Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,857
Inajulikana kuwa mimi si Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ningekuwa Bungeni, labda ningeutoa mchango wangu huu kwa kuusema au kuuandika na kukufikishia humohumo Bungeni. Nikuombe uupitie mchango wangu huu ninaouweka humu JF kwakuwa ndiyo njia pekee ninayoweza kukufikishia.
Nakuomba, mwanzo mwanzoni, tukubaliane kuwa Bajeti kama ulivyoiwasilisha jana inahitaji uelewa mpana katika kuielewa, kuichambua, kuipitisha na kuitekeleza. Kwa sisi tuliobahatika kupata elimu ya kutosha, tumeisikia Bajeti na tunaendelea kuichambua mitandaoni, vijiweni na kadhalika. Wachambuzi ni sisi wenyewe wenye uelewa wa hiyo Bajeti.
Mhe. Waziri, watanzania walio wengi hawaelewi maana halisi ya Bajeti ya Serikali, yaani matumizi yake, uzuri wake na hata ubaya wake. Hii inatokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kuzichambua nyaraka za kibajeti. Wananchi hawa walio wengi wanayajua tu maisha yao ya kila siku na wanaendelea nayo.
Mhe. Waziri, itoshe kusema kuwa Bajeti ya Serikali inapaswa kuakisi maisha halisi ya watanzania. Inapaswa kupunguza au kumaliza matatizo sugu ya kimaisha yanayowakabili mfano kudhibiti mfumuko wa bei hasa za chakula; ukosefu au upungufu wa miundombinu, masoko ya mazao yao, pembejeo, mikopo kwa watoto wao kusoma, ajira kwa vijana na tegemezi wao na kadhalika.
Mambo hayo yanapaswa kuakisiwa na Bajeti ya Serikali. Ni mbali sana kwao kuelewa umuhimu wa ndege au road licence. Ni ngumu na mbali sana kwao kujua mrabaha katika madini na tozo mbalimbali kwa wawekezaji na wafanyabishara. Hayo ni mambo ya juu sana kwao. Hayo ni mambo wanayoyahitaji baada ya yale ya muhimu: chakula, malazi na makazi.
Hoja yangu ni kuwa, pamoja na nyaraka zote za kibajeti na makofi ya kutosha Bungeni, Bajeti inapaswa kubadili kwa namna ya kuboresha maisha ya watanzania. Kila la heri Mhe. Waziri katika kuitetea na kuisimamia Bajeti ya Serikali. Cheers!