Dr. Magufuli na usanii wa Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili

Tunahitaji kumpa sapoti kubwa Rais na si kupinha kila kitu bwana, isitoshe Rais kufanya maamuzi magumu anajenga maadui wengi sana wananchi tumpe sapoti kubwa
haha..yaani yeye achagua njia ngumu na mbaya halafu sisi tum support?Tukimwambia achukue njia rahisi ili nasi iwe rahisi kumpa ushirikiano hataki?Watz sasa muache jilisha upuuzi.
 
Angalia utapigwa ban!
Wanajua ndilo nalitaka. Niliwaambia wanifute hawakutaka.Hakuna mods wa hovyo km wa JF ktk miaka hii.Wana edit thread za watu, wanaanzisha nyingine ili waunganishe thread wasizotaka,Wanafuta nyingine.HAwajui hata nini ni muhimu ktk kuibu fikra.Kwao kila thread inafanana na nyingine au inawaumiza watawala.
 
Msd wana vitanda tayari. Suala ni fedha za kuvinunua. Kama pesa imepatikana, unavipata hata ndani ya nusu saa.
Ninachokupenda ni jinsi ulivyo na majibu ya short cut..Kwani MSD ni ya nani?Na Kwanini wasitoe tendering?Ijumaa muda ule,na Jmosi serikali haifanyi kazi , ilikuweje hayo yakafanyika namna hiyo?Magufuli kavunja sheria ya manunuzi pia.
 
msd ni agency ya serikali kusambaza madawa na vifaa tiba hivyo bei inajulikana na kwa kuwa ni agency ya serikali sio lazima walipwe cash siku hiyo hiyo hata kampuni binafsi zinafanya biashara kwa mkopo. angalizo mi ni ukawa asilia
Shida ni kwamba sheria za manunuzi zilivunjwa.Na huo uharaka haukuwepo kihivyo.
 
Mchakato wa kuhamisha fedha huko bungeni kwenda Muhimbili kwa TISS it takes 24 hrs achana na mchakato wa manunuzi. Lakini inawezekana kama Muhimbili tayari wana shortlist ya suppliers, so wanajua bei na kila kitu kwa hiyo issue inakuwa kuandika LPO malipo yatafuata baada ya supply ila swali la kujiuliza siku hiyo hiyo LPO iliandikwa na kusainiwa siku hiyo hiyo ilipelekwa msd na baada ya kupokea tu taratibu za ku deliver zikakamilika hapo si sawa labda kwa kuruka other procedures
Aha supply ya LPO kwani muhimbili walikuwa na Make/Model ya hivyo vitanda?Usanini unachosha na kuumbua.Km alivyoiba show kwa TB Joshua halfu akaachwa siku ya kuapishwa?
 
Wewe ni Thomaso utabaki na umbumbumbu wako hivyohivyo. Hizo fedha siku ya Ijumaa alikuwa anatolea ufafanuzi wa maamuzi waliokuwa wamekubaliana na Speaker allipopelekewa kwa ajili ya kuidhinisha. Na kama ulimsikia vizuri siku ile alipokuwa anazungumzia akasema naambiwa tayari fedha zimekwisha tolewa na zimewafikia. Aidha Moi na mhimbili kuwa taasis tofauti hilo si dhani kama ni suala la kujadili kwa mwenye akili kubwa maana Muhimbili ndio taasis ya kwanza na kubeba jina la hospital hiyo ya Rufaa. hata wa kijijin anaelewa hivyo, Moi imejengwa ndani ya maeneo ya muhimbili. na ndio maana kuna mkakati wa taasisi hiyo kupelekwa Mbweni Teta kuiondoa hapo muhimbili. Tujadilini vitu vya msingi kwa maendeleo ya Taifa. Sio kudhihaki kazi nzuri inayofanywa na Rais hata kama ni ndogo kiasi gani lakin kumbuka inathamani kubwa kwa wananchi wa kawaida. Mungu atatulipa mema tuyatendayo hata kama ni madogo kiasi cha uzani wa mdudu chungu. TUJISAHIHISHE TUSIWE WANASIASA WAPINZANI, TUWE WANASIASA MBADALA.
Usiwe mtoto kihivyo.Unajua Magufuli aliingia saa ngapi ktk hiyo tafrija,na muda gani alitangaza hivyo?Hiyo saa hakuna mtu kwa office labda awe kaarifiwa mapema.
 
unawezekana marekebisho ya sheria ya manunuzi nawe ukawa miongoni mwa wahanga watakaopata madhara.Vitandani vipi Msd bei inajulikana,Rais anazo fedha mikononi,wewe unashauri kwanza aitishe kikao cha bodi waanze kupiga hela Kama ya vitandani 70 Halafu waanze kutafuta watu wa tenda waweke 10 yao pale huku vitandani vipi pale Keko Msd.Nyie ndo wale wale.Kwanza bodi hiyo alishaipiga kiberiti.watu wa sample yako mmetukwaza muda mrefu Mkombozi wa taifa kashatua.Ahsante Mungu.Magufuli usiwaachie pumzi hao.Hapa kazi tu.
l
 
Hao wabunge walichangaisha cash au kwa cheque na mpesa?What a ajoke?wote walikuwa bank moja na msd hadi cheque ziweze mature?hizo cash walideposit lini?Au magufuli anataka tuambia kwamba walishafanya sanaa mapema.
 
MSD wametoa maelezo. Walijulishwamapema kabla hajatoa tamko rasmi.
Km msd walishakuwa nayo ktk stock kwanini tena walisubiri kulipwa hela na serikali wakati nao ni mradi wa serikali?Ina maana taasisi ya serikali inaweza igomea serikali kupeleka vitanda kwa wananchi walipa kodi?Nani anaimiliki MSD km si wananchi?What a bunch of conflicts.
 
Hebu tafakari kuhusu vitanda vya Muhimbili Magufuli alitoa kauli hiyo ijumaa jioni na jumamosi mchana vitanda vikawa tayari vimewasili Muhimbili.

Je pesa jizo alikabidhiwa mkurugenzi saa ngapi na kuanza process ya kuzitoa bank saa ngapi na afisa manunuzi wa Muhimbili alitafuta QUOTATIONS tatu saa ngapi na bodi yao ya manunuzi walikaa kikao saa ngapi ili kupitisha quotation moja ambayo itatumika ktk manunuzi hayo?

Je huyo supplier wa hizo vitanda alikuwa na stock kubwa kiasi hicho ambapo Muhimbili walipofika wakapewa chapuchapu?na ninavyojua manunuzi yanayozidi 10M huwezi kufanya kwa CHEQUE ni lazima ufanye kwa TISS sasa na mizunguko yote hiyo na jana ilikuwa ni siku yamapumziko je procedures zote za manunuzi ya UMMA zilifuatwa vipi jamani mbona wanaanza kutudanganya mapema hivyo?

Mimi ninavyooamini ni kwamba hivyo vitanda vitakuwa vilikuwa vimenunuliwa tayari kwa kipindi cha JK na jana ndo viliwasili wametaka kucheza na akili zetu ili tumpatie sifa rais lakini mimi najua hili haliwezekani kwa siku moja na HAIWEZEKANI KABISA tusidanganywe mchana kweupe. Namtakia rais ufanisi mwema na awe msema kweli kwani atakuwa mpenzi wa Mungu kama anavyosemaga aachane na mfumo wa ccm wa uongo uongo.

Unaumwa!!...na ukitaka kupona badilika ili dawa ikuingie. Kajifunze na uijue MSD kisha uje ukiri mwwnyewe kuwa umepona maradhi yanayokusumbua.
 
Msd ndio supply wa dawa na vifaa vya hosp serikalini na bei zao wanatoa za mwaka mzima na haihitaji quotation kwani bei zao hazina kodi ndio maana kesi nyingi CAG kwenye halmashauri ni kuwa hawajapeleka oda msd ili wapate out of stock ili waweze kununua kwa wazabuni ambao wako shortlisted na taasisi husika zaidi ya hapo siwezi kutoa siri maana na mm ni mdau watakuja kubana nikashindwa kupata ada za watoto
 
Wakuu jana nimeona taarifa ambazo ziliniacha na bumbuazi kuhusu kitanda maalum cha kuzalishia watoto eti bei yake ni milioni 2 .5 nimejiuliza ni kitanda cha namna gani cjaelewa. Hebu wenye taarifa zaidi wanijuze maana naona kama wanacheza sarakas kwani badala waongeze majengo wao wanaongeza vitanda kwani kuna jengo ambalo halikuwa na vitanda na kwanini wacweke vitanda vya double deckar ndo kulala chini ingekuwa historia
 
Wakuu jana nimeona taarifa ambazo ziliniacha na bumbuazi kuhusu kitanda maalum cha kuzalishia watoto eti bei yake ni milioni 2 .5 nimejiuliza ni kitanda cha namna gani cjaelewa. Hebu wenye taarifa zaidi wanijuze maana naona kama wanacheza sarakas kwani badala waongeze majengo wao wanaongeza vitanda kwani kuna jengo ambalo halikuwa na vitanda na kwanini wacweke vitanda vya double deckar ndo kulala chini ingekuwa historia


Inawezekana kabisa tena hata ikawa zaidi kwani vitanda vya Hospitali siyo kama vitanda vyetu vya nyumbani vina mambo mengi maalumu kulingana na mahitaji ya mgonjwa, vingine vina magodoro maalumu pia!
 
Back
Top Bottom