Dr. Mwakyembe, David Mattaka hakuwa Mstaafu alipoteuliwa kuwa CEO wa ATCL? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mwakyembe, David Mattaka hakuwa Mstaafu alipoteuliwa kuwa CEO wa ATCL?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanga, Jun 8, 2012.

 1. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Nimepata wasiwasi na utendaji wa viogozi wetu jinsi wanatoa maamuzi katika masuala mbalimbali.Sakata la kufukuzwa kazi kwa CEO wa ATCL hivi karibuni Eng,Chizi kwa sababu ya ukiukaji wa taratibu za ajira yake kunaacha maswali mengi kuliko majibu yanayotolewa na ofisi ya Mwakyembe.
  Sababu moja kubwa ambayo Mwakyembe ameitoa akiongea na watumishi wa ATCL ni kwamba Eng. Chizi alikuwa amekwisha staafu kazi hivyo hakusathili kuajiriwa na ATCL.Sababu hii naona ni nyepesi sana kuzingatia mifano mbalimbali ambayo ipo kwa jinsi wastaafu wengi wameendelea kuajiriwa kwa mikataba ya ajira kwa kipindi cha miaka miwili au mitatu.Mfano mmojawapo ni uteuzi wa DAVID MATTAKA ambaye aliteuliwa kuwa CEO wa ATCL wakati huo alikwisha staafu kama CEO wa PPF.David Mattaka ndiye alimwachia ofisi Chizi kama mrithi wa ofisi yake kama CEO je swali kwa Mwakyembe Uteuzi wa Mattaka na Chizi una tofauti gani?.Kinachoonekana hapa ni mambo binafsi sana ndiyo yanaleta kelele zote hizi.Na kama kuna sababu nyingine ni ufisadi katika ATCL wakati wa CEO Chizi vyombo vya dola kama TAKUKURU na CAG wanatakiwa waagizwe kufanya ukaguzi maalum na siyo kuteua tume.
  Inaonekana Mwakyembe ni mtu asiye jifunza na anapenda umaarufu rahis kwa vitu vyenye kuhitaji uchambuzi wa kina.Na hapa Mwakyembe akionekana ameboronga Lowasa atachekelea vizuri akimaanisha na kuthibitisha Mwakyembe alitumika kwenye Kamati ya Richmond kumuonea na nia ilikuwa UWAZIRI MKUU WAKE.:majani7:
   
 2. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Aliyekamatwa na ngzoi ndie mwizi ... mengineo nni majunguu
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu inaonekana umeumia sana kuondolewa kwa Chici ATCL, pole. Unachokosea ni kukwepa ukweli unaposema sababu kuu ya kuondolewa Chizi ni kwamba alikuwa tayari mstaafu mpaka unatoa mfano wa David Mataka ambaye pia aliwahi kuongoza ATCL akiwa "mstaafu". David Mataka hakustaafu PPF bali alifukuzwa kazi ilikuwaje akapewa nafasi ya kuongoza ATCL mimi sijui. Watanzania tunalalamikia sana utendaji dhaifu wa viongozi wetu wengi wakiwemo mawaziri, inapotokea waziri anaamua kutenda kazi zake kikamilifu tunaanza kulalamika. Mkuu unasema suala la ustaafu ndiyo limemtoa kazini Chizi hii si kweli hata kidogo bali ni DEAL ndiyo zimesababisha Mwakyembe amtoe kazini na si vinginevyo.

  Wote tumemsikia vizuri Mwakyembe alivyoeleza kizungumkuti cha pesa ya malipo ya bima ya ndege ya ATCL iliyoanguka Kigoma. Mwakyembe alitaka pesa hiyo iwekezwe katika ununuzi wa ndege mbili mpya ili in the long run ATCL iachane na utaratibu wa kukodisha ndege ambao hauna manufaa makubwa kwa shirika. Chizi na wenzake wakacheza deal kuhujumu huo mpango wenye nia njema kwa mustakabari wa ATCL. Sasa hapo nani mwenye nia njema na ATCL, Chizi au Mwakyembe. Acheni viongozi wafanye kazi.
   
 4. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mwakidondo pamoja na ufafanuzi wako mzuri,Mimi sina maslahi na Chizi ya aina yoyote ile ila napigania Corporate good governance ,rejea barua ya Wizara ya kutengua uteuzi wa Eng.Chizi kuwa CEO wa ATCL,Sababu kubwa iliyotolewa ni utaratibu wa ajira yake haukufuata taratibu,haya mengineyo ya ufisadi wa Bima ya ndege ya Kigoma ni mengineyo na tayari ufafanuzi wake umeanza kutolewa na weledi wazuri tu.Katika Corporate good governance principles Mwakyembe hajafanya la maana hata kidogo na kama anauhakika kuwa kuna fraud yoyote ilikuwa jukumu la ofsi yake kuwasilisha maelezo yake kwenye vyombo vya mamlaka ambavyo ni POLISI,TAKUKURU na OCAG.Kuunda tume ya watu watatu siyo sahihi maana report yao siyo conclusive ikizingatia kuwa kuna elements za criminal offences ambazo kisheria zinashughulikiwa na vyombo nilivyotaja.TUSUBIRI REPORT HIYO KAMA .......................
   
 5. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  taarifa yeyote ikitolewa someni kwa makini....taarifa ya kusimamishwa kazi chizi iliwekwa hapa,ukisoma kwa makini, Dr Mwakyembe ametengia uteuzi wake, sababu uteuzi wake ulikuwa na makosa, lakini chini kuna maafisa kadha wa ATCL wanasimamishwa kazi, inaendelea kusema kuna kamati ya wataalamu wa fedha itaundwa kuchunguza....... sasa kwa mwelewa ni kwamaba pale ATCL kuna ufisadi umefanyika, huwezi fanya uchunguzi wa maana kana hawa watu wako ofisini, kwa hiyo lazima uwasimamishe, kisha ndio hatua stahiki zifanyike

   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Kuna kosa gani kusimamishwa ukisubiri uchunguzi ufanyike? Si ndio dhana ya uwajibikaji? Taifa gani hili tunalojenga ambalo linaenda kwa kujuana juana na kushabikia wizi wa mali ya umma? Kila siku hela zinafujwa na wahusika wakiguswa wanasema wameonewa.
   
 7. BABU CHONDO

  BABU CHONDO JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Chizi ni mkweo nini,Mbona umeumia sana.
  Sasa hivi hakuna kufanya kazi kwa uzofu,tunahitaji wataalam na wapo wengi humu mtaani wamesoma vizuri.sio kwa sababu alikuwa ATCL muda mrefu ndo aachwe.

  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
 9. Wilawela

  Wilawela Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hi Kanga!
  Nakushukuru kwa Mchango wako Jamvini
  Naomba kutofautiana na wewe kama ifuatavyo:
  1.Kipi ni Kikubwa Sheria au matendo ya Mtangulizi ? Kuna sheria ya kazi na mahusiano Kazini na Kuna Uteuzi wa Mataka kuwa CEO wa ATCL (chukulia alikuwa amestaafu)?Tunahitaji kuwa "Objective" hata kama watangulizi wetu wali "mess up" mahali fulani kwa mazoea tu. 2. Kama sikosei David Mataka alistaafishwa na Mkapa kwa manufaa ya Umma si kwa Umri hivyo hizi ni kesi mbili Tofauti! 3. Wewe kama Mtanzania Mpenda maendeleo, muuminii wa utawala bora (good Governance) unaona afadhali huyo angeachwa aendelee kuua ATCL,Kukodisha ndenge ovyo ovyo ,Kununua Unifomu kwa 49,0000 USD na Kuzisubiri china kwa siku 45 n.k? utawala bora niujuwavyo mimi una nguzo zake kama Uwazi,uwajibikaji nk vyote hivi vinafaminyika kwa maslahi ya wengi na si ya wachache kama Lowasa ulivyodokeza. yawezekana Mwakyembe pia kama binadamu kafanya pia kwa maslahi yake lakini maslahi yake na ya umma katika hili yame "
  intersect!" Ahsante "I stand to be corrected"
   
 10. D

  DURACEF JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  bora useme wewe,jana kuna karedio stesheni kamoja kanaitwa mawingu,walichonga sana kwenye kuperuzi magazeti,na hii ilitokana na mwenzao kula msele na moja ya ndege iliyotuingiza hasara,sijui wanajisikiaje,hata siku moja usishindane na msomi mzalendo utaumia........na bado
   
 11. a

  artist Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa ndo unaona dhahiri madhara na athari za kusoma katika lugha ya watu kisha kufanyakazi katika lugha yako ya nyumbani. Mkuu hiyo nadharia ya "good corporate governance." unaonekana umeikariri tu huielewi. Mwakyembe alikuwa wazi kwamba baada ya kuona ubabaishaji wa Chizi ndipo akaamua kufungua mafaili yake. Akabaini uteuzi wake haukufuata Sheria ya Utumishi wa umma (2002) na Kanuni zake za (2003). Mfano huwezi kumpa mtu wadhifa mkubwa kama huo bila vetting tena aliyetoka nje ya system 10 years ago. Pili sheria inasema nafasi hiyo ilipaswa itangazwe haikutangazwa na kumkaimisha mtu kutoka nje ya taasisi ni kosa. Unapofika kuona uteuzi wenyewe ni batili na kanuni zinampa waziri mamlaka ya kuteua na kubatilisha uteuzi hayo maneno yako matamu ya Kiingereza cha kubandikiwa na wazungu yanakosa maana.

  Tukija katika la pili sasa la tuhuma kwamba aliiba au la. hilo ni kazi ya timu iliyoundwa na vyombo vingine. Nasisitiza hujataka kujibidiisha kuelewa alichofanya waziri bali umekariri maneno ya kukaririshwa na wazungu tu.Pole sna
   
 12. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,313
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Kama hivyo ndivyo, kwani lazima Chizi ndie awe CEO wa ATCL? Ikiwa Mwakyembe anasema uteuzi wake haukufuata utaratibu, basi kama wewe hukubaliani na hili unapaswa kutueleza ni kwa vipi uteuzi wa Chizi ulifuata taratibu zote, sio kuja na kauli za kishabiki hapa.
   
 13. mito

  mito JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,607
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada jaribu kuwa uzalendo na mali za umma. Usishabikie kitu kilicho wazi kiasi hiki hata kama chizi ni ndg yako! Madudu yamefanyika ATCL, hivyo yeye kama CEO lazima apishe ili uchunguzi ufanyike, hauwezi kufanyika akiwepo. After all, who is chizi? Kwanza alishastaafu, hivyo mwache akae zake pembeni ale pension yake, apishe watanzania wengine nao wafanye kazi, kwani umeambiwa bila yeye hakuna ATCL? jaribu objective mzee, siyo kukurupuka tu kwa ajili ya kulinda uhusiano wako na chizi! Ina maana wewe binafsi unaridhishwa na utendaji wa hili shirika letu?
   
 14. M

  MTK JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280

  Huu wako ni mtazamo maslahi na Ni watanzania wachache sana watakuunga mkono katika swala hili kama unavyoona hapa kwenye jamvi!!; kwa bahati mbaya sana ulilolisikia kwa waziri ni swala la kustaafu kwa Chizi tu?! je mkataba wa kukodi ndege? na sare 15 za miilioni 80? kama EL atashangilia dr. Mwakyembe kuharibu OK but does it in any way cleanse him of corruption allegations over the richmonduli saga in which he wobbles till todate??!!
  Usijidhalilishe; try to engage your gray matter before going public with your myopic views!
   
 15. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mwacheni mwekyembe afanye kazi yake mnaniudhi sana wana jf mlikuwa na mada mmja hapa april yakuikashf atcl mkaponda sana sana uongozi huo rais wenu hakuweza ona kule mbali mmepata mtu wakung'oa mafisadi then mnamgeuka eti kakosea ,kweli nimemsikiliza mwakyembe jana ana reason yakuwafukuza -je nikampuni yako maafisa wawili wakuu wanasafiri kwenda china kukaa miezi miwili kusimamia sare za afisi wewe unaona kuna usawa hapa hilo ni dogo tu kati ya mambo aloyoeleza ,kumbuka hao watu wanalipwa per dm,msosi malazi,kila kitu mpaka kujisaidia wanalipiwa kumbuka mlipiga kelele atcl haina hta ndege mja.leo mnatetea nini nyie watu kakosea nini hapo mnataka afanyaje vile, wana jf hapa mliomba oh mwakyembe chunguza na atcl leo hii mnageuka .msiifanye jf kigenge cha kahawa bana hapa tupo gt
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Unajua kwa hali ilivyo Tz kwa sasa watu wamezoea madudu such that likifanyika jambo la kizalendo lazima wengi wamind bse wananufaika na the existing system.
  Kwa kifupi Chizi kapigwa chini porojo zenu humu haziwezi mrudisha kazini na ata yeye alipohojiwa alikuwa mnyenyekevu tuu bse he was born to be Chizi huo UCEO nii matokeo tuu in life.
  Sasa akingolewa ndo iwe nongwa.
  Nchi ya bora liende hii!
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba Chizi anatafutiwa ulaji wa uhakika, badala ya kuajiriwa atachukuliwa kama "consultant" kwa mkwanja zaidi. Jamani, mbona mnataka kumtilia kitumbuwa chake mchanga!
   
 18. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,046
  Likes Received: 7,257
  Trophy Points: 280
  Kanga,
  Hata kama TAKUKURU walitakiwa kuchunguza, bado hatua ya kwanza kabla ya uchunguzi wao ingekua ni Kumsimamisha Chizi.

  Tuhuma alizotaja Mwakyembe kwenye barua zaweza kua chache kulingana na akizotaja kwenye kikao na Staff, but suala bado linabaki pale pale kua nazo pia ni tuhuma zake vilevile.

  Suala la kwamba why hakuwashirikisha Takukuru truly huko ni kutokuelewa majukum ya Takukuru.

  Katika shirika ambalo uendeshaji wake ni wakibabaishaji wa wazi kama ATCL ilikua ni wajibu wa Takukuru wenyewe kufuatilia badala ya kusubiri kuitwa.

  Malalamiko ya aina yako yanapatikana hata Maliasili na Utalii kwa Kagasheki au TBL kwa Kigoda, but ukweli lazima tukubali kua Speed walizoanza nazo mawaziri hawa zinatia moyo kwani hii nchi imezidi kua shamba la bibi.
   
 19. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,046
  Likes Received: 7,257
  Trophy Points: 280
  Me likes this
  (Mods wapi LIKE kwenye mobile??)
   
 20. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Acha kuweka maslahi binafsi mbele bana Huyu Chizi ni fisadi kama mafisadi wengine hivyo kuondolewa ni sahii japo Wizara ilificha sababu sahihi za kufukuzwa kuwa ni wizi kama kautaratibu ka CCM kanavyotaka kale ka kulindana.Lakini huyu jamaa baada ya kukaliwa kooni amesema sababu ni kufisadi ATCL na mojawapo ni kushona uniform 15 nchini China za ATCL Cabin ... Uniforms Cost USD49,000 ambazo ni zaidi ya milion mia saba na thelasini(730mil) na kupeleka watu wawili eti kusimamia.Uniform zenyewe hata fundi wa mtaani anaweza kiushona tena kwa ubora mkubwa zaidi...hebu ziangalie hapa View attachment 55799
   
Loading...