogo kidogo nikaanza kuvutiwa na kukuelewa uzuri. Una hoja za nzito sana ingawa wengi wanatatizwa na hiyo kauli ya kutomuonea huruma huyu mgonjwa regardless mchango wake katika mfumo mzima na hali ya wananchi kwa ujumla.

Endelea kukunjuka wengi watakuelewa hata wale wabishi ambao hawako tayari kubadilika hata baada ya kuwekewa ukweli wote. Nimekufahamu, na hii ndio JF kila mtu anakuja na lake kwa upeo wake, tatizo ni jinsi ya kutetea hoja yako ukaeleweka. Laiti huyu jamaa angekuwa mbabaishaji basi angekuwa ameshaingia mitini saa nyingi maana alishaanza kushambuliwa.
 
Mwakyembe aliongoza jopo la wasomi waka mu interview rais Mkapa miaka ile lakini hakuukiza maswali yeyote ya maana alibaki anacheka cheka tuu! Mi namuona hana msimamo na ni mzandiki mkubwa bora aseme ukweli auammbie umma anaumwa nini kama anaona ugonjwa wake unatuhusu sisi wananchi...
 
Hamna la zaid..kwa sasa dr ni mgonjwa tumwombee apone....unaijua golden rule? Angekuwa anakuhusu ungeyasema hayo
 
Wewe std seven? Najua ni ticha kihiyo wa udsm haueleweki kabisa. Ebu rudia uone umeaddress nini kwenye post yako. Sisi regardless what as long as Dr. bado anaumwa priority ni kumuombea uzima mambo mengine na kama kuna jambo subiri apone um-face.
huyu alikuwa discontinued ndo maana ana hasira na Mwakyembe,mbona hatuambii hata moja la Lowassa kuhusika?hata yeye kama kibaraka bosi wake hatambakiza asije banwa kidogo akasema ukweli
 
Kama mwanadamu DrHM Hajakamilika! Jee madhaifu yake yanastahili adhabu ya mateso na machungu makuu ya aina hiyo?
Akili iliopanga uovu huo! Miguu iliyo kimbilia uovu huo! Na mikono iliyo tekeleza uovu huo! Mungu ulie mkuu waaibishe na uwafishe kifo cha aibu! watangulie kuzimu na Dr ashuhudie mazishi yao!
MMungu waweza3!
A M I N A!
 
Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.

Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda
Sikuona mantiki ya walaka huu japo umekuwa mrefu kuzidi report ya kuuzwa kwa migodi ya Buzwagi!
Kwanza nakuuliza wewe mleta mada umesema kuna maneno aliyoyasema lakini cha kusikitisha haujasema hata neno moja! moja kwa moja nakuona ni mbea mzandiki kwa kuleta thread yenye maslahi binafsi!! kama unauadui nae aihitajiki kueneza unafiki kwa jamii!!Kuhusu hawa waliokufa sishangai kila serikali inamifumo yake yakuendesha nchi hakuna serikali isiyopambana na wasaliti wake!Ndiyo maana ya kulinda katiba na siri za serikali ukikiuka na kuivua nguo serikali lazima uwajibike!Kuna njia nyingi za kuwajibika Ila ukiona baadhi yavitu vinafanywa nawatu wachache wakitaka kujihodhi mali ya umma lazima useme!! na ukisema siyo uhukumiwe kifo kwa sababu ya kulinda mali ya umma!.Hata Dr Mwakyembe aliamua kutanguliza maslahi ya nchi siyo ya yeye binafsi kama ilitokea watu wakaguswa kwa njia moja au nyingine hawana mamlaka ya kuhukumu mtu kwa kifo!!Nawewe umepotea kwakutoa tamshi lenye kuhukumu kwakusema hiyo ndo stahili ya Mwakyembe nasikitika kwako wewe kuwa kibaraka cha mfumo wa ufisadi!!Umesema povu hakuna kitu kilichona mashiko kwenye uzi wako!!!
 
sosoliso hembu rudia tena kuyasoma vizuri na taratibu maandishi ya Domokaya na utayaelewa vyema. Indirect inasaidia kufikirisha, usitake kutafuniwa kilakitu, ubongo wako utalemaa.
Mkuu Domokaya unahoja. Sifurahii bmwanadamu mwenzangu awaye yeyote kuumia namna ile, bali wengine walio kwenye mkondo huo wajifunze kutokana na makosa ya wenzaao, tusisubiri mpaka yatukute. Unafki haufai hata kidogo. Tuwe na nia ya dhati inayotoka mioyoni mwetu ya kuliinua taifa letu.
Tusiwatendee wengine vibaya, na tuenende kwa haki.
Usikubali kujiunga na genge lolote lenye nia mbaya kwa awaye yeyote. Tusimamie haki maana kwa haki kamwe hatutoumbuka.
Kumbuka ukijiunga na genge lauhalifu ukawa mmoja wao, baadae ukijifanya unalipinga kwakuwa umepunjwa mahali ujue hauto poana na nivigumu kulishinda.
Nibora kuyapiga vita hayo magenge tangu awali tukiwa wasafi.
 
Kama huwezi kuyaanika hapa bora ungeacha, wote tuache kufanya mambo ya muhimu kwa maendeleo yetu tukaanze kufanya utafiti juu ya nini Mwakyembe alifanya miaka kadhaa iliyopita?. Then, tutapata degree??
 
Back
Top Bottom