shikulaushinye
JF-Expert Member
- Aug 29, 2014
- 828
- 456
Hebu tafakari kuhusu vitanda vya Muhimbili Magufuli alitoa kauli hiyo ijumaa jioni na jumamosi mchana vitanda vikawa tayari vimewasili Muhimbili.
Je pesa jizo alikabidhiwa mkurugenzi saa ngapi na kuanza process ya kuzitoa bank saa ngapi na afisa manunuzi wa Muhimbili alitafuta QUOTATIONS tatu saa ngapi na bodi yao ya manunuzi walikaa kikao saa ngapi ili kupitisha quotation moja ambayo itatumika ktk manunuzi hayo?
Je huyo supplier wa hizo vitanda alikuwa na stock kubwa kiasi hicho ambapo Muhimbili walipofika wakapewa chapuchapu?na ninavyojua manunuzi yanayozidi 10M huwezi kufanya kwa CHEQUE ni lazima ufanye kwa TISS sasa na mizunguko yote hiyo na jana ilikuwa ni siku yamapumziko je procedures zote za manunuzi ya UMMA zilifuatwa vipi jamani mbona wanaanza kutudanganya mapema hivyo?
Mimi ninavyooamini ni kwamba hivyo vitanda vitakuwa vilikuwa vimenunuliwa tayari kwa kipindi cha JK na jana ndo viliwasili wametaka kucheza na akili zetu ili tumpatie sifa rais lakini mimi najua hili haliwezekani kwa siku moja na HAIWEZEKANI KABISA tusidanganywe mchana kweupe. Namtakia rais ufanisi mwema na awe msema kweli kwani atakuwa mpenzi wa Mungu kama anavyosemaga aachane na mfumo wa ccm wa uongo uongo.
Ndiyo maana procurement ni professional siyo kila mtu anaweza kufanya, unafahamu aina za taratibu manunuzi. unajua km kuna single source, emergency procurement, direct buy limit?