Dr Magufuli au Dr Slaa rais wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Magufuli au Dr Slaa rais wangu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kachanchabuseta, May 18, 2010.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  WanaJF haya ni maoni yangu, nimechekecha na kuchuja nakaona mpaka sasa sina Rais. Nakawaza saaana nikaona kati ya Dr Slaa au Dr Pombe ndo wangefaa na wanafaa kuwa Rais wangu kwa wakati huu na wakati ujao. Hapa siangalii mtu anatoka chama gani these are my President

  WanaJF mnasemaje kuhusu hawa wawili HIZI NI HISIA ZANGU TU
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Wanasifa za urais - wasomi, wanasoma na kuelewa, wako wazi, hawataki ubabaishaji, sio vigeugeu (mara utani mara ohh), wakianza kazi wanahakikisha wameimaliza: tatizo mifumo ya vyama!!
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu yaana hapatungekuwa na mfumo wa vyama kama UK etc tungekuwa na Viongozi bora sio bora viongozi
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nami Babu nakubaliana nawe. Umetafakari vizuri. Ngoma, ni watafikaje huko?
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu Babuyao(kweli wewe babuyao) Dr Slaa anaweza kubadilisha mawazo kwa nguvu ya umma Dr Pombe bado sijamsikia lakini kama atasikiliza nguvu ya umma apitie CCJ etc
   
 6. M

  Mkono JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii nchi ingekaa juu ya mstali kama mh Slaa awe rais na mhMagufuli PM Sendeka waziri wa mambo ya ndani.
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa safu hii nchi ingenyooka
   
 8. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hiyo safu ni nzuri hila nani ataipitisha kwa manufaa ya watanzania? Kwa kuwa wanafaa washauri watafute chama au waungane na Mtikila ktk kuhakikisha mgombea binafsi anakubalika. Otherwise nnakubaliana na mtoa hoja
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu mgombea binafsi mahakama itapigwa zengwe mpaka sera hii isitokee Tanzania, na mkuu huyu:flypig::flypig: hawezi kukubali hii sheria ipitishwe na mahakama
   
 10. K

  Kikambala Senior Member

  #10
  May 19, 2010
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  imekaa vizuri sana rais Dr slaa,magufuli Pm mambo ya ndani Col mfuru Rc wa musoma
   
 11. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni watu waadilifu, wenye akili, hawatabasamu bila sababu, hawafanyi utani kwenye masuala nyeti ya nchi, wanawaheshimu wafanyakazi, hawaendekezi mambo ya ngono na sio washirikina.
   
 12. H

  Haika JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hizi ni ndoto zetu wengi wenye kupenda kuona u kweli, japo unauma. Pia tuko tayari kuvumilia ili tunyooshe mstari wa kujenga nchi yetu.

  Naunga mkono hoja, ila kuwezekana kwake kunahitaji nguvu yetu wengi, kushinikiza kuwepo sera ya mgombea binafsi, japo uchaguzi wa 2015.

  Kuna anaefahamu namna ya kushiriki katika kushinikiza hilo swala? mimi ningependa kuwa mmoja wa maactivist wa hilo jambo, tusimuachie mtikila tu. Imekuwa rahisi kushambuliwa na kubadili agenda, kwa kwa kumshambia ishu zake nyingine.
   
 13. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I berg to differ!

  Rais awe Dr. Salim then watendaji wawe kina Slaa, Magufuli and the like!
  A good salesman doesn't necesarily make a good manager!
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Dr Salim bado hatujasikia msimamo wake tokea 2005 alipopigwa majungu mpaka leo kimya labda ataibukia CCJ au CHADEMA
   
 15. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kwa upande wangu mimi ningependa safu hii:

  Rais - Mizengo K. Pinda
  Makamu - Dr. Magufuli
  PM - Dr. Slaa

  Reason; Magufuli na Slaa ni watendaji zaidi na ni wazuri kwenye kukimbiza mwenge wa baraza la mawaziri. Slaa anatakiwa kubaki bungeni ili awakimbize wale wazee wanaosinzia. Pinda anafaa kupanda juu kidogo kwani ameonyesha uwezo wake kwenye u-PM and najua anashindwa tu kufanya mambo kwa sababu ya "SYSTEM". Pinda ana hekima fulani kwenye kuongea na kujibu hoja, huwezi mkuta akijigamba kuwa, "hata msiponichagua poa tu". Ameonekana akihandle issues nyingi na migogoro mbali mbali na the way anavyorespond to issues. Pinda pia ananitia hamasa kutokana na uwezo wa kurespond to questions faster tofauti na ndugu yetu ambaye kama hajaandaliwa lazima tutie aibu. Fuatilia interviews zake za kushtukizwa then mtaniambia wadau. Magufuli tumeona maneno yake kwenye wizara ya ardhi nyumba na makazi alivyopunguza uozo. Angepewa muda kidogo tu, tusingesikia migogoro ya kijinga ya ardhi inayosababishwa na wizara. Kaletwa kwenye mifugo, balaa lake tumeliona. Aliwekwa kwenye miundo mbinu, mchaka mchaka wa barabara mliouona.

  Nawasilisha hoja ndugu wajumbe.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ipo kazi kubwa sana kwa mtu kuweza kuupata uongozi wa juu katika nchi. Kikubwa ambavyo ni vigezo vya awali kabisa ni historia yako, elimu yako, na uadilifu wako na utendaji wako kwa jamii kupitia nafasi mbalimbali alizoshika.

  Sasa Dr Slaa kidogo upo wasiwasi pamoja na utendaji wake mzuri lakini elimu yake inatia mashaka kwa upande mwingine wa shiling. Je ataweza kuwa muadilifu kwa wenye imani tofauti na yeye? Je hatakuwa kama Chiluba huyu kwa kuitangaza TZ ni nchi ya dhehebu lake?

  naamini wazi kama angekuwa mtu makini sana katika uongozi wake hata chama chake kisingepata kashfa hususan hizi za ukabila.


  Magufuli ni mzuri sana lakini angalieni utendaji wake wakati wa Mkapa. Alijaza kabila lake ofisini kwake ujenzi na hata kuzigawa nyumba sio kwa ndugu zake tu bali hata kwa vimada wake.

  nafikiri kashfa hii pekee inamtosha kumpunguzia marks zake za kugonga ikulu.

  Pinda hana kashfa yoyote na mchapa kazi mzuri
   
 17. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  jamani nafikiri pinda tumtoe ni mchapa kazi lakini system inamkaba. hao wengine poa tuwashawishi wagombee.naunga mkono hoja
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kuchagua viongozi na vizuri kuangalia record zao za utendaji wao na elimu zao.

  Dr Slaa anafanya vizuri sana kama mbunge lakini hapo kwenye ngazi ya juu ya uongozi wa nchi ni pazito kidigo kwake SABABU YA ELIMU YAKE. Hii itatia sana mashaka kwa watu walio na imani tofauti na yeye na kuona kama hataweza kuwa kama CHILUBA ambaye alitangaza wazi zambia ni nchi ya imani yake. Yeye inachomsibu ni makuzi yake na elimu yake.

  Vile vile kama angekuwa muadilifi basi aanze kusafisha chama chake kuindokane na jinamizi la UKANDA.

  Dr Magufuri huyu ni mtendaji mzuri ila kuna vikashfa alipokuwa waziri wa Ujenzi aliweka watu wengi wa kanda yake wizarani na vile alizigawa nyumba za Serikali kwa ndugu zake na nyingine kwa vimada wake.

  Anapendelea sana watu wa kwake kwani kwa wale wa kule wataona Gengerema hakuna lami ila lami imeanzia kasamwa, geita, Buseresere, Bwanga , Buziku na kuingia chato. Vipi wa Sengerema hawastahiki lami kuunganisha na mwanza?

  Pinda na Salim sioni hawa kama wana kashfa.
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu mchango wako Mzuri lakini umekaa kiitikadi na kisisimu
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  usihofu kaka, mabadiliko yana matatizo yake lakini kuliko ccm ya sasa tupo tayari hata kumpa mwislam wa siasa kali kwa miaka mitano tu.slaa nafikiri hana shida ila hataweza kumfurahisha kila mtu kama ambavyo marais wate walio pita hawkuafurahisha kila mtu.mfano mwinyi aliipeleka tz oic hilo lilikuwa kosa. kikwete anaingiza mambo ya kidini kwenye yaasisi za uma hayo ni makosa[baada ya utawala wake ndio utaona vizuri makosa yake]kwa hiyo nashauri tusiogope mabadiliko,uwe na amani hatutapata rais ambae hana mapungufu tukimpata asiye na dini yoyote nafikiri itakuwa balaa zaidi.
   
Loading...