Dr magufuli amsaidia jk kutimiza ahadi za kujenga barabara

KadamaKadama

Member
Oct 9, 2013
86
65
Serikali imetia saini mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Tsh.538 za Kitanzania kwa ushirikiano toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kutia saini mikataba hiyo,Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrck Mfugale alisema kati ya fedha hizo ADB wanachagia asilimia 65.80 , JICA asilimia 29.2 ambazo wametoa mkopo na Serikali inachangia asilimia tano.

“Mikataba iliyotiliwa saini hii leo ni pamoja na ujenzi wa sehemu ya Mayamaya hadi Mela yenye urefu wa kilomita 99.35 inayojengwa na Kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya zaidi bilioni mia moja kwa muda wa miezi thelasini na sita,” alisema Mfugale.

Alizitaja barabara nyingine ni Mela hadi Bonga yenye urefu wa kilomita 88.8 inayojengwa na Kampuni ya China Railway Seventh Group kwa gharama ya zaidi Sh. bilioni 88 , ambapo muda wa utekelezaji ni miezi thelasini na sita.

Mkataba wa mwisho ni wa ujenzi wa barabara ya Mangaka hadi Mtambaswala yenye urefu wa kilomita 65.5 itakayojengwa na Kampuni ya Sichuan Road and Bridge (Group) Corporation kwa gharama ya zaidi ya Sh.bilioni 59 na muda wa utekelezaji ni miezi ishirini na nne.

“Napenda kuwapongeza Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan kwa ushirikiano wao kwani sio mara ya kwanza kutupatia mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara zetu na tunaahidi kuzisimamia ili ziwe katika ubora unaotakiwa”, alisema Mfugale.

Aidha naye Waziri mwenye dhamana ya ujenzi Dkt. John Magufuli alishukuru ADB na JICA kwa mkopo huo na kutoa angalizo kwa wakandarasi wasio makini na kazi zao kukaa chonjo kwani sasa hakuna huruma kwao tena.

“Napenda kuwatahadharisha nyie makandarasi mlioko hapa kama kuna yeyote kati yenu hataweza kufanya kazi kwa ubora na wakati basi asisaini mkataba huu”, alisema Dkt Magufuli.

Nao wawakilishi toka ADB na JICA walimshukuru Waziri Magufuli kwa usimamizi imara wa miradi mbalimbali ujenzi inayoendelea kote nchini.

Hii si mara ya kwanza kwa ADB na JICA kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwani Machi mwaka , 2010 walitoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Iringa mpaka Dodoma yenye urefu wa kilomita 260 na barabara ya Namtumbo mpaka Tunduru yenye urefu wa kilomita 193.
 
Ofcoz anamsaidia lakini jifunze kujua, mtafuta hela ni JK na wala si Magufuli kama thread yako inavyosema!
 
Naungana na Mloganzila JK ni mtafuta fedha not Magufuli, huyu anabaki kuwa jembe la kulimia na mlipa posho ni JK.

Nilikuwapo kipindi mikataba inasainiwa:

Serikali yatia saini mikataba yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Tsh.538 ujenzi wa barabara

Pix-01.jpg

Wakandarasi na Washauri wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa TANROADS mhandisi Patrick Mfugale (hayupo pichani).

Pix-02.jpg

Mameneja wa TANROADS toka Mikoa mbalimbali ya Tanzania wakiwa wamehudhuria sherehe za kuweka saini mikataba hiyo.

Pix-03.jpg

Baadhi ya wabunge wanaotoka katika mikoa ambayo miradi hiyo ya ujenzi wa barabara itafanyika wakishuhudia sherehe za kutia saini mikataba ya ujenzi wa barabara hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Pix-04.jpg

Mwakilishi toka Benki ya Maendeleo ya Afrika bwana Patrick Musa akielezea mipango ya Benki hiyo kuendelea kutoa mikopo katika maradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Pix-05.jpg

Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Bwana Onishi Yasunori akieleza mikakati ya shirika hilo kutoa mikopo katika shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini huku akionesha moja ya ramani ya ujenzi wanaotarajia kufanya hapa nchini.

Pix-06.jpg

Waziri wa Ujenzi Dkt John Magufuli akisistiza jambo kwa waandishi wa wakandarasi mapema hii leo jijini Dar es Salaam, wakati wa utiaji saini mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara.

pix-07.jpg

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (wa pili kulia) akiweka saini Mkataba ujenzi wa barabara ya Mayamaya hadi Mela, wa pili kulia ni mwakilishi wa Kampuni ya china Henan International Cooperation Group Co. Ltd. Bwana Ghuo Zhijian, kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Bwana Onishi Yasunori na kushoto ni Mwakilishi toka Benki ya Maendeleo ya Afrika bwana Patrick Musa.
 
kwa kweli kwa barabara CCM watapata kura yangu 2015,wamejitahidi sana halifichiki ni ukweli,bado elimu na Afya,hv magufuli angepewa hizi wizara zingekuwaje?
 
Huyu Magufuli ni janga la kitaifa. Barabara ya Lamadi Bariadi imeishazinduliwa Mara tatu toka 2010 kwa usanii. Kuna barabara inajengwa toka Dumila kwenda Kilosa imechakaa kabla hata haijaisha, wachina wanamwaga lami kwa makoleo wanasema ni Bitumen standard. Nyingine ya Dumila Turiani toka 2009 hadi leo hakuna hata kilomita moja ya lami. Magufuli amechakachuliwa, sio Yule wa awamu ya tatu.
 
Mbona Wachina tupu kwenye hizi deals? Wadenmark wameishia wapi?

Mbona kulikuwapo kampuni za Kijerumani (Consultant), Kibongo (Consultant) etc, pia hizi tenda ni za kimataifa na mtu yeyote anaomba kutoka kona yeyote ya dunia - hivyo ni ushindani!
 
Serikali imetia saini mikataba mitatu ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Tsh.538 za Kitanzania kwa ushirikiano toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kutia saini mikataba hiyo,Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrck Mfugale alisema kati ya fedha hizo ADB wanachagia asilimia 65.80 , JICA asilimia 29.2 ambazo wametoa mkopo na Serikali inachangia asilimia tano.

“Mikataba iliyotiliwa saini hii leo ni pamoja na ujenzi wa sehemu ya Mayamaya hadi Mela yenye urefu wa kilomita 99.35 inayojengwa na Kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya zaidi bilioni mia moja kwa muda wa miezi thelasini na sita,” alisema Mfugale.

Alizitaja barabara nyingine ni Mela hadi Bonga yenye urefu wa kilomita 88.8 inayojengwa na Kampuni ya China Railway Seventh Group kwa gharama ya zaidi Sh. bilioni 88 , ambapo muda wa utekelezaji ni miezi thelasini na sita.

Mkataba wa mwisho ni wa ujenzi wa barabara ya Mangaka hadi Mtambaswala yenye urefu wa kilomita 65.5 itakayojengwa na Kampuni ya Sichuan Road and Bridge (Group) Corporation kwa gharama ya zaidi ya Sh.bilioni 59 na muda wa utekelezaji ni miezi ishirini na nne.

“Napenda kuwapongeza Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan kwa ushirikiano wao kwani sio mara ya kwanza kutupatia mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara zetu na tunaahidi kuzisimamia ili ziwe katika ubora unaotakiwa”, alisema Mfugale.

Aidha naye Waziri mwenye dhamana ya ujenzi Dkt. John Magufuli alishukuru ADB na JICA kwa mkopo huo na kutoa angalizo kwa wakandarasi wasio makini na kazi zao kukaa chonjo kwani sasa hakuna huruma kwao tena.

“Napenda kuwatahadharisha nyie makandarasi mlioko hapa kama kuna yeyote kati yenu hataweza kufanya kazi kwa ubora na wakati basi asisaini mkataba huu”, alisema Dkt Magufuli.

Nao wawakilishi toka ADB na JICA walimshukuru Waziri Magufuli kwa usimamizi imara wa miradi mbalimbali ujenzi inayoendelea kote nchini.

Hii si mara ya kwanza kwa ADB na JICA kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwani Machi mwaka , 2010 walitoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Iringa mpaka Dodoma yenye urefu wa kilomita 260 na barabara ya Namtumbo mpaka Tunduru yenye urefu wa kilomita 193.

SAWA LAKINI MBONA KILIO CHA MAKANDARASI HAO HAO KUWA HAWALIPWI KWA WAKATI NA MIRADI KARIBU 30 NCHINI YA BARABARA AU INASUASUA AU IMESIMAMA?
Magufuri wa leo sio yule wa awamu ya tatu. Huyu ni mpiga domo tu!
 
Wewe ni muongo kilosa umeenda lini? Acha chuki binafsi sasa hivi yanashinda pambaf
 
Magufuli alikuta wachovu kina Mramba, Chenge na Kawambwa wameharibu Wizara vibaya sana kiasi cha kudaiwa na makandarasi hela kibao, yalifanyika haya pindi alipoondolewa na Mkwele. Japo kwa sasa hali Si mbaya sana kama alivyoikuta!
 
kwa kweli kwa barabara CCM watapata kura yangu 2015,wamejitahidi sana halifichiki ni ukweli,bado elimu na Afya,hv magufuli angepewa hizi wizara zingekuwaje?

Practically - angepewa Uchukuzi na Ujenzi zote zikawa kama ilivykuwa zamani, hope pangechimbika.
 
Huyu Magufuli ni janga la kitaifa. Barabara ya Lamadi Bariadi imeishazinduliwa Mara tatu toka 2010 kwa usanii. Kuna barabara inajengwa toka Dumila kwenda Kilosa imechakaa kabla hata haijaisha, wachina wanamwaga lami kwa makoleo wanasema ni Bitumen standard. Nyingine ya Dumila Turiani toka 2009 hadi leo hakuna hata kilomita moja ya lami. Magufuli amechakachuliwa, sio Yule wa awamu ya tatu.
Wewe mburula kwani magufuli ndiyo anajenga hiyo miundo mbinu.
 
Mpaka sasa magufuli atabaki kama kiongozi bora kuwahi kutokea kwa mtazamo wangu.
 
Mbona kulikuwapo kampuni za Kijerumani (Consultant), Kibongo (Consultant) etc, pia hizi tenda ni za kimataifa na mtu yeyote anaomba kutoka kona yeyote ya dunia - hivyo ni ushindani!
Kwa nchi ya kifisadi kama Bongo, tenda ni kiini macho. Ndiyo maana Wachina ambao usafi wao ni wa shaka wanapata sana hizi tenda Bongo.
 
Mbona jumla ya Barabara zote hizo hapo juu hazifiki billioni 250 hiyo billioni 538 umeitoa wapi?
 
Wewe mburula kwani magufuli ndiyo anajenga hiyo miundo mbinu.

Wewe Mbulumundu unajua maana ya usimamizi,,, kupumuliwa hapo Lumumba kusikupe upofu wa kujua kuwa Magufuli anatakiwa kusimamia standards za barabara. Njaa ndio inakutuma kufanya kazi humu 24hrs kwa mshahara wa buku saba, nani alikwambia uwe masikini, utakoma mwaka huu na bado, utakesha sana humu fa.la wewe
 
Huyu Magufuli ni janga la kitaifa. Barabara ya Lamadi Bariadi imeishazinduliwa Mara tatu toka 2010 kwa usanii. Kuna barabara inajengwa toka Dumila kwenda Kilosa imechakaa kabla hata haijaisha, wachina wanamwaga lami kwa makoleo wanasema ni Bitumen standard. Nyingine ya Dumila Turiani toka 2009 hadi leo hakuna hata kilomita moja ya lami. Magufuli amechakachuliwa, sio Yule wa awamu ya tatu.
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom