Dr Mhede aja kijapani zaidi, hamna tena mambo ya Yono, minada ya TRA sasa kielectronic

TRA yasitisha minada ya hadhara, sasa kufanyika kielektroniki

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Edwin Mhede amesitisha kuuza bidhaa balimbali kwenye minada ya hadhara ambayo awali ilikua ikitumia madalali.

Amesema minada hiyo kwa sasa itakuwa kwa njia ya mtandao na kulipiwa kwa njia hiyo licha ya kwamba mteja ataruhusiwa kuona bidhaa alizochagua kwa njia ya mtandao.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa utaratibu uliokuwa ukitumika awali wa minada ya forodha kwa bidhaa mbalimbali ulikuwa ukifanywa kupitia dalali aliyepewa kandarasi na TRA kufanya minada hiyo.

“Wakati tulikuwa tukitumia madalali kumejitokeza changamoto mbalimbali ikiwamo kufanyika mara moja kwa wiki na kusababisha bidhaa hizo kutouzwa kwa wakati hivyo serikali kutokomboa kodi kwa wakati pia.

“Pia washiriki wa mnada wamekuwa ni wale wale kwa kujirudia rudia na hata hivyo wengi wao kutokuwa wanunuzi na mara kadhaa kuingilia minada na kuharibu na kufanya wanunuzi wenye nia kushindwa kununua bidhaa hizo,” amesema.

Aidha, amesema kumekuwa na vitendo vya kuzuia wengine na kupanga bei ambayo ni kinyume na busara ya msingi ya uchumi kunakofanywa na baadhi ya watu wenye hila kwa mtandao waliouweka.

Pamoja na mambo mengine, amesema pia tuhuma mbalimbali na vitendo vya rushwa vikihusisha hata baadhi ya Maofisa wa TRA.

Chanzo: Mtanzania

Uyu kamishina ni smart sana

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nisaan patrol->start up prices --7m
mr.kiatu.........................................7.5m
mr.kisigino......................................8m
mr. chatu.........................................9m
mr.kifutu...........................................9.5m
No aproch...
No Aproach
No Aproach again.
MR. KIFUTU HAS WON.
################
 
TRA yasitisha minada ya hadhara, sasa kufanyika kielektroniki

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Edwin Mhede amesitisha kuuza bidhaa balimbali kwenye minada ya hadhara ambayo awali ilikua ikitumia madalali.

Amesema minada hiyo kwa sasa itakuwa kwa njia ya mtandao na kulipiwa kwa njia hiyo licha ya kwamba mteja ataruhusiwa kuona bidhaa alizochagua kwa njia ya mtandao.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa utaratibu uliokuwa ukitumika awali wa minada ya forodha kwa bidhaa mbalimbali ulikuwa ukifanywa kupitia dalali aliyepewa kandarasi na TRA kufanya minada hiyo.

“Wakati tulikuwa tukitumia madalali kumejitokeza changamoto mbalimbali ikiwamo kufanyika mara moja kwa wiki na kusababisha bidhaa hizo kutouzwa kwa wakati hivyo serikali kutokomboa kodi kwa wakati pia.

“Pia washiriki wa mnada wamekuwa ni wale wale kwa kujirudia rudia na hata hivyo wengi wao kutokuwa wanunuzi na mara kadhaa kuingilia minada na kuharibu na kufanya wanunuzi wenye nia kushindwa kununua bidhaa hizo,” amesema.

Aidha, amesema kumekuwa na vitendo vya kuzuia wengine na kupanga bei ambayo ni kinyume na busara ya msingi ya uchumi kunakofanywa na baadhi ya watu wenye hila kwa mtandao waliouweka.

Pamoja na mambo mengine, amesema pia tuhuma mbalimbali na vitendo vya rushwa vikihusisha hata baadhi ya Maofisa wa TRA.

Chanzo: Mtanzania
Yule mama mkurugenzi wa yono auction, atakula wapi tena.du .dar kumekucha.madalali wakalime Sasa.
 
Madalali, Kumekucha Sasa Mambo Mengi Sana Muda Mchache. TRA Wamekwenda Kugonga Kisu Cha Mfupa 😃
 
Je mitandao yetu ya Internet itaweza kweli ama ni siasa,Unajikuta unaenda tra,tpa ama ofisi nyingine ya serikali wakati wa malipo utasikia jamani msubiri network haipo vizuri,Sasa tpa imejidhatiti vipi na hilo swala
 
Mkuu mambo yote yanaishia kwenye ka TECNO
 
Back
Top Bottom