Kuna kipindi sisi wanaume huwa tunajipalilia maanguko yetu sisi wenyewe. Haijalishi umempenda mtu kiasi gani, ikifikia wakati upendo ukaisha ni busara kukubali kuachia na maisha yaendelee.
Kupitia hili sakata la Mwaka na mke wake, Mwaka anaweza akahisi ameshinda, ila daima mwanamke sio wa kumfanya adui yako, hasa mwanamke ambae anajua undani wako.
Bila kujua Mwaka anapigwa laana na machozi ya mkewe, watoto wake na hata watu wengine wanaouguswa na haya mambo.
Sio kwa kuwa biased, ila Mwaka ana kila traits za Sadisit (mtu anaepata faraja katika maumivu ya wengine) na hili halitamalizika vyema kwake.