Dr. Mpango (Waziri wa Fedha), huu ni mchango wangu kwenye Bajeti Kuu ya Serikali

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,176
25,446
Inajulikana kuwa mimi si Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ningekuwa Bungeni, labda ningeutoa mchango wangu huu kwa kuusema au kuuandika na kukufikishia humohumo Bungeni. Nikuombe uupitie mchango wangu huu ninaouweka humu JF kwakuwa ndiyo njia pekee ninayoweza kukufikishia.

Nakuomba, mwanzo mwanzoni, tukubaliane kuwa Bajeti kama ulivyoiwasilisha jana inahitaji uelewa mpana katika kuielewa, kuichambua, kuipitisha na kuitekeleza. Kwa sisi tuliobahatika kupata elimu ya kutosha, tumeisikia Bajeti na tunaendelea kuichambua mitandaoni, vijiweni na kadhalika. Wachambuzi ni sisi wenyewe wenye uelewa wa hiyo Bajeti.

Mhe. Waziri, watanzania walio wengi hawaelewi maana halisi ya Bajeti ya Serikali, yaani matumizi yake, uzuri wake na hata ubaya wake. Hii inatokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kuzichambua nyaraka za kibajeti. Wananchi hawa walio wengi wanayajua tu maisha yao ya kila siku na wanaendelea nayo.

Mhe. Waziri, itoshe kusema kuwa Bajeti ya Serikali inapaswa kuakisi maisha halisi ya watanzania. Inapaswa kupunguza au kumaliza matatizo sugu ya kimaisha yanayowakabili mfano kudhibiti mfumuko wa bei hasa za chakula; ukosefu au upungufu wa miundombinu, masoko ya mazao yao, pembejeo, mikopo kwa watoto wao kusoma, ajira kwa vijana na tegemezi wao na kadhalika.

Mambo hayo yanapaswa kuakisiwa na Bajeti ya Serikali. Ni mbali sana kwao kuelewa umuhimu wa ndege au road licence. Ni ngumu na mbali sana kwao kujua mrabaha katika madini na tozo mbalimbali kwa wawekezaji na wafanyabishara. Hayo ni mambo ya juu sana kwao. Hayo ni mambo wanayoyahitaji baada ya yale ya muhimu: chakula, malazi na makazi.

Hoja yangu ni kuwa, pamoja na nyaraka zote za kibajeti na makofi ya kutosha Bungeni, Bajeti inapaswa kubadili kwa namna ya kuboresha maisha ya watanzania. Kila la heri Mhe. Waziri katika kuitetea na kuisimamia Bajeti ya Serikali. Cheers!
 
Ni vigumu sana Bajeti ndiyo Kwanza imekuwa tabled jana tu halafu leo kila Mtu akaanza kutiririka na kuserereka nayo wakati hata hao wenyewe tu ( Wabunge / MP's ) wamepewa siku mbili tatu za kuipitia taratibu na kiumakini kabisa ili Jumatatu ijayo wakianza kuijadili wajue wanajadili nini na siyo kupayuka payuka ( Wakwere wanasema Kuzoza ) kama wengine. Kitu cha almost dakika 125 kinahitaji umakini mkubwa kukikabili ili usionekane Kituko cha msimu na Wadau.
 
Tunao mfano tayari wa bajeti hewa ya 2016/2017 ambayo ilikuwa 29 trillions lakini pesa iliyotolewa ni 34% tu. Hii ya 2017/2018 ni 31.6 trillions na tayari imeshatamkwa kwamba karibu 10 trillions zitalipa deni la Taifa na pia kutokana na hali mbaya ya uchumi nchini mapato ya Serikali yataendelea kushuka na hivyo bajeti hii nayo kuwa hewa, lakini Serikali haitasema hili la bajeti hewa itaficha ukweli halisi kama kawaida yake. HAPA NI MAJANGA TU!

kinya09062017.jpg
 
Mkuu BAK Nakushukuru kwa kumaliza kila kitu hapo kwenye comment yako.
Bajeti ya mwaka huu ni Hewa zaidi ya mwaka uliopita.
 
Inajulikana kuwa mimi si Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ningekuwa Bungeni, labda ningeutoa mchango wangu huu kwa kuusema au kuuandika na kukufikishia humohumo Bungeni. Nikuombe uupitie mchango wangu huu ninaouweka humu JF kwakuwa ndiyo njia pekee ninayoweza kukufikishia.

Nakuomba, mwanzo mwanzoni, tukubaliane kuwa Bajeti kama ulivyoiwasilisha jana inahitaji uelewa mpana katika kuielewa, kuichambua, kuipitisha na kuitekeleza. Kwa sisi tuliobahatika kupata elimu ya kutosha, tumeisikia Bajeti na tunaendelea kuichambua mitandaoni, vijiweni na kadhalika. Wachambuzi ni sisi wenyewe wenye uelewa wa hiyo Bajeti.

Mhe. Waziri, watanzania walio wengi hawaelewi maana halisi ya Bajeti ya Serikali, yaani matumizi yake, uzuri wake na hata ubaya wake. Hii inatokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kuzichambua nyaraka za kibajeti. Wananchi hawa walio wengi wanayajua tu maisha yao ya kila siku na wanaendelea nayo.

Mhe. Waziri, itoshe kusema kuwa Bajeti ya Serikali inapaswa kuakisi maisha halisi ya watanzania. Inapaswa kupunguza au kumaliza matatizo sugu ya kimaisha yanayowakabili mfano kudhibiti mfumuko wa bei hasa za chakula; ukosefu au upungufu wa miundombinu, masoko ya mazao yao, pembejeo, mikopo kwa watoto wao kusoma, ajira kwa vijana na tegemezi wao na kadhalika.

Mambo hayo yanapaswa kuakisiwa na Bajeti ya Serikali. Ni mbali sana kwao kuelewa umuhimu wa ndege au road licence. Ni ngumu na mbali sana kwao kujua mrabaha katika madini na tozo mbalimbali kwa wawekezaji na wafanyabishara. Hayo ni mambo ya juu sana kwao. Hayo ni mambo wanayoyahitaji baada ya yale ya muhimu: chakula, malazi na makazi.

Hoja yangu ni kuwa, pamoja na nyaraka zote za kibajeti na makofi ya kutosha Bungeni, Bajeti inapaswa kubadili kwa namna ya kuboresha maisha ya watanzania. Kila la heri Mhe. Waziri katika kuitetea na kuisimamia Bajeti ya Serikali. Cheers!

Wewe ni mwanasheria uko chuo kikuu cha dar es salaamn bajeti inasema kipaumbele kikubwa kimojawapo ni kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu je hilo haliwapi unafuu wa maisha watanzania wanafunzi walioko vyuo vikuu? Na je haliwapi unafuu wazazi ambao watoto wao wamepata mikopo?

Hii bajeti umeisoma kwa mtizamo wa chama chako cha chadema badala ya kuangalia kama msomi na kuangalia vipengele vya eneo ulipo kama liko covered kwenye bajeti. Unapojadili bajeti hata kama ya chuo chako kama upeo wako Mdogo basi walau angalia eneo lako.

Ninachokiona kwako unataka kujadili bajeti Ya nchi wakati hata ya kijiji chako hapo ulipo chuo kikuu hujui kitu
 
Wewe ni mwanasheria uko chuo kikuu cha dar es salaamn bajeti inasema kipaumbele kikubwa kimojawapo ni kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu je hilo haliwapi unafuu wa maisha watanzania wanafunzi walioko vyuo vikuu? Na je haliwapi unafuu wazazi ambao watoto wao wamepata mikopo? Hii bajeti umeisoma kwa mtizamo wa chama chako cha chadema badala ya kuangalia kama msomi na kuangalia vipengele vya eneo ulipo kama liko covered kwenye bajeti. Unapojadili bajeti hata kama ya chuo chako kama upeo wako Mdogo basi walau angalia eneo lako. Ninachokiona kwako unataka kujadili bajeti Ya nchi wakati hata ya kijiji chako hapo ulipo chuo kikuu hujui kitu
Kwanza, muache kunihusisha na uanachama wa vyama vyenu. Si kila mmoja wetu humu ana chama. Pili, mimi nimetoa mawazo yangu ya ujumla kwa Waziri, nawe toa yako. Tatu, huna uwezo wowote wa kunikosoa kwa hoja ninapojenga hoja, utaishia kucomment kwa kejeli kama ulivyofanya tu. Nne, acha U-fa fa fa fa fa fa, Ph.D. Candidate hapaswi kuwa hivyo.
 
Inajulikana kuwa mimi si Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ningekuwa Bungeni, labda ningeutoa mchango wangu huu kwa kuusema au kuuandika na kukufikishia humohumo Bungeni. Nikuombe uupitie mchango wangu huu ninaouweka humu JF kwakuwa ndiyo njia pekee ninayoweza kukufikishia.

Nakuomba, mwanzo mwanzoni, tukubaliane kuwa Bajeti kama ulivyoiwasilisha jana inahitaji uelewa mpana katika kuielewa, kuichambua, kuipitisha na kuitekeleza. Kwa sisi tuliobahatika kupata elimu ya kutosha, tumeisikia Bajeti na tunaendelea kuichambua mitandaoni, vijiweni na kadhalika. Wachambuzi ni sisi wenyewe wenye uelewa wa hiyo Bajeti.

Mhe. Waziri, watanzania walio wengi hawaelewi maana halisi ya Bajeti ya Serikali, yaani matumizi yake, uzuri wake na hata ubaya wake. Hii inatokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kuzichambua nyaraka za kibajeti. Wananchi hawa walio wengi wanayajua tu maisha yao ya kila siku na wanaendelea nayo.

Mhe. Waziri, itoshe kusema kuwa Bajeti ya Serikali inapaswa kuakisi maisha halisi ya watanzania. Inapaswa kupunguza au kumaliza matatizo sugu ya kimaisha yanayowakabili mfano kudhibiti mfumuko wa bei hasa za chakula; ukosefu au upungufu wa miundombinu, masoko ya mazao yao, pembejeo, mikopo kwa watoto wao kusoma, ajira kwa vijana na tegemezi wao na kadhalika.

Mambo hayo yanapaswa kuakisiwa na Bajeti ya Serikali. Ni mbali sana kwao kuelewa umuhimu wa ndege au road licence. Ni ngumu na mbali sana kwao kujua mrabaha katika madini na tozo mbalimbali kwa wawekezaji na wafanyabishara. Hayo ni mambo ya juu sana kwao. Hayo ni mambo wanayoyahitaji baada ya yale ya muhimu: chakula, malazi na makazi.

Hoja yangu ni kuwa, pamoja na nyaraka zote za kibajeti na makofi ya kutosha Bungeni, Bajeti inapaswa kubadili kwa namna ya kuboresha maisha ya watanzania. Kila la heri Mhe. Waziri katika kuitetea na kuisimamia Bajeti ya Serikali. Cheers!
Ulitaka nini kiwekwe basi ili uone bajeti inaakisi maisha?
 
Ni vigumu sana Bajeti ndiyo Kwanza imekuwa tabled jana tu halafu leo kila Mtu akaanza kutiririka na kuserereka nayo wakati hata hao wenyewe tu ( Wabunge / MP's ) wamepewa siku mbili tatu za kuipitia taratibu na kiumakini kabisa ili Jumatatu ijayo wakianza kuijadili wajue wanajadili nini na siyo kupayuka payuka ( Wakwere wanasema Kuzoza ) kama wengine. Kitu cha almost dakika 125 kinahitaji umakini mkubwa kukikabili ili usionekane Kituko cha msimu na Wadau.
Mmmmh sasa mbona kusomwa tu Jana spika na Wabunge wa ccm walishangilia mpaka wakainuka kwenye viti kwa mbwembwe kibao!
Nini kilitokea? Najiuliza mpaka leo sipati jibu mkuu
 
Ni vigumu sana Bajeti ndiyo Kwanza imekuwa tabled jana tu halafu leo kila Mtu akaanza kutiririka na kuserereka nayo wakati hata hao wenyewe tu ( Wabunge / MP's ) wamepewa siku mbili tatu za kuipitia taratibu na kiumakini kabisa ili Jumatatu ijayo wakianza kuijadili wajue wanajadili nini na siyo kupayuka payuka ( Wakwere wanasema Kuzoza ) kama wengine. Kitu cha almost dakika 125 kinahitaji umakini mkubwa kukikabili ili usionekane Kituko cha msimu na Wadau.
Uelewa unapishana. Mtoa thread keshaelewa na kutoa maoni. Yuko sahihi.
 
Petro Mselekwa katoa maoni yake na kwa kutumia usomi wake, tatizo watanzania ushabiki wa vyama, ingependeza kila mtu akatoa maoni na ushauri kama aonavyo Petro!
Hilo moja,

Nakubariana na Petro kuwa Bajeti inahitaji uelewa mpana katika kuichambua, napata shida sana kwa jinsi waheshimiwa wabunge pamoja na kiranja wao Mh Spika kushangilia na kusimama pamoja na kutaka waziri Mpango asiendelee kuisoma maana imeeleweka na kuzidi kupigilia kwamba haijawahi kutokea!!!!

Sijaelewa maana yake, ngoja tusubiri jumatatu labda kwa mchango wa mbunge mmoja mmoja tutaona kama ilieleweka zaidi.
 
Mkuu, uko sahihi. Lakini, naitwa Petro E. Mselewa na si Petro Mselekwa. Asante
 
Wewe ni mwanasheria uko chuo kikuu cha dar es salaamn bajeti inasema kipaumbele kikubwa kimojawapo ni kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu je hilo haliwapi unafuu wa maisha watanzania wanafunzi walioko vyuo vikuu? Na je haliwapi unafuu wazazi ambao watoto wao wamepata mikopo? Hii bajeti umeisoma kwa mtizamo wa chama chako cha chadema badala ya kuangalia kama msomi na kuangalia vipengele vya eneo ulipo kama liko covered kwenye bajeti. Unapojadili bajeti hata kama ya chuo chako kama upeo wako Mdogo basi walau angalia eneo lako. Ninachokiona kwako unataka kujadili bajeti Ya nchi wakati hata ya kijiji chako hapo ulipo chuo kikuu hujui kitu

Hivi ni wakati gani huwa unafikiri sawasawa? Unapovhangia hoja acha kufanya comparisons kati ya hoja na mleta hoja pamoja na mazingira anamoishi na hata Elimu na kazi yake kwani ni kuwavunja moyo na wewe kuonekana upon kimaslahi humu!

Heshimu mchango na acha hizo person attacks zisizotusaidia humu. Na kama umetumwa kuwafukuza wengine humu kwa kuwa mwiba wa waliokutuma ili mbaki wenyewe semeni tuwapishe!
 
Wewe ni mwanasheria uko chuo kikuu cha dar es salaamn bajeti inasema kipaumbele kikubwa kimojawapo ni kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu je hilo haliwapi unafuu wa maisha watanzania wanafunzi walioko vyuo vikuu? Na je haliwapi unafuu wazazi ambao watoto wao wamepata mikopo? Hii bajeti umeisoma kwa mtizamo wa chama chako cha chadema badala ya kuangalia kama msomi na kuangalia vipengele vya eneo ulipo kama liko covered kwenye bajeti. Unapojadili bajeti hata kama ya chuo chako kama upeo wako Mdogo basi walau angalia eneo lako. Ninachokiona kwako unataka kujadili bajeti Ya nchi wakati hata ya kijiji chako hapo ulipo chuo kikuu hujui kitu
Awamu hii hamtaki kuona mtu akikosoa,mleta mada angesifia bajeti nzima ungempa likes za kitosha,ila kwakuwa kakosoa ushamvika na uanachama wa CDM juu
 
Yaani vijana wa CCM wana mambo sana. Kila mmoja wanamuona CHADEMA. Who is CHADEMA to take in all of us?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom