Dr Mwakyembe hapaswi kuhurumiwa, amevuna alichokipanda

Wewe ni tatizo na huhitajiki uwanjani na kauzi kako ka unakumbuka,unakumbuka,unakumbuka,sema watu wakuelewe,ama wewe ni tunda wa zile shule zetu zilizoanzishwa na kaka ENL kwa nguvu nyingi sana....aibu kwelkweli..Umechosha mkuu?
Naheshimu fikra zako lakini nakushauri siku nyingine angalau uujue ukweli kidogo halafu ujenge joha juu yake hata kama itakuwa ya uongo. Unaposema mtu wa makamu wa miaka arobaini hivi na Ushee amesomea shule za kata, ooh unapoteza uhalali wako wa kuaminika. Kama kukumbuka kwako ni kosa na kwa wengine pia hakuna shida kwani hilo ni tatizo la kitaifa kila mtu hataki kukumbuka na unayekumbuka unaonekana mzushi halafu eti watu tunataka mabadiliko bila hata kujijua sisi ni akina nani, tumetoka wapi, sishangai kuona hatujui tunapotaka kwenda. Habari za 2000 na 2002 watu wamezisahau, hawazijui eti wanajiita great thinkers, Lol!
 
Unasumbuliwa na Chuki binafsi, unabwabwaja tu maneno bila vivid examples.. Wewe ukilishwa sumu utafurahi.
 
Narudi nyuma miaka kadhaa wakati DR Mwakyembe alipoona siasa inalipa kuliko taaluma alipoamua kukimbia chaki Chuo Kikuu cha Dar es laam na kwenda kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. Mwakyembe kwa kutaka kupendwa na chama chake aliyatamka maneno ambayo yalikuwa dhihaka kwa wananchi wa nchi hii, maneno ambayo, yaliidhalilisha taaluma yake, maneno yaliyodhalilisha wasomi na maneno yaliyodhalilisha jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Aliyasema hayo kwani alijua chama chake kinapenda kuyasikia, na alisema akijua akiyasema hayo atapata nafasi moja ya kuwa mbunge kilaini.

Nakumbuka yote, nakumbuka kila kitu. Nakumbuka hasira za wenye tafakuri nziti zilivyomrukia na kumsuta, alionekana dhahiri anajitongozesha kwa gharama ya wananchi kuumia ili yeye aneemeke. Nakumbuka jinsi alivyomuudhi Jenerali Ulimwengu hata wakaanza kujibizana kwa kalamu na maneno ya vinywani.

Nakumbuka, sijasahau ni Dr Mwakyembe huyu huyu chaguo kipenzi cha CCM. Alishirikiana nao kuwagandamiza wananchi, akataka kwenda mbali kushiriki zaidi kuwagandamiza ili aendelee kufaidi na kuneemeka yeye na familia yake. Alipowekewa kigingi akijifanya yeye na wanafiki wenzake eti wanatetea wananchi. Kumbe wapi wamekutana na kichaka cha simba sasa wanataka sapoti ya kukishinda, wote wao na kile kichaka lengo lao ni kutufanya kitoweo.

Dr Mwekyembe ni mmoja wa watengenezaji mifumo hiyo michafu na ya kinyama ambayo leo imemrudi yeye mwenyewe. Wanajua na wanajuana namna ya kuzitengeneza hizo sumu na kuwalisha sijui kuwagusisha watu. Wameshawau wengine wengi tu leo imefika zamu yao wanapiga kelele.

Wenye kumbukumbu nzuri watakubaliana nami kuwa Mwenyekiti wa CCM alilizungumzi hili katika sherehe za kuzaliwa chama mwaka juzi. Alisema wazi watu ndani ya chama wamehasimiana kiasi cha kushindwa kuachiana glasi mezani.

Hivyo ndivyo siasa za CCM zilivyo na kila mwenye upeo kidogo tu anafahamu hilo achilia mbali DR wa sheria. Ukiwa nao fanya kama wanavyofanya wao na malengo ya chama chao. Uongo, uzandiki, wizi, uzabizabina, kujipendekeza, ulafi, majivuno, dharau na uchafu mwingine mwingi waufanyao. Ukikiuka haya umekiuka miiko, umekuwa msaliti lazima uadhibiwe.

Kuna waliosema chama kimekosa dira na mwelekeo wakakiona cha moto. Kuna alioaga kwenda London eti akirudi awaambie watanzania ukweli kuhusu nchi yao ilivyotafunwa na kubaki makapi, lakini thubutu yake hakurudi. Mifano ni mingi hata ile ya waliotaka kusema ukweli kuhusu jambo fulani wote wamepotea, kuanzia Stan Katabalo mpaka ile tume ya unga wa ngano wa sumu, tume nzima ilipotea. Walipita kulalamika kuwa wanataka kuuliwa hakuna aliyewasikiliza, wakaishia. Yote haya Mwakyemba anayafahamu na bado akaenda kujiunga na kusaidia kutekeleza haya, sasa leo zamu yake anang'aka. Anang'aka nini mwache aone shida wanazopata watanzania wengine ambayo kwa sababu ya yeye na wenzake kujenga mfumo wa kidhalimu kuna watanzania wanakufa kwa kukosa barabara za kuwafikisha mahosipitalini, aone jinsi watanzania wanavyojilundika hospitalini wakisubiri vifo vyao huku wakipozwa na panadol, bora yeye amepelekwa Appolo.

Hili liwe fundisho kwa watu wote wenye kutumia migongo yetu wanyonge kujipatia nafasi ya kujilimbikizia mali na madaraka. Kuna siku madaraka na mali havitatosha sasa wataanza kunyang'anyana walivyopeana kwani kila mtu atataka kumzidi mwenzie. Mbinu zingine zinaposhindikana na msaliti anapoelekea kutoa siri ndipo watarudi kwenye ile mbinu yao ya "Costra Nostra" maiti haisemi.

Dr Mwakyembe na wenzake wasilie kama zamu yao imefika basi wajue kuwa hata wenzao waliowatanguliza walipitia machungu hayo hayo, zaidi wajue kuwa maisha ya watanzania waliootaabika na kufa kwa ajili ya udhalimu wao ni dhaidi ya wao kunyweshwa sumu. Wanavuna walichopanda

Domokaya; mimi nakubaliana na wewe katika mambo fulani ambayo umeyasema
1. Ni kweli hakuna mtu mwenye akili timamu, mwenye kujua anachofanya, mwenye nia nzuri na nchi yetu ambaye yuko CCM bila kujali maslahi binafsi.
2. Kosa kubwa ambalo Dr. alilifanya ni kuingia kwenye Chama Cha Majambazi na kuona amefika
3. Ni kweli CCM hiko kulinda watu wachache wenye kuila nchi yetu na wengine wanashangilia tu baada ya kupewa kofia na kanga.
4. HUWEZI KUWA NA MAPENZI MEMA NA TANZANIA, UKAWA NDANI YA CCM.
 
nadhani ndio maana wakiambiwa waende upinzani wanakaa kimya.kweli ccm=chama cha maslahi.

Mkuu wangu meningitis unajua wakati huo Mwl. Nyerere aliposema upinzani wa kweli utatokea pale CCM itakapo gawanyika alikua anadhani kkt CCM kulikua kuna wanachama wasafi ambao wangekataa kuishi na wanachama wachafu,kwa hiyo aidha wasafi wangeamua kujitoa na kuanzisha chama chao ama wangewafukuza wachafu. Hii haikutokea kwasababu karibia wote siyo wasafi na CCM ilikua ni njia ya mkato kupata madaraka na mali. Mleta hoja amemzungumzia Dr. Mwakyembe,lakini kwangu mimi Mwakyembe anawakilisha aina ya viongozi na wanachama ndani ya CCM wanaodanganya watanzania kupigana vita bandia ya ufisadi wakati na wao ni mafisadi wasaka tonge zaidi!
 
Hivi mvi nae huwa naingia humu JF na kutuma posts?
Sababu katika malalamiko yake huwa anapenda sana ku refer taaluma ya Dr.. Mwakyembe. Kipindi cha kuachia madaraka, aliwahi semakuwa Dr. ni mwalimu wa sheria pale mlimani na anafahamu na kufundisha kuhusu natural justice na hapa napo naona ma-mvi umerudia tena kuwa ametukana taaluma yake.
Vipi inakuwasha sana elimu yake nini? Mbona afya ya mvi inayozorota kwa kasi sasa hivi huiongelei?
Pole sana ndugu yangu unafanya speculation sehemu ambayo haihitajiki kabisa. Acha kumshabikia mtu, kuwa objective, umsifie na kumpongeza mtu kwa mazuri anayoyafanya na umkosoe kwa mabaya yake. Tuache ushabiki, tusishabikie tu na wala tusijaribu kuweka kambi kila jambo linalogusa maslahi ya nchi yanapoongelewa. Hebu jiulize swali wewe mwenyewe je unadhani kuna mwanasiasa yeyote mwenye dhamira ya kweli ya lutukomboa wanyonge wa nchi hii tukapata neema? Unamwona yeyote bila kujali anatoka chama gani? Tuache itikadi na ushabiki, kama yupo tummunge mkono na kumpa ajenda zetu, kama hayupo tujiulize tutampata wapi? je nani atamtengeneza? Je tutasubiri azaliwe? Shida hzina vyama, mgomo wa madaktari hauchagui unashabikia upande upi, elimu mbovu inatuathiri sote, kosefu wa madawa mahospitali ni wetu wote, wao wakilishana sumu wanaenda appolo, sisi tukila sumu bahati mbaya tena kwenye uyoga au kasa tunakufa. Tunazikana bila kuulizana wewe chama gani, tunakaa matanga pamoja huku tukitafuta maji na kuni za kupikia wafiwa. Wakija na Ma land Cruiser yao kutupa pole na kilo mbili za sukari wanakaa dakiak tano haooo wanaondoka, wanamikutano muhimu sisi twabaki kushabikia,wamelishana sumu! upuuuzi mtupu.
 
watu bwana.. hujaona kabisa dr mwankyembe alichoifanyia tz.. tena naamini angeendelea kuwa mwalimu asinge fanya chochote kikubwa zaido ua kuifanyi akazi tu CCM kama huyo ndugu yenu Mkandara/Mukandara(rekebisha mwnyw).. yani we unawafagilia sana hao waalimu wenu wanaowafelisha na kuwalala wanafunzi ili wafaulu????

tafuta huyo mwanasiasa unaemfikiria ambae angesoma ile report kama mwankyembe... MNATAKA MFANYIWE NINI???????

You have hit the snake right at the head.
 
Mkuu, wazalendo wa nchi hii tunawajua wazalendo halisi wanaiisaidia nchi.
Jitu kama domokaya, ni aina ya watu waliozoea kutandikiwa vitanda na wanaume wenzao-mahouse boy!!
Hawaelewi hata thamani ya uhuru wao na kwamba kuna watu walimwaga damu kuhakikisha hicho-kutandikiwa vitanda.
 
Baada ya kusoma ripoti what next?
Baada ya kusoma ripoti hali ya umeme imetengamaa, tunatumia umeme wa dharura. Jamani tufikiri japo kidogo kisha tuamue tunafanya nini? Dharura miaka minne?!!!!!
 
Wewe std seven? Najua ni ticha kihiyo wa udsm haueleweki kabisa. Ebu rudia uone umeaddress nini kwenye post yako. Sisi regardless what as long as Dr. bado anaumwa priority ni kumuombea uzima mambo mengine na kama kuna jambo subiri apone um-face.
Kwani siku hizi std seven wanafundisha UDSM? acha kutokwa mapovu bila sababu, jibu hoja iliyobandikwa. Usjifanye unahuruma sana!
 
Domokaya ndewedi habari nja ndiima. Utidhe. Kumbe hata Wapare ni wabishi kiasi hicho? Kuwa na roho ya kibinadamu japo thread moja. Mwakyembe hajakukosea personally usishangilie kuumwa kwake namna hiyo. Nahavome!!!
 
Mkuu, wazalendo wa nchi hii tunawajua wazalendo halisi wanaiisaidia nchi.
Jitu kama domokaya, ni aina ya watu waliozoea kutandikiwa vitanda na wanaume wenzao-mahouse boy!!
Hawaelewi hata thamani ya uhuru wao na kwamba kuna watu walimwaga damu kuhakikisha hicho-kutandikiwa vitanda.
Angalau wewe mwenzangu unawajua wazalendo halisi wa nchi hii. Mimi sijawajua bado na ndio maana nina mashaka na kila anayejifanya mzalendo huku kipato chake kikiwa mara laki moja zaidi ya kipato cha mwananchi wa kawaida. Akimwa anaenda Appolo, India wakati kuna hospitali nyingi nchini na India ni nchi kama ilivyo nchi nyingine, halafu huyo ni mwakilishi wa wananchi anatakiwa azijue shida zao na kuzipigania, Mwaisela hapajui! Sijui anamwakilisha nani. Barabara mbovu amezinunulia Landcruiser, kwake Tuandamane huyo ndiye bonge la mzalendo
 
kuhusu rafu za chama umesema vizuri kabisa, ila kuhusu swala la kufurahia hali ya ugonjwa wa Mwakyembe just kwa sababu hizi ulizozitoa kwa inductive meaning umedhihirisha bias inakutafuna hususani katika maswala yako binafsi unayoyapigania kwa nguvu yote hii.
Prejudice is lesser evil than bias.
 
Domokaya ndewedi habari nja ndiima. Utidhe. Kumbe hata Wapare ni wabishi kiasi hicho? Kuwa na roho ya kibinadamu japo thread moja. Mwakyembe hajakukosea personally usishangilie kuumwa kwake namna hiyo. Nahavome!!!

Namuheshimu Mwakyembe kama mtu, namhurumia kama mwananchi wa Tanzania. Sipendi aina ya uongozi wake, sipendi jinsi anavyofanya siasa, sipendi unafiki wake kisiasa na sipendi anyojisahau kuwa yeye ni baba, kaka, shemeji, ndugu, jirani, mwalimu na mtoto.

Hii ndio imekuwa tabia ya wanasiasam wengi nchi hii, wamekuwa miungu watu, kwao wananchi si mali kitu mpaka wanapofikwa na majanga wanajua kuwa kuna kundi lenye nguvu kuliko kitu chochote nalo ni wananchi wanyonge, wanakimbilia kwetu kupata huruma yetu, wanataka tuwatetee wakati kipindi fulani walituacha, kutudharau na kutusahau ndi maana nasema tusikubali watutumie!
 
Mkuu, hukuhitaji kuandika bandiko refu kiasi hicho kutoa hoja yako. Masuala ya "makamanda dhidi ya ufisadi" ndani ya CCM yanaeleweka. Lakini kwanza kabisa, hivi sasa Mh. Mwakyembe anahitaji maombi yetu na faraja apone. Mateso ya binadamu na kifo si vitu vya kufurahia. Aidha, jaribu kumuona Mh. kama mmoja wa wahanga wengi tu wa mfumo kiritimba uliojengwa na CCM (uliodhibiti mianya yote ya mafanikio hadi ulambe viatu vya "wenyewe"). Tungetegemea mtu kama Mwakyembe awe juu ya mtazamo wa aina hiyo; lakini naye, kama wengine, kakubali yaishe na kujipeleka atumike vibaya na watemi wenye chama chao akijiaminisha kwamba ndio njia muhimu ya kutoka kimaisha.

Mimi kinachonipa taabu sana ni zile tuhuma kwamba anao undani wa kadhia nzima ya Richmond lakini alikubali kutoa taarifa isiyo kamili Bungeni (tena kwa hamasa nzito) yenye kuuangamiza upande mmoja (wa Lowasa) ili kuulinda upande mwingine (unaodaiwa kuhusika hasa na umiliki wa dili zima). Kama kweli alifanya hivyo huku akijua basi najiuliza dhamiri yake ikoje? Na sitashangaa kama ule upande anaoulinda nao ukahusika na maangamizi yake. Waingereza wanasema: there is no honour among thieves. Hivyo, tunapomuombea ndugu yetu apone na masahibu yaliyompata mwilini, tunaomba pia na nafsi yake itakasike katika mambo haya.
 
Domokaya; mimi nakubaliana na wewe katika mambo fulani ambayo umeyasema
1. Ni kweli hakuna mtu mwenye akili timamu, mwenye kujua anachofanya, mwenye nia nzuri na nchi yetu ambaye yuko CCM bila kujali maslahi binafsi.
2. Kosa kubwa ambalo Dr. alilifanya ni kuingia kwenye Chama Cha Majambazi na kuona amefika
3. Ni kweli CCM hiko kulinda watu wachache wenye kuila nchi yetu na wengine wanashangilia tu baada ya kupewa kofia na kanga.
4. HUWEZI KUWA NA MAPENZI MEMA NA TANZANIA, UKAWA NDANI YA CCM.
Na hilo ndio kosa kubwa lililofanywa na wasomi kutoka vyuo vikuu hasa UDSM waliingia CCM na kugombea ubunge kama sehemu ya kujineemesha na sio vinginevyo. Uliza michango ya akina Maghembe, Kapuya, Mwakyembe, Bilal,...............ni ipi katika kuondosha umaskini wa wawatanzania ?
 
Mkuu, wazalendo wa nchi hii tunawajua wazalendo halisi wanaiisaidia nchi.
Jitu kama domokaya, ni aina ya watu waliozoea kutandikiwa vitanda na wanaume wenzao-mahouse boy!!
Hawaelewi hata thamani ya uhuru wao na kwamba kuna watu walimwaga damu kuhakikisha hicho-kutandikiwa vitanda.
Wacha matusi na ushabiki usio na maana, Mwakyembe alimwaga damu lini kupigania haki za wanyonge?
 
kuhusu rafu za chama umesema vizuri kabisa, ila kuhusu swala la kufurahia hali ya ugonjwa wa Mwakyembe just kwa sababu hizi ulizozitoa kwa inductive meaning umedhihirisha bias inakutafuna hususani katika maswala yako binafsi unayoyapigania kwa nguvu yote hii.
Prejudice is lesser evil than bias.
Inawezekana niko biased sijui prejudiced. Mara nyingi nimekuwa nikisikia watu wakisema chama si kibaya bali watu ndio wenye matendo mabaya, Nisemehe tu ndugu yangu mimi nimeshindwa kabisa kutofautisha watu na chama. Sifurahii ugonjwa nasisitiza kusema wacha mfumo waliouweka ufanye kazi waliyoitaka hata kama huo mfumo utawaathiri waliouweka. Ingawa haikuwa lengo lao uwaaathiri wenyewe angalau basi wajue ubaya wa mfumo wao kwa wale waliowawekea
 
prof shivji ni mpiganaji kuliko mwakyembe.....leo yamempata anakumbuka kugonga hodi kila mlango huku akilia kwa uchungu....kwa nini alificha sehemu ya riport ya richmond?!!!...wacha mfumo waliouweka uwatafune wenyewe!!!!
 
Back
Top Bottom