Dr. Magufuli na usanii wa Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili

Makombeni10

Member
Jul 29, 2015
34
64
Hebu tafakari kuhusu vitanda vya Muhimbili Magufuli alitoa kauli hiyo ijumaa jioni na jumamosi mchana vitanda vikawa tayari vimewasili Muhimbili.

Je pesa jizo alikabidhiwa mkurugenzi saa ngapi na kuanza process ya kuzitoa bank saa ngapi na afisa manunuzi wa Muhimbili alitafuta QUOTATIONS tatu saa ngapi na bodi yao ya manunuzi walikaa kikao saa ngapi ili kupitisha quotation moja ambayo itatumika ktk manunuzi hayo?

Je huyo supplier wa hizo vitanda alikuwa na stock kubwa kiasi hicho ambapo Muhimbili walipofika wakapewa chapuchapu?na ninavyojua manunuzi yanayozidi 10M huwezi kufanya kwa CHEQUE ni lazima ufanye kwa TISS sasa na mizunguko yote hiyo na jana ilikuwa ni siku yamapumziko je procedures zote za manunuzi ya UMMA zilifuatwa vipi jamani mbona wanaanza kutudanganya mapema hivyo?

Mimi ninavyooamini ni kwamba hivyo vitanda vitakuwa vilikuwa vimenunuliwa tayari kwa kipindi cha JK na jana ndo viliwasili wametaka kucheza na akili zetu ili tumpatie sifa rais lakini mimi najua hili haliwezekani kwa siku moja na HAIWEZEKANI KABISA tusidanganywe mchana kweupe. Namtakia rais ufanisi mwema na awe msema kweli kwani atakuwa mpenzi wa Mungu kama anavyosemaga aachane na mfumo wa ccm wa uongo uongo.
 
Hivxo bvitanda ni kwa ajili ya jengo jipya karibu na moi, wala siyo hivi vya magufuli! Ni wapambe tu wana wanajaribu kujipendekeza kwa magufulli kwa sababu wanamjua anayopenda sifa za kwenye media!
 
Ha ha ha haaaaaaa, daaah
nothing to add on that ila huenda ni kweli manunuzi yalifanyika kwa njia ya kielektroniki
 
Vile vitanda vimepelekwa kwny jengo jipya la MOI, Magufuli alisema vitanda vipelekwe Muhimbili, MOI na Muhimbili ni institutions mbili tofauti kabisa, usanii wa Magufuli ulianzia kwny ziara aliyofsnya Muhimbili kwa kutengua uteuzi wa DG wa hospital na Board of Directors wakati tayari walishamaliza mda wao ajira!

Ni kweli kuwa issue zinazohusu hospital huwa hazihitaji sana Government Procurement Procedures lakini kwa hili la vitanda ni usanii uliopitiliza!

Magufuli aangalie sana, nguvu yake inaweza ikawa ni zaidi ya gesi ya Fanta#
 
Makombeni10

Bwana mdogo kauli ya raisi haina quotation kama unavyodhani na ile pesa kilichofanyika ni kuhamishia MSD tu ambayo ni ya serikali na na wao ndo wamesupply vitanda,we subiri mchakato wa quotation kama utaiusikia after all ile hela si ya serikali ilichangwa na wafadhili wa sherehe za bunge kama crdb,nmb na wengine kwa hiyo haina cha kuulizwa taratibu za manunuzi ukumbuke pia magufuli ana mpango wa kubadilisha hii sheria kama ulimsikiliza kwenye hotuba yake
 
Last edited by a moderator:
si mheshimiwa raisi, ikulu, bunge wala muhimbili ambao wamesema vile vitanda vimetokana na uamuzi wa raisi juu ya pesa za tafrija ya bunge. ila ni wapambe ambao wananjaa ya angalau habari njema kutoka serikali ya ccm ndio wameleta stori. naamini pesa hizo alizosema raisi zikitumika basi vyombo husika vitatutaarifu wananchi.
 
Mchakato wa kuhamisha fedha huko bungeni kwenda Muhimbili kwa TISS it takes 24 hrs achana na mchakato wa manunuzi. Lakini inawezekana kama Muhimbili tayari wana shortlist ya suppliers, so wanajua bei na kila kitu kwa hiyo issue inakuwa kuandika LPO malipo yatafuata baada ya supply ila swali la kujiuliza siku hiyo hiyo LPO iliandikwa na kusainiwa siku hiyo hiyo ilipelekwa msd na baada ya kupokea tu taratibu za ku deliver zikakamilika hapo si sawa labda kwa kuruka other procedures
 
Back
Top Bottom