Dr. Magufuli apindua mipango ya ufisadi TANROADS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Magufuli apindua mipango ya ufisadi TANROADS

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Nov 29, 2010.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  SIKU moja baada ya kuapishwa,Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amemtaka Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Ephraim Mrema kusimamisha mara moja nafasi za kazi za mameneja wa mikoa alizozitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa zipo wazi.

  Magufuli amewataka mameneja wote ambao wamesimamishwa kazi, warudi kazini mara moja na kwamba tangazo hilo halina nguvu.

  Kutokana na uamuzi huo, Dk. Magufuli amemtaka Mrema kutoa tangazo haraka kuanzia leo katika vyombo vya habari, kusitisha tangazo lake la awali la kuwasimamisha kazi mameneja wa Tanroads mikoani kwa kuwa hatua aliyoichukua inaonekana ni ya kulipizana visasi.

  Dk. Magufuli alitoa maagizo hayo jana, Dar es Salaam katika mkutano wake na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali vya wizara hiyo wakati akijitambulisha kwao.

  Katika maagizo yake, Dk Magufuli alimtaka Mrema asifanye kazi kama mtu anayeondoka kesho, bali atekeleze majukumu yake kama atafanya kazi hiyo kwa miaka 100 ijayo.

  “Tanroads jipangeni sawasawa, blaablaa ziishe, wewe Mkurugenzi uliona nafasi yako inatangazwa na wewe ukaamua kutangaza za mameneja wa mikoa ili kuchomeana na kila kitu kisimamishwe, kwanini ulitangaza kwamba waliopo hawachapi kazi?”

  Alihoji Dk. Magufuli. Aliagiza mameneja wa mikoa waelezwe mara moja kuwa wamerudishwa kazini isipokuwa kwa nafasi ya Dodoma tu ambayo meneja wake hayupo. “

  Nakuagiza Mrema, uandike katika vyombo vya habari kuwa umefuta tangazo hilo na mengine yatafuatia.”

  Alimtaka Mkurugenzi huyo wa Tanroads, kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba kama Waziri na Naibu wake Dk. Harrison Mwakyembe watauliza jambo lolote, wajibiwe haraka, la sivyo itakuwa ni dharau.

  Mkurugenzi huyo wa Tanroads inadaiwa kipindi chake cha kuongoza wakala huo kimemalizika kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi, lakini ameendelea kukalia ofisi hiyo.

  Dk. Magufuli alisema wao hawakufika katika wizara hiyo kwa ajili ya kutengua Torati, bali kuitekeleza na kwamba wanaweza kufanya kazi na yeyote na kusisitiza kuwa yaliyopita yaachwe na wafanye kazi kwa pamoja.

  “Tushirikiane, tupendane, majungu yaishe, tuache rushwa kwa kuwa tutawategeshea hata fedha ya Polisi… na hivi ndio maana Rais ametuteua mimi na Naibu mwenye taaluma ya Sheria,” alisema.

  Kuhusu rushwa, waziri huyo aliahidi kupanda lori lililozidisha uzito na kutoa rushwa na akasema akikamilisha kazi hiyo watakaohusika watamtambua. Aliwataka watendaji wa mizani kusimamia sheria, kukamata magari na kupiga faini na kuteremsha mizigo bila kujali mmiliki wa gari au mzigo.

  Awali akizungumza katika mkutano huo, Dk. Mwakyembe, alisema uteuzi wao hautakuwa na maana kama wataachia kirusi aliyeingia katika Wizara hiyo na kutia doa kuendelea.

  Alisema mwanzoni wizara hiyo ilikuwa mfano wa kuigwa lakini anashangaa kuona ufanisi umepotea na sasa imekuwa sehemu ya kunyoosheana vidole bila kujua ni kirusi gani huyo aliyeingia.

  Alisisitiza kuwa sasa wanahitaji kuongea lugha moja na kuimba wimbo mmoja na kuifanya wizara hiyo kuwa ya mfano na kuagiza taarifa za kukinzana zisipewe nafasi kwa kuwa hawaendeshi wizara kwa majungu na umbeya.
   
 2. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  DU!!!!
   
 3. HIMO ONE

  HIMO ONE Senior Member

  #3
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana na hii pombe mwaka huu lazima wainywe huko ujenzi na tanroads
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hilo huyo jamaaa ni jembe achana naye kabisa yupo kikazi zaidi.
   
 5. F

  Ferds JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  lazima wampe ulizi kama alivyofanya baba ben la sivyo ....................
   
 6. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamani huyu jamaa hii wizara anaiweza sana,ilikuwa kiburi chao tu.
   
 7. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kuhusu rushwa, waziri huyo aliahidi kupanda lori lililozidisha uzito na kutoa rushwa na akasema akikamilisha kazi hiyo watakaohusika watamtambua. Aliwataka watendaji wa mizani kusimamia sheria, kukamata magari na kupiga faini na kuteremsha mizigo bila kujali mmiliki wa gari au mzigo.

  Teh teh teh! watakoma jamaa nadhani hawana raha kabisa saa hizi
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nashindwa kupata picha iwapo huyu jamaa angekuwa ndiye mtoto wa Mkulima Pinda wetu!
   
 9. minda

  minda JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  inavyosemekana huyo bw anabebwa na wazito.
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kwa hali hii, daraja la Kigamboni linawezekana!
   
 11. M

  Mnyalu wa Kweli JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Pamoja na ukweli kuwa mimi si shabiki wa rangi ya kijani hawa jamaa wawili nawakubali sana. Ephraim Mrema sasa akae chonjo pale Tanirodi, maana sasa ni saa mbaya.
   
 12. p

  posh77 Member

  #12
  Nov 29, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Go Mgufuli go,wamezoea kufanya kazi kwa uzoefu na kutokuwa serious ,fanya kazi baba Mungu anakuona na atakulipa tu,twatutakia maisha marefu ikiwezekana uzunguke wizara zote unafaa sana
   
 13. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  mtoto wa mkulima anahemea madaraka tu pale... yale madaraka ni makubwa kwake mambo ya kujipendekeza kumridhisha kila mtu yanaharibu kazi always...
   
 14. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kazi imeshaanza na moto utawaka ..:embarrassed::embarrassed:
   
 15. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Kama ni mori, basi huu umeanzia kileleni. Natumai nguvu hii iliyooneshwa asubuhi hii itaendelea mchana hadi jioni. Hadi atakapochoka, atakuwa ametiisha adabu kidogo na heshima kurudi mahala pake.

  Magufuli baba, lianzishe tu, barabara michosho zishatukifu, majengo yanayoanguka hovyo, sasa basi!

  Bofya kifute hapo umsikilize kiduuuchu kilichorekodiwa kupitia TBC one. Taarifa ya maandishi inafuatia...  Siku moja tu baada ya kuapishwa, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na naibu wake Dk. Harrison Mwakyembe wamefanya kikao na Watumishi wa Wizara na kutoa maagizo kadha wa kadha.

  Magufuli vs TanRoads vs Mrema

  Mojawapo ya maagizo makuu, Waziri Magufuli alitengua maamuzi ya Mkurugenzi Wakala wa Barabara nchini (TanRoads), Ephraim Mrema na kuagiza mameneja wa mikoa waelezwe mara moja kuwa wamerudishwa kazini isipokuwa kwa nafasi ya Dodoma tu ambayo meneja wake hayupo. "Futeni hiyo mara moja, mameneja wa sasa waliopo nasema waendelee na kazi, maamuzi mliyochukua hayafai," akamwagiza Mrema kutoa tangazo haraka kuanzia leo katika vyombo vya habari, kusitisha tangazo lake la awali la kuwasimamisha kazi mameneja wa TanRoads mikoani kwa kuwa hatua aliyoichukua inaonekana ni ya kulipizana visasi. "Nimesoma katika gazeti moja wiki hii, umetangaza nafasi za kazi…kuna utaratibu kwa kazi zozote zinapotangazwa, hivyo waandikie vyombo vyahabari kuwa umefuta nafasi hizo..." "Nakuagiza Mrema, uandike katika vyombo vya habari kuwa umefuta tangazo hilo na mengine yatafuatia." alisema na kukamtaka Mrema asifanye kazi kama mtu anayeondoka kesho, bali atekeleze majukumu yake kama atafanya kazi hiyo kwa miaka 100 ijayo.

  "TanRoads jipangeni sawasawa, blaablaa ziishe, wewe Mkurugenzi uliona nafasi yako inatangazwa na wewe ukaamua kutangaza za mameneja wa mikoa ili kuchomeana na kila kitu kisimamishwe, kwanini ulitangaza kwamba waliopo hawachapi kazi?" alihoji Dk. Magufuli.

  Kutokana na umuhimu wa usimamizi wa ujenzi wa barabara, Akamtaka Mkurugenzi huyo wa TanRoads, kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba kama Waziri na Naibu wake Dk. Harrison Mwakyembe watauliza jambo lolote, wajibiwe haraka, la sivyo itakuwa ni dharau. Mkurugenzi huyo wa TanRoads inadaiwa kuwa kipindi chake cha kuongoza wakala huo kimemalizika kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi, lakini ameendelea kukalia ofisi hiyo.

  Kunyang'anywa nyumba na kufikishwa mahakamani

  Waziri Magufuli ameagiza wote waliouziwa nyumba za serikali ambao hawajamaliza madeni yao kufikishwa mahakamani pamoja na kunyangíanywa nyumba hizo. "Muwaandikie barua wote walipe au muwapeleke mahakamani na wasipolipa wanyangíanywe," alisema Magufuli na kushangaa kwa nini Wizara inahangaika suala la uhaba wa nyumba za watumishi wakati kuna pesa nyingine nje. Akasema kwa kawaida, hana lugha ya kidiplomasia na amewataka wenye madeni kuyalipa mara moja.

  Magufuli vs Rushwa na Mizani

  Dk. Magufuli alisema kasi ya ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege imepungua kwa kiasi kikubwa, huku wafanyakazi wengi wakijihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwapa kazi makandarasi wababaishaji ambao lengo lao ni kuchuma. Waziri Magufuli aliahidi kupanda lori lililozidisha uzito na kutoa rushwa na akasema akikamilisha kazi hiyo watakaohusika watamtambua. Aliwataka watendaji wa mizani kusimamia sheria, kukamata magari na kupiga faini na kuteremsha mizigo bila kujali mmiliki wa gari au mzigo.

  "Ukienda barabara ya Mandela, hujui kama kuna mkandarasi kwenye eneo lile ujenzi wa barabara nyingi kasi yake si nzuri, kama mkandarasi wa Mandela rafiki yako hafanyi kazi vizuri fukuza. Lazima niwaambiwe ukweli, mtu asiyetaka kuambiwa ukweli ajiandae kuondoka...," "...wananchi wamechoka kuona ubabaishaji huo, na kuanzia ni barabara ya Mandela, nataka taarifa ya ujenzi ndani ya mwezi mmoja, kwa maana mkandarasi sijui ni rafiki yenu au ni ndugu yenu kwani, hata kituo cha kazi hayupo sasa nataka ripoti yake alipofikia..." alisema Magufuli.

  Akasema Watanzania wamechoshwa na maneno ya kubabaishwa na wataka barabara. "Maisha bora ni pamoja na barabara nzuri, nawapa mwezi mmoja mtafakari tuanze kujenga barabara za juu, tunaweza," alisema Magufuli.Alisema hakuna haja ya kuwasumbua askari wa usalama barabarani kuongoza msongamano wa magari, huku wakazi wa jiji wakilia na kulalamikia kero hiyo wakati nchi imesheheni wahandisi wa kutosha. Akasema kama maghorofa yanaweza kujengwa kipindi kifupi, iweje ishindikane kwa barabara za juu. "Hata barabara za juu zinawezekana, hivyo kazi ya matrafiki ibakie kukaa na kutulindia nguzo zetu na kukamata magari yanayofanya makosa," aliweka wazi.

  Waziri Magufuli alitoa maelekezo kwa bodi ya makandarasi kuwafutia vibali na kuwafukuza wale ambao wameweka zaidi maslahi kuliko kazi walizoomba. "Tutatumia sheria, lazima tuzihurumie fedha za Watanzania," alisema na kuongeza kuwa "...Serikali haiwezi kuendelea kuona kila kukicha makandarasi wanapanga bei wanazotaka," alisema.

  Alionya wale wote wanaojihusisha na rushwa na kuwapatia ushindi wa zabuni makandarasi ambao ama hawana uzoefu au kwa kutaka pesa nyingi kutokana na gharama zao kuwa juu. "Tunajua rushwa ipo, hivi sasa makandarasi wapo katika mchakato tuache rushwa tutawaletea hata pesa za polisi...," "Magari yanazidisha uzito, ipo siku nitafanya msako wa kushtukiza kwa magari yanayozidisha uzito… nitaingia katika lori moja na kupanda halafu nitajibadilisha kwa kuvaa miwani na kofia ili nikamate wale wafanya kazi wenu wa mizani maana wanachukua rushwa sana..." "Sisi pia tutakuwa na kazi tutavamia maeneo na tukikuta mmeshindwa kufanya kazi tutafukuza mkandarasi na wewe ukifuata, hatutacheka na mtu tumekuja kufanya kazi maana barabara nyingi zilizochini ya Tanroads ndizo zenye matatizo, hivyo lazima malengo yatimizwe kipindi cha miaka mitatu,"alisema Waziri Magufuli na kuongeza kwamba kumezuka mtindo wa mtu anayetoa gharama za juu katika zabuni ndiye anapewa nafasi ya kwanza.

  Ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Uwanja wa Ndege Songwe

  Kuhusu mradi sugu wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Magufuli alionyesha kushangaza kuona ujenzi unasuasua na kutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuweka bayana kama hauwezi, atahakikisha linajengwa kwa fedha za serikali kwa kuomba kutoka Benki Kuu (BoT). "Kuna daraja moja refu sana kule China, urefu wake ni kwenda na kurudi Zanzibar mara tatu, walijenga kwa mwaka mmoja, sasa kwanini tunashindwa Kigamboni" alihoji. Aliitaka idara inayoshughulikia vivuko kuangalia uwezekano wa kununua vivuko vingine vinne, vitakavyokuwa vinafanya safari hadi Tegeta na Bahari Beach ili kupunguza msongamano wa magari barabarani.

  "Tutasaidia wananchi badala ya kukaa kwenye foleni kwa saa nne hadi tano, sasa waweze kutumia dakika 45 kufika Tegeta," alisema na kuongeza kuwa kama serikali imenunua vivuko viwili, haishindwi kununua vingine kwa ajili ya kutoa huduma.

  Kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege Songwe, alisema Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Prosper Tesha, anapaswa kuhakikisha na kusimamia kukamilika kwa uwanja huo uliopo mkoani Mbeya kutokana na mkandarasi kuchukua muda mrefu. "Lazima usimamie ukweli ni suala la kujiuliza kwanini ule uwanja haukamiliki na hauishi, inawezekana mnawabembeleza nini hao wakandarasi? naomba usimwogope mtu, fanya kazi hata siku ukifa amini utakwenda kuwa mkurugenzi mkuu wa viwanja vya ndege mbinguni," alisema.

  Kupoteza muda kwenye Majungu badala ya Kazi

  Alisema baada ya kuapishwa, alikubaliana na naibu wake waanze kazi rasmi jana, kwani miaka mitano si mingi, ambapo aliwapa muda wa miaka mitatu wakurugenzi hao kuhakikisha yale yote yaliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi yanatekelezwa ndani ya kipindi hicho.

  "Hatujawaambia wote muwe CCM, ila kwa sababu wananchi wameamua, serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, mnapaswa kuteleleza yale yote yaliyoahidiwa humu, kwa bahati mbaya sana mmeangukia katika mikono yetu, lazima mfanye kazi," alisisitiza.

  Alisema wizara hiyo hivi sasa imegubikwa na majungu na rushwa, huku utendaji wa kazi ukiwa umezorota kwa hali ya juu. Alisema watendaji wazuri wamekuwa hawapewi umuhimu kwa sababu ya kuendesha majungu na kuwepo kwa makundi.

  "Kuna mtu hapa amechora daraja la Umoja na lile na Mkapa, amefanya kazi nzuri sana, lakini hata siku ya ufunguzi, waliona kazi kumtambua kwa kumtaja jina tu, sasa nakurudisha kwenye madaraja endelea na kazi, najua ni fitina," alisema.

  Muda wote wakati anazungumza, ukumbi ulizizima kiasi kwamba hakuna mtu yeyote aliyeweza kumnongíoneza mwenzie jambo, ambapo hata baada ya mawaziri hao kutoka, watumishi hao walikaa ndani kwa dakika kadhaa kila mmoja akisubiri nani aanze kutoka.

  Kauli ya Dk. Mwakyembe

  Awali, akizungumza Naibu Waziri Dk. Mwakyembe alisema Wizara ya Ujenzi katika miaka ya karibuni imepoteza sifa yake ya awali ya kuwa wachapakazi pamoja na kuwepo kwa wasomi wazuri. Alisema mwanzoni wizara hiyo ilikuwa mfano wa kuigwa lakini anashangaa kuona ufanisi umepotea na sasa imekuwa sehemu ya kunyoosheana vidole bila kujua ni kirusi gani huyo aliyeingia. Alisisitiza kuwa sasa wanahitaji kuongea lugha moja na kuimba wimbo mmoja na kuifanya wizara hiyo kuwa ya mfano na kuagiza taarifa za kukinzana zisipewe nafasi kwa kuwa hawaendeshi wizara kwa majungu na umbeya. Aliwataka wafanyakazi kuwa wakweli na kufanya kazi kwa uwazi zaidi. "Mmepoteza sifa, sioni kama wizara hii ni kitovu tena cha ufanisi, nasema bila kuchakachua, uteuzi wetu hautakuwa wa maana kama tutaachia hali hii iendelee," alisema. Aliwataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii, kwani muda ni mdogo na mambo ni mengi.

  Ushirikiano "lay a strong foundation first" Mwanzo-Mwisho

  Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli na Naibu wake, Dk. Harrison Mwakyembe, walikuwa na kikao rasmi jana na wakurugenzi wa idara na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, ambapo walitangaza kuanza kazi kwa kukabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Walisema wao hawakufika katika wizara hiyo kwa ajili ya kutengua Torati, bali kuitekeleza na kwamba wanaweza kufanya kazi na yeyote na kusisitiza kuwa yaliyopita yaachwe na wafanye kazi kwa pamoja, "ndiyo maana tumeamua kufanya ibada yetu leo hapa," "Tushirikiane, tupendane, majungu yaishe, tuache rushwa kwa kuwa tutawategeshea hata fedha ya Polisi… na hivi ndio maana Rais ametuteua mimi na Naibu mwenye taaluma ya Sheria," alisema.

  Waziri alisema ujenzi wa barabara mpya kwa kiwango cha lami utaanza kutekelezwa mara moja kama ilivyoanishwa katika Ilani, na kutaka apewe taarifa ya barabara zinazoendelea kujengwa za Tunduma/Sumbawanga, Sumbawanga/Mpanda, Arusha/Namanga, Singida/Kateshi/Babati na Babati/Dodoma/ Iringa.

  credit ya habari magazeti ya UhuruPublications, HabariLeo na Mwananchi  from: Oho hou! Moto wa Magufuli umeanza... aluuu! -
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hata mimi kuuu sipati picha kwani mtoto wa mkulima ni msukule tuu!
   
 17. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  DR unaweza tunakuaminia.
   
 18. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jakaya angeota na kumpa uwaziri mkuu magufuli angekuwa amecheza pele!!!!!!!manake ingekuwa safi sana!!!!!!!!!!!!!!!!!imagine magufuli na mwakyembe!!! Patamu hapo mwanangu. Manake ile kutangazwa tu! Magufuli waziri wa ujenzi na mwakyembe naibu waziri wafanyakazi wa ujenzi na tanrods walianza kuji-position wenyeweee!!!!!!!!!!!
   
 19. M

  Matarese JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Du hapa ipo shughuli! Hebu piga picha wewe ndio Ephraim Mrema! Jamaa anatoa live, kama noma na iwe noma!
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  duuuh yaaani nchi ingekuwa mchakamchaka january to desemba...Dr.Magufuli namzimia sana katika utendaji wake.yaani haumiumi maneno
   
Loading...