Dr. Mpango (Waziri wa Fedha), huu ni mchango wangu kwenye Bajeti Kuu ya Serikali

Inajulikana kuwa mimi si Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ningekuwa Bungeni, labda ningeutoa mchango wangu huu kwa kuusema au kuuandika na kukufikishia humohumo Bungeni. Nikuombe uupitie mchango wangu huu ninaouweka humu JF kwakuwa ndiyo njia pekee ninayoweza kukufikishia.

Nakuomba, mwanzo mwanzoni, tukubaliane kuwa Bajeti kama ulivyoiwasilisha jana inahitaji uelewa mpana katika kuielewa, kuichambua, kuipitisha na kuitekeleza. Kwa sisi tuliobahatika kupata elimu ya kutosha, tumeisikia Bajeti na tunaendelea kuichambua mitandaoni, vijiweni na kadhalika. Wachambuzi ni sisi wenyewe wenye uelewa wa hiyo Bajeti.

Mhe. Waziri, watanzania walio wengi hawaelewi maana halisi ya Bajeti ya Serikali, yaani matumizi yake, uzuri wake na hata ubaya wake. Hii inatokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kuzichambua nyaraka za kibajeti. Wananchi hawa walio wengi wanayajua tu maisha yao ya kila siku na wanaendelea nayo.

Mhe. Waziri, itoshe kusema kuwa Bajeti ya Serikali inapaswa kuakisi maisha halisi ya watanzania. Inapaswa kupunguza au kumaliza matatizo sugu ya kimaisha yanayowakabili mfano kudhibiti mfumuko wa bei hasa za chakula; ukosefu au upungufu wa miundombinu, masoko ya mazao yao, pembejeo, mikopo kwa watoto wao kusoma, ajira kwa vijana na tegemezi wao na kadhalika.

Mambo hayo yanapaswa kuakisiwa na Bajeti ya Serikali. Ni mbali sana kwao kuelewa umuhimu wa ndege au road licence. Ni ngumu na mbali sana kwao kujua mrabaha katika madini na tozo mbalimbali kwa wawekezaji na wafanyabishara. Hayo ni mambo ya juu sana kwao. Hayo ni mambo wanayoyahitaji baada ya yale ya muhimu: chakula, malazi na makazi.

Hoja yangu ni kuwa, pamoja na nyaraka zote za kibajeti na makofi ya kutosha Bungeni, Bajeti inapaswa kubadili kwa namna ya kuboresha maisha ya watanzania. Kila la heri Mhe. Waziri katika kuitetea na kuisimamia Bajeti ya Serikali. Cheers!


Kama hujasoma uchumi, na mchango/mawazo yako yanadhihirisha hivyo, huwezi na wala hukusudiwa kujadili bajeti bali kuipokea.

Kwa mfano hayo unayoyaita mapungufu, tayari yamo na bajeti imabainisha namna ya kuyatafutia ufumbuzi. inasikitisha kuwa wewe umeshindwa kuyaona.

Ni kwa sababu wewe siyo mchumi; lakini una muda wa kutosha kujiendeleza kusoma na kuhitimu uchumi.
 
Ningepata nafasi ningeishauli selekali ipunguze bei kwenye bandali zetu kwasababu tunazo nyingi kutoka asilimia ishilini na tano mpaka saba tu nafikili tungepata faida kubwa pia vijana wengi tungepata ajira kwenye maloli
 
hivi huyu ni lecture au anakazi gani hapo mlimani? harufu zote za vyeti feki, ulihakikiwa mzee kweli?
 
hivi ni wakati gani huwa unafikiri sawasawa? Unapovhangia hoja acha kufanya comparisons kati ya hoja na mleta hoja pamoja na mazingira anamoishi na hata Elimu na kazi yake kwani ni kuwavunja moyo na wewe kuonekana upon kimaslahi humu! Heshimu mchango na acha hizo person attacks zisizotusaidia humu. Na kama umetumwa kuwafukuza wengine humu kwa kuwa mwiba wa waliokutuma ili mbaki wenyewe semeni tuwapishe!
Hotelini huwezi tofautisha mhudumu na huduma anayokupa chukulia hoteli inayopika Hotel Chakula First Class duniani lakini mhudumu anayekuletea chakula ni mchafu kajinyea inzi wanamfuata utakula hicho chakula First Class? Mhudumu lazima ajadiliwe si kujali tu chakula anacholeta kuwa achana na mhudumu jali chakula tu
 
hivi huyu ni lecture au anakazi gani hapo mlimani? harufu zote za vyeti feki, ulihakikiwa mzee kweli?
Ni legal officer sijui kama ana uwezo mkubwa kutetea chuo kikuu wakiwa Na kesi naona kama uwezo wake ni Mdogo mno
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Kama hujasoma uchumi, na mchango/mawazo yako yanadhihirisha hivyo, huwezi na wala hukusudiwa kujadili bajeti bali kuipokea. Kwa mfano hayo unayoyaita mapungufu, tayari yamo na bajeti imabainisha namna ya kuyatafutia ufumbuzi. inasikitisha kuwa wewe umeshindwa kuyaona. Ni kwa sababu wewe siyo mchumi; lakini una muda wa kutosha kujiendeleza kusoma na kuhitimu uchumi.

Nakubariana kutokubariana na mawazo yako,
Kama hivyo ndivyo ilivyo kwamba bajeti ijadiliwe na wachumi tu,
Swali kwako,

Kwa nini sasa bajeti hiyo imesomwa bungeni ambamo zaidi ya nusu hawajui uchumi na baadhi yao hata kidato kimoja hawajagusa, ina maana hawaruhusiwi hata kuijadiri?
asante...
 
Hotelini huwezi tofautisha mhudumu na huduma anayokupa chukulia hoteli inayopika Hotel Chakula First Class duniani lakini mhudumu anayekuletea chakula ni mchafu kajinyea inzi wanamfuata utakula hicho chakula First Class? Mhudumu lazima ajadiliwe si kujali tu chakula anacholeta kuwa achana na mhudumu jali chakula tu
Mkuu, hakuna hoteli uliyoisema dunia nzima.
 
Nakubariana kutokubariana na mawazo yako,
Kama hivyo ndivyo ilivyo kwamba bajeti ijadiliwe na wachumi tu,
Swali kwako,
Kwa nini sasa bajeti hiyo imesomwa bungeni ambamo zaidi ya nusu hawajui uchumi na baadhi yao hata kidato kimoja hawajagusa, ina maana hawaruhusiwi hata kuijadiri?
asante...
Mkuu, huyo hana hoja. Anazungumzia Wachumi wakati kuna Wabunge darasa la saba na ndio watakaoijadili na kuipitisha!? Inachekesha
 
Dada nakuheshimu, nawe niheshimu. Kwanza, muache kunihusisha na uanachama wa vyama vyenu. Si kila mmoja wetu humu ana chama. Pili, mimi nimetoa mawazo yangu ya ujumla kwa Waziri, nawe toa yako. Tatu, huna uwezo wowote wa kunikosoa kwa hoja ninapojenga hoja, utaishia kucomment kwa kejeli kama ulivyofanya tu. Nne, acha U-fa fa fa fa fa fa, Ph.D. Candidate hapaswi kuwa hivyo.


Tano nakupongeza kwa kumjibu vizuri ila ukaharibu point ya 4 pale ambapo na wewe umepanic ukajishusha hadhi kwa kutaka kulipiza kwa matusi mkuu.

Point 1-3 zillikuwa zimetosha, ulipoweka ya 4 na wewe umejishusha hadhi kwa kukaribisha hasira za haraka haraka kwa hoja muhimu, hvyo hamna utofauti.
 
Kujadili hatima yako usisubiri mbunge dada cocochanel.....
Bajeti ya nchi ni dira yetu kwa kipindi cha mwaka, wabunge wana nafasi yao na sisi kujadili ni sawa kabisa.

Labda mimi mwenyeji kwenye haya, huu mchango wa humu utapokelewa na Waziri au Wabunge? Na je ikitokea hawajasoma humu inakuwaje? Hakuna njia zingine za kumfikishia ujumbe?
 
Back
Top Bottom