Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

Kwani Mwakyembe alifanya nini katika huo mtanange wa Timu ya Uhuru na Habari?.
 
BUBU, angalia jinsi cheap politics inavyotumiwa na Mwakyembe. Nini lengo la kumtaja Nyerere? kupata sapoti ya wananchi wasioelewa mambo. Nafikiri kwa wewe mwelew unajuwa kuwa viwanda karibu vyote vilivyoanzishwa wakati wa nyerere tuliviua na baadae majengo tukauza. Huoni desperation ya Mwakyembe na badala yake eti unaita kuwa anasema kwa maslaha ya Taifa. Kama ni mfuasi wa Nyerere basi asingekuwa na hisa huku akiwa Mbunge. Najua kuwa hakuna tatizo kuwa na hisa baada ya sisi wenyewe kuamuwa hivyo nakwa njia hiyo hiyo najuwa kuwa hakuna tatizo la kuweka godowns kwenye majengo ya kiwanda tulichokiuwa.

Mkuu shujaa wetu kaamuwa kututelekeza na kutetea maslahi yake kwa kutumia migongo yetu.

Huu ndiyo unafiki wetu Watanzania anaposimama mtu kutaka kupambana na mafisadi tunamgeuzia kibao na kumuona yeye mbaya badala ya yule mbaya wetu wa kweli. Rostam kahusika na wizi wa mapesa ya EPA kupitia Kagoda wa shilingi bilioni 40, lakini hadi hii leo hajaguswa kwa kisingizio cha hakuna ushahidi wa kutosha. Rostam kahusika na kashfa ya Richmond kwa kutudanganya Watanzania kwamba kampuni yake ilikuwa na HQ Houston, Texas na wana utaalamu katika kuzalisha umeme kumbe ilikuwa ni kanyabwoya tu. Amelipwa bilioni 200 bila kuzalisha hata tone la umeme na juzi karibu aiuze mitambo yake michakavu kwa shilingi bilioni 60 kinyume na taratibu za manunuzi serikali. Kama siyo Watanzania kuja juu basi mitambo hiyo ya kanyabwoya ingenunuliwa kwa hiyo 60 Billioni na Rostam kuendelea kuwafanya Watanzania kama kichwa cha mwendawazimu. Sasa yeye hapa ndiyo anaonekana shujaa na kuanza kutetewa!!

Ama kweli Waafrika ndivyo tulivyo!!!! wizi wa bilioni 240 uliofanywa na fisadi Rostam (Richmond 200 bilioni na Kagoda 40 billioni) Anatokea mtu anapambana na na Rostam bila woga, yeye ndiye anaonekana mbaya kwamba eti kajiharibia!!!!! Siku yoyote nitamthamini mtu ambaye anaweka mbele maslahi ya Watanzania mbele bila kujali maslahi yake mwenyewe hata kama kufanya hivyo kunaweza kabisa kukaharibu hadhi yake ndani ya chama cha mafisadi. Chenge fisafi bado anapeta ndani ya chama, Mramba fisadi bado anapeta ndani ya chama, Lowassa fisadi bado anapeta ndani ya chama, Karamagi fisadi bado anapeta ndani ya chama lakini leo hii Mwakyembe ndiyo anaonekana mbaya ndani ya chama na machoni mwa baadhi ya wanachama hapa jamvini!!!! Ama kweli tenda wema uende zako!!!! lakini history haidanganyi inawezekana kabisa ndani ya chama Mwakyembe akaonekana ni mkorofi lakini miongoni mwa Watanzania wengi tuliochoshwa na unafiki na ufisadi uliokithiri ndani ya CCM na Serikali siku zote tutauheshimu mchango wake katika vita dhidi ya mafisadi.

Unafiki uliokithiri miongoni mwa Watendaji wa juu wa ndani ya chama na Serikali ndiyo unaifanya Tanzania kuwa katika hali mbaya kama tuli nayo. Sijamsikia Chiligati wala huyo Malecela wakikemea ufisadi uliokithiri ndani ya chama na serikali ukiwemo ule uliofanywa na Mkapa wa kujiuzia mgodi wa Kiwira wenye thamani ya shilingi bilioni 7, kwa shilingi milioni 700 tu ambayo ni 10% ya thamani ya mgoni na hadi hii leo alicholipa Mkapa ni shilingi 70 milioni tu ambayo ni 1% ya thamani ya mgodi huo!!!! Mgodi unakufa hauzalishi chochote wafanyakazi wanahaha hawana mishahara miezi minane sasa lakini wanafiki na watetezi wa mafisadi ndani ya CCM hawajatoa kauli yoyote kuhusu mgodi huo!!!! Rais wa nchi naye yuko kimya kuhusu mgodi huo ambao unakufa taratibu huku wanafiki wakiogopa kumgusa Mkapa ambaye alijipatia mgodi huo kwa njia za kifisadi, lakini leo hii wako tayari kutumia makucha yao dhidi ya Mwakyembe!!!!!!! Mungu inusuru Tanzania!!!
 
Habari za kutoka hapa Kyela ni kwamba dr. Mwakyembe leo kamvaa Rostam kweli kweli. Kamwita fisadi namba moja, kaiba mali ya Tanzania na ni mbumbumbu, hajui kitu, hata bungeni haongei. Anasema Rostam katumia ufisadi kuiba viwanda viwili alivyoanzisha Nyerere na sasa kafanya godowns zake.

Katika mkutano wake alikuwa ameongozana na waandishi habari kutoka Mbeya baada ya wale wa Kyela kupigwa marufuku kuhudhuria mkutano huo kwa madai kwamba huwa wanamwandika vibaya.

Alitumia muda mwingi kumtukana Rostam.

Pia kasema yeye ni kweli anamiliki shares kwenye hiyo kampuni pamoja na vijana wengine kama 50 wazalendo wa nchi hii na kwamba hiyo kampuni bado haijaanza.

Anasema alipoenda Singida alishangiliwa sana na wananchi wakamwambia kama Kyela hawamtaki basi wao Singida wapo tayari kumpa ubunge.

Kuna mengi mheshimiwa kaongea ambayo mpaka mtu unajikuna kichwa, hivi kweli ni muhimu? Labda ndio siasa zetu zilipofikia sasa. Inaelekea maneno ya Malecela hawajayasikia kabisa.

Wenye taarifa zaidi mnaweza kuongea.

Mkuu kwanza karibu jamvini.
Pili inawezekana wewe ni mmojawapo wa hao waandishi kutoka Kyela? Kwasababu umesikiliza hotuba yake hiyo na kuja hapa kuweka conclusions zako,ingekuwa jambo la maana kama ungetuwekea hapa hotuba hiyo na sisi tu ijudge accordingly.

Mwakyembe siyo mjinga kiasi mnachodhani,CCM wamebweteka na wananchi wanatakiwa walijuwe hilo,halafu eti mkuu wa nchi anatoa pongezi juzi hapa kuwa eti kwa Mama Kilango kwasababu ya vita dhidi ya ufisadi,yani ccm wapumbavu wana acknowledge kwamba kuna ufisadi na mafisadi,na kuna vita dhidi ya mafisadi ambao wako ndani ya chama,lakini ikifikia wakati wa kuzungumzia kuhusu ufisadi huo na kuwazungumzia mafisadi hao,wao ni wa kwanza kudai ushahidi. na kuitana kwenye vikao vya chama. Hivi ndugu zangu mnatoa wapi balls za kuzungumza upupu kama huo? Mnadai ushahidi na wakati huo huo mlisha acknowledge kuwa kuna ufisadi?Mwakyembe si mjinga na ccm mtafikia mahali mchague kati ya mafisadi na wazalendo,katika political situation ya sasa kama kuna watu wanafananisha situation ya Mwakyembe na Mrema basi ni ccm waliopofushwa macho na ufisadi kiasi cha kushindwa kuona kama ufisadi wenyewe upo....Ufisadi Umekuwa halali na ndio maana ni mazungumzo tu...Kama kuna watu wanamtetea RA kwasababu hajapelekwa mahakamani na huku wakijua mizizi ya ufisadi ilivyo ndani ya ccm basi hao hawana nia njema na Taifa na ndio maana hata bado tunaendelea kutawaliwa na no wonder tulifanywa watumwa kiurahisi na bado sisi ni kama watumwa tu, especially kifikra! Yani RA ni malaika kwasababu kuna wanaodai kuwa kaonewa na mswahili ambaye yeye ndiyo anataka kuwa na pesa kama RA,ROHO KOROSHO YA KITUMWA NA FIKRA FINYU,Kwasababu ni mswahili,kuna watakaotamani hata kumtoa roho mswahili mwenzao kwasababu si utamaduni wetu sisi miafrika kufurahia maendeleo ya wenzetu,kama ni mzungu ama mwarabu wala hakuna atakeyejiuliza. Mwakyembe anatolea mfano wa viwanda ambavyo viliuwawa na mafisadi halafu kuna wanaodai eti ni cheap popularity kwa kumtaja mwalimu....Wananchi wamedharauliwa mpaka mwisho na tuna vibaraka watumwa wa akili wanaozidi kutufukarisha...La ajabu ni kwamba kuna wanaoheshimika kuwa ndio wasomi wengi sana hapa JF lakini ndio hao hao current days Mangungo,haingii akilini kabisa kusahau ufisadi wote wa kina RA kwasababu tu eti kuna wanaodai hayo mambo yamalizwe ndani ya chama ambacho ndicho mwanzilishi na mlezi wa mafisadi na ufisadi...Mtavutana sana nyie ccm lakini siku ya kufa nyani miti yote huteleza....Na kama nyie mnaojidai kuwa ni wastaarabu sana kwa kuendelea kuzikumbatia sheria za kifisadi kwa kuzitumia loopholes ni wazi hamtaki mabadiliko na chama chenu cha mafisadi ni kigumu kwa wazlendo wa kweli wanaotaka mabadiliko ya kweli...Tatizo ni kwamba wengi wamebakia kwenye upuuzi ule ule wakidhani mambo ni yale yale...Kama mama Kilango alisema mambo hayo yalishamalizwa bungeni,halafu mme wake naye anakuaja na kudai yakamalizwe ndani ya chama..Then wapi utofauti kati ya maslahi ya Taifa na ya chama?
Ufisadi umeanzia ndani ya chama,na licha ya ccm kukubali kuwa ufisadi huo upo,hakuna aliyechukuliwa hatua zozote za kichama ili kuweza kusema kweli wanapiga vita ufisadi.

Kuna kauli nyingine za kipuuzi kuwa eti MK anatumia issue ya ufisadi,hili neno "Ufisadi" mmeshalifanya lionekane kama ni sifa nzuri na ndio maana mna brush off,wananchi wanatakiwa wasisahahu kuwa ufisadi ndio rushwa na machafu yote yanayotufanya masikini hadi leo,sasa hilo lisipokuwa the maini issue then si ni sawa na kujaza maji kwene gunia?

This is a defining moment,hilo sasa liko wazi...Tusubiri tuone wananchi watakavyoamua coming 2010, maana kelele zetu hapa JF hazisaidii kama wananchi hawatafanya mabadiliko kwasababu kama kuna watetezi wa wazi wazi wa ufisadi,then ni wananchi wamewapa nguvu hizo watu hao...Wananchi wakiwapa ccm fundisho kwa kutowachagua next time,then watajiuliza mara mbili mbili kabla ya kuzungumza ama kufanya maamuzi yenye kutetea ufisadi.....Sijui sana kuhusu huko mitaani kwamba maoni hasa ya wananchi wa kawaida ni yapi hayo,najua wananchi wa kawaida hapo bongo hawana access ya internet na sidhani kama mawazo yao ni swa na ya wanaotetea mafisadi humu ndani,hata hivyo kipimo kikuu ni hapo 2010.
 
Kama kweli hayo yanayodaiwa kuwa Mwakyembe kasema, basi huyu jamaa atakuwa ni bonge la reckless kwa sababu kama hawezi kuyathibitisha hayo madai yake, Rostam anaweza ku counter na slander lawsuit! Mwakyembe should know better (if what is said to be said is true).
 
Kama kweli hayo yanayodaiwa kuwa Mwakyembe kasema, basi huyu jamaa atakuwa ni bonge la reckless kwa sababu kama hawezi kuyathibitisha hayo madai yake, Rostam anaweza ku counter na slander lawsuit! Mwakyembe should know better (if what is said to be said is true).

Huyu fisadi Rostam kama angekuwa wa kufungua kesi angeshafanya hivyo siku nyingi sana lakini hana ubavu huo. List iliyotolewa na CHADEMA ya mafisadi jina la Rostam lilikuwemo sijui kama alikuwa mmoja wa waliotishia kufungua kesi lakini hakuna hata mmoja aliyethubutu kufungua kesi dhidi ya CHADEMA maana wanajijua kwamba ni mafisadi na walikuwa na wasiwasi mkubwa kwamba CHADEMA labda ilikuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yao hivyo wote waliishia kuingia mitini.
 
Huyu reporter wetu naona amechanganya vitu alivyo komwa RA usoni na Mwakyembe yeye anaona matusi lakini ndo ukweli wenyewe.Itabidi tumkome mpaka akimbie nchi.
 
Gozi gumu,
Katika suala la kununuliwa mitambo ya Dowans Mwakyembe ametajwa na nani?
Mwakyembe ameingia kwenye mgogoro kwa kutajwa kuwa alikuwa na conflict of intererst juu ya umeme. Alijitetea na kuanzia hapo alikuwa na sapoti nzuri tu. Hata waliomakini wamejaribu kumtahadharisha lakini sikio la kufa.
..
Mkuu soma maandiko yako utaona jibu umeliandika mwenyewe.. Ametajwa na nani kisha unasema Ametajwa kuhusika na.. wewe umeipata wapi hiyo kama hakutajwa..
Hoja ilikuwa Dowans na sio Richmond! na kama haya mashirika hayahusiani imekuwaje kesi ya Dowans yarudishwe maswala ya Richmond ambayo kesi imekaliwa bungeni..Je, mnakubali kuna uhusiano..au?..
Hakuna hata sehemu moja ya maelezo ya kamati ya Nishati na madini (Mwakyembe) kuhusiana na Dowans wamegusia Richmond au hata kumtaja Rostam isipokuwa Dowans na kile walichokuwa wakiuza..Leo yeye karudishiwa kesi nzima ya Richmond wakati hakuna mtu aliyeuliza kuhusiana na Richmond.. mbona hamtaki bunge ilizungumzie swala la Richmond tena kesi mmeifunga tayari..Kama kweli mnataka ushahidi na ukweli kuhusiana na Richmond liambieni Bunge lifungue mara moja kesi ya Richmond tutamjua mchawi nani!..Ya Dowans yabakie Dowans na utapeli wake..Na mkitaka kuunganisha yote then hata Mwakyembe ana haki ya kuunganisha toka kule anakokufahamu yeye iwe hata Igunga!
 
Kuna tetesi ambazo nimezisikia hapa, nasema tetesi kwasababu siwaamini wanaozisema. Wanasema Dr. Mwakyembe anatafuta njia ya kuhamia CHADEMA.

Wanasema kwenye mkutano wa leo yule kijana wa CHADEMA aliyewahi kuwekwa ndani wakati ule wa ziara ya JK ndiye alikuwa mbele katika waandaaji. Pia wanataja uhusiano wa Dr. Mwakyembe na Mbowe pamoja na Mengi kama sababu za kuamini hivyo.

Pia inaelekea kuna mpambano mkali unaandaliwa Kyela 2010 kati ya Dr. Mwakyembe na jamaa mmoja nasikia yuko nje ya nchi.

Mimi nilikuwa hapa kwa muda na niliyoyaona leo sina hamu, hii wilaya imegawanyika kweli kweli. Sikuona viongozi wowote wa CCM pale mbele badala yake kulikuwa na wapambe wa mheshimiwa waliokuwa wanamwaga sifa kibao.

Angalieni hili jimbo 2010 inaelekea kutakuwa na vituko.

..mmmmhhhh....haya bana

.......anyway.......Mwaka huu wachonganishi walioshibishwa na Mafisadi watapiga sana kelele baada ya kuumizwa.......na kipigo cha Richmond/DOWANS.......dah

They are really trying to capitalize on issues ambazo sasa zimetuchanganya sana hata sisi hapa JF.............uchonganishi usio kuwa na miguu wala kichwa.......aisee Mafisadi kiboko
 
Hujaeleweka, sijui umeunganisha mechi, political hustling na unyerere, histroy kidogo ya mwakyembe, etc. etc.

Oh, i need to see a doctor!! really...
 
Game Theory,
Mkuu kama Mwakyembe alikula mchango wa Rostam asingeinua hata kidole, tunawajua wote waliokula hizo fedha wanaingia Bungeni na kuuchapa usingizi kusubiri kura za kupinga hoja zote zinazohusiana na Rostam..Wanajulikana mkuu wangu, Mwakyembe hayupo ktk hesabu hizo wala Rostam asingemwacha unajua yaliyomkuta Mtikila...tena basi hata kugombea tu Ubunge ilikuwa shughuli kubwa hawakumtaka kabisa asimame isipokuwa yule msomi mwingine aliyekula hela akapigwa chini.....mara umeshalisahau vagi ile!
 
Halafu sijakuelewa, kumfagilia Rostam. Soma Mtanzania ya Jumapili tarehe 29-03-2009 utaona kuna uzushi pale unasema Mwakyembe aendelea kuumbuliwa pia Selelii afilisika Kisiasa hapo utajua kuna jambo
 
Halafu sijakuelewa, kumfagilia Rostam. Soma Mtanzania ya Jumapili tarehe 29-03-2009 utaona kuna uzushi pale unasema Mwakyembe aendelea kuumbuliwa pia Selelii afilisika Kisiasa hapo utajua kuna jambo

Thanks Mkuu;

Kama zito anaweza kubadilika... then anyone anaweza kubadilika!!! Too bad ni pale mtu anapomsifia RA; hii njaa itatumaliza wooote
 
Mwakyembe inaelekea kuwa yuko so bitter...yaani vagi lake na Rostam juzi jumamosi alilihamishia kwenye fainali ya kombe la NSSF kwenye mechi ya timu ya UHURU v/s HABARI CORP.

So sad huyu jamaa nilikuwa namheshimu miaka ileee alipokuwa na kile kiofisi chao cha LEGAL AID na Dr MVUNGI pale kwenye jengo la SUKITA enzi hizo Mwakyembe alikuwa ni mtu kweli kweli sasa tangu aingie kwenye siasa amekuwa kama mwehu vile

Mpka leo sielewi what was the point ya kupandishana pesa jumamosi...lakini ndio hao wanasiasa wetu

AMA KWELI PESA MWANA HARAMU

Lakini hata kama akitambika uchi huyu mwakyembe, ukweli utabaki pale pale kuwa yeye ni miongoni mwa wale wabunge waliokula milioni 5 za Rostam wakati wa Kampeni sasa leo hii asitake kujidai yeye ni msafi kuliko wote.

In short Rostam ni kama Nyerere tena naweza kusema zaidi kwenye hii game ya Politics za TZ, Maana mwalimu yeye alikuwa ni mcheza Game kwenye politics tuu lakini Rostam ni mpaka Biashara in other words HE OWNS THE CURRENT RULING ELITES na hawana cha kumfanya baada ya kula pesa zake

So Mwakyembe should spare himself further embarrassment kuendelea kutukanana na mtu ambaye hamjibu except ana rewind ule mkanda wa makabidhiano now and then

Mwisho zaidi nasema I CANT KNOCK ROSTAM'S HUSTLE....jamaa ni mtafutaji na anaitumia opportunity anavyoona itamnufaisha

Ugonjwa wetu mnajua tatizo lake lilianzia wapi na dawa yake wote mnaijua

Wewe na Balile ni wale wale, sijui kama Rostam ni nani kila anapotajwa kuna watu wanaugua ukimwi. Anachofanya Mwakyembe ni sawa, ana akili timamu, ila kuna watu ukiwagusa Tanzania unatafutiwa kila aina ya jina.

Pili, Sidhani kama mwakyembe ni mfuasi wa Rostam kwa kupewa fedha za kampeni anyway Rostam ndiye aliyekuwa na mgao wa Kagoda, je aligawa zake au za Kagoda?

Tatu dhiki zitawauwa kwa kumkumbatia huyu mwarabu wenu!
 
Naomba niulize huu umma wa wanamapinduzi.

Wakati Zitto na Dr. Slaa walipotoa tuhuma za Ufisadii kuhusu Buzwagi, EPA, na kwingineko hata na Richmond, kwa nini hawa Wabunge wa CCM ambao leo wanahubiri kuwa wanapigana dhidi ya mafisadi walikaa mguu pande?

Kama Slaa na Zitto walidiriki kutoa ushahidi ambao umetupa nuru kuhusu Buzwagi na EPA, na kisha juhudi wetu kusukuma hoja ya Richmond kwa Bunge na Watanzania na kumpa sifa Mwakyembe, kwa nini watu wa CCM bado wako kimya na wanajivutavuta?

Je tumesahau walipojikusanya Butiama na wakaoneana aibu na kuongoka kimya kimya?

Huu ukasuku uliozuka ghafla bin vup kutoka kwa CCM siuamini ikiwa kelele hizi si ndani ya vikao vyao vikuu iwe ni NEC au CC au kamati ya Bunge.

Hili kwangu ni changa la macho na kannyaboya, alimradi tuendelee kuamini kuwa ndani ya CCM kuna walio bora.

Ni heri na wale ambao tumewajua misimamo yao tangu awali kuwa mapenzi yao ya CCM hayawezi kufutika, lakini hawa wanaojifanay mashujaa ni wa kuogopwa kama ukoma.

Kama kweli Mwakyembe ana ushahidi wa wizi na hojuma za Rostam, ameshaufikisha kwa Mwenyekiti wake au kuwasilisha kwa Spika ombi maalum la kuundwa tume kumchunguza Rostam?

Zitto alifungiwa miezi mitatu kwa kusema Karamagi kahujumu, na mkataba tukauona wazi umehujumiwa. Dr. Slaa aliongea kuhusu EPA, akatoa listi ya watuhumiwa na makampuni yaliyohusika na uhujumu, kwa shingo upande watu wanaingia mahakamani.

Swali linarudi nililouliza awali, je ukiachia hisia na hasira yetu kwua Rostam ni mhujumu, je ni nani kati yetu mwenye ushahidi kamili aulete tuupeleke mahakamani na tuuanike hadharani kama yanayomsibu Chenge na Rada?

Namuonea huruma Mwakyembe, maana kama ni kifo cha kisiasa amechukua kitanzi na kujitundika mwenyewe.

Huko CCM hakuna salale, ni wanyama wabaya wasio na huruma, atatengwa na ajiunge na kina Kasyupa, Njelu na Lamwai. Na kama alitegemea kuachana na Siasa na kuwa mfanyabiashara, basi haijui Tanzania na Chama alichokuwa akikitumikia.

Mwambieni siku anafungua duka,TRA na TBS watakuwa mlangoni kwi kwi kwi!

What a sad story! Miseducation and Miscalulations of Harrison Mwakyembe!
 
This is a defining moment,hilo sasa liko wazi....

JMushi,

Hasira zetu kutokana na kudhulumiwa na kunyanyaswa zisitupofushe tukaacha kutumia mkondo halali wa Sheria au kupoteza utu.

Tunapoanza kuacha kufuata sheria au kupindisha sheria ili zikidhi mahitaji yetu, hatuna tofauti na CCM au mafisadi.

Hivyo usiniite shujaa kwa kuwa nimevunja sheria na nimeshatoa fatwa ya kuwachapa viboko mafisadi!

Tanzania tunalilia Utawala bora na siasa safi. Gharama zake ni kubwa na ni kazi ngumu katika kipindi hichi. Kama tutafanya kafara ya kupindisha sheria kisa This is the Moment na kila mtu akashangilia uhaini huu, then siku CCM na Mafisadi wakishika hatamu na kufanya lile tusilolipenda tusiwashikie Bango na kuwalaani.

CCM wameshavunja miiko na Sheria kwa kupindisha sheria na katiba ziipendelee wao wenyewe. CCM imetumia dola kutishia upinzani na hata sisi tusiofungamana ambao tunaikosoa.

Leo nasi tukianza kufanya na kuiga anachokifanya CCM au Mafisadi, kunaweza kukalika?

This is the moment for us to do the right things and right way not the other way round!
 
Vita vya Rostam na Mwakyembe amevianzisha Rostam mwenyewe na hii vita sio ya mwakyembe pekee ni wengi wako kwenye vita hii kwani kundi la Rostam likiongozwa na Lowasa linawaonea wengi.

Kiini cha mgogoro huu kimeanzia kwenye research results za power pool ea, Rostam alitaka kuiba results na baadhi ya wadau akishirikiana na Lowasa, walivyoshindwa waliamua kuhakikisha kuwa mradi ule hautafanikiwa, moja wanahakikisha hakuna bank au serikali ya tanzania kuisaidia kampuni ile.
pili, hawapati sehemu yeyote ya kuwekeza mradi huo, vita yao ikaanzia singida.

Tatu watawapaka matope wote wanaoshiriki mradi huo kwa kutumia magazeti walioyaanzisha na wabunge waliowaingiza bungeni na wafuasi wao mawaziri kama Ngeleja nk.

Nne kwa sababu mradi huo hauna vigogo wanaotambulika basi haufai tanzania.

Hapa hakuna maslahi kwenye kamati bali kuna ile dhana ya mweusi asiwe na kampuni kwani huwa wanawasumbua sana waburushi wachache.
Ikumbukwe baada ya uhuru wa bendera bado mtanzania hajapata uhuru wa kiuchumi ndio maana leo hakuna mweusi mwenye nguvu ya kweli kupigana na mafisadi kwani wengi wanategemea hawa mafisadi kuishi, kufanyakazi, na kuwa wanasiasa. Najua hoja itakuwa kinepi ni mmbaguzi la hasha hii ni hali halisi haya ndiyo yaliyotokea mareakani mweusi kutawaliwa baada ya ubaguzi kwisha kwa sababu za kiuchumi vilelvie Afrika ya kusini bado mweusi ana njia ndefu kabla hajawa na nchi lazima tubadilishe mtizamo wetu kwenye uchumi na kuwaona na tusio wategemea kuwa wanaweza

Tusipokata hii chain hatuwezi kuendelea. hatuwezi kuwa na wabunge ndani ya bunge walionunuliwa na kina rostam, jeetu kama tu wale wa Mobutu.

Naomba kuwasilisha hoja
 
mh sasa hawa si wa chama kimoja? badala ya kujenga chama ili kishinde uchaguzi mkuu mwakani wao wanaweka mambo ya binafsi mbele! Poor them hawana lolote wote mafisadi tu hapa wanaonyesha jinsi walivyo wabinafsi na wanatetea interest zao binafsi si kwa manufaa ya mtanzania yeyote.

Kama Rostam ni fisadi na mbaya kiasi hicho hakuna chombo cha Chama kinachoshughulikia kesi za namna hii pasipo kushirikisha hadhara nzima ya watanzania? Mbona Nnauye aliongelea vitu kama hivi hadharani wakamvua cheo?

Ama keli CCM mmeishiwa sera na msipoangalia 2010 mtavuna mabua
 
game theory
naomba nianze hivi, hii habari umeandika wewe au wewe umeifanyia summary na kuiweka humu kwa maana haileweki kabisa, kichwa cha habari ni RA vs AM katika mashindano ya NSSF. lakini ndani ya hiyo habari hakuna kabisa kilichotokea hapo kwenye hiyo mechi
sasa huu ni huo uandishi tunaosema wa kununuliwa, m2 ananununliwa na kuambiwa amchafue fulani sasa kwa sababu taaluma ni ndogo anaamua kuandika vitu ambavyo havieleweki mara uhuru, mara kama nyerere, mara kala milion 5, mara kigeugeu, hebu kaa chini na lete hoja za maana tujadili
 
Back
Top Bottom