Dr. Mashinji mpaka sasa ndio Katibu Mkuu bora wa chama cha siasa nchini

Naona watu wazito wa Ufipa mnaanza kutetea bomu lenu.
Weka facts za utofauti , shawishi kuwa ni bomu kwa hoja na sio kwa viroja ......kuna ukweli na kuna Propaganda sasa hapa umewekwa ukweli wenye mashiko ..........Mtakaa tu mwaka huu mlizoea kujua mipango kabla ya utekelezaji kwa sababu ya Dr.Slaa kuongea sana na media sasa huyu ni silent operator na mjue tu kuwa huyu ni Daktari anatafuta kiini cha ugonjwa ndio anashughulika nacho na sio dalili.....
 
Mkuu kinana kashavurugwa anataka kupumzika na siasa,mambo ya kufokewa kama mtoto nani anataka?
Kumbe ndivyo kulivyo nyumba ya mtaa wa pili ......Lizabon anatoa wapi nguvu za kumwaga povu daily humu kama hali yenyewe ndio hiyo ? Au anafikiri mafanikio ya akina Mwampamba naye yataweza kumfikia ?
 
Nimeweka kichwa cha habari hicho sio kwa sababu sina sababu ila nataka kuweka facts hapa kuwa ni kwanini Dr.Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa kipindi cha miezi minne mpaka sasa ambayo amekaa ofisini na mambo ambayo yamefanyika kwa kipindi hicho cha miezi minne Naweza kusema kuwa ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha siasa kwa sasa hapa nchini.

Nasema amekaa kwa miezi minne tu kwani aliingia ofisini rasmi mwezi Juni 2016, na tangu alipoingia mipango na mikakati ambayo miminimeona ikifanyika kwa ufundi mkubwa ni kama ifuatavyo;

1. Alipoingia tu aliibadilisha Secretariat ya Makao Makuu- na kubadilisha baadhi ya wakurugenzi na wengine kuachwa kabisa na wapya kuteuliwa jambo ambalo tunashuhudia utendaji kazi za kila siku na mipango mbalimbali ikiendelea kufanyika --nitaeleza mipango hiyo hapo baadaye kidogo. Amekifanya chama kuwa taasisi imara zaidi kwani sasa ile tabia ya kila mtu kuwa msemaji wa chama inatoweka -hii naamini ni mipango ya Dr.Mashinji

2. Aliweza kuwaratibu Wabunge wake na wa UKAWA katika kuendesha mapambano mbalimbali ndani na nje ya Bunge mnaokumbuka sakata la BUNGE LIVE! UDOM nk , kiasi kwamba mipango mbalimbali ilifanyika na kuweza kuitetemesha nchi ,

3. Bunge la Bajeti , alionyesha umahiri wake kwa kuwaratibu wabunge wa CHADEMA kuigomea bajeti ambayo leo wabunge wa CCM wanalia hakuna fedha za kwenda kukagua miradi wakati walipitisha kwa mbwembwe kiasi cha shilingi milioni 10 kwa kila kamati kwa ajili ya ziara , sasa sijui zinatosha nauli au posho.....Ila kwa kuwa CCM hawana katibu mkuu imara hakuweza kuliona hilo na kuwasimamia wabunge wake waweze kuisimamia serikali.

4.UKUTA - mara baada ya bunge kupitisha bajeti yake kwa nguvu kubwa hakuishiwa nguvu na mbinu bali aliweza kuratibu chama chake na kuja na operation kabambe iliyojulikana kama UKUTA na kwa kweli joto la UKUTA halijawahi kutokea katika historia ya mfumo wa vyama vingi tangu ulipoanza hapa nchini.UKUTA bado unaendelea kwa sababu ni mapambano ya kifikra na sio tukio la siku moja na wanachama wa UKUTA wameendelea kuongezeka kila siku , wapya kabisa ni walionyimwa mikopo ya Vyuo Vikuu ambao ni maelfu , hawa ukiwatangazia tarehe watatoka kwani hawana tumaini tena . Ni kazi ya Dr.Mashinji hiyo.

5.Ameanzisha mkakati wa kukitambulisha chama Kimataifa zaidi na aliongoza jopo la viongozi wenzake kwenda katika mataifa mbalimbali kueleza kuhusu hali ya kisiasa na kidomokrasia nchini , jinsi ambavyo utawala wa sheria unaminywa nk.....La kujifunza ni kuwa anatambua kuwa Tanzania sio kisiwa na hivyo inahitaji kushirikiana na mataifa mengine mbalimbali Duniani.

6. Kadi mpya za Kilectroniki - Huu nao ni ubunifu wa Dr.Mashinji , ameweza kukishauri chama chake utaratibu mzuri wa kuwatambua wanachama wake na pia kuweza kujipatia kipato cha uhakika, ni jana tu Mbowe alitangazia taifa kuwa mkakati huo utaweza kukiingizia chama zaidi ya shilingi 13 bilioni kwa mwaka , sasa utamlinganisha na nani kwenye kubuni vyanzo vya mapato? Naambiwa wanachama tayari wameshaanza kusajiliwa kwa mfumo huu mpya silently .....

7.Ziara za viongozi wakuu ngazi za chini- ni juzi tuu Viongozi wote wakuu na wajumbe wa kamati kuu kwenda kuzungumza na viongozi wa ngazi za chini kwenye majimbo mbalimbali nchini na jana walimaliza kanda ya kati Dodoma - Mipango hii mizuri ya kuwakutanisha viongozi wakuu na wale wa chini kwenye majimbo yao ni kitu ambacho hakikuwa kikifanyika huko miaka ya nyuma ila chini ya Dr.Mashinji imewezekana -utamlinganisha na nani?

8.Kazi ya kawaida ya kuitisha vikao vya kikatiba kama kamati kuu na Baraza Kuu ameifanya sana katika kipindi hiki na kwa taarifa wale ambao hawajui ukiitisha kikao cha Kamati Kuu nyaraka zote zinaandaliwa na ofisi ya Katibu Mkuu.----kwa kuwa mimi sio mjumbe huko yawezekana nisijue sana juu ya ubora wa nyaraka husika ila naamini kwa vichwa vilivyomo mle ndani huwezi peleka nyaraka dhaifu ukavumiliwa .

Mafanikio mengine nitaomba muongezee kwani mimi nakumbuka haya, na hii ni kazi ya miezi minne tu hivi akikaa miaka 7 kama Dr Slaa itakuwaje kwa mipango kama hii?

Ikumbukwe kuwa kazi ya Katibu Mkuu ni kukiratibu Chama na sio kuwa mtu wa kupayuka kila siku , anatakiwa kuratibu na kuendesha chama , yeye ni Injini inapaswa kusukuma mifumo yote iweze kwenda , anaweza akalaumiwa kwa sababu watu walishazoea kuwa na Katibu Mkuu mgombea Urais ambaye alikuwa anajiprofile so wakiona wa tofauti wanafikiri amelala .

KINANA.

Niulize swali hivi tangu baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 Katibu Mkuu wa CCM Kinana amefanya kazi ipi moja ya kujenga chama chake ?

Kinana ameshindwa hata kuitisha vikao vya kikatiba vya chama chake , hivi nani anakumbuka mara ya mwisho kamati kuu ya CCM kuitishwa chini ya uongozi mpya ?

Kinana ameshindwa kwenda kukagua uhai wa chama , ameshindwa kuwalipa wafanyakazi wa uhuru kwa zaidi ya miezi sita na walilalamika hadharani ......Madeni yamemzidi kiasi kwamba amezua msemo maarufu mtaani kwa sasa wa [HASHTAG]#KUNYWA[/HASHTAG] MAJI MWANANGU...

Dr.Mashinji kwa maoni yangu ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha Siasa Nchini kwa sasa na ushahidi nimeweka hapo juu , mwenye maoni tofauti aje na ushahidi kupinga hizi facts .

Naomba kuwasilisha , tupingane bila kutukanana.....ndio Maturity hiyo.
Ndio nani huyo au wa Chama kipya? Hasikiki na hafahamiki na sijui kama anafahamu majukumu yake!!
 
mkianza kusajili wanachama electronically...tutakamata mashine zenu kama wale vijana wa IT...natania tu
 
Ivi uyo katibu si alichaguliwa siku moja na makonda embu piama utendaji wao bas hata kama ni sikio la kufa embu sikia hyo dawa.
Huwezi mlinganisha Kinana na vitu vya kipumbavu Cv ya kinana huyo nyumbu hawezi mfikia hata miaka 100
 
Ivi uyo katibu si alichaguliwa siku moja na makonda embu piama utendaji wao bas hata kama ni sikio la kufa embu sikia hyo dawa.
Huwezi mlinganisha Kinana na vitu vya kipumbavu Cv ya kinana huyo nyumbu hawezi mfikia hata miaka 100
Acha matusi , jibu maswali juu ya Kinana kwenye hiyo post ........Makonda amepambana na Shisha na Mashoga dunia inajua ....
 
Ki ukweli Mashinji anafanya kazi, na mbinu anayotumia ni muafaka ktk mazingira ya sasa.Yaani anajenga chama kimya kimya na kwa vitendo zaidi.Hii ni nzuri kwani ukiongea sana maadui wanajua mbinu zako hivyo wanaweza kukukwamisha.Mafanikio yake mengine ni ule mkakati wake wa kujenga ofisi kila kanda na kukarabati makao makuu
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom