Zero
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 299
- 17
Mimi ninachoona hapa ni ushabiki mkubwa unaofanywa na FMES bila kujibu tuhuma halisi zilizotolewa na Bangusule. Bangusule ametoa tuhuma kadhaa kubwa. Moja ni kuhusu wilaya ya Same kufanya vibaya kielimu, pili ni suala la ugonjwa uliokumba zao la mpunga, tatu ni ubovu wa barabara, na nne ni ufyekaji wa misitu ambao umesababisha kuharibiwa kwa vyanzo vya maji. FMES anakuja na hoja kwamba mbunge Anne Kilango amechimba visima 30 na kutoa msaada wa baisikeli 20 kwa walemavu. Huu ni upotoshaji mkubwa wa mada na hakuna jibu liliotolewa kuhusu tuhuma alizotoa Bangusule.
Mkuu FMES, tuambie katika tuhuma nne alizotoa Bangusule, mbunge wako Anne Kilango amefanya nini katika kuzitatua? Visima vya maji siamini kama vinatumika kumwagilia mpunga. That is insane! Taumbie visima vyako 30 vinahusiana vipi na ugonjwa uliokumba zao la mpunga. Tuambie visima vinahusiana vipi na wanafunzi kufanya vibaya katika mitihani yao. Tuambie visima vinahusiana vipi na ufyekwaji wa misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji.