Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Kitila,

..hata mimi Dr.Mwakyembe aliniboa sana alivyodai kuna ktk ile Ripoti yake kuna mambo ameyaficha ili serikali isiaibike.

..mimi naamini kuisetiri serikali hii iliyopo hakuwezi kuwa na manufaa kwetu sisi wananchi.

..sasa kama huu ugomvi wa Rostam na Dr.Mwakyembe, unaweza kumlipua Dr.Mwakyembe mpaka kufikia kuropokwa yale aliyoyaficha kwenye ripoti yake basi wacha uendelee.

..mbele ya safari tutaweza ku-deal na Dr.Mwakyembe, lakini kwasasa inaonekana he is the only CCM MP with the courage[to some naivete] to take on Rostam Aziz.

NB:

..Dr.Mwakyembe asisikilize kabisa watu kama Mzee Cygwiyemwishi Malecela ambaye amekuwa kama punching bag huko CCM.

Granted Mwakyembe amepoteza credibility aliyokuwa nayo mwanzo, na hili tumelisema sana kwenye thread ya press conference yake.

Lakini hili haliondoi wingu kubwa la ufisadi linalomkabili Rostam, kwa hiyo mlime Mwakyembe unavyotaka, in the final analysis unakuta kuna ma issue makubwa zaidi yanamkabili Rostam.

Na kama unafanya upembuzi yakinifu kwa kutumia uchumi wa cost benefit/ quantitative analysis, kama unaweka dollar bill kwenye decision making process yako, kama una prioritize issues kutokana na gravity, basi Rostam ni jua wakati Mwakyembe hajafika hata size ya Jupiter.

Not that we are excusing Mwakyembe, but lets do first thing first.

Unaweza hata kusema acha tumtumie Mwakyembe kum dismantle Rostam (au at least to take a good shot at him) na tukimalizana na Rostam tunaweza kumuangalia Mwakyembe naye vizuri.
 
Nsesi na Engineer.

Habari zenu zinapishana. Au wote mko sawa ila kila mtu aliona kipande au mmoja wenu anadanganya. Na au wote mwadanganya. Time will tell who!!!

Sikonge,

Vipofu wawili na tembo mkubwa! Mimi nimeulizia na ninajua ukweli kamili. Kuna mmoja kati ya hao wakuu wawili amejaribu kuigeuza chumvi iwe sukari. Tuachia hapo tu na tujadili yenye tija.
 
Bubu Ataka Kusema,

Wizi wowote ni mbaya, juhudi lazima zifanywe kukabiliana na madhambi yote Tanzania. Kuanzia kwa wanasiasa mpaka sisi wenyewe maofisini ambao tunanyanyasa Watanzania kila siku kwasababu mbalimbali.

It's simplistic kuamini matatizo yetu yote ni Rostam. Sawa tuendelee kumwandama Rostam na mafisadi wengine wote na wakati huo huo kuendelea kuboresha capacity kwenye sehemu mbalimbali hasa kwenye halmashauri ambako pesa nyingi sana zinatumiwa vibaya. Wakati mwingine sio ufisadi au wizi, ni uwezo mdogo wa kuamua lipi linafaa na lipi halifai. Wabunge ni wajumbe wa vikao hivi vya halmashauri, mimi ningependa kuwaona ndio wanasaidia kuongeza uwezo kwenye hizo halmashauri. Bahati mbaya wengi wao huwa hawahudhurii hivyo vikao hata kwa muda ule ambao hawawi bungeni.

Tujitahidi kupambana na matatizo ya Tanzania kwa pamoja (holistic approach).

Hakuna simplistic yeyote. Pamoja na kuwa tuna matatizo chungu nzima ambayo nami nayafahamu kwa kina sikusema popote pale kwamba matatizo yetu yote yanatokana na fisadi Rostam, kama una ushahidi wa kuthibitisha vinginevyo uweke hapa ushahidi huo. Pia kutaka kuonyesha kwamba matatizo yaliyasababishwa na ufisadi wa Rostam ni madogo ni kutaka kuwadangaya Watanzania . Shilingi bilioni 240 ($240 million approximately) ambazo fisadi Rostam ameifisadi Tanzania ni pesa nyingi sana kwa kusaidia matatizo yetu mbali mbali. Hizi pesa kama zingeelekezwa katika kununua vitanda vya mahospitali yetu na pia kununua madawati katika shule zetu au kuhakikisha upatikanaji wa maji katika baadhi ya miji yetu basi tungeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa matatizo ya hayo. Hivyo kutaka kuplay down ufisadi uliofanywa na fisadi Rostam si sawa hata kidogo.
 
Imesomwa na Gabriel Mwakalinga, Katibu wa Kamati ya Maadalizi ya Maandamano ya Amani ya Wapigakura wa Kyela, tarehe 29 Machi, 2009.

Huyu Gabriel Mwakalinga si ndiye alimwibia Kajumulo pesa baada ya kukutana naye TZ? Naona kama jina ni lenyewe. Kama sio mwenyewe samahani.
 
Recta na Susuviri,

Wakuu naona kuna hoja nyingi sana zimeisha pita na sasa hivi mko ukurasa mwingine kabisa.. Hata hivyo nitawarudisha nyuma kujibu hoja zenu kwani yanibidi kuweka record sawa...
Yote mliyaandika ni ya kweli kabisa lakini yakiwa ndani ya kabati.. Mnashindwa kutazama nje ya kabati hilo kuwa hawa watu, Lowassa, Rostam na wengine wote mnaotaka wafikishwe mahakamani ni RAIA tu hawana madaraka yoyote ndani ya chama (sectretariat) wala serikalini.. Hakuna implication yoyote ya kisiasa..
Swala kubwa tunalozungumzia ni Richmond ambalo nadhani ndio somo la mada hii kutokana na huyu Mwakyembe..
Ikumbukwe tu kwamba ni Dr. Slaa aliyefunua kimba hili bungeni, wakataka kulizima.. Lowasssa akiwa Waziri mkuu worked tireless kuhakikisha hakuna uchunguzi..sijui kama bado mnakubuka maanake mimi nakumnbuka hapa T-dot Lowasssa aliingia mitini mkutano wa Watanzania..kama sikosei ilikuwa Nov 2006..
Taarifa zote alizosema Dr. Slaa zilikuja bainika na kamati ya Mwakyembe, hapakuwa na jipya zaidi ya kupewa majina ya wahusika na mfululizo wa taratibu zilizotumika..
Na ni baada ya ukweli huo ndipo Lawassa alipojiuzuru, na ajabu sana mnaposema kajiuzuru tuu hivi hivi bila kumfikia mkulu kupata uhakika.. Watu wetu wa ndani walituambia Lowassa alikwenda kumwona Kikwete hata kabla report hiyo haijamfikia yeye. Lowassa alikwenda tena kumwona Kikwete baada ya JK kumwambia Mwakyembe aiwakilishe Bungeni kama alivyoikusanya..Kikwete alimtosa Lowassa!.
Wakuu, Kikwete sio tu alimtosa waziri mkuu na kuweka record, Kikwete kawatosa marafiki zake ambao walikuwa team moja kabla ya Uchaguzi na kawaacha nje hadi leo hii tunavyozungumza.. hata mwalimu hakuwahi kufanya hivyo..
Nasikitika kusema tena kwamba Kikwete pia alimtosa Ditto mshikaji wake ambaye alijaribu kupata msamaha wa JK, na kimtaani naweza kusema Ditto hakufa kifo cha kawaida tu inawezekana kabisa ali commit suicide baada ya kuona hana pa kutokea..
Hizi habari za kusema hafai kwa sababu ambazo hata roibo yake Mwinyi wala Mkapa hakufanya wakati mafisadi walikuwepo tena kwa nguvu ya ajabu, nashindwa hata kufikiri. yaani kweli kuna watu wanasema Mkapa angefanya hivi ama vile wakati wanajua kabisa Yona na Mramba, Balali, Megji, Karamagi, Rostam, Lowassa na mwengine wote hawa, Ufisadi wao haukuanza wakati wa JK isipokuwa toka kwa hao mnaojaribu kuwasifia viongozi upupu kama hawa..Damn!..

Jamani huyu ndiye Kikwete ninayemsikia mimi na hizi ni facts ambazo hazina Ubishi kabisa na kwetu waswahili naweza kusema jamaa ana roho mbaya...Na hakuishia hapo tu, akifahamu kwamba Lowassa na team yake bado wanaweza kununua wabunge mwaka 2010, Kikwete amepitisha sheria ya mgombea wa CCM 2010 atakuchaguliwa na wanachama wote wa jimbo husika na sio kamati ndogo ya watu 200 ambayo wengi wao wanaweza kununuliwa.. sasa kama Lowassa na Rostam wanaweza kutoa takrima kwa wananchama wote wa CCM na wafanye hivyo..Yote haya anacheza within his boundaries..na mtu asiwadanganye hata kidogo kuwa Sitta, Mwakyembe na Kilango wamesimama kwa miguu yao.. magongo kawapa Kikwete na hawa ni watu wake kwa hiyo kila analosema Sitta, Mwakyembe au mama Kilango ni toka team ya Kikwete..na hivi sasa naona Malecela ka join the wagon.

Hata hivyo nachelea chachu ya mjadala huu kwa kusema issue hapa sio Kikwete hata kidogo.. ni Mwakyembe na aliyoyasema Kyela..I would have said the same, kama ningekuwa ktk situation yake. Walioleta Richmond nchini hawazungumzwi, aliyeleta issue ya Richmond hazungumzwi leo Mwakyembe aliyepewa ruksa ya kuchunguza ukweli ndiye kawa mbaya na sijui Conflict of interest lakini hao waliokuwa Waziri mkuu na wengine wizara za Miundombinu, wizara ya nishati na Tanesco wote ni victims wa report ambayo imekusanywa kama kimba lililoachwa ukumbini...
Mbona sijasikia mtu akiuliza kama Dr. Slaa ana hisa ktk nishati na madini kwa sababu wanamwogopa!..Mwakyembe ni ndama ambaye predators wameona kuna urahisi sana wa kumshinda kwa hoja au fedha kwani hana ubavu, lakini nitawa taarifu tu kuwa mnashindwa kuona nje ya kabati..
 
Mkandara said:

Mkandara,

..Mkapa alimtema Prof.Simon Mbilinyi baada ya kubainika kwamba alitoa msamaha wa kodi kwa makampuni ya minofu ya samaki. Prof.Mbilinyi alikuwa bestman ktk harusi ya Mkapa na mama Anna.

..unapomsifia Kikwete kwa kumtema Ditopile unakuwa una-exagerate kidogo. mtu yeyote yule aliyetegemea kwamba Kikwete angemuokoa Ditopile kwa mashtaka yale anahitaji kupimwa akili. Ditopile alijisalimisha mwenyewe kwa Tibaigana na kukiri kila kitu sasa ulitegemea Kikwete amsaidie vipi?

..unajua wakati mwingine nashangaa sana unavyojaribu kumpamba Raisi Kikwete hata katika masuala ambayo hastahili, and do not make sense at all.

..Raisi huyu, pamoja na wabunge wa CCM, wamechaguliwa kwa fedha za wizi wa Kagoda. sasa sijui Kikwete atawageuka na kuwasaliti watu wangapi ili kujitoa na kajisafisha na kashfa hiyo.

..suala la Richmond ni ajali ya kisiasa tu iliyowakuta Lowassa,Karamagi,na Msabaha. ajali hiyo isingetokea leo hii hawa jamaa wangekuwa bado wanapeta kwenye cabinet ya Kikwete.
 
..Mkapa alimtema Prof.Simon Mbilinyi baada ya kubainika kwamba alitoa msamaha wa kodi kwa makampuni ya minofu ya samaki. Prof.Mbilinyi alikuwa bestman ktk harusi ya Mkapa na mama Anna.
.

Mkuu Jokakuu,

Heshima mbele, una uhakika kwamba bestman wa Mkapa hakuwa Balozi Nyakyi? Maana enzi hizo Mkapa hakua na time kabisa his fellow Southians kama Mbilinyi, kwa sababu walikuwa ni washamba kwake!, au?

- Hawa kina Mbilinyi alilazimishwa ku-socialize nao in the process ya kwua rais na Kingunge pamoja na Mnauye RIP, ili ku-polish political image yake as a new unpopular president, lakini siku zote za nyuma Mkapa alikuwa close na mashemeji tu!, au?
 
Kazi ipo!
RC aingilia kati sakata la Rostam, Mwakyembe

Na Mwandishi Wetu,Singida

MVUTANO wa kugombea eneo la kuwekeza mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia upepo kati ya kampuni mbili zinazomilikiwa na wanasiasa nchini, sasa umeingia katika sura mpya baada ya mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone kuingilia kati na kueleza kuwa kila moja itapata eneo lake.

Kampuni za Power Pool East Africa, ambayo mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe amekiri kuwa na hisa na Wind East Africa, inayohusishwa na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, zinadaiwa kugombea ardhi katika kijiji cha Kisekida wilayani Singida Vijijini kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo.

Kampuni hizo zinatarajiwa kuzalisha jumla ya megawati 500 kama miradi hiyo itaanza.

Habari za wanasiasa hao kuhusika katika mzozo huo wa ardhi ziliibuliwa na Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa wakati sakata la ununuzi wa mitambo ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited likiwa moto wakati Dk Mwakyembe alipodaiwa kukiuka kanuni za bunge kwa kutotangaza kuwa na hisa katika masuala ya umeme wakati akiomba nafasi ya makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

Tuhuma hizo zilimfanya Dk Mwakyembe kujibu vikali akikiri kuwa na hisa kwenye kampuni hiyo, lakini akasema habari hizo zilichapishwa na magazeti ya Rostam kwa lengo la kumchafua. Mvutano huo tayari uliiweka pabaya serikali ya mkoa wa Singida ambayo ilituhumiwa na wananchi kuwa inatoa upendeleo kwa kampuni mojawapo.

Akizungumza na waandishi wa habari wiki hii, Kone alisema serikali ya mkoa haijatoa upendeleo kwa kampuni yoyote inayotaka kuwekeza umeme katika kijiji hicho, kutokana na taratibu za uwekezaji kuwa wazi na kila kampuni kutakiwa kuzifuata.

Alisema kilichotokea ni kuwa makampuni hayo mawili yaliingia katika mgogoro wa kugombea eneo hilo bila kujua kuwa maeneo wanayopatiwa ni tofauti, hivyo kuanza kuwatumia wananchi kwa kuwatia hofu juu ya kampuni nyingine.

Kone alisema kampuni ya Wind East Africa ipo katika mchakato wa kufanya tathmini ya mali katika eneo ambalo itawekeza ili iweze kutoa fidia kwa wananchi watakaotakiwa kuhama.

Aliwataka wananchi kuwa na subira kwani mgogoro huo umekwisha na serikali yao ipo makini kuhakikisha kuwa wananchi hawaporwi haki zao, bali ni kuona kuwa wanalipwa fidia kulingana na thamani halisi za mali zao.

Pia aliwataka wawekezaji kufuata taratibu za kisheria katika uwekezaji ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza baina yao na wananchi katika maeneo husika.

Alisema pia wanatakiwa kuwashirikisha wananchi kwenye eneo husika katika kila hatua ili wapate ushirikiano wa kutosha, na wamalize tofauti zao kabla ya kuja kuwekeza mkoani Singida.

Katika sakata la Dowans, Dk Mwakyembe na wengine wanapinga vikali serikali kununua mitambo hiyo kwa kuwa inapingana na Sheria ya Manunuzi ya Umma ambayo inaielekeza serikali kutonunua vitu vilivyotumika.

Dk Mwakyembe, ambaye aliongoza kamati teule ya Bunge iliyobaini ukiukwaji wa taratibu wakati wa kutoa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development (LLC) ambayo mkataba wake ulirithiwa na Dowans, na wengine wanaonekana kuhisi kuwepo kwa ufisadi katika suala zima la ununuzi wa mitambo hiyo.

Rostam, ambaye alitajwa kwenye ripoti ya kamati ya Dk Mwakyembe, amekuwa hajitokezi kuzungumzia suala la Dowans na aliibuka hivi karibuni kujibu tuhuma za Mwakyembe kuwa alitumia magazeti yake kumchafua.

Rostam alimtuhumu Mwakyembe kuwa na ubaguzi na kumtaka ajibu tuhuma zake badala ya kuzungumzia wengine.

Akizungumzia sakata hilo, mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa alisema tofauti za wabunge hao wawili wa CCM zinatokana na kugombea eneo la kufua umeme kwa kutumia upepo.

Hata hivyo, wakazi wa kijiji hicho wameiomba serikali kuamua ni nani mwekezaji halisi kati ya kampuni hizo kwa vile mpaka sasa moja ya kampuni hizo imewalipa fidia wananchi na nyingine bado.

Akizungumza juzi na waandishi wa habari, msemaji wa wakazi wa kijiji hicho, Josephat Isango aliyekuwa ameambatana na mwenyekiti wa kijiji, Iddi Dadia na ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Jumanne Mtipa, alisema wamefikia uamuzi huo ili waweze kutoa wasiwasi unaowakabili.

Alisema katika kijiji hicho, kuna kampuni moja inayojulikana kwa jina la Power Pool East Africa, ambayo imeonyesha nia yake ya kuwekeza kuzalisha umeme unaotokana na nguvu za upepo na kwamba, tayari imejadiliana na wananchi na kuwalipa fidia wanaotakiwa kupisha mradi huo.

Isango alisema kampuni hiyo imeomba na kupewa eneo lenye ukubwa wa ekari 550 na imelipa fidia baada ya tathmini kufanywa na mthamini wa serikali katika eneo hilo na wananchi waliolipwa fidia wameanza kuhamia maeneo mengine kupisha utekelezaji wa mradi huo.

Isango alisema pamoja na kampuni hiyo, kuna taarifa ambazo zinatolewa na viongozi wa serikali kuwa kuna kampuni nyingine inayojulikana kwa jina la Wind East Africa ambayo imepewa eneo la kijiji hicho kwa ajili ya kuzalisha umeme bila kuwashirikisha wananchi.

Alisema hali hiyo imezusha mgogoro kati ya wananchi na viongozi wa serikali ya kijiji hicho kwa kuwa viongozi hao wametoa eneo hilo bila kuwashirikisha wananchi.

"Kimsingi tunaipokea kwa mikono miwili miradi yote, lakini tunahofu kwanini hawa Wind East Africa wasifike kijijini kwetu na kushirikiana na uongozi pamoja na wananchi katika kutenga eneo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo," alihoji.

Alisema mpaka sasa Wind East Africa hawajawahi kufika kijijini hapo kwa ajili ya majadiliano na wananchi, lakini wamekuwa wakisikia kutoka kwa viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa wakitambulisha kampuni hiyo.
 
Habari za kutoka hapa Kyela ni kwamba dr. Mwakyembe leo kamvaa Rostam kweli kweli. Kamwita fisadi namba moja, kaiba mali ya Tanzania na ni mbumbumbu, hajui kitu, hata bungeni haongei. Anasema Rostam katumia ufisadi kuiba viwanda viwili alivyoanzisha Nyerere na sasa kafanya godowns zake.

Katika mkutano wake alikuwa ameongozana na waandishi habari kutoka Mbeya baada ya wale wa Kyela kupigwa marufuku kuhudhuria mkutano huo kwa madai kwamba huwa wanamwandika vibaya.
Alitumia muda mwingi kumtukana Rostam.

Hivi ndivyo aliandika Engineer. Hapa tunaona WAANDISHI WA HABARI WAMEPIGWA MARUFUKU KUHUDHURIA. Pia Mwakyembe katumia muda mwingi kumtukana Rostam, ingawa baadaye unasoma kuwa ni RISALA ya Mwakalinga imetumia muda mwingi kumtukana RA

La kwanza ni maelezo kwamba waandishi wa habari waliopo Kyela walipigwa marufuku kwa sababu wanamwandika vibaya, hilo sio kweli hata kidogo, na ni uzushi mkubwa. Kyela wapo waandishi wa habari wa kujitegemea wawili tu na wasio na chombo maalumu cha kukiandikia, na siku hiyo walikuwepo na ushahidi ni Richard Kilumbo ambaye siku hiyo alipeleka habari hiyo Tanzania Daima baada ya kuombwa na mwakilishi wa gazeti hilo mkoani Mbeya ambaye siku hiyo alikuwa Dar, hivyo alishirikiana na mwenzie kutoka Mbeya. Wawakilishi wa makampuni ya habari wote wako Mbeya mjini hivyo husambaa kule kwenye tukio kubwa kwa mkoa kwa wakati ule, ni magazeti machache sana yenye waandishi wake wilayani. Waandishi waliokuwepo Kyela siku hiyo walifika kila mtu mmoja kwa utaratibu wake, baadhi ni baada ya kupata maelekezo toka kwa wahariri wao Dar na wengine waliandamana na Naibu Waziri wa Fedha ambaye siku hiyo alienda Kyela na wengine walienda rasmi kwa ajili ya mkutano huio baada ya kupata taarifa kutoka mjini kyela kuhusu kuwepo maandamano na mkutano.

Nsesi anakuja na maneno SI KWELI, Waandishi walikuwepo hapo. Anaweka RISALA ya Mwakalinga na kuweka maelezo mawili matatu zaidi ambayo yanamwamsha Engineer na kuja kuandika zaidi hapa chini........

Nsesi,

Hao waandishi wa Kyela wawili unaowasema umeongea nao kuthibitisha ulichokiandika hapo juu? Hao waandishi mimi nilikaa nao kule nyuma kabisa na walipigwa marufuku ndio maana hawakusogelea lile jukwaa kama inavyokuwa kawaida yao kwenye mikutano mingine.

Kwa taarifa yako hao vijana wanafahamiana na hao waandishi kutoka Mbeya na walikuwa wote hata kwenye internet cafe kabla ya mkutano huo. Hao waandishi kutoka Mbeya ndio waliwataka hao vijana waende wote lakini wakasema wao wamepigwa marufuku.

Kama unataka uhakika kwanini hao vijana hawakuwa pale mbele sawa na waandishi wengine, basi wapigie simu wao wenyewe kuwauliza. Au mpatie mwana JF mwingine yeyote namba yao awaulize, mmoja wao anaitwa Mwaisaka na mwulize ilikuwaje hakuwa kule mbele?

Ehhh, kumbe walikuwepo hawa waandishi wa habari ila walikaa nyuma!!! Tulisikia wamepigwa marufuku WASIFIKE KWENYE MKUTANO, ila wao wakakaidi? Na Wapambe wa Mwakyembe wakaawacha siyo? Sasa Mhandisi ndiyo anaelezea zaidi kuwa "walipigwa marufuku kukaa mbele" na si "kutokufika kwenye mkutano..."

Nsesi hakusema kuwa wale waandishi walikaa nyuma na si sehemu ya Waandishi. Engineer hakusema kuwa "waandishi walipigwa marufuku kukaa mbele ila walifika kwenye kikao..." Ndiyo maana nikasema time will tell. Nyie nyote naona ni WAWAMBA NGOMA.......

Kujua kuilichotokea kwenye mkutano ni kwamba, soma maelezo yote na changanya yote na ugawanye kwa mbili, utapata wastani ambao ndiyo ukweli wa habari yenyewe......
 
Mkuu Mkandara, heshima kwako. Nataka kukuonyesha tu kuwa niko nje ya kabati na si ndani yake kama unavyodhani. Mkuu sijui kama unafahamu fika ukweli ya yote uliyoyasema. Ngoja niweke kumbukumbu sawa hapa.

Recta na Susuviri,

Wakuu naona kuna hoja nyingi sana zimeisha pita na sasa hivi mko ukurasa mwingine kabisa.. Hata hivyo nitawarudisha nyuma kujibu hoja zenu kwani yanibidi kuweka record sawa...
Yote mliyaandika ni ya kweli kabisa lakini yakiwa ndani ya kabati.. Mnashindwa kutazama nje ya kabati hilo kuwa hawa watu, Lowassa, Rostam na wengine wote mnaotaka wafikishwe mahakamani ni RAIA tu hawana madaraka yoyote ndani ya chama (sectretariat) wala serikalini.. Hakuna implication yoyote ya kisiasa..
Ni vyema ufahamu kuwa wote uliowataja hapo juu ni viongozi wa juu wa CCM. Ni members wa Central Committee ya CCM na pia ni members wa NEC-CCM. Sasa sijui una maanisha nini unaposema kuwa hawana madaraka yoyote ndani ya chama (Secretariet).

Swala kubwa tunalozungumzia ni Richmond ambalo nadhani ndio somo la mada hii kutokana na huyu Mwakyembe..
Ikumbukwe tu kwamba ni Dr. Slaa aliyefunua kimba hili bungeni, wakataka kulizima.. Lowasssa akiwa Waziri mkuu worked tireless kuhakikisha hakuna uchunguzi..sijui kama bado mnakubuka maanake mimi nakumnbuka hapa T-dot Lowasssa aliingia mitini mkutano wa Watanzania..kama sikosei ilikuwa Nov 2006..
Taarifa zote alizosema Dr. Slaa zilikuja bainika na kamati ya Mwakyembe, hapakuwa na jipya zaidi ya kupewa majina ya wahusika na mfululizo wa taratibu zilizotumika..

Hapana, Mkuu suala linalozungumziwa hapa si Richmond. Suala kubwa ni matokeo ya vita ambavyo RA na Mwakyembe wamejikuta nayo kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa kupambana na ufisadi. Inawezekana pia kuwa, baadhi ya jitihada hizo zimechipukia kutokana na Richmond scandal, lakini si hiyo pekee inayosababisha mjadala huu. Kama unafuatilia kwa makini utagundua hivyo.

Na ni baada ya ukweli huo ndipo Lawassa alipojiuzuru, na ajabu sana mnaposema kajiuzuru tuu hivi hivi bila kumfikia mkulu kupata uhakika.. Watu wetu wa ndani walituambia Lowassa alikwenda kumwona Kikwete hata kabla report hiyo haijamfikia yeye. Lowassa alikwenda tena kumwona Kikwete baada ya JK kumwambia Mwakyembe aiwakilishe Bungeni kama alivyoikusanya..Kikwete alimtosa Lowassa!.

Hata mimi naungana na wewe katika imani hiyo ya support ya JK katika kuweka bayana mambo ya Richmond. Naamini kuwa, Kamati ya Bunge, Bunge lenyewe na baadhi ya Wabunge waliojitokeza kwa nguvu zote kukemea viongozi waliojihusisha na Richmond walipata nguvu kubwa kutoka kwa JK. Katika utamaduni uliozoeleka, si rahisi kwa wanasiasa wa CCM kuwa na uhuru ulioonekana katika Bunge wakati ule. Hii inajidhihirisha zaidi baada ya kuona jitihada za awali zilivyokuwa zikizimwa kwa mafanikio makubwa.

Wakuu, Kikwete sio tu alimtosa waziri mkuu na kuweka record, Kikwete kawatosa marafiki zake ambao walikuwa team moja kabla ya Uchaguzi na kawaacha nje hadi leo hii tunavyozungumza.. hata mwalimu hakuwahi kufanya hivyo..

Kikwete hajamtosa mtu yeyote. Inawezekana kuwa watu unaosema wametoswa na JK walitegemea ange-react tofauti katika nia ya kuwalinda kwenye maovu yao. JK alisema wazi kuwa uRais wake hauna ubia na mtu yeyote. Alisema pia kuwa anataka wanamtandao waache umtandao wao na kukijenga chama kwa kuwa uchaguzi umekwisha.

Hivyo, si sahihi kusema aliwatosa. Ila mimi ningependa kusema walim-disappoint na hivyo kujiweka katika nafasi ya kutopata/kutofaidi support yake.

Mwalimu aliwahi kufanya mengi zaidi ya kuwatosa wenzake. Aliwahi hata kufunga baadhi ya mawaziri.

Nasikitika kusema tena kwamba Kikwete pia alimtosa Ditto mshikaji wake ambaye alijaribu kupata msamaha wa JK, na kimtaani naweza kusema Ditto hakufa kifo cha kawaida tu inawezekana kabisa ali commit suicide baada ya kuona hana pa kutokea..

Sidhani kuwa JK alimtosa Ditto. Nadhani ni kumuonea kudhani kuwa alifanya pungufu ya kilichowezekana kufanyika katika jitihada za kumuokoa.

Mkuu kumbuka kuwa kesi ya Ditto ilipelekwa kwa kasi sana, alipewa dhamana ambayo ilishangaza wengi, aliwekwa kwenye mazingira bora zaidi. Naweza kusema kuwa JK alijitahidi sana kumsaidia Ditto katika suala lililomkuta. Watu wengi walilalamika kuwa Ditto alipewa special treatment ambayo haikuwahi kutolewa kwa wafungwa wengine kabla ya tukio lile. Sasa sijui ulitaka JK afanyeje kabla kesi haijakwisha. JK angeweza tu kumsamehe kifungo baada ya kumalizika kwa kesi na si vinginevyo (katiba inamruhusu). Na nina uhakika alikuwa tayari kufanya hivyo mara tu kesi hiyo ingemalizika. Mungu aliamua tofauti.

Sijui unawezaje kutuhakikishia kuwa Ditto alijiua (commit Suicide). Ila nafikiri kama hakuna ushahidi kwa hilo, si vyema kumsingizia marehemu.

Hizi habari za kusema hafai kwa sababu ambazo hata roibo yake Mwinyi wala Mkapa hakufanya wakati mafisadi walikuwepo tena kwa nguvu ya ajabu, nashindwa hata kufikiri. yaani kweli kuna watu wanasema Mkapa angefanya hivi ama vile wakati wanajua kabisa Yona na Mramba, Balali, Megji, Karamagi, Rostam, Lowassa na mwengine wote hawa, Ufisadi wao haukuanza wakati wa JK isipokuwa toka kwa hao mnaojaribu kuwasifia viongozi upupu kama hawa..Damn!..

Nadhani nijibu hivi:

1. Sijui umenukuu wapi niliposema JK hafai. Ninachoamini ni kuwa matarajio ya wengi hayajafikiwa kwa asilimia kubwa sana. Matarajio hayo hayalinganishwi na kiongozi mwingine yeyote alietangulia.
2. Mzee Mwinyi alichukua uRais katika kipindi ambacho nchi ilikuwa masikini sana kuliko kipindi ambacho JK aliingia madarakani. Mzee Mwinyi alifanya mageuzi makubwa sana ya kiuchumi ambayo yamelibadilisha sana Taifa hili. Nadhani unakumbuka siasa za "Pesa si msingi wa Maisha". Sasa hivi ukisema hivyo unaweza kupingwa mawe.

Huyu Mzee alikuwa mkali sana na ufanisi wake ulivutia sana katika kipindi chake cha kwanza. Ufisadi uliimarika kupita kiasi katika kipindi chake cha 2. Hasa alipoachia nchi iongozwe na wabinafsi wachache, na yeye ku-retire prematurely.

3. Mzee Mkapa aliingia kwenye uRais kipindi ambacho nchi ilikuwa imeanza kuanguka kabisa. Elimu ilikuwa haina maana, wasomi waliamua kuacha kazi na kushinda mitaani (matapeli), tenda hewa, kukithiri kwa wafanyakazi hewa (serikalini), n.k. Nchi ilikuwa haikopesheki, haisaidiki. Nchi ilikaribia kusimama. Mkapa alifufua uchumi, aliongeza uwekezaji, aliweka usawa kati ya kazi na mapato. Alirudisha wasomi kazini. Nchi iliongeza mapato sana.

Baada ya kumaliza kipindi chake cha pili, ndipo ilipoonekana kuwa kulikuwa na ufisadi mkubwa uliofanyika katika miezi yake ya mwisho ya uongozi (karibu na uchaguzi wa awamu ya 4). Haya yote yalionekana baada ya yeye kutoka.

On the other hand, Awamu ya 4 inadhihirisha ufisadi uliotukuka na unaofanywa waziwazi na viongozi wa serikali. Mambo haya yangeeleweka zaidi kama yangetokea katika kipindi cha pili, na kazi kubwa (kama watangulizi hapo juu). Wizi umeanza mapema mno.
 
Hivi ndivyo aliandika Engineer. Hapa tunaona WAANDISHI WA HABARI WAMEPIGWA MARUFUKU KUHUDHURIA. Pia Mwakyembe katumia muda mwingi kumtukana Rostam, ingawa baadaye unasoma kuwa ni RISALA ya Mwakalinga imetumia muda mwingi kumtukana RA

Nsesi anakuja na maneno SI KWELI, Waandishi walikuwepo hapo. Anaweka RISALA ya Mwakalinga na kuweka maelezo mawili matatu zaidi ambayo yanamwamsha Engineer na kuja kuandika zaidi hapa chini........

Ehhh, kumbe walikuwepo hawa waandishi wa habari ila walikaa nyuma!!! Tulisikia wamepigwa marufuku WASIFIKE KWENYE MKUTANO, ila wao wakakaidi? Na Wapambe wa Mwakyembe wakaawacha siyo? Sasa Mhandisi ndiyo anaelezea zaidi kuwa "walipigwa marufuku kukaa mbele" na si "kutokufika kwenye mkutano..."

Nsesi hakusema kuwa wale waandishi walikaa nyuma na si sehemu ya Waandishi. Engineer hakusema kuwa "waandishi walipigwa marufuku kukaa mbele ila walifika kwenye kikao..." Ndiyo maana nikasema time will tell. Nyie nyote naona ni WAWAMBA NGOMA.......

Kujua kuilichotokea kwenye mkutano ni kwamba, soma maelezo yote na changanya yote na ugawanye kwa mbili, utapata wastani ambao ndiyo ukweli wa habari yenyewe......
Na kama hoja ya Mhandisi ya waandishi wa Kyela kupigwa marufuku kuudhuria ina maana wapenzi wa Mwakyembe hawakustukia kuwa wasaliti wao wasiopaswa kuandika chochote wapo pale mkutanoni? je kuna njia yoyote waliitumia kuficha uwepo wao hapo mkutanoni?kwa namna ulivyowasilisha hoja basi uwepo wao pale mkutanoni ulikuwa ni hatari kwa maisha yao unless usahihishe kidogo hoja yako ili kuwa fair...,kwa kuficha kwako kuwa WALIKUWEPO mkutanoni inaonyesha ulikuwa umekusudia kumisread watu,na hii siyo nzuri kwa mjadala wowote..!!
 
Upinzani waziwazi ndani ya CCM.

Mara kadhaa utasikia mitaani "ah yule jamaa na mke wake huwa wanazozana na wanapigana kila siku..yaane pale wanaegesha tu", leo tunajionea wenyewe, wanapigana, nje ya nyumba, mtaani, mchana kweupee... baada ya siku kadhaa waweza kusikia, talaka.

Japo kwa sasa wote (RA na Mwakembe) wanaonekana kutapatapa, binafsi kiasi fulani naegamia upande wa Mwakyembe. Kuna kichwa cha habari katika Tanzania Daima ya leo kinasema "habari za mitaani ndiyo habari". Haiwezekani watu wakasema yote haya wanayomsema RA ikawa wote ni uzushi tu. Inaonekana pia RA na Mwakymbe wamekamatana pabaya, kila mmoja anweza kumdondosha mwenzie.. hapa ni taimingi tu..Lisemwalo...

Huu "mkono/kibano" cha mtaani sisi yetu macho... Utaona mara mmoja kachaniwa nguo yake, usijekuta hajavaa nguo ya ndani... mbele ya kadamnasi...

Lakini... huyu RA ni nani huyu? Iweje ana ujasiri mkubwa hivi? Haongei... yeye ni Mzee wa Kimyakimya. Ni kama "Genious" flani hivi wa mikakati, ya maovu. Hivi ukimpa urais leo (japo watu wanadai yeye ndiye rais, kingmaker) itakuwajee?
 
Kwa hali hii inaonesha Mwakyembe kaishiwa kisiasa.

...Naona hata wewe umeishiwa fikra.
Chambua kama aliyoyasema ni sahihi au uongo, maana NINYI hampendi mtu anaposema ukweli kwa maslahi ya taifa ila mnakumbatia majinamizi yanayonyonya jasho na damu za wasio na hatia...
Mtalegea hivi karibuni ninyi msiojali TAIFA letu
 
Niliteleza ila lengo lilikuwa kwamba ni Majaji wengi ni Republican au wako zaidi upande huo. Hili halikuwa muhimu sana anayway. Ila mzee wa SPINNING katika yote hayo kaona hilo. Ungeliandika tu yale ya juu ningelijua ni katika kuelekezana (lengo la JF) ila hiyo nimeweka NYEKUNDU, duuu!!! Utafikiri mtu kakaa wee anakusubiri ufanye tu kosa, huyoo kashakurukia koo. Kuhani, TAFADHALI!!!

Hata Tanzania unaweza kukuta majaji wengi wamewekwa na Mkapa/Mwinyi. Ila bado inakuwa ni CCM walewale. Sasa hapa inatosha tu kukumbushana. Wengine hatuweki kichwani kila siku mambo haya tu. Kuna siku nyingine inabidi kuweka kichwani uzito na upana wa AIRBUS 380, ili uwanja mpya wa Dodoma na Dar es salaam uweze kuhilimi dege hilo siku likishuka hapo. So, Kuhani, PULIZIIIII!!!!!!!!!!!

Sikonge,

Ukikubali kwamba "umeteleza" basi uchune, usimlaumu aliyesema umeteleza. Mkuki kwa Aziz, kwa wana JF?

Unasema wengine hamuweki kichwani mambo yale, well, ni wewe ndio umeyaleta yale. Ha hahahaaaa aa aaaa
 
Hivi ndivyo aliandika Engineer. Hapa tunaona WAANDISHI WA HABARI WAMEPIGWA MARUFUKU KUHUDHURIA. Pia Mwakyembe katumia muda mwingi kumtukana Rostam, ingawa baadaye unasoma kuwa ni RISALA ya Mwakalinga imetumia muda mwingi kumtukana RA

Nsesi anakuja na maneno SI KWELI, Waandishi walikuwepo hapo. Anaweka RISALA ya Mwakalinga na kuweka maelezo mawili matatu zaidi ambayo yanamwamsha Engineer na kuja kuandika zaidi hapa chini........

Ehhh, kumbe walikuwepo hawa waandishi wa habari ila walikaa nyuma!!! Tulisikia wamepigwa marufuku WASIFIKE KWENYE MKUTANO, ila wao wakakaidi? Na Wapambe wa Mwakyembe wakaawacha siyo? Sasa Mhandisi ndiyo anaelezea zaidi kuwa "walipigwa marufuku kukaa mbele" na si "kutokufika kwenye mkutano..."

Nsesi hakusema kuwa wale waandishi walikaa nyuma na si sehemu ya Waandishi. Engineer hakusema kuwa "waandishi walipigwa marufuku kukaa mbele ila walifika kwenye kikao..." Ndiyo maana nikasema time will tell. Nyie nyote naona ni WAWAMBA NGOMA.......

Kujua kuilichotokea kwenye mkutano ni kwamba, soma maelezo yote na changanya yote na ugawanye kwa mbili, utapata wastani ambao ndiyo ukweli wa habari yenyewe......

Sikonge,

Wacha kufurahisha watu hapa. Mkutano ulikuwa wa wazi hivyo hakuna mtu anayeweza kumzuia mwingine asiende. Wanachoweza kufanya ni kukuzuia usiende kule mbele. Ukikaa kule nyuma na wakaja kukutoa watakuwa wanataka kuleta vurugu na polisi watakulinda tu.

Mikutano ya wilayani, waandishi wana nafasi zao, huwa wanakaa mbele karibu na jukwa la mhusika, wakipiga picha na kuandika habari. Hao vijana nilioandika walikatazwa kwamba wasionekane pale.

Wao wakaamua kujiendea kama wananchi wa kawaida na kukaa nyuma wakisikiliza. Hawakwenda kuandika habari kama ambavyo wangefanya wasingekatazwa. walipigwa marufuku kuhudhuria kama waandishi wa habari.

Hiyo ndiyo ilikuwa maana ya taarifa yangu na sio vinginevyo.
 
Wakuu nisaidieni nimeona ippmedia wanasema Rostam Azizi abanwa.....,amwita Mwakyembe mbaguzi wa Rangi.....

Nomaaa,wenye pc hapo tuwekeeni hiyo news wakuu.
 
Engineer, Hebu nawe acha kuchanganya mambo, mwandishi wa habari yeyeyote makini hakai jukwani kwenye mikutano ya hadhara, kwani anahitaji kupata feelings za wasikilizaji pia, huyo mwandishi unayemsema nami nilimuona na kuongea naye, alikuwa akirandaranda uwanjani kama waandishi wengine. Yawezekana mwandishi akaenda jukwani lakini hawakai moja kwa moja pale jukwani, sasa hizo picha utapigaje ukiwa jukwani.

Lengo la kurekebisha taarifa yako ni kuufanya mjadala kuwa na mwelekeo sahihi badala ya ushabiki. Mbona kuna mambo mengi tu yanatokea pale Kyela hayaandikwi, au nayo wamekatazwa na Dk Mwakyembe? Kulikuwa na uhalifu wa baadhi ya wafanyabiashara kulawiti watoto wa shule za msingi pale kyela mjini tena wakitumia Guest House ya huyo diwani wako, walipewa taarifa tena na watu wa UWT walikaa kimya, jamaa wakawataarifu waandishi waliopo Mbeya mjini wakaenda na uozo ukaanikwa wakakamatwa na kufikishwa mahakamani na kijiwe chao cha uhalifu pale four ways kitawanywa, wafanyakazi Kiwira wanadhulumiwa wako kimya pamoja na kupelekewa malalamiko, hawaandiki hadi wafanyakazi hao wameamua kupitishia malalamiko yao kwa waandishi walioko Mbeya na udhalimu wa wamiliki wa kiwira kuanikwa.

Ni vizuri unapoweka hoja iwe sahihi ili watu wajadili katika mstari ulio sahihi kulingana na mitazamo yao kwa maada husika na si kuwaelekeza kwenye mitazamo yako.
 
Recta,
Mkuu wangu sasa hivi sina muda ila nitakujibu baadaye..(Mwakyembe vs Rostam)..

Kifupi tu kuwepo kwa watu hao (mafisadi alowatosa) ktk Central Committe ya CCM na pia members wa NEC -CCM haina maana kabisa kuwa hawa watu wana wadhifa ndani ya Uongozi wa nchi hii, hata Asha Baraka ni member wa kamati za chama.. na kuamini kwamba member wa chama CCM ni mtu mkubwa sana ni imani ya kupotosha Demokrasia inavyofanya kazi.. CCM ni chama tu kama kilivyo chama Chadema au CUF, hivyo hizo Committe zinafanya kazi za chama na wakivuruga ktk maslahi ya Taifa wanatakiwa kushtakiwa kwa taratibu sawa na raia mwingine yeyote.. Na mfano mzuri ni Chenge kama nilivyosema hapo awali..JK hakushirikishwa ktk kumkamata, na kumfungulia mashtaka kwa sababu ni member wa kamati za CCM...
Kuhusiana na Ditto, nimesema kwa Lugha ya mtaani inawezekana nikasema Mkulu alijiua kutokana na JK kumbwaga..
Recta, mkuu kwa lugha nayotumia usidhani najaribu kumlaumu JK kumbwaga Ditto isipokuwa ni kuonyesha jinsi anavyoweza kuwa tofauti na viongozi wengine waliopita na hasa viongozi wa Kiafrika..Nyerere asingeweza kumtupa Ditto, Mwinyi asingeweza na wala Mkapa asingeweza kufanya hata nusu ya aliyofanya Kikwete ktk swala la Mafisadi tena watu wake wa karibu... Pamoja na sifa zote ambazo mimi humbwagia Nyerere naelewa kabisa kuwa alikuwa akiwalinda baadhi ya watu na kila walipoharibu aliwabadilisha wizara au madaraka tu. Mwinyi ambaye alihusika na mauaji ya vizee huko Shinyanga alikuja kuwa rais wa nchi.. Lakini tunaona JK kawabwaga kabisa viongozi wote aliowaondoa ktk serikali yake na sehemu za chama ambazo ana madaraka... Kikwete hana madaraka wala mamlaka ya kuwavua Mafisadi nafasi zao ktk kamati za chama ikiwa wamechaguliwa kulingana na taratibu za chama..Yeye ni mwenyekiti tu na inatakiwa nguvu kubwa ya wajumbe kuwavua uanachama au ujumbe wa kamati hizi..nguvu hiyo hana na ndicho nachotaka kuwaambia..He is (almost) standing alone!
Hivyo tusijaribu kumbebesha mzigo usio kuwa wake...
 
Date::4/1/2009
RC aingilia kati sakata la Rostam, Mwakyembe

Na Mwandishi Wetu,Singida

Mwananchi

Back
Top Bottom