johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,819
- 141,727
Mtafiti wa masuala ya siasa za Afrika nchini Kenya ndugu Jonathan Otieno amesema Rais Magufuli ndiye mwenyekiti bora na aliyeleta mabadiliko makubwa kwenye chama chake ukilinganisha na wenyeviti wengine barani Afrika.
Otieno amesema ni juhudi binafsi za Dr Magufuli zilizorudisha uhai kwenye chama kikongwe cha CCM ambacho kilishaanza safari ya kuelekea kule iliko TANU ya Kenya.
Otieno anasisitiza kuwa katika utafiti mdogo alioufanya amegundua kuwa wananchi wa Tanzania wanamkubali zaidi Rais Magufuli kuliko wanavyoikubali CCM, ndio maana hata wapinzani wanahamia CCM kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na sio chama.
Hivyo ameshauri viongozi walio chini ya mwenyekiti kutobweteka bali wafanye kazi kwa bidii ili kukuza imani ya wananchi kwa chama.
Kadhalika Otieno amemtaja Maalim Seif wa Zanzibar kama kiongozi wa upinzani mwenye maono, jasiri na asiyekata tamaa.
Maendeleo hayana vyama!