Dr Magufuli & NSSF na ujenzi wa daraja la Kigamboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Magufuli & NSSF na ujenzi wa daraja la Kigamboni

Discussion in 'Major Projects in Tanzania' started by Saint Ivuga, Mar 27, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  Dr Magufuli awataka NSSF kuanza ujenzi wa daraja la Kigamboni mwaka huu

  By admin– March 25, 2011Posted in: Habari Mchanganyiko


  Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dar es salam

  Serikali imeliagiza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni na jirani yake.

  Daraja hilo linatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 130 hadi litakapokamilika kwa ajili ya matumizi ,ambapo NSSF itatoa bilioni 100 na Serikali bilioni 30.

  Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutembelea eneo la Kurasini Vijibweni ambapo Daraja hilo linatarajiwa kujengwa.

  Alisema kuwa asilimia 60 ya fedha walizonazo NSSF ambazo ni sawa na bilioni 100 zinatosha kuanza ujenzi wa daraja hilo wakati Wizara ya Ujenzi inatafuta asilimia 40 sawa zaidi ya bilioni 30 zilizobaki ili kukamilisha ujenzi wa daraja zima.

  “Tumezungumza siku nyingi kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ifike wakati tuanze kwani Serikali haiwezi kukosa asilimia 40 ya fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi huo” alisema Magufuli.

  Alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Serikali itajitahidi kutafuta fedha ikiwemo kutenga katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa Daraja hilo unakamilika kabla ya uongozi wa awamu ya nne haujamaliza muda wake.

  “NSSF nawaomba mjitahidi kukamilisha taratibu zote na kisha wiki ijayo (Ijumaa ) mtangaze zabuni ili ikiwezekana ujenzi uanze mara moja …ili likikamilika litusaidie katika kupunguza msongamano katikati ya Jiji kwani feli zitaanza kusafirisha abiria kwenda Tegeta na Bagamoyo badala ya kutumia barabara” alisistiza Dkt Magufuli.

  Alisema kuwa ki msingi NSSF kutokuwa na asilimia 100 za fedha zinazohitajika katika ujenzi wa daraja hilo hakuwezi kuwafanya wasianze mradi kwani katika mradi wowote mkandarasi anaanza kwa kulipwa fedha kiasi na kisha anaongezewa kulingana na anavyoondelea na mradi.

  Dkt. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa Daraja la Kigamboni ni muhimu kwa kuwa eneo hilo linachukua wananchi wengi wanaofanyakazi katikati ya Jiji la Dar es salam halikadhalika kuna miradi mingi inayotarajiwa kuanzishwa ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo katika Mikoa ya Mtwara na Lindi na kuwepo kwa viwanja 10,000 vya NSSF.

  Kufuatia umuhimu wa Daraja hilo Waziri huyo aliwahakikishia viongozi waandamizi wa NSSF kuwa Serikali kupitia Wizara yake watachangaia asilimia 40 ya fedha zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi wake.

  Alisema watatumia kipindi cha miaka mitatu kuhakikisha wanamaliza fedha hizo ambazo Serikali inapaswa kuchangia.

  Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Crescentius Magori alisema kuwa NSSF hadi hivi sasa ina kiasi cha bilioni 100 kati ya bilioni 130 zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi haraka.

  Alisema kuwa daraha hilo litakuwa na njia nne za magari na mbili kwa ajili ya watembea kwa miguu kupita.

  Hivyo Magoro amemuhakikishia Waziri huyo kuwa watajitahidi kutangaza zabuni wiki ijayo mara baada ya kuhakikishiwa kuwa Serikali itachangia asilimia 40 ya gharama za ujenzi wa daraja hilo.

  Daraja la kigamboni linatarajia kuchukua miaka mitatu hadi kukamilika pindi ujenzi wake utakapoanza.

  MWISHO
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  my take: Magufuli hizi zisije zikawa ni siasa tena na tunaomba haya uliyoyaongea yatendeke kwani tumechoka kusikia huu wimbo
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160

  Hivi kweli hili litafanyika kabla ya 2015? Yangu macho!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  si ameenda hadi kurasini kukagua, ngoja tusikilize kam hiyo zabuni itaitngazwa next week
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  Binafsi mpaka nione wanaanza kupeleka vifaa vya ujenzi site otherwise sitaki kuisumbua akili yangu kuamini vitu visivyoaminika - hivi project ya Mji mpya wa Kigamoni nayo inaanza April Mosi 2011?
   
 6. J

  Jikombe Senior Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Daraja linawezekana. Muhimu utashi wa dhati.
  Kutokana na muda uliobaki ya 4yrs na umuhimu wa daraja,nashahuri NSSF pamoja na serikali watumie design and build tendering kwani itapunguza muda mwingi wa procurement.
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Lini hii nchi itachwa kuendeshwa ki - Abunuasi?
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mi naona hyo miaka 3 maana yake nin! Mpka kukamilika ndo itakuwa gia ya kuombea kura yaleyale ya machinga complex ndo yatajitokeza muda si mrefu
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  wakuu zabuni ishatangazwa?? au ulikuwa ni wimbo
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,525
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  tanzaniaa
   
 11. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Huko Kurasini kakagua nini wakati hamna kitu?
   
 12. Jambazi

  Jambazi JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2016
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 14,445
  Likes Received: 12,629
  Trophy Points: 280
  Limesha zinduliwa madu
   
 13. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2017
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,642
  Likes Received: 3,019
  Trophy Points: 280
  VP bado upo ktk ndoto
   
 14. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2017
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,487
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Hala
  fu tunaambiwa gharama za ujenzi zilikua zaidi ya hizi.
   
 15. serio

  serio JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2017
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,929
  Likes Received: 1,144
  Trophy Points: 280
  Vipi, bado ni siasa?
   
Loading...