Rais aliahidi kupunguza UKUBWA wa serikali, na GHARAMA za matumizi.
Pamoja na kupunguza idadi ya mawaziri bado tumeelemewa na gharama za "utitiri" wa Makatibu wakuu, pamoja na manaibu wao.
Binafsi sioni mantiki ya kuwa na makatibu wakuu wengi kiasi hiki alichoteua Dr.Magufuli.
Nchi hii ni kama vile tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele. Wakati wa Mwalimu Nyerere wizara zilikuwa chache, na hatukuwa na makatibu wakuu wengi mpaka inachanganya akili kama hawa wa Magufuli.
Wakati wa Mwalimu Nyerere njia za mawasiliano hazikuwa advanced kama sasa hivi. Hakukuwa na COMPUTERS, CELL PHONE, SIMU ZA UHAKIKA, BARABARA NZURI, etc etc kama ilivyo sasa hivi.
Wakati wa Mwalimu Nyerere Makatibu wakuu hawakuwa wasomi wa PhD na Maprofesa kama hawa wa Dr.Magufuli. Lakini makatibu wakuu hao walibeba majukumu[PORTFOLIO] mengi na makubwa kuliko hawa wa sasa hivi.
Kwa msingi huo serikali yetu ilitakiwa iwe ndogo kuliko wakati wowote ule kutokana na maendeleo hayo ktk vitendea kazi na nyenzo za mawasiliano.
Inashangaza Rais Magufuli kuwa na wizara yenye makatibu wakuu watatu, pamoja na naibu katibu mkuu, wakati wizara kama hiyo wakati wa utawala wa Baba wa Taifa ilikuwa na Katibu Mkuu na Naibu wake.
Huu "utitiri" wa Makatibu Wakuu hauendani na Falsafa ya "HapaKaziTu." Makatibu wakuu wa leo wana nyenzo rahisi na bora za mawasiliano. Wamesoma vizuri zaidi, ni Ma-PhD na Maprofesa. Sasa kwanini wabebe PORTFOLIO ndogo kuliko wale wa wakati wa Mwalimu Nyerere?
Naomba kuwasilisha.
cc Pasco, Nguruvi3, Manyerere Jackton, The Boss, MTAZAMO, Mchambuzi, Barubaru

Last edited by a moderator: