Dr. Mpango: Kufungwa kwa biashara nchini ni jambo la kawaida!

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
2,087
2,193
Wakati akiwasilisha
bajeti,waziri wa fedha Dr
Phili Mpango alitetea kasi
ya kufungwa kwa
biashara nchini kwa
kusema hilo ni jambo la
kawaida!
Dr Mpango ambaye ni
mchumi mwandamizi na
mbobezi,alitetea hoja
yake kwa kusema hata
mataifa ya ulaya yaliwahi
kukutwa na changamoto
kama hizi ambapo uchumi
wao uliyumba kati ya
mwaka 1929-1939 na
kuitwa The great
depression pamoja na
kusinyaa kwa biashara
huko China Mwaka 1980.
Dr Mpango alitumia kigezo
cha The Great depression
kuwataka watanzania
wasiwe na hofu na
ufungwaji huu wa
biashara!.
Dr Mpango anataka
kutuamijisha kuwa
mataifa ya Ulaya
hayakushtushwa na
mporomoko huo wa
Uchumi?chanzo na
madhara ya Great
depression hayahitaji
kuwa umesoma uchumi ili
kuyajua!.
Ina maana Dr Mpango
haoni shida uchumi
ukiseleleka kwenda
kwenye depression?nili
dhani Dr Mpango
akiwaeleza watanzania
tunafanyaje ili kurudi
kwenye recovering stage?
kwa maelezo ya Dr
Mpango uchumi wetu
unaelekea kutoka kwenye
recession stage na
unaelekea kwenye
depression ndiyo maana
akatumia mfano wa The
Great Depression?
kuhusu kusinyaa huku
kwa biashara,Dr Mpango
alisema tuangalie upande
wa pili ambapo serikali
imesajili biashara mpya
zaidi ya laki mbili,hii ni
kweli kabisa lakini hizi ni
biashara zilizosajiliwa na
bado hazijaanza kufanya
kazi,wala hazina mchago
wowote!.
Mwaka huu wa fedha
unaokwisha
tumeshuhudia jinsi serikali
iliyopata mapato kidogo
kutoka serikali za mitaa
makadirio yalikuwa kama
Bilioni 600 ,serikali
ikakusanya kama bilioni
mia 3.9 sawa na asilimia
60 ya ilichopanga!.
Kuna ukweli watu
hawataki kuusema lakini
ni kilio kikubwa huku
mtaani,Sekta binafsi ipo
nusu kaputi,inaelekea
kufa,uwezo wa sekta
binafsi unadhoofu kila
kukicha na serikali haioni
kama hli ni tatizo,tunabaki
kuambiana historia ya The
Great depression ambayo
mazingira yake
hayafanani hata kidogo na
mazingira ya Tanzania!.
Kazi ya serikali ni
kuziamsha sekta binafsi ili
ziisaidie serikali kukuza
uchumi,uwezo wa sekta
binafsi kuajiri,kulipa
mshahara wafanyakazi
wake umeshuka kwa zaidi
ya asilimia 80,bahati
mbaya hili hatutaki
kulitafutia suluhisho,kwa
hali hii tunakoenda siuo
kuzuri,tuache kutoa
historia ya The Great
depression na kuifanya
kama jambo jema,sekta
binafsi inasinyaa!.
Uwezo wa serikali kwa
sasa hata kwenye sekta
zake unahitaji mjadala wa
pamoja kwa wachumi na
wataalam wa masuala ya
sera za maendeleo,kasi ya
kuajiri toka serikali ya Rais
Magufuli iingie
madarakani
imeshuka,tuna kundi
kubwa la vijana wapo
mitaani wakiwa na
shahada zao mkononi!
Serikali haitaki
kuajiri,sekta binafsi
zinakufa,sera za mikopo
kutoka kwenye taasisi za
fedha si rafiki kwa vijana
hawa wahitimu wa vyuo
na vyuo vikuu,hawana tu
pa kuzungumza na
hawana pia wa
kuwazungumzia kwa
sababu wawakilishi wao
wanasaka huruma ya
serikali waondokewe ada
ya magari yao
waliyoyapaki!.
Rafiki yangu mmoja wa
Chuo kikuu kimoja
kikubwa cha serikali
ameniambia namnukuu
"kaka hapa chuoni kwetu
hali si nzuri,chuo hakina
mpaka pesa za gharama
za Dessertation kwa ajili
ya external readers,tafiti
za wanafunzi wa shahada
ya pili na wale Phd,zipo
tu,chuo hakina pesa,hata
pesa ya kodi ya
makazi,sasa haiji".
Serikali ifahamu,sekta
binafsi ilisinyaa ni
mtikisiko mkubwa
sana,hizo Bil 31,ambazo
serikali inazitafuta bila
kuwa na sekta binafsi
imara hatutaweza
kuzipata!.
Tunaona jinsi nchi
wafadhiri zinzvyotoa pesa
kidogo kwenye bajeti
yetu,dola milioni
500,tunazisaka mpaka leo
hatujapewa na wahisani
tena kama
mkopo,nimesikia Serikali
ya Ujerumani inatazama
upya mahusiano yake na
serikali zetu za Afrika
mashariki kutokana na
kauli za viongozi wetu!.
Tutake tusitake,lazima
tuhakikishe sekta binafsi
inakuwa imara,bila sekta
binafsi imara,tutayumba!
Tunapojadili masuala haya
ya uchumi,tusijitazame sisi
peke yetu,tusitazame
kundi dogo,tuwatazame
watanzania kwa ujumla
wao!.
 
Dr Mpango ambaye ni mchumi mwandamizi na mbobezi,alitetea hoja yake kwa kusema hata mataifa ya ulaya yaliwahi kukutwa na changamoto kama hizi ambapo uchumi wao uliyumba kati ya mwaka 1929-1939 na kuitwa The great depression pamoja na kusinyaa kwa biashara huko China Mwaka 1980. Dr Mpango alitumia kigezo cha The Great depression kuwataka watanzania wasiwe na hofu naufungwaji huu wa biashara!
Hivi wale wafuasi wanaoamini kila kitu kipo sawa wamemuelewa vizuri Dk. Mpango hapo juu?! Binafsi nilipomsikia Dk Mpango akisoma hicho kipengele nilishituka sana sema nikakausha!!! Nilishituka si kwa sababu sikufahamu bali nilishituka kuona Waziri mwenye dhamana anakiri hadharani kwamba hali si shwari na hivyo kupelekea ufungwaji wa biashara!!!

Enzi zile ilikuwa tukisema wale wenzangu na mimi walikuwa wanadai hao wanaofunga biashara ni wakwepa kodi!!!! Lakini hata sasa usishangae wakitokea wengine wakasema "biashara zilizofungwa ni chache sana ukilinganisha na zile zilizofunguliwa" as if hizo zilizofunguliwa zimefunguliwa kwa sababu tu kuna zile zilizofungwa!
 
[HASHTAG]#chige[/HASHTAG]
yaan tz tunasafari ndefu sana. Ngoja tuendelee kushuhudia hizi jokes
 
Ile kauli ya Tanzania inaweza kujiendesha yenyewe bila hata wahisani ilipotelea wapi?
 
Back
Top Bottom