Dr. Magufuli songa mbele, upande wako tuko wengi zaidi

jaruri

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2014
Messages
716
Points
500

jaruri

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2014
716 500
Nipende kuchukua fursa hii kumtia moyo Rais wangu mpendwa Dr Magufuli,Rais pekee mkombozi wa Taifa letu.Ni kiongozi ambae ameleta matumani mapya kwa watanzania tangu aingie madarakani miaka miwili iliyopita.
Rais huyu ameleta mabadiliko makubwa katika sera na utendaji wa serikali.Rushwa,nidhamu kazini,upatikanaji wa huduma za kijamii kama elimu bure,madawa hospitalini na vita dhidi ya madawa ya kulevya na ufisadi.Hakuna mtu mwenye akili timamu ambae anaweza bisha kuwa haya niliyo yatamka hayaonekani.Mtu huyu akipatikana miongoni mwetu(watanzania) basi atakuwa na lake jambo

Ni kweli changamoto zipo kama upungufu wa waalimu,vyumba vya madarasa,vifaa vya kufundishia kama vitabu na vifaa vya maabara.Lakini hili sio tatizo sana maana kila mafanikio yana changamoto zake,Na serikali inafanya jitihada za dhati kutatua haya mapungufu machache.Jitihada hizi zinaonekana dhahiri.

Mosi ELIMU,
Suala waalimu.
Serikali imeimarisha vyuo vya diploma ya ualimu na kuvikarabati ili kutoa waalimu bora kwa ajili ya shule zetu za msingi na sekondari.Na katika hili serikali imeongeza viwango vya udahili ili kupata kupata waalimu wazuri na mwisho wa siku wanafunzi wetu wapate elimu bora.Atakuja mtu mwingine na maneno yake ya hovyo kuwa serikali haijafanya lolote katika hili apuuzwe haraka.
Suala la madawati
Serikali ya awamu ya tano ilipoingia tu madarakani ilianza na suala la madawati na hivi sasa tatizo la madawati limebaki historia kwa kiwango kikubwa.
Vifaa vya maabara
Serikali imesambaza vifaa vya maabara kwa kiwango kikubwa sana na tatizo hili limepungua sana.Hakika mtanzania maskini ambae mwanae anasoma katika shule za kata anafaidi matunda ya uhuru.
Maslahi ya waalimu na watumishi wengine
Bilioni zaidi ya mia sita zimetengwa na muda wowote watalipwa.

PILI,UFISADI
Mafisadi wanaisoma namba dhahiri shahiri mchana kweupe.

TATU,WAFANYA BIASHARA WADOGO NA WAKULIMA
.
Kodi kero hazipo tena,mafisadi wa mbolea na mbegu za wakulima wameshughulikiwa kikamilifu
Wamachinga wanafanya bishara bila bughudha kama unabisha njoo Dodoma ujionee walivyotengenezewa mazingira rafiki

NIDHAMU KAZINI
Kwa sasa unaweza fika ofisi yoyote na ukahudumiwa kama mfalme,urasimu sasa ishakuwa zilipendwa kama nyimbo ya wasafi

TABIA YA KUJITUMA KUFANYA KAZI
Rais ni msema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.Katujengea tabia ya kujituma katika kazi na kuthamini pesa kidogo tunayopata.Habari ya kuweka heshima baa chini ya JPM imekuewa zilipendwa ya wasafi

Kwa ufupi serikali imefanya na inaendelea kufanya mambo mengi makubwa kwa maslahi ya watanzania.Wapo wachache kwa sababu wanazo zijua wao wameendelea kuzipuuza juhudi hizi za serikali.Wapo waliodiriki kutoa lugha kali na zenye ukakasi dhidi ya Rais wetu.Lakini Rais kwa kuwa ni kiongozi shupavu na mwenye uthubutu mkubwa hatakatishwa tamaa na maneno ya hovyo ya wapinga maendeleo popote walipo nje na ndani ya nchi.Na mimi kama mtanzania wa kawaida kabisa nikiwakilisha watanzania wenzangu wengi tuko pamoja na wewe Rais wetu no matter what.
Wananchi hatutaki ujuvi wa kuongea na kupiga porojo tunataka maendeleo na hakika tunayaona kupitia serikali ya CCM chini ya JPM.

Long live JPM;HAPA KAZI TU
Jaruri,,0712207633
 

gemmanuel265

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2016
Messages
8,526
Points
2,000

gemmanuel265

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2016
8,526 2,000
Mshughulikiaji wa wanasiasa wa upinzani tumeona matokeo yake kwa Lissu hongera zake, lakini mwambie kabisa kuwa hawezi kushughulikia roho za wapinzani ambazo zitaishi tu hata baada ya umauti kuwafika isipokuwa ni mwili tu ndio anaweza ambao hauna thamani baada ya umauti
 

Joseverest

Verified Member
Joined
Sep 25, 2013
Messages
42,676
Points
2,000

Joseverest

Verified Member
Joined Sep 25, 2013
42,676 2,000
Magufuli mzugaji tu kama wale wa mizengwe.
We jamaa nikuulize swali?? Unaona faida gani kudukua/kuiba avatar yangu aisee...Yaani hii avatar nimeibadilisha kwa kuwa mtu mwingine aliniibia nimeweka na hii na wewe umeeiba unaweka kwako kirahisi tu??

Acha usanii mkuu, Kuna mamilioni ya picha (avatar) huko lakini unaona SAWA kutumia hii ya kwangu ambayo nimeweka na jina langu kabisa...

kiroho safi nakuomba ubadilishe hii avatar kwa maana mimo nitaonekana msanii na hata sifa mbaya huku jukwaani..

Hapa JF kila mtu ana avatar yake inayomtambulisha...nakuambia hivi kwa kuwa wewe ni mgeni na hata kama ni mwenyeji umefungua ID mpya hilo jambo unalofanya ni UZINGUAJI MKUU..

ACHA WIZI WA KUIBA AVATAR ZA WATU

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk

Sent from my iDevice using Tapatalk
 

64-bits

Senior Member
Joined
Aug 21, 2017
Messages
118
Points
225

64-bits

Senior Member
Joined Aug 21, 2017
118 225
Ànajaribu kucheza na saikolojia za watu wa kusifiwa..hahahaaa blaza amekwama Sana sikuizi wanasema pambana na hali yako hata ushowshine hupati
 

Forum statistics

Threads 1,381,428
Members 526,090
Posts 33,799,933
Top