Dr Mengi umetuficha swala hili, bado hujasaidia wajasiriamali/wafanyabiashara wenye lengo la kufuata nyayo zako

nanga mstafu

JF-Expert Member
Aug 12, 2016
381
648
Tumeskia tu mara ulifanya kazi ukaacha ukaanza kuanzisha viwanda na hukuanza na ipp moja kwa moja vipo ilivyoanzisha vikafeli kwanza, je ULIPATA WAPI MTAJI, wengi tunajua kuanzisha kiwanda sio kazi ndogo kwa siku hizi sasa sembuse vipindi vya ujamaa kwa nyerere ambapo pesa ilikua ngumu na mazingira si rafiki?
Hapo kuna swala kubwA umetuficha sijui kwa nn waliofanikiwa wengi hawapendi kusema walipopatia mitaji
 
Hapa kuna haja ya kusubiri maoni ya wadau,watuambie ukweli Mengi alitoa wapi mtaji?
 
Hapa kuna haja ya kusubiri maoni ya wadau,watuambie ukweli Mengi alitoa wapi mtaji?
Tena kipindi cha ujamaa ambapo pesa ilikua ngumu na uwekezaji wa namna hiyo lazima alipata maswali mengi toka kwa watawala wa kipindi hicho......
 
Tena kipindi cha ujamaa ambapo pesa ilikua ngumu na uwekezaji wa namna hiyo lazima alipata maswali mengi toka kwa watawala wa kipindi hicho......
Aliacha kazi akiwa PARTNER kwenye Co. Ya Coopers and Lybrand kwa sasa(PWC) akiwa kwny miaka ya 30's.

Kama unajua maana ya PARTNER utakua unajua kama ni pesa aliipata akiwa chalii tu.
 
Alichota pesa NBC bank.Ikumbukwe jamaa alikuwa internal auditor wa NBC.akatumia nafasi yake kufanya ujangiri ndani ya NBC Bank kupitia vyama vya ushirika.Na ndio maana kwenye Law relating to bank kuna case study nyingi za NBC Bank Vs R.Mengi....na huenda walio sababisha Bank hii ya gvt kwa enzi hizo kuanza kufilisika hadi ikabinafsishwa na yeye ni miongoni .nimeendelea kuchokoza mada
 
Mkuu kwenye mtaji kila yule ana njia yake, kuna uwezekano hata angekuambia usingeweza/usingepata huo mtaji kwa njia km yake, either hutaweza njia yake au hutaipenda. Kwa wengne kikubwa ni kufika fainali haijalish kwa njia gani, ndio maana ukishindwa kwenda UEFA kwa kupitia top 4 basi unapambana upitie FA au EUROPA ila mwisho wa siku umefika.

Huyu tumuache ameshaenda na ameshamaliza kazi yake iliyomleta duniani, kama laa atajuana na muumba, ukiona umebaki ujue una madeni na unahitajika zaid ya mfu, kuyatimiza au kutoyatimiza hilo ni suala jingne, sasa sisi sio tupambane kulipa kodi ya pango tuu nakat kuna lundo linatusubiri nyuma.
 
Aliacha kazi akiwa PARTNER kwenye Co. Ya Coopers and Lybrand kwa sasa(PWC) akiwa kwny miaka ya 30's.

Kama unajua maana ya PARTNER utakua unajua kama ni pesa aliipata akiwa chalii tu.
Akiwa na 30?
Sio 47? Mbona viwanda tunaona kuwa kaanza 1988 au mm ndio sijaelewa?
 
Alichota pesa NBC bank.Ikumbukwe jamaa alikuwa internal auditor wa NBC.akatumia nafasi yake kufanya ujangiri ndani ya NBC Bank kupitia vyama vya ushirika.Na ndio maana kwenye Law relating to bank kuna case study nyingi za NBC Bank Vs R.Mengi....na huenda walio sababisha Bank hii ya gvt kwa enzi hizo kuanzi kufilisika hadi ikabinafsishwa.nimeendelea kuchokoza mada
Nakubaliana na ww kidogo ila alikua GENOUS bz ni mafisadi wangapi wanakwiba pesa wanazikumbatia tu benki au nje ya nchi?
 
Mkuu kwenye mtaji kila yule ana njia yake, kuna uwezekano hata angekuambia usingeweza/usingepata huo mtaji kwa njia km yake, either hutaweza njia yake au hutaipenda. Kwa wengne kikubwa ni kufika fainali haijalish kwa njia gani, ndio maana ukishindwa kwenda UEFA kwa kupitia top 4 basi unapambana upitie FA au EUROPA ila mwisho wa siku umefika.

Huyu tumuache ameshaenda na ameshamaliza kazi yake iliyomleta duniani, kama laa atajuana na muumba, ukiona umebaki ujue una madeni na unahitajika zaid ya mfu, kuyatimiza au kutoyatimiza hilo ni suala jingne, sasa sisi sio tupambane kulipa kodi ya pango tuu nakat kuna lundo linatusubiri nyuma.

Well said
 
Niongezee nyama kabisa! Imagine alianzisha kiwanda enzi za akina Sokoine wakiwa hai,kwangu mazingira yote haya kwa wakati ule yananipa ukakasi kidogo !
Hapa kuna haja ya kusubiri maoni ya wadau,watuambie ukweli Mengi alitoa wapi mtaji?
 
Ipo hivi: ni ngumu sana mtu aliyeendelea kukuambia amefikaje hapo.
Kuna watu wanafanya biashara kwa mikopo ya wake zao, kaka zao, nk lakini ukitaka kujua inabidi usikilize watu wa pembeni.
Mimi mwenyewe siwezi kumwambia mtu siri ya mafanikio yangu japo siyo makubwa sana.
 
Back
Top Bottom