Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Mmmhh!!! siasa za Kyela nazo kichwa cha mwenda wazimu. Wacha wengine tunyamaze, tusije tukaambiwa tunaandaliwa kwi kwi kwi!!!!.

Hivi hakuna mwenye audio clip!

Nasikia UNAANDALIWA na Wachina :) Achana na Kyela, njoo huku Sikonge...
 
Mwakyembe inaelekea kuwa yuko so bitter...yaani vagi lake na Rostam juzi jumamosi alilihamishia kwenye fainali ya kombe la NSSF kwenye mechi ya timu ya UHURU v/s HABARI CORP.

So sad huyu jamaa nilikuwa namheshimu miaka ileee alipokuwa na kile kiofisi chao cha LEGAL AID na Dr MVUNGI pale kwenye jengo la SUKITA enzi hizo Mwakyembe alikuwa ni mtu kweli kweli sasa tangu aingie kwenye siasa amekuwa kama mwehu vile

Mpka leo sielewi what was the point ya kupandishana pesa jumamosi...lakini ndio hao wanasiasa wetu

AMA KWELI PESA MWANA HARAMU

Lakini hata kama akitambika uchi huyu mwakyembe, ukweli utabaki pale pale kuwa yeye ni miongoni mwa wale wabunge waliokula milioni 5 za Rostam wakati wa Kampeni sasa leo hii asitake kujidai yeye ni msafi kuliko wote.

In short Rostam ni kama Nyerere tena naweza kusema zaidi kwenye hii game ya Politics za TZ, Maana mwalimu yeye alikuwa ni mcheza Game kwenye politics tuu lakini Rostam ni mpaka Biashara in other words HE OWNS THE CURRENT RULING ELITES na hawana cha kumfanya baada ya kula pesa zake

So Mwakyembe should spare himself further embarrassment kuendelea kutukanana na mtu ambaye hamjibu except ana rewind ule mkanda wa makabidhiano now and then

Mwisho zaidi nasema I CANT KNOCK ROSTAM'S HUSTLE....jamaa ni mtafutaji na anaitumia opportunity anavyoona itamnufaisha

Ugonjwa wetu mnajua tatizo lake lilianzia wapi na dawa yake wote mnaijua

Kama mtu aliyepata exposure ya jinsi ulimwengu ulivyo halafu anaishia kuandika utumbo kama huu, ni jambo la kusikitisha kwa kweli.
 
Hivi maendeleo kumbe yanaletwa na mafisadi? Mimi nilifikiri wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao wanajiletea maendeleo yao wenyewe? Fisadi Rostam atakwamisha vipi maendeleo ya Kyela?

Au wote wanafanya kama Mtikila, kwenda kukopa kwa Rostam ili waje waziendeleze wilaya zao?

Sisi Kyela tunajiletea maendeleo yetu wenyewe. hatuna mjomba wa kutuazima pesa za EPA. Muhimu tu ni umoja na kuacha kugombana.

Hakuna sehemu yoyote inayopata maendeleo kwa kutumia hela za mtu mmoja kutoka mfukoni mwake; atakuwa na uwezo gani? Kama kuna mahali umeona kitu kama hicho tupe mifano. Ninachojua mimi ni kuwa budget ya serikali inaelekezwa majimboni kwa priorities mbalimbali kwa shughuli za maendeleo kama kujenga barabara, mashule, umeme n.k. Kama nchi inaongozwa na mafisadi, ina maana wao haohao (mafisadi) ndio wenye say ya kipi kifanyike na kipi kisifanyike. Ukitofautiana nao si wanao uwezo wa kuhamisha fungu la jimbo lako likaelekezwa kwingine? Kwani unafikiri serikali imeshindwa kuweka askari wa kutosha kudhibiti mauaji ya wananchi huko Tarime? Ufinyu wa watu kufikiria unawa-limit kudhani kuwa ufisadi uko kweye EPA na Richmond tu! Think beyond that.
 
Nasikia UNAANDALIWA na Wachina :) Achana na Kyela, njoo huku Sikonge...

Wewe mkuu Sikonge,

Wachina waniandae mimi, si wataacha na virusi ndani viwe vinawapelekea siri za Kyela?

Itabidi nimwombe JK agawe wilaya nami nipate kajimbo kangu kwi kwi kwi!!!

Yaani kule kwetu balaa tupu, inabidi watu tuogope hata kwenda likizo maana mtu akidondoka, tutaambiwa tulipeleka ile sumu ya KGB. Watu wanatumia umaskini na ujinga wa vijana ili kuwayumbisha watu. Badala ya hao vijana kuwa chachu ya maendeleo, kazi zao ni kukaa kwenye vijiwe na kupeleleza nani anafanya nini, kisha kupewa visenti vya soda.

Mimi nitakuwa huko summer nikafaidi kipunga cha kwetu. Njoo unitembelee huko, ila ukipigwa panga usije ukanilaumu mimi.
 
Mwakyembe inaelekea kuwa yuko so bitter...yaani vagi lake na Rostam juzi jumamosi alilihamishia kwenye fainali ya kombe la NSSF kwenye mechi ya timu ya UHURU v/s HABARI CORP.

So sad huyu jamaa nilikuwa namheshimu miaka ileee alipokuwa na kile kiofisi chao cha LEGAL AID na Dr MVUNGI pale kwenye jengo la SUKITA enzi hizo Mwakyembe alikuwa ni mtu kweli kweli sasa tangu aingie kwenye siasa amekuwa kama mwehu vile

Mpka leo sielewi what was the point ya kupandishana pesa jumamosi...lakini ndio hao wanasiasa wetu

AMA KWELI PESA MWANA HARAMU

Lakini hata kama akitambika uchi huyu mwakyembe, ukweli utabaki pale pale kuwa yeye ni miongoni mwa wale wabunge waliokula milioni 5 za Rostam wakati wa Kampeni sasa leo hii asitake kujidai yeye ni msafi kuliko wote.

In short Rostam ni kama Nyerere tena naweza kusema zaidi kwenye hii game ya Politics za TZ, Maana mwalimu yeye alikuwa ni mcheza Game kwenye politics tuu lakini Rostam ni mpaka Biashara in other words HE OWNS THE CURRENT RULING ELITES na hawana cha kumfanya baada ya kula pesa zake

So Mwakyembe should spare himself further embarrassment kuendelea kutukanana na mtu ambaye hamjibu except ana rewind ule mkanda wa makabidhiano now and then

Mwisho zaidi nasema I CANT KNOCK ROSTAM'S HUSTLE....jamaa ni mtafutaji na anaitumia opportunity anavyoona itamnufaisha

Ugonjwa wetu mnajua tatizo lake lilianzia wapi na dawa yake wote mnaijua

GT

Wewe ni sawa kabisa na wale babu zatu waliokuwa wanapewa pipi halafu wanawagawa ndugu zetu kwenda kuwa watumwa kwa waarabu. Umejisghushia sana hadhi yako humu jamvini inabidi tu sasa ubadiri jina. Hivi nyinyi watanzania mmelogwa na nini kinachofanya muuze utu wenu?
 
acheni kwa akili zenu za kuchambua mambo humu ndani tatizo la Tanzania ni Rostam? kama nilivyosema siwezi ku knock his hustle jamaa ni mtafutaji na nafasi imepatikana asiitumie? hivi mngekuwa nyinyi mngefanya nini?

Na tusitake kumfanya Mwakyembe saint humu kwa sababu hana usaint wowote ule...tatizo langu kwa mwakyembe kama msomi na mwanasheria angeachana na kubwatuka bila mpango kwa sababu in this poltical game hakuna aliye msafi

tuache kuzunguka mbuyu hapa...matatizo yetu si Rostam wala Mwakyembe matatizo yetu mnajua chanzo chake nini, na ufumbuzi wake mnajua nini sasa hili la kutaka kutufanya tuamini mtu mmoja ndiye mla rushwa na hakuna chombo chochote cha sheria kilichomhukumu kwa hilo ni upuuzi mtupu
 
Unaishi Tanzania ama, ina maana majimbo yote yasiyo na maendeleo toka enzi na enzi walikuwa wanapinga mafisadi. Kuna majimbo toka tupate uhuru yako yako tu. Kama huna cha kuandika soma ya wenzako. Mwakyembe huu ni mwaka wake wa ngapi Ubunge?, wakati kuna Mbunge mwingine kulikuwa na maendeleo gani?.

Sikuelewi hapa. Tafadhali soma hoja ya msingi iliyopelekea response yangu. Wacha kukurupuka! Kwa ufupi nilichosema ni kuwa control ya maendelo ya Kyela iko beyond Dr. Mwakyembe na hasa kwa kutofautiana kwake na mafisadi (uongozi wa nchi) ambao ndio una-allocate resources, usitegemee kuona chchote cha maendeleo jimboni humo kwa kipindi hiki. Maana watafanya kila wawezacho (kumbuka wanalindana) kuwafanya wananchi waone kuwa yeye Dr. ndio hakuwaletea maendeleo kipindi chake.
 
Hakuna sehemu yoyote inayopata maendeleo kwa kutumia hela za mtu mmoja kutoka mfukoni mwake; atakuwa na uwezo gani? Kama kuna mahali umeona kitu kama hicho tupe mifano. Ninachojua mimi ni kuwa budget ya serikali inaelekezwa majimboni kwa priorities mbalimbali kwa shughuli za maendeleo kama kujenga barabara, mashule, umeme n.k. Kama nchi inaongozwa na mafisadi, ina maana wao haohao (mafisadi) ndio wenye say ya kipi kifanyike na kipi kisifanyike. Ukitofautiana nao si wanao uwezo wa kuhamisha fungu la jimbo lako likaelekezwa kwingine? Kwani unafikiri serikali imeshindwa kuweka askari wa kutosha kudhibiti mauaji ya wananchi huko Tarime? Ufinyu wa watu kufikiria unawa-limit kudhani kuwa ufisadi uko kweye EPA na Richmond tu! Think beyond that.

Pesa za maendeleo zinapelekwa kupitia halmashauri ya wilaya. Kila halmashauri ina budget yake kama ilivyo wizara. Ni kweli kuna mambo ambayo wizara inaweza kufanya moja kwa moja kwenye wilaya, lakini kwa taarifa yako ni machache mno. Mambo mengi hufanywa kupitia halmashauri ya wilaya.

Huko nyuma ilikuwa tofauti na waziri alikuwa na nguvu sana ya kuamua mambo mbalimbali. Pia kulikuwa hakuna vyombo vya habari vya kuwaumbua kwamba mbona mkoa huu una shule 50 wakati ule mwingine una shule moja tu? Kwasasa waziri anaweza kupeleka kwao kamradi kamoja, lakini usitegemee apeleke kwao miradi mitano bila kuumbuliwa.

Priorities zetu kule kwenye halmashauri ndio mbovu. Si umesikia madiwani wanapeana 65,000 kwenye vikao vyao? Hizo pesa zingetumika kwa maendeleo, zinaweza kufanya mambo mangapi? Sawa ufisadi ni tatizo TZ lakini tatizo kubwa zaidi ni ujinga na kushindwa kuwajibika kwa viongozi wetu. Inatakiwa kuwe na njia za wazi za kuwawajibisha viongozi hao na kufanya tathmini ya uongozi wao.

Hii ya kila siku kutafuta mchawi wa matatizo yetu nafiki ni weakness kubwa sana.
 
acheni kwa akili zenu za kuchambua mambo humu ndani tatizo la Tanzania ni Rostam? kama nilivyosema siwezi ku knock his hustle jamaa ni mtafutaji na nafasi imepatikana asiitumie? hivi mngekuwa nyinyi mngefanya nini?

Na tusitake kumfanya Mwakyembe saint humu kwa sababu hana usaint wowote ule...tatizo langu kwa mwakyembe kama msomi na mwanasheria angeachana na kubwatuka bila mpango kwa sababu in this poltical game hakuna aliye msafi

tuache kuzunguka mbuyu hapa...matatizo yetu si Rostam wala Mwakyembe matatizo yetu mnajua chanzo chake nini, na ufumbuzi wake mnajua nini sasa hili la kutaka kutufanya tuamini mtu mmoja ndiye mla rushwa na hakuna chombo chochote cha sheria kilichomhukumu kwa hilo ni upuuzi mtupu

Kwa maana hiyo hata wewe ukipata nafasi ya kuihujumu hii nchi utaikamua mpaka damu ya mwisho kama anavyofanya huyu fisadi Rostam? Ama kweli nchi hii watu wengi wameoza na akili zao ni kutafuta mali kwa namna yoyote ile. Rostam ni mmoja wa watu wanaochangaia kuharibu uchumi wa nchi hii na kuendelea kuweka mzigo mzito juu ya wananchi wa kawaida wanaoishi kwa kubangaiza. Tuna huduma mbovu mahospitalini na miundo mbinu mibovu ya umeme na barabara kisa kuna watu wana matrilioni ya pesa kwenye akaunti zao huku wakiwa na uraia wa nchi tatu kama Rostam. Jua ya kuwa mtu anapokuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja na huku ana mapesa lukuki kama Rostam mtu huyo ni jangili wa kutupwa na anapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote. Tangu lini mwarabu na mhindi akawa na uchungu wa kuona maendeleo kwenye nchi za Kiafrika? Wengi wapo kwa maslahi yao binafsi na kwa ndugu zao walioko India, Canada na Uarabuni. Waangalie watu kama akina Manji na Dewji wanatoa pesa zao kwenye klabu za mpira kama na kulipia watu waingie bure kwenye mpira mamlioni ya pesa, Akina Somaia wanachangia uchanguzi wa UVCCM milioni 400 lakini na wanajua namana ya kuzirudisha pesa zao iwe ni kwa kukwepa kulipa kodi au "deals" chafu za kibiashara lakini hawachangii miradi yoyote ya maendeleo.
Kalaghabaho
 
Mwakyembe inaelekea kuwa yuko so bitter...yaani vagi lake na Rostam juzi jumamosi alilihamishia kwenye fainali ya kombe la NSSF kwenye mechi ya timu ya UHURU v/s HABARI CORP.

So sad huyu jamaa nilikuwa namheshimu miaka ileee alipokuwa na kile kiofisi chao cha LEGAL AID na Dr MVUNGI pale kwenye jengo la SUKITA enzi hizo Mwakyembe alikuwa ni mtu kweli kweli sasa tangu aingie kwenye siasa amekuwa kama mwehu vile

Mpka leo sielewi what was the point ya kupandishana pesa jumamosi...lakini ndio hao wanasiasa wetu

AMA KWELI PESA MWANA HARAMU

Lakini hata kama akitambika uchi huyu mwakyembe, ukweli utabaki pale pale kuwa yeye ni miongoni mwa wale wabunge waliokula milioni 5 za Rostam wakati wa Kampeni sasa leo hii asitake kujidai yeye ni msafi kuliko wote.

In short Rostam ni kama Nyerere tena naweza kusema zaidi kwenye hii game ya Politics za TZ, Maana mwalimu yeye alikuwa ni mcheza Game kwenye politics tuu lakini Rostam ni mpaka Biashara in other words HE OWNS THE CURRENT RULING ELITES na hawana cha kumfanya baada ya kula pesa zake

So Mwakyembe should spare himself further embarrassment kuendelea kutukanana na mtu ambaye hamjibu except ana rewind ule mkanda wa makabidhiano now and then

Mwisho zaidi nasema I CANT KNOCK ROSTAM'S HUSTLE....jamaa ni mtafutaji na anaitumia opportunity anavyoona itamnufaisha

Ugonjwa wetu mnajua tatizo lake lilianzia wapi na dawa yake wote mnaijua

Mkuu GT,

Sijakusoma vizuri hapa. Ulitaka kusemaje sasa, manake mtiririko wa habari nzima umechanganywa changanywa!
 
Priorities zetu kule kwenye halmashauri ndio mbovu.

Mkuu umelonga sawa kabisa ila ninawasiwasi na hili la vipaumbele. Utaratibu wa bajeti za halmashauri unafuata mwongozo unaotolewa na Wizara kila mwaka. Mwongozo unaelekeza sekta na asilimia ya bajeti. Hivyo unaweza kuona kuwa wananchi wanawezakuwa na vipaumbele vyao lakini bajeti inafuata mwongozo toka Wizarani. Hii ni kwa fedha kutoka Serikali kuu.

Fedha za wafadhili mara nyingi kama siyo zote huja na mwongozo wake wa matumizi. Hairuhusiwi kabisa kwenda kinyume na mwongozo huo.

Kuhusu own source (mapato ya ndani ya halmashauri) yanatumika kwenye utawala kama hizo posho za madiwani, watendaji, vibarua kama vile walinzi wa zahanati, shule nk. Kibaya zaidi hata D.C, Mbunge, Viongozi wa Chama Tawala ktk halmashauri wanaomba mafuta na posho mbalimbali kutoka kwenye fungu hili.

Labda kwenye miradi kama vile TASAF ndo vipaumbele vya wananchi vinazingatiwa.
 
utake usitake matatizo yetu hayasabaishwi na Rostam na kukosekana kwa checks and balances serikalini si kosa la Rostam, mikataba mibovu hakuandikwa na Rostam yote hayo mnayajua

Mnaboa pale mnapoanza kugun for a wrong target. Jaribuni kupanua upeo wa mwono wenu. Hivi kesho mfano Rostam akihama nchi au akiachana na siasa rushwa itaisha Tanzania?

Cha ajabu huyu Rostam ambaye mnadai ni fisadi na anahusika na kesi za kifisadi mbona mpaka leo yuko free na anaendelea na shughuli zake kama kawaida? Mahakama tunazo,PCCB wapo, DPP tunao sasa tangu muanze kumtaja leoni mwaka wa 4 na hajachukuliwa hatua yoyote ile

I cant knock his hustle kwa sababu tuuu kagombana na mwakyembe au kwa sababu ni CCM

Tukubali kuwa hatuwezi kuendesha mijadala based on politics of envy na innuendos.
 
Mwakyembe ni mtu makini na shujaa pia.Pamoja na kelele zote za kuwa RA ni mtu hatari lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kumsema waziwazi kama Mwakyembe na Mtikila,sana sana tuna waandishi njaa wanaonunulika kirahisi kwa kuandika mema ya RA
 
WELL,game theory kasema ROSTAM,ni kingmaker and he pulls the strings,sasa pambana naye at your own peril-is this not the reality? HAPA,naona fact zimejiweka wazi,why do we have to argue vitu ambavyo viko wazi kama daylight or are we thumping the keyboard just for the sake of keeping ourselves busy?
 
...
Mimi bado naamini kuwa Mwakyembe amatanabahi kuwa alifanywa mbuzi wa kafara na sasa amebaini kuwa ngoma aliyocheza ni nzito. Naamini pia kuwa anaelewa hata akienda upinzani hatofanikiwa na hivyo ameamuwa to hell to whatever may come. Si unakumbuka aliposema kuwa hana mkataba na Bunge anayo profession yake? Kauli ile ilikuwa na maana kubwa.wabunge machachari wanalikiuka hili na kibaya MZEE MALECELA keshajikosha kuwa yeye anamuunga mkono JK. Patamu hapo.
Hebu angalia hata

...hiyo jeuri ya kwamba ana profession yake, hana mkataba wa Bunge na blah blah nyingine hazitamsaidia... Kabla yake walikuwapo kina Masumbuko Lamwai, na Mabere Marando, ambao walipiga kelele miiiiiiiiiiingi, leo hii wamerejea ngamani. Kimyaaaaaaaaaaa!

Kuna msemo "You are always a Genius until you open your mouth!", na Mh.Rostam analithibitisha hili kwa jinsi (if true, indirectly) alivyoweza mprovoke Mwakyembe kwa kutumia wahariri wake...

Mheshimiwa Mwakyembe, umeongea yametosha, uliitisha mkutano na waandishi wa habari lakini hukukidhi kiu ya watanzania walio wengi, na kuzunguka majukwaani kwa maneno hayo hayo ya mipasho, binafsi imani kwako inapungua.

Kumbuka, "fisadi hawi fisadi bila kuwezeshwa na fisadi mkuu"... who is behind Ufisadi wa Rostam Aziz, Mh.Mwakyembe lipuwa hilo bomu heshima yako irudi.
 
Sijui kwa nini unafikiri kuna bomu la kulipua hapo, kwani we humjui anayemlinda?
 
Kwa maana hiyo hata wewe ukipata nafasi ya kuihujumu hii nchi utaikamua mpaka damu ya mwisho kama anavyofanya huyu fisadi Rostam?

1)wapi nimesema Rostam anahujumu nchi?

2)kama ni fisadi au la hiyo ni kazi ya vyombo vya sheria na hakuna chombo hata kimoja kilichomshitaki au kumhukumu

Ama kweli nchi hii watu wengi wameoza na akili zao ni kutafuta mali kwa namna yoyote ile. Rostam ni mmoja wa watu wanaochangaia kuharibu uchumi wa nchi hii na kuendelea kuweka mzigo mzito juu ya wananchi wa kawaida wanaoishi kwa kubangaiza.
1) kuna ubaya gani watu kutafuta mali kihalali?

2) kachangia kuharibu uchumi wa Tanzania kivipi?
Tuna huduma mbovu mahospitalini na miundo mbinu mibovu ya umeme na barabara kisa kuna watu wana matrilioni ya pesa kwenye akaunti zao huku wakiwa na uraia wa nchi tatu kama Rostam.
1)kuna ubaya gani mtu kuwa na na matrilioni kwenye akaunti?

2)Hospitali kukosa dawa, mtaro wa haideri plaza kutozibwa,posta mpya kunuka maji machafu na wananchi kukosa maji safi ni majukumu ya Rostam pia?

3)Lete ushahidi kuwa Rostam ana uraia wa nchi tatu

4)Zitaje na namba zake za uraia wa nchi hizo

Jua ya kuwa mtu anapokuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja na huku ana mapesa lukuki kama Rostam mtu huyo ni jangili wa kutupwa na anapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote.

1) Rejea majibu yangu hapo juu

2)Lete ushahidi kuwa Rostam ni Jangili

3)Je Mengi naye ni Jangili kwa sababu ana pesa luluki?

Tangu lini mwarabu na mhindi akawa na uchungu wa kuona maendeleo kwenye nchi za Kiafrika?

1)Prof Issa Shivji ni mhidi je hana uchungu na Tanzania?

2)Kuwa na uchungu na nchi lazima uwe na ngozi nyeusi kama Grey Mgonja?
Wengi wapo kwa maslahi yao binafsi na kwa ndugu zao walioko India, Canada na Uarabuni.
1)kuna ubaya gani kuwa na ndugu India,Canada na Uarabuni?
2)kuna ubaya gani kuwa na maslahi binafsi?

Waangalie watu kama akina Manji na Dewji wanatoa pesa zao kwenye klabu za mpira kama na kulipia watu waingie bure kwenye mpira mamlioni ya pesa,
1)ushasahau kuwa hapo juu lisema hivi:Tangu lini mwarabu na mhindi akawa na uchungu wa kuona maendeleo kwenye nchi za Kiafrika?

2)Kwa hiyo kuwaingiza watu mpirani bure ndio kigezo chako kikubwa cha kuwa mtu anafaa?
Akina Somaia wanachangia uchanguzi wa UVCCM milioni 400 lakini na wanajua namana ya kuzirudisha pesa zao iwe ni kwa kukwepa kulipa kodi au "deals" chafu za kibiashara lakini hawachangii miradi yoyote ya maendeleo.
Kalaghabaho

Lete ushahidi kuwa Somaia kakwepa kulipa kodi
 
huyu jamaa ni GAME THERY HASWA HASWA, he is playing another game, kabla ya hapo nilikuwa najiuliza maswali mengi
1. Jamaa kaamka vibaya?
2. huyu jamaa kaibiwa password ya JF?
3. huyu mtu katumwa???

sasa hivi hata sijiulizi tena keep on PLAYING THE GAME. gAmE tHeOrY
 
Nionavyo mimi humu JF kuna mapandikizi ya mafisadi, kazi yao kubwa ni kuchomekea posts za kutetea au kuvuruga mada iluiyopo dhidi ya mafisadi. Bila shaka wanafanya hivyo kwa malipo maana bila ya fedha hawa hawawezi kutetea chchote, achilia mbali mafisadi -- ni mamluki. Lakini napata faraja kubwa kuona kwamba hawa ni wachache mno, tena mno, idadi kubwa sana ya wanaochangia mada ni wapiganaji wa dhati wa ufisadi, HONGERA SANA!!!!

...ni rahisi kabisa kuwajua!! Even the devil has friends?
 
acheni kwa akili zenu za kuchambua mambo humu ndani tatizo la Tanzania ni Rostam? kama nilivyosema siwezi ku knock his hustle jamaa ni mtafutaji na nafasi imepatikana asiitumie? hivi mngekuwa nyinyi mngefanya nini?

Na tusitake kumfanya Mwakyembe saint humu kwa sababu hana usaint wowote ule...tatizo langu kwa mwakyembe kama msomi na mwanasheria angeachana na kubwatuka bila mpango kwa sababu in this poltical game hakuna aliye msafi

tuache kuzunguka mbuyu hapa...matatizo yetu si Rostam wala Mwakyembe matatizo yetu mnajua chanzo chake nini, na ufumbuzi wake mnajua nini sasa hili la kutaka kutufanya tuamini mtu mmoja ndiye mla rushwa na hakuna chombo chochote cha sheria kilichomhukumu kwa hilo ni upuuzi mtupu

Huna lolote wewe unatumika tu pamoja na kukjifanya unajenga hoja . ebo eti mwizi kaiba unasema mwacheni kwa sababu siyo yeye aliesababisha hali ya maisha iwe ngumu ala! ooooooovyo!
 
Back
Top Bottom