Dr. Mashinji mpaka sasa ndio Katibu Mkuu bora wa chama cha siasa nchini

Ki ukweli Mashinji anafanya kazi, na mbinu anayotumia ni muafaka ktk mazingira ya sasa.Yaani anajenga chama kimya kimya na kwa vitendo zaidi.Hii ni nzuri kwani ukiongea sana maadui wanajua mbinu zako hivyo wanaweza kukukwamisha.Mafanikio yake mengine ni ule mkakati wake wa kujenga ofisi kila kanda na kukarabati makao makuu

kuna watu wamezoea kuwa ukiona kelele nyingi na kazi ni nyingi kumbe ni kinyume chake , unaweza ukapiga sana kelele kumbe ni mkakati wa kuficha madhaifu yako......
 
Nimeweka kichwa cha habari hicho sio kwa sababu sina sababu ila nataka kuweka facts hapa kuwa ni kwanini Dr.Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa kipindi cha miezi minne mpaka sasa ambayo amekaa ofisini na mambo ambayo yamefanyika kwa kipindi hicho cha miezi minne Naweza kusema kuwa ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha siasa kwa sasa hapa nchini.

Nasema amekaa kwa miezi minne tu kwani aliingia ofisini rasmi mwezi Juni 2016, na tangu alipoingia mipango na mikakati ambayo miminimeona ikifanyika kwa ufundi mkubwa ni kama ifuatavyo;

1. Alipoingia tu aliibadilisha Secretariat ya Makao Makuu- na kubadilisha baadhi ya wakurugenzi na wengine kuachwa kabisa na wapya kuteuliwa jambo ambalo tunashuhudia utendaji kazi za kila siku na mipango mbalimbali ikiendelea kufanyika --nitaeleza mipango hiyo hapo baadaye kidogo. Amekifanya chama kuwa taasisi imara zaidi kwani sasa ile tabia ya kila mtu kuwa msemaji wa chama inatoweka -hii naamini ni mipango ya Dr.Mashinji

2. Aliweza kuwaratibu Wabunge wake na wa UKAWA katika kuendesha mapambano mbalimbali ndani na nje ya Bunge mnaokumbuka sakata la BUNGE LIVE! UDOM nk , kiasi kwamba mipango mbalimbali ilifanyika na kuweza kuitetemesha nchi ,

3. Bunge la Bajeti , alionyesha umahiri wake kwa kuwaratibu wabunge wa CHADEMA kuigomea bajeti ambayo leo wabunge wa CCM wanalia hakuna fedha za kwenda kukagua miradi wakati walipitisha kwa mbwembwe kiasi cha shilingi milioni 10 kwa kila kamati kwa ajili ya ziara , sasa sijui zinatosha nauli au posho.....Ila kwa kuwa CCM hawana katibu mkuu imara hakuweza kuliona hilo na kuwasimamia wabunge wake waweze kuisimamia serikali.

4.UKUTA - mara baada ya bunge kupitisha bajeti yake kwa nguvu kubwa hakuishiwa nguvu na mbinu bali aliweza kuratibu chama chake na kuja na operation kabambe iliyojulikana kama UKUTA na kwa kweli joto la UKUTA halijawahi kutokea katika historia ya mfumo wa vyama vingi tangu ulipoanza hapa nchini.

UKUTA bado unaendelea kwa sababu ni mapambano ya kifikra na sio tukio la siku moja na wanachama wa UKUTA wameendelea kuongezeka kila siku , wapya kabisa ni walionyimwa mikopo ya Vyuo Vikuu ambao ni maelfu , hawa ukiwatangazia tarehe watatoka kwani hawana tumaini tena . Ni kazi ya Dr.Mashinji hiyo.

5.Ameanzisha mkakati wa kukitambulisha chama Kimataifa zaidi na aliongoza jopo la viongozi wenzake kwenda katika mataifa mbalimbali kueleza kuhusu hali ya kisiasa na kidomokrasia nchini , jinsi ambavyo utawala wa sheria unaminywa nk.....La kujifunza ni kuwa anatambua kuwa Tanzania sio kisiwa na hivyo inahitaji kushirikiana na mataifa mengine mbalimbali Duniani.

6. Kadi mpya za Kilectroniki - Huu nao ni ubunifu wa Dr.Mashinji , ameweza kukishauri chama chake utaratibu mzuri wa kuwatambua wanachama wake na pia kuweza kujipatia kipato cha uhakika, ni jana tu Mbowe alitangazia taifa kuwa mkakati huo utaweza kukiingizia chama zaidi ya shilingi 13 bilioni kwa mwaka , sasa utamlinganisha na nani kwenye kubuni vyanzo vya mapato? Naambiwa wanachama tayari wameshaanza kusajiliwa kwa mfumo huu mpya silently .....

7.Ziara za viongozi wakuu ngazi za chini- ni juzi tuu Viongozi wote wakuu na wajumbe wa kamati kuu kwenda kuzungumza na viongozi wa ngazi za chini kwenye majimbo mbalimbali nchini na jana walimaliza kanda ya kati Dodoma - Mipango hii mizuri ya kuwakutanisha viongozi wakuu na wale wa chini kwenye majimbo yao ni kitu ambacho hakikuwa kikifanyika huko miaka ya nyuma ila chini ya Dr.Mashinji imewezekana -utamlinganisha na nani?

8.Kazi ya kawaida ya kuitisha vikao vya kikatiba kama kamati kuu na Baraza Kuu ameifanya sana katika kipindi hiki na kwa taarifa wale ambao hawajui ukiitisha kikao cha Kamati Kuu nyaraka zote zinaandaliwa na ofisi ya Katibu Mkuu.----kwa kuwa mimi sio mjumbe huko yawezekana nisijue sana juu ya ubora wa nyaraka husika ila naamini kwa vichwa vilivyomo mle ndani huwezi peleka nyaraka dhaifu ukavumiliwa .

Mafanikio mengine nitaomba muongezee kwani mimi nakumbuka haya, na hii ni kazi ya miezi minne tu hivi akikaa miaka 7 kama Dr Slaa itakuwaje kwa mipango kama hii?

Ikumbukwe kuwa kazi ya Katibu Mkuu ni kukiratibu Chama na sio kuwa mtu wa kupayuka kila siku , anatakiwa kuratibu na kuendesha chama , yeye ni Injini inapaswa kusukuma mifumo yote iweze kwenda , anaweza akalaumiwa kwa sababu watu walishazoea kuwa na Katibu Mkuu mgombea Urais ambaye alikuwa anajiprofile so wakiona wa tofauti wanafikiri amelala .

KINANA.
Niulize swali hivi tangu baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 Katibu Mkuu wa CCM Kinana amefanya kazi ipi moja ya kujenga chama chake ?

Kinana ameshindwa hata kuitisha vikao vya kikatiba vya chama chake , hivi nani anakumbuka mara ya mwisho kamati kuu ya CCM kuitishwa chini ya uongozi mpya ?

Kinana ameshindwa kwenda kukagua uhai wa chama , ameshindwa kuwalipa wafanyakazi wa uhuru kwa zaidi ya miezi sita na walilalamika hadharani ......Madeni yamemzidi kiasi kwamba amezua msemo maarufu mtaani kwa sasa wa [HASHTAG]#KUNYWA[/HASHTAG] MAJI MWANANGU...

Dr.Mashinji kwa maoni yangu ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha Siasa Nchini kwa sasa na ushahidi nimeweka hapo juu , mwenye maoni tofauti aje na ushahidi kupinga hizi facts .

Naomba kuwasilisha , tupingane bila kutukanana.....ndio Maturity hiyo.

Chama hakina mwelekeo. Mliitelekeza ajenda kuu iliyowapatia umaarufu mlionao leo, ajenda ya ufisadi, kisa kumridhisha Lowassa. Na hicho ndio kitanzi chenu. Huyo Mashinji anendesha chama kama parokia ya Kanisa. Talking of Kanisa, mtamkumbuka sana Dkt Slaa.

By the way, where is Dkt Mashinji to tell us what has he been up to hadi aanze kutumia wapambe mitandaoni kutuonyesha (yasiyoonekana) kuhusu utendaji wake? Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
 
Ajenda ya Ufisadi Magufuli ameianzishia Mahakama maalum tunataka kuona utekelezaji wake na Mafisadi wakiwa vizimbani .
Dr.Slaa alishafanya yake kamaliza sasa usukani upo kwa Mashinji , hamkutaka aliyofanya kwa miezi minne yajulikane ili muendeleze propaganda zenu ? Kipi ambacho hakionekani kati ya hayo niliyoeleza hapo juu? Au kisu kimefikia mfupa ? Jibu hoja kwa hoja sio kwa jazba .....
 
hakuna kitu kama hicho , hakuna hata fact moja hapo...
Masihinji ndiyo katibu wa hovyo kweli kwa vyama vya kisiasa Tanzania wakati wa mashinji tumeshuhudia mambo ya ajabu kutoka chadema kama yafuatayo
1.Wabunge wa chadema kugomea vikao vya bunge kisa Naibu spika na katibu mashinji yupo..
2. Wabunge wa chadema hasa mwenyekiti kutoa tuhuma za wabunge wa ccm bila kupeleka takukuru na kusubiri huruma ya Rais kuingilia sakata hilo.
3. Kutafuta Udhaifu wa serikali kwa tochi hii ikumbukwe pale mbuge Lema alipo taka kuharibu mkutano wa mkuu wa mkoa Arusha.
4. Madiwani wa chadema kususia vikao halali vya halmashauri na kupoteza kiti cha umeya.
5. Chama hakina hoja tena kwenye jamii sasa zaidi ya kudandia hoja za matukio na kuambulia viroja
6. Chama kuingilia vyama vingine vya siasa kumbuka mbowe anatangaza kutomkutambua mwenyekiti wa CUF .
7.Chama kukosa ushawishi wenye tija hasa kwa kuwakilisha miswaada mbalimbali yenye tija na taifa kama Enzi za Slaa.
8.Kuendesha oparesheni UKUTA bila mkakati matokea yake ukuta ukaanguka milele.
KUNA MENGI NIANZE NA HAYO
Hahahahahaha...!mkuu povu jingi lkn cjaona point zaidi ya majungu,Masihinji anatisha hata mm nakubali,kama ungeweza kujipa ufahamu ungemwelewa vzuri mtoa mada
 
Hivi na UKUTA ni sehemu za success ya chadema??
UKUTA sio tukio la siku moja ni dhana na ni fikra .......UKUTA unaendelea kujengeka hapo juu nimeweka unavyojengwa soma kwa ufasaha tuliza akili utaelewa tu.

By the way kwanini mtu akisemwa kwa mema au mafanikio wengine wananuna na kutukana ?Au mtu kusemwa kwa ubaya tu ndio linalofurahisha watu?
 
Ndo aliwaambia mbowe hivyo nanyi mmemeza.
 
Nilifikiri Lizabon baada ya semina iliyomalizika Lumumba angekuja na maelezo hapa , ila simuoni kapotelea kusikojulikana , kapigwa na kitu kizito chenye ncha kali .........
 
Nimeweka kichwa cha habari hicho sio kwa sababu sina sababu ila nataka kuweka facts hapa kuwa ni kwanini Dr.Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa kipindi cha miezi minne mpaka sasa ambayo amekaa ofisini na mambo ambayo yamefanyika kwa kipindi hicho cha miezi minne Naweza kusema kuwa ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha siasa kwa sasa hapa nchini.

Nasema amekaa kwa miezi minne tu kwani aliingia ofisini rasmi mwezi Juni 2016, na tangu alipoingia mipango na mikakati ambayo miminimeona ikifanyika kwa ufundi mkubwa ni kama ifuatavyo;

1. Alipoingia tu aliibadilisha Secretariat ya Makao Makuu- na kubadilisha baadhi ya wakurugenzi na wengine kuachwa kabisa na wapya kuteuliwa jambo ambalo tunashuhudia utendaji kazi za kila siku na mipango mbalimbali ikiendelea kufanyika --nitaeleza mipango hiyo hapo baadaye kidogo. Amekifanya chama kuwa taasisi imara zaidi kwani sasa ile tabia ya kila mtu kuwa msemaji wa chama inatoweka -hii naamini ni mipango ya Dr.Mashinji

2. Aliweza kuwaratibu Wabunge wake na wa UKAWA katika kuendesha mapambano mbalimbali ndani na nje ya Bunge mnaokumbuka sakata la BUNGE LIVE! UDOM nk , kiasi kwamba mipango mbalimbali ilifanyika na kuweza kuitetemesha nchi ,

3. Bunge la Bajeti , alionyesha umahiri wake kwa kuwaratibu wabunge wa CHADEMA kuigomea bajeti ambayo leo wabunge wa CCM wanalia hakuna fedha za kwenda kukagua miradi wakati walipitisha kwa mbwembwe kiasi cha shilingi milioni 10 kwa kila kamati kwa ajili ya ziara , sasa sijui zinatosha nauli au posho.....Ila kwa kuwa CCM hawana katibu mkuu imara hakuweza kuliona hilo na kuwasimamia wabunge wake waweze kuisimamia serikali.

4.UKUTA - mara baada ya bunge kupitisha bajeti yake kwa nguvu kubwa hakuishiwa nguvu na mbinu bali aliweza kuratibu chama chake na kuja na operation kabambe iliyojulikana kama UKUTA na kwa kweli joto la UKUTA halijawahi kutokea katika historia ya mfumo wa vyama vingi tangu ulipoanza hapa nchini.

UKUTA bado unaendelea kwa sababu ni mapambano ya kifikra na sio tukio la siku moja na wanachama wa UKUTA wameendelea kuongezeka kila siku , wapya kabisa ni walionyimwa mikopo ya Vyuo Vikuu ambao ni maelfu , hawa ukiwatangazia tarehe watatoka kwani hawana tumaini tena . Ni kazi ya Dr.Mashinji hiyo.

5.Ameanzisha mkakati wa kukitambulisha chama Kimataifa zaidi na aliongoza jopo la viongozi wenzake kwenda katika mataifa mbalimbali kueleza kuhusu hali ya kisiasa na kidomokrasia nchini , jinsi ambavyo utawala wa sheria unaminywa nk.....La kujifunza ni kuwa anatambua kuwa Tanzania sio kisiwa na hivyo inahitaji kushirikiana na mataifa mengine mbalimbali Duniani.

6. Kadi mpya za Kilectroniki - Huu nao ni ubunifu wa Dr.Mashinji , ameweza kukishauri chama chake utaratibu mzuri wa kuwatambua wanachama wake na pia kuweza kujipatia kipato cha uhakika, ni jana tu Mbowe alitangazia taifa kuwa mkakati huo utaweza kukiingizia chama zaidi ya shilingi 13 bilioni kwa mwaka , sasa utamlinganisha na nani kwenye kubuni vyanzo vya mapato? Naambiwa wanachama tayari wameshaanza kusajiliwa kwa mfumo huu mpya silently .....

7.Ziara za viongozi wakuu ngazi za chini- ni juzi tuu Viongozi wote wakuu na wajumbe wa kamati kuu kwenda kuzungumza na viongozi wa ngazi za chini kwenye majimbo mbalimbali nchini na jana walimaliza kanda ya kati Dodoma - Mipango hii mizuri ya kuwakutanisha viongozi wakuu na wale wa chini kwenye majimbo yao ni kitu ambacho hakikuwa kikifanyika huko miaka ya nyuma ila chini ya Dr.Mashinji imewezekana -utamlinganisha na nani?

8.Kazi ya kawaida ya kuitisha vikao vya kikatiba kama kamati kuu na Baraza Kuu ameifanya sana katika kipindi hiki na kwa taarifa wale ambao hawajui ukiitisha kikao cha Kamati Kuu nyaraka zote zinaandaliwa na ofisi ya Katibu Mkuu.----kwa kuwa mimi sio mjumbe huko yawezekana nisijue sana juu ya ubora wa nyaraka husika ila naamini kwa vichwa vilivyomo mle ndani huwezi peleka nyaraka dhaifu ukavumiliwa .

Mafanikio mengine nitaomba muongezee kwani mimi nakumbuka haya, na hii ni kazi ya miezi minne tu hivi akikaa miaka 7 kama Dr Slaa itakuwaje kwa mipango kama hii?

Ikumbukwe kuwa kazi ya Katibu Mkuu ni kukiratibu Chama na sio kuwa mtu wa kupayuka kila siku , anatakiwa kuratibu na kuendesha chama , yeye ni Injini inapaswa kusukuma mifumo yote iweze kwenda , anaweza akalaumiwa kwa sababu watu walishazoea kuwa na Katibu Mkuu mgombea Urais ambaye alikuwa anajiprofile so wakiona wa tofauti wanafikiri amelala .

KINANA.
Niulize swali hivi tangu baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 Katibu Mkuu wa CCM Kinana amefanya kazi ipi moja ya kujenga chama chake ?

Kinana ameshindwa hata kuitisha vikao vya kikatiba vya chama chake , hivi nani anakumbuka mara ya mwisho kamati kuu ya CCM kuitishwa chini ya uongozi mpya ?

Kinana ameshindwa kwenda kukagua uhai wa chama , ameshindwa kuwalipa wafanyakazi wa uhuru kwa zaidi ya miezi sita na walilalamika hadharani ......Madeni yamemzidi kiasi kwamba amezua msemo maarufu mtaani kwa sasa wa [HASHTAG]#KUNYWA[/HASHTAG] MAJI MWANANGU...

Dr.Mashinji kwa maoni yangu ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha Siasa Nchini kwa sasa na ushahidi nimeweka hapo juu , mwenye maoni tofauti aje na ushahidi kupinga hizi facts .

Naomba kuwasilisha , tupingane bila kutukanana.....ndio Maturity hiyo.
Bahati nzuri unatufariji kwa kushindwa na hii ni baada ya watu kuhoji ukimya Wa Katibu Mkuu na moja ya gazeti Jana kuandika kuwa ukatibu Mkuu wa Dk Slaa wamtesa Mashinji Wa Chadema
 
ITOSHE NIKIKUAMBIA NI MAPEMA MNO NDUGU MASHINJI KUANZA KUJISIA HIVI. CHA MSINGI KIPIMO CHAKO KIWE UCHAGUZI SASA KUNA MAJIMBO MAWILI KULE LONGIDO NA KULE ZANZIBAR SASA WEKA WAGOMBEA HALAFU FANANISHA KURA UTAKAZOPATA NA ULINGANISHE NA WAKATI UKIWA HUPO MADARAKANI HALAFU JIPIME. NA LABDA NIKUULIZE SWALI NDUGU MASHINJI HIVI MMEMSUSA NDUGU LEMA? SWALI LA MWISHO HIVI WALE VIONGOZI WA DINI WALIO WAAMBIA UKUTA USIWEPO WALIKUONYESHA VITAMBULISHO AU MLIKUBALIANAJE? ISIJE IKAWA MLIPIGWA FIX NA MADALALI WA KARIAKOO WALIOVAA KANZU HAHAHAHAAAA.
 
Back
Top Bottom