Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam; Kyela! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam; Kyela!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Engineer, Mar 29, 2009.

 1. E

  Engineer JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za kutoka hapa Kyela ni kwamba dr. Mwakyembe leo kamvaa Rostam kweli kweli. Kamwita fisadi namba moja, kaiba mali ya Tanzania na ni mbumbumbu, hajui kitu, hata bungeni haongei. Anasema Rostam katumia ufisadi kuiba viwanda viwili alivyoanzisha Nyerere na sasa kafanya godowns zake.

  Katika mkutano wake alikuwa ameongozana na waandishi habari kutoka Mbeya baada ya wale wa Kyela kupigwa marufuku kuhudhuria mkutano huo kwa madai kwamba huwa wanamwandika vibaya.

  Alitumia muda mwingi kumtukana Rostam.

  Pia kasema yeye ni kweli anamiliki shares kwenye hiyo kampuni pamoja na vijana wengine kama 50 wazalendo wa nchi hii na kwamba hiyo kampuni bado haijaanza.

  Anasema alipoenda Singida alishangiliwa sana na wananchi wakamwambia kama Kyela hawamtaki basi wao Singida wapo tayari kumpa ubunge.

  Kuna mengi mheshimiwa kaongea ambayo mpaka mtu unajikuna kichwa, hivi kweli ni muhimu? Labda ndio siasa zetu zilipofikia sasa. Inaelekea maneno ya Malecela hawajayasikia kabisa.

  Wenye taarifa zaidi mnaweza kuongea.
   
  Last edited by a moderator: Mar 30, 2009
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Mar 29, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..CCM sasa itabidi wachague kati ya Mwakyembe na Rostam.

  ..wakati wa kunyamazisha watu, na kutishana umepita.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,207
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe ananifurahisha sana. Maana tatizo la nchi yetu ni unafiki mkubwa wa kuwasikiliza watu kama akina Malecela na Chiligati ambao siku zote huweka mbele maslahi ya CCM kwanza badala ya yale ya nchi.

  I hope ataendelea kuongea maana tutayajua mengi ambayo tulikuwa hatuyajui. Hongera Mwakyembe Watanzania wengi tuko nyuma yako. Hata hapa jimbo la JF tunaweza kabisa kukupa ubunge maana tumechoshwa na unafiki na ufisadi uliojaa ndani ya nchi yetu.
   
 4. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2009
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I am just wondering how this will help a common mwananchi!

  Njimba
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,207
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe ni mtu makini sidhani kama alivurumisha matusi ya nguoni maana anajua athari yake, tusubiri habari zaidi.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,318
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  RA jamani ni fitina saana....nasikia hata elimu yake ni fake na ana uraia nchi 3....alianzia kutumwa tumwa deals za watu...hapa mjini nae akapata access a wanene wenye tamaa...wanaomkumbatia shauri yao....hongera Kyembe...
   
 7. E

  Engineer JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi ambazo nimezisikia hapa, nasema tetesi kwasababu siwaamini wanaozisema. Wanasema Dr. Mwakyembe anatafuta njia ya kuhamia CHADEMA.

  Wanasema kwenye mkutano wa leo yule kijana wa CHADEMA aliyewahi kuwekwa ndani wakati ule wa ziara ya JK ndiye alikuwa mbele katika waandaaji. Pia wanataja uhusiano wa Dr. Mwakyembe na Mbowe pamoja na Mengi kama sababu za kuamini hivyo.

  Pia inaelekea kuna mpambano mkali unaandaliwa Kyela 2010 kati ya Dr. Mwakyembe na jamaa mmoja nasikia yuko nje ya nchi.

  Mimi nilikuwa hapa kwa muda na niliyoyaona leo sina hamu, hii wilaya imegawanyika kweli kweli. Sikuona viongozi wowote wa CCM pale mbele badala yake kulikuwa na wapambe wa mheshimiwa waliokuwa wanamwaga sifa kibao.

  Angalieni hili jimbo 2010 inaelekea kutakuwa na vituko.
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,936
  Trophy Points: 280
  Ndio ukweli wenyewe, nadhani sasa ni MBWAI, MBWAI
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,207
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe kujiunga na CHADEMA sioni kama ni tatizo, lakini huu si wakati muafaka wa kufanya hivyo kama kweli ana nia ya kujiengua CCM. Kwa maoni yangu Mwakyembe ana nafasi nzuri zaidi ya kubaki CCM na kupambana na mafisadi akiwemo ndani ya chama hicho. Akiamua kuingia CHADEMA wakati huu basi CCM itammaliza kabisa kisiasa maana mashambulizi dhidi yake yatakuwa si ya kawaida lakini hawatakuwa tayari kumshambulia akiwemo ndani ya CCM.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa hali hii inaonesha Mwakyembe kaishiwa kisiasa.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mh! nna wasiwasi na hapa pia... au wana dini tofauti nini?
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,207
  Trophy Points: 280
  Anayesimama na kutetea maslahi ya nchi kaishiwa kisiasa, na yule anayesimama na kuweka maslahi ya CCM mbele badala ya yale ya nchi kama akina Chiligati na Malecela ndiyo wanaonekana wanasiasa wanaokubalika!!! Kazi kweli kweli!!!!
   
 13. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Huyu Mwakyembe ange concertrate tu kwenye kueleza ukweli pale ambapo anaona wananchi wamepotoshwa kuhusu yeye then awaachie watu wenyewe ndo wachague mchele toka kwenye pumba, kitendo cha kuendelea kumshambulia Rostam kwa mtazamo wangu kinamfanya aonekane yuko desperate kusafisha jina lake, na alimtuhumu RA kwa kutaka kjisafisha huku akiwachafua wenzie- he is doing exactly the same. Bado nakumbuka kamsemo ka Dr Slaa alikokatoa hapa kwamba "mwendawazimu akichukua nguo zako wakati unaoga mtoni na kukimbia, ukimkimbiza wote mtaishia kuonekana wendawazimu".
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Maneno ya Malecela hayana mpango.

  Alichofanya Mwakyembe, that's what's up.

  Whether yuko wrong or right, unajua anaposimama.Sio mambo ya kupeleka issues into our sissy parliament ambako yule bureaucrat Samwel Sitta ataya filter na kuya censor mpaka watu waitiwe kikao cha chama na kuamulia issue behind closed doors ambako hata muandishi wa habari hataruhusiwa.Tushachoka hayo, so 1989!.

  Mwakyembe ana michemsho fulani fulani hivi, mambo ya conflict of interest and all, lakini in the grand scheme of things Rostam ni fisadi kweli na Mwakyembe yuko sawa tu kum blast.

  Ningependa kuona mtu msafi zaidi ya Mwakyembe anam blast Rostam, lakini sasa hivi inaonekana mtu pekee mwenye balls ni huyu Mwakyembe.

  Mwacheni amblast Rostam tu.

  Halafu zaidi ya hapo, Mwakyembe anatoa statement kwa Malecela, mzee wewe ni old school, kaa pembeni, watu tunapaka tu hatujali vikao vya CCM wala bunge.

  Saafi sana.
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Nani anayemwandaa huyu jamaa ama jamaa anajiandaa mwenyewe
   
 16. E

  Engineer JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama atahama CCM sasa, kinachosemwa ni kwamba akishindwa 2010 huko jimboni kwake atahamia CHADEMA kwa kisingizio kwamba mafisadi wamefanya mipango ili yeye aangushwe. Hiyo ndio strategy ya Dr. Mwakyembe kwasasa. Na jinsi leo alivyokuwa anaongea, napata hisia kwamba huenda mtaji wa Dr. kwa mwaka 2010 ni vita dhidi ya ufisadi.

  Tatizo linaweza kutokea pale atakapokuja mtu mwingine ambaye hana uhusiano na mafisadi. Kuna mfanyabiashara mmoja aliashaanza kujitangaza kugombea, nasikia ana uhusiano na akina Lowassa na pia hana elimu kubwa. Alikuwa amefit vizuri kwenye huo mtego wa Dr. Mwakyembe. Ghafla upepo umebadilika, sasa kuna watu wengine wanatajwa wakiwemo ambao walimwunga mkono Dr. hiyo 2005. Hapo ndipo kazi inaanza kuwa ngumu na pressure kupanda.

  Hawa CCM watamalizana kweli 2010.
   
 17. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mbona huyo jamaa hajawahi kufanya kazi bongo sasa Mwakyembe mchecheto wa nini?
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Mar 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kana -Ka-Nsugu,
  Mkuu wangu katika siasa siku zote ni Offense tu usitake kujisafisha hata siku moja mahala ambapo huna ulazima kwa sababu watu wanakufahamu vizuri zaidi ya unavyofikiria..DUkiwa defensive mara nyingi unaacha mwanya wa watu kukushambulia na mara nyingi unaweza fanya kosa ambalo hukulitegemea litatafsirika vibaya... ikitoka imetoka mkuu wangu.
  Mwakyembe kwa kila hali mgonvi wake ni Rostam na kisiasa inatakiwa amvurugevuruge hadi wananchi waamini kile anachowakilisha. hayupo pale kujiwakilisha/kujisafisha yeye bali kulinda maslahi ya wananchi na jinsi gani wananchi wajihadhari na watu kama Rostam..
  Nimefurahi sana kuona usiri wa huyu Rostam unaanza kutoka kwani watu wengi wanampa heshima na kumwogopa wakifikiria ni Kichwa fulani hivi.. huyu kajaliwa tu Mifedha na Personality ambayo kwa namna fulani ni tishio la walalahoi..
   
 19. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Sio popcorn tena sasa inabidi kupata kikombe cha kahawa tena Cappuccino maana ngoma ishaanza kunoga. Tusubiri RA kama sio wapambe wake sasa. Lazima watarusha kombora tu!

  Whistling!!!
   
 20. M

  Mundu JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mwakyembe na apumzike tu.. hana haja ya kumblast zaidi RA. Sote tunajua kuwa Rostam ni fisadi namba wani Tanzania.There is an Engish saying 'never argue with a fool' cause people might not notice the difference.

  Sasa anapaswa kutueleza yale ambayo hakuyasema kwenye kamati ya Bunge ya Richmond. Ya Rostam tunayajua Mh. Mwakyembe
   
Loading...