Dr. Mpango anajichanganya kuhusu nafasi ya miundombinu katika hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2019

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
Heri ya mwaka mpya, 2020 wana JF.

Ukisoma kipengele cha 1.1(Ukuaji wa Pato la Taifa) katika taarifa ya wizara ya fedha kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2019, iliyotolewa na waziri Dr. Mpango utaona miundombinu ikitajwa kuwa ni moja ya sababu ya kukuwa kwa pato la taifa kama ifuatavyo.

"Katika kipindi cha Januari–Juni 2019, Pato la Taifa lilikua kwa 6.9% ikilinganishwa na 6.8% katika kipindi kama hicho mwaka 2018.  Ukuaji huu ulichochewa zaidi na kuongezeka kwa uwekezaji, hasa katika miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege; kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini hasa dhahabu & makaa ya mawe; na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo..."

Lakini utashangaa katika kipengele cha 1.3 (Mfumuko wa Bei) usafirishaji umeoneshwa kuwa ni changamoto.

Mfumuko wa bei wa chakula uliongezeka kufikia wastani wa asilimia 6.7 Novemba 2019, ikilinganishwa na asilimia 2.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Ongezeko hili lilitokana na:  changamoto za usafirishaji, miundombinu ya masoko, maghala na ugavi wa bidhaa za vyakula kimaeneo."

Sasa hapo tueleweje kuhusu hali ya miundombinu ya usafirishaji; imeboreshwa na kutoa mchango chanya katika ukuaji wa uchumi au bado ni changamoto inayochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei?
 
Mpango ni magumashi bora angesema mfumuko Wa bei umesababishwa na watu kuitikia wito Wa hapa kazi tu watu wanafanya kazi kuogopa maneno ya kijinga yanayosema asiyefanya kazi na asile! Ndiyo maana wanakula mpaka kupitiliza
 
Chamsingi ripoti ya mwaka ipo wenyewe wamatimiza wajibu wao, hayo mengine mtajua wenyewe, maisha ya Bongo sio yakuambiwa na mtu changa karata zako mwenyewe.
 
Back
Top Bottom