Dr Migiro karibu nyumbani. Mrithi wake UN atangazwa

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon amemtangaza Bw Jan Eliasson raia wa Sweden kuwa mrithi wa kiti cha naibu katibu mkuu wa UN nafasi ambayo aliishikilia Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro kwa miaka takriban mitano..

Hata hivyo pamoja na uteuzi huo, Bw Eliasson atasubiri muda wa nyongeza aliopewa Dr Migiro hadi Jjuni 30 mwaka huu, na hivyo kushika wadhifa wake huu mpya kuanzia Julai 1 mwaka huu.

Karibu nyumbani Dr Migiro. Tunakuandalia ubunge wa kuteuliwa na uwaziri katika wizara moja nyeti mara utakaporejea. Then harakati zetu zileeeeeee zianze mara moja
 
Labda ndo msubiriwa kabla ya kufanya mabadiliko ya Cabinet.
Welcome back anyway
 
Bila hiyana na bila aibu Jk anaweza kuongeza wizara kwa ajili ya mpendwa

Mungi that's the given! Hawezi kumuacha mpendwa akae miaka mitatu ijayo bila bila tena wizara nyeti!
 
Labda ndo msubiriwa kabla ya kufanya mabadiliko ya Cabinet.
Welcome back anyway

kwa sasa atafanya ya kiushkaji kuwaondoa akina Mponda, lakini akirejea Dr Migiro kutafanyika reshuffle ya nguvu ili apenyezwe ndani
 
Wizara ya mambo ya nje inakusubiri maana imezoeleka kuwa waziri wa mambo ya nje ana uwezekano mkubwa wa kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM. Karibu nyumbani na hongera kwa kutimiza wajibu wako UN
 
Msimdanganye mama wa watu bure , urais aupati hata kidogo . Labda tumpe arudie umembe aliouacha . Hatutaki tena rais aliyetoka wizara ya mambo ya nje , wanakuwa ni kiguu na njia mwaka mzima .
 
Urais kwa ccm 2015 kama uspika wa 2010!

Lowasa kwa upande mmoja na sitta kwa upande mwingi wote nje.

Atateuliwa mwanamke! Alimradi wote wakose!
Nchi hii bwana!
Kuna wakati huwa natamani kulia kama alivyo lia okol kwenye song of lawino-oh mother,mother why?..why was i born black?
 
Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon amejuata kuzaliwa alipofanya uteuzi wa Kaimu wake kwa mtazamo wa itikadi, siasa na mahusiano ya urafiki wa nchi yake na Tanzania bila kupima uwezo wa mtu aliyemteua.

Mimi binafsi nilimwona huyu mama Migiri kama anaishi Tanzania vile, maana haipiti miezi miwili utamkuta yupo Dar, na mara Kikwete wapo pamoja wanateta Marekani. Labda Kikwete atapunguza sasa misafara ya Marekani.

Kama umewahi kuishi au kufanya kazi na wazungu huko kwao, hawana ile kawaida kama wabongo kunyoosheana vidole na kumwambia mtu kwa nini unafanya hivyo kama anaenda kinyume, wanachojua wao kila mmoja amekomaa na kabisa anapopewa jukumu kubwa kama hilo. Sasa mbongo uhuru huo ameshindwa kuutumia na hivo kujipangi visafari visivyo kwisha hadi kumgarimu kutoongezewa mkataba wa kumalizia ingwe ya mwisho.
 
Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon amemtangaza Bw Jan Eliasson raia wa Sweden kuwa mrithi wa kiti cha naibu katibu mkuu wa UN nafasi ambayo aliishikilia Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro kwa miaka takriban mitano..

Hata hivyo pamoja na uteuzi huo, Bw Eliasson atasubiri muda wa nyongeza aliopewa Dr Migiro hadi Jjuni 30 mwaka huu, na hivyo kushika wadhifa wake huu mpya kuanzia Julai 1 mwaka huu.

Karibu nyumbani Dr Migiro. Tunakuandalia ubunge wa kuteuliwa na uwaziri katika wizara moja nyeti mara utakaporejea. Then harakati zetu zileeeeeee zianze mara moja

Harakati gani hizo ambazo ameandaliwa na nani amemwandalia?Yaani hakuna watanzania walio na sifa ya kuongoza nchi hadi leo?wewe vipi mbona unaandika vitu vya ajabu?Wapeni wengine wafanye kazi kama za akina magufuri hatutaki longolongo watanzania.acheni hadithi za alfu lela ulela.
 
Ni mtalii mwingine anarudi nchini kutoka ughaibuni alikokwenda kuwashangaa wazungu kwa maslahi yake Binafsi.
Sioni chochote ambacho huyu mama anaweza kusema amekifanya huko kimataifa,ambacho watanzania tunaweza kwenda kifua mbele kwa kuitumia nafasi yake kuitangaza nchi yetu.
 
Bila hiyana na bila aibu Jk anaweza kuongeza wizara kwa ajili ya mpendwa
Hivi Kikwete amebakisha miaka mingapi, what i think it is a good idea that they should start preparing pre-retirement planning than distribution of posts.
 
Karibu nyumbani mama.nadhani itafaa, mara utakaporudi, ukawaona watawala wa UDSM wakupe nafasi ya kufundisha pale School of Law hasa kwa kuzingatia jinsi wana CCM wenzenu walivyomtendea mwanataaluma mwenzako Dkt Mwakyembe eti kisa power politics.
Yawezekana ushauri wangu ni wa kihisia na kuwa hauna grounds na hivyo utaupuuza.well!
Nakupa ushauti wa pili: kagombee uenyekiti wa UWT ya CCM.
 
Wizara ya mambo ya nje inakusubiri maana imezoeleka kuwa waziri wa mambo ya nje ana uwezekano mkubwa wa kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM. Karibu nyumbani na hongera kwa kutimiza wajibu wako UN

Membe naye ataenda wapi? au ameacha kuutaka urais??
 
Hivi Kikwete amebakisha miaka mingapi, what i think it is a good idea that they should start preparing pre-retirement planning than distribution of posts.

Retirement planning inahitaji kamati kwani? hope atajaribu kumu-attach kwenye winning team ya 2015
 
Back
Top Bottom