Dr Magufuli, mteue W.Malecela DC Kinondoni

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
13,783
2,000
Mheshimiwa,Mtukufu Dr John Pombe Magufuli kwa heshima na tahadhima nakusihi na kukuangua chini ya Miguu yako mpatie nafasi kijana wa zamani Willy Malecela ukuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Kwanza nikupongeze na kukutakia afya njema katika kutekeleza majukumu yako mazito kwa taifa letu changa.Nikupongeze pia kwa kuanza vyema katika nafasi yako nyingine ya ukigoda wa chama chetu pendwa.Umejitahidi kuondoa masalia ya yule rafiki yetu wa Msoga lakini safari hii haujawatupa wengine wamekuwa wakuu wa Mikoa,wengine Mabalozi na wengine wanasubiria nafasi kedekede ulizopewa na katiba yetu inayohitaji mabadiliko makubwa.

Ngoja nirejee kusudio la kuandia waraka huu kwakuwa najua utakufikia basi natarajia utafanyia kazi mawazo yangu.Kwakuwa yule Mheshimiwa aliyekuwa anapambana na chama chetu umemwondoa Wilaya ya Ubongo na sasa umempatia kile cheo cha kubwabwaja pasipo kutumia akili nakuomba umkumbuke Bwana Willy Malecela katika nafasi hiyo hasa ukizingatia heshima ya familia ya Malecela jinsi ilivyokumbwa na misukosuko tangu utawala wa awamu ya tano uingie madarakani.Mama Anna Kilango ulimtimua katika nafasi ya ukuu wa Mkoa kabla mambo hayajatulia jana umemtumbua Mtoto wa Mzee Malecela Dr Mwela Malecela katika nafasi ya Mkurugenzi NIMR.

Kwakuwa wewe ni Mtukufu teuzi zako hazihojiwi wala hazipigiwi kura kama kuleee kwa Mzee Trump basi ipooze familia ya Mzee Malecela kwa kumteua Kijana wake Willy ukuu wa Wilaya ya Ubungu unamtosha sana familia itafarijika na kupunguza machungu na kinyongo

Ni hayo tu Mtukufu Dr Magufuli nafasi nyingine zikitokezea hasa tukizingatia tumbua tumbua haijakoma unikumbuke na mimi katika utukufu wako niko tayari kulitumikia taifa letu katika nafasi za Ukuu wa Wilaya,Ukuu wa Mkoa,Ubalozi,Ukurugenzi,katibu mkuu wizara,katibu tawala mkoa na wilaya zote hizo ziko chini ya mamlaka yako ya uteuzi na utumbuaji.

Nawasilisha kwa unyenyekevu wa hali ya juu.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,905

Mawazo yako yanaheshimiwa.
 
Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
13,783
2,000
Willy Malecela = Le Mutuz
Haswaaa ebu fikiria kuelekea sikukuu ya Xmas na Mwaka mpya familia ikikutana Dodoma Mama analia Mtoto analia unafikiri machozi yao yataenda bure.Lakini Le Mutuz akitinga na Kilimo kwanza la Mkuu wa Wilaya walau machungu yatapungua kiduchu.
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
10,608
2,000
Hata wewe ni Mkuu wa Wilaya nyumbani kwako usihofu sana,hii ndio dunia kuna watawala na watawaliwa,kuna wapiganaji na wapiganishaji,kuna watukufu na wasiokuwa na utukufu ridhika na hali yao.
***
Kwa hiyo kuna -class1 citizen na class 2,ha ha ha.../ mm nipo class 3 au 4.ambao ndio kipenzi cha rais wa wanyonge...
 
Jan 12, 2014
93
125
Ukifanya ovyo unatumbuliwa bila kujari udungu, ufamilia wala ukoo ufanisi wako ndio utakao kufanya udumu katika nafasi yako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom