Dr Magufuli usimsahau yule mkulima wa Kigoma

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,733
239,337
Hakika katika watu wenye roho ngumu na mapenzi ya dhati kwa ccm basi huwezi kumuacha yule mkulima wa kigoma aliyejitosa kuwania urais .

Pamoja na ukweli kwamba hakuwa na ' BAHASHA ZA KHAKI ' ambazo ni kivutio kikubwa kwa wanaccm na wajumbe wa mkutano mkuu lakini aliamua kujitosa na kupigana hadi tone la mwisho !

Sasa mkuu wewe ndio mwenye dhamana ya kuteua viongozi , nakuomba umkumbuke mzalendo yule ambaye alirudisha fomu yake huku mkononi akiwa ameshika chupa ya maji ya kunywa ya PANGANI yanayotengenezwa wilayani temeke katika eneo duni la Keko torori ( si kilimanjaro kama wagombea wengine ) , taarifa zaidi zinadokeza kwamba hata fomu zake za uteuzi alizilipia kwa TIGO PESA .

Apewe hata U-DC , kwa uzalendo aliouonyesha , haonekani kukata tamaa na kushindwa jambo na anaweza kufanya maajabu katika uongozi wake .
 
Hakika katika watu wenye roho ngumu na mapenzi ya dhati kwa ccm basi huwezi kumuacha yule mkulima wa kigoma aliyejitosa kuwania urais .

Pamoja na ukweli kwamba hakuwa na ' BAHASHA ZA KHAKI ' ambazo ni kivutio kikubwa kwa wanaccm na wajumbe wa mkutano mkuu lakini aliamua kujitosa na kupigana hadi tone la mwisho !

Sasa mkuu wewe ndio mwenye dhamana ya kuteua viongozi , nakuomba umkumbuke mzalendo yule ambaye alirudisha fomu yake huku mkononi akiwa ameshika chupa ya maji ya kunywa ya PANGANI ( si kilimanjaro kama wagombea wengine ) , taarifa zaidi zinadokeza kwamba hata fomu zake za uteuzi alizilipia kwa TIGO PESA .

Apewe hata U-DC , kwa uzalendo aliouonyesha haonekani kushindwa jambo na anaweza kufanya maajabu katika uongozi wake .
Yule mkulima alikuwa mkulima jina tu.

Ni mtu wa system aliyejivika gwanda la kijani kunogesha zoezi la uchukuaji fomu kwa kazi maalumu.

Ni mtu mkubwa kuliko unavyofikiri.
 
Yule mkulima alikuwa mkulima jina tu.

Ni mtu wa system aliyejivika gwanda la kijani kunogesha zoezi la uchukuaji fomu kwa kazi maalumu.

Ni mtu mkubwa kuliko unavyofikiri.
Duh ! sasa kunogeshaje tena ? hebu funguka kidogo mkuu .
 
Taja nafasi aliyonayo ili tujue nguvu yake kiuchumi na tuondoe mawazo kuwa ni maskini
Hahahaaaaaa! Watu bhana. Bahati nzuri jamaa nakaa naye mtaa mmoja hapa mlole mkoani kigoma.
Kesho nampiga picha niiweke hapa.
 
Hahahaaaaaa! Watu bhana. Bahati nzuri jamaa nakaa naye mtaa mmoja hapa mlole mkoani kigoma.
Kesho nampiga picha niiweke hapa.
Unafahamu ajira yake?ana muonekanao wa kipato tunachoanzakuaminishwa?,maana wengi wetu tunamjua kuwa ni kapuku tu.
 
Hahahaaaaaa! Watu bhana. Bahati nzuri jamaa nakaa naye mtaa mmoja hapa mlole mkoani kigoma.
Kesho nampiga picha niiweke hapa.
nimeitafuta sana picha zake bila mafanikio , sasa kama utaziweka hapa itakuwa bomba sana .
 
Back
Top Bottom