Dr.Milton Mahanga afungua kesi dhidi ya Msemakweli

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Aliyedaiwa kuwa ni "FISADI WA ELIMU" Dr.Milton Makongoro Mahanga amefungua Civil case No.145 ya mwaka 2009 dhidi ya;
1.KAINERUGABA MSEMAKWELI.
2.MUHIBU SAIDI.
3.MANAGING EDITOR,NIPASHE.
4.THE GUARDIAN LTD.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 23/03/2010

SOURCE:Tangazo lililopo katika gazeti la Daily News Tar.26/12/2010 uk.20

Natafuta Tusker zangu Bariiiidi!!!...na supu ya pweza...huku nikiisubiria Movie hii kali...
 
Hicho ndo alichoambiwa toka mwanzo akifanye...kwenda mahakamani!
Namsikitikia, maana kama hana uhakika na anachofanya, ndo ataangukia pua sasa!
 
kwanza ni mjinga kuwashitaki Nipashe na the Gurdian, atashindwa kwa hao, na hakika atatakiwa kuwalipa gharama za kuendeshea kesi, eti jiulizeni kitabu kimechapwa na kinauzwa barabarani, waandishi wasiandike uwepo wa kijitabu hicho mitaani.
apeleke Vyeti vyake TCU kwanza, anaogopa nini.....wakala wa mafisadi huyu.
 
safi sana sasa ndio tutajua ukweli uko wapi maana sio tunabishana tu wakati mahakama ipo tunasubiri kwa hamu mie ngoja nikatafute popcorn na soda niangalie hii movie inaendaje!!!!
 
He he heeee.Kwanini anahangaika kufungua kesi,si awasilishe vyeti vyake TCU kama mwenzio Dr David Mathayo?
 
Aliyedaiwa kuwa ni "FISADI WA ELIMU" Dr.Milton Makongoro Mahanga amefungua Civil case No.145 ya mwaka 2009 dhidi ya;
1.KAINERUGABA MSEMAKWELI.
2.MUHIBU SAIDI.
3.MANAGING EDITOR,NIPASHE.
4.THE GUARDIAN LTD.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 23/03/2010

SOURCE:Tangazo lililopo katika gazeti la Daily News Tar.26/12/2010 uk.26

Natafuta Tusker zangu Bariiiidi!!!...na supu ya pweza...huku nikiisubiria Movie hii kali...

Mkuu ni Ukurasa wa 20, Daily News. Mambo hadharani sasa, tuone ngoma ya kwetu itachezwa vipi. Pata Mtama na Mchele kama hivi:

attachment.php
 
Attachments

  • Mahanga.jpg
    Mahanga.jpg
    94.6 KB · Views: 872
Huo ni ujanja wa kuzuia hilo suala lisijadiliwe tena kwa kuwa 'kesi iko mahakamani, na kuijadili ni kuingilia uhuru wa mahakama'. Na kesi itaendelea kuwa mahakamani hadi jamaa ashinde ubunge 2010, halafu itamalizwa 'kishkaji', au itakuwa tu haisikiki tena.
 
hapo umenena, anacheza na muda, ila ataumbuka tu, ni fisadi la elimu, wakala wa kina Rostam na Mafisadi papa hapa TZ
 
huyu jamaa mbona huwa hajiamini hata akiwa anahojiwa tu, hana elimu huyu..hawezi hata ku make points kwenye public, kwanza jimbo lake la ukonga limemshinda..hajafanya lolote jimboni kwake..sasa hivi ndio anajifanya kukwangua kwangua barabara za huko ukonga mazizini ili aonekane anafaa..hapiti safari hii!
 
Huo ni ujanja wa kuzuia hilo suala lisijadiliwe tena kwa kuwa 'kesi iko mahakamani, na kuijadili ni kuingilia uhuru wa mahakama'. Na kesi itaendelea kuwa mahakamani hadi jamaa ashinde ubunge 2010, halafu itamalizwa 'kishkaji', au itakuwa tu haisikiki tena.

Mkuu ni kweli kabisaaa...
 
Jamani msiendelee kujadili humu, kwa kuwa kesi iko mahakamani. Kuendelea kulijadili ni kukiuka sheria na kuingilia uhuru wa mahakama. Mimi sijadili tena. :D
 
Jamani msiendelee kujadili humu, kwa kuwa kesi iko mahakamani. Kuendelea kulijadili ni kukiuka sheria na kuingilia uhuru wa mahakama. Mimi sijadili tena. :D
aaah Gabu,
huyu makongoro ni wakala wa mafisadi ndo maana watu wengi wanatamani angeenda haraka TCU kisha aongoze Mahakamani, mjinga huyu.
 
Total joke!Kila mtu anajua hiyo ni Phd feki.Tungekuwa na demokrasia njema,huyu asingekubaliwa kugombea Ubunge tena maana amejikuza kwa Phd feki.
Wana UKONGA vipi?
 
Lets wait and see,..ninachofahamu kuhusu huyu jamaa,mbali ya kuwa fisadi wa elimu,pia ni kuwadi wa Mafisadi.
 
jamani mwacheni mwenzenu ataute hela ya kampeni kwa nguvu zote!jimboni kwake hawamtaki na bungeni kutamu,how do u think he will make it back in there?ans: he has to act
 
Yes, wakati umefika watu kuacha kubwatuka ovyo!!!
Mahanga hana ulazima wa kwenda TCU, hiyo ni hiari yake... Mahakama ndio mahali pake... si jamaa ameandika vitabu na vimesambazwa nchini kote na no body can retrieve them.... dawa ni adabishwe kwa ajili ya kuondoa tabia hiyo kwa jamiii!!!!
 
- Great Thinkers tunatakiwa ku-applaud mwananchi yoyote au hata kiongozi anapokimbilia kwenye sheria kwanza, badala ya kulia lia majukwaani na kwenye media, au kwenye compromise za wananchi jimboni.

- Mahanga ni lazima aheshimiwe kwa kitendo kwa sababu ndio mfano bora kwa wengine wote na ndivyo alivyofanya Dr. Salim aliandikwa upuuzi na majungu akawatangulia kwenye sheria gazeti likahukumiwa kumlipa Shilingi Millioni 500 kidogo lifungwe kama sio huruma yake Salim kuwasamehe, sasa hapa sheria inataka kuchukua mkondo wengine tena mnabeza, hivi huwa mnataka nini hasa!

- I mean sometimes tunakua kama walevi bwana, Msemakweli ameandika habari ya kuwadhalilisha viongozi, mmoja wao ameamua kwenda kwenye sheria, eti mlitaka aende wapi kwa Rais au vikao vya NEC na CC?

- Sometimes tunawachanganya sana wananchi na hizi Great Thinking!

Respect.

FMEs!
 
Mbona hata hivyo kachelewa aliambiwa mapema aende mahakamani lakini angeanzia kwanza TCU maana mahakama hai certify degree yenyewe inaangalia haki itabidi ipate ushahidi toka vyuoni na TCU.
 
Back
Top Bottom