Dr Lwaitama amuomba Nape awe mfano wa Kukiwezesha CCM kuwa chama Pinzani Makini

Dk Lwaitama mwanachama mfu wa ccm (kama anavyopenda kujiita) kaamua kuweka mambo hadharani. Nasikia harufu ya mabadiliko. Tena inanukia vizuri mno! Mfano wa waridi. Tena mfano wa uoto wa asili msimu wa masika. Ajenda ya uhuru iliisha pale mwaka 1961.
 
Dr Lwaitama akichangia kwenye Kongamano la kumuenzi mwalimu juu ya Jukumu la vijana katika kumuenzi Mwalimu,Akimshukuru Jerry Slaa kwa kuweka hoja ya kiongozi kukubali ukomo wake na kumwachia Mwingine.

Atafurah kama atamuona Nape Nnauye akiongoza CCM kuwa Chama pinzani Makini.

Mods msiunganishe huu uzi ili tuijadiri hii kauli kwa undani zaidi.

Tatizo mnakuja na details kidogo sana. Hoja hii ingeweza kujadilika vizuri kama Mchango wa Lwaitama ungeuleta in details.
 
Nape huwa anakuwa na busara akiona wasomi maana anajua itakuwa rahisi wao kuchuja pumba atakazo toa! In short ni mzugaji tu mwenye kusoma mazingira, ingekuwa kauli ya Lwaitama kaisikia kwenye vyombo vya habari halafu nae akawaita waandishi pale Lumumba msidhanie kuwa angeongea the same kama alivyo mjibu Dr palepale!

Angeanza kumtukana mzee wetu kwa kauli za kijinga, lazima tungesikia akisema "mwalimu lwaitama anazeeka vibaya" au " yule ni ccm mfu na ccm kazi yake sio kujibu wafu" Nape! Hana maana sentitano.
 
kwa kweli Nape amekubali kwa thati kabisa wazo la Dk.Lwaitama kuwa CCM aisadie iwe chama cha upinzani cha mfano.hakumjibu Dokta,badala yake amesema dk ni mzee mwenye busara na huwa anamshauri mambo mengi.
mimi nape nimefanya naye kazi Masasi.Ana akili sana na mchapa kazi.ni mwadilifu vile vile.kwa namna alivyozungumza leo na ukimya wake tangu kikao cha NEC amaanza kuwa na mawazo tofauti juu ya CCM.


Nape anawaza kimbunga cha EL!!!!!!!!!!!!
 
hana lolote huyo mzee hafai hat ushauri wa kijiji amejaa ushbiki badala ya kuonyesha njia
 
Nape kiongozi mzuri,ila waliomzunguka!leo alikuwa na busara sana.
huwa sikubaliani na mitazamo ya aina hiyo, eti jk ni kiongozi mzuri ila anashauriwa vibaya. Kumbuka ukikubali ushari mbaya wewe ndo kuliko hata mtoa ushauri mbaya!
 
Nape 2015 hatasikika tena kama EL atashika hatam ya kuongoza nchi. Huu ni walkati wake wa mwisho kumalizia ngwe ya siasa na atakua kijana mdogo ndani ya magamba kusaulika mapema kisiasa baada 2015.
 
Baada ya Lweitama kudai CCM isaidiwe na Nape kuwa chama kizuri na imara cha upinzani, Kitilya Mkumbo akataka kumtumbukiza Nape kwenye mtego wa kumjibu Dr. Lweitama......... haya ndo majibu ya Nape

"..sijasimama kumjibu Dr. Lweitama, ni mzee wangu na ninamheshimu sana, mnisamehe sana kwani siko tayari kumjibu.(makofi). Namheshimu sana anabusara na kazungumza maneno mazuri sana. Nataka nimnukuu mwl akisema...INAWEZEKANA IKIWA KILA MMOJA WETU ATATIMIZA WAJIBU WAKE.....wanasiasa wetu leo wanajenga jamii inayojua kudai haki tu bila kutimiza wajibu wake.... mwalimu anasisitiza INAWEZEKANA IKIWA KILA MMOJA WETU ATATIMIZA WAJIBU WAKE......


SASA DOGO NAPE ...mbona umeamua kumvua nguo Dr.wangu bhana....?kwanini hukumjibu ili tukuzomee leo?!!! aaaaakhaa unajifanya mjanja sio? tutakupata tu, makamanda tuko kazini kwa ajili yako.
 
Ninyi hamumfahamu Nape vizuri! Yani akisha sikia sauti ya muziki wa ccm na kuona kundi la wakina mama wenye kijani, anachanganyikiwa kabisa! Anasau kua kunasiku ataalikwa UDSM au maeneo mengine ambapo atakua juu ya moto wa gesi !.
 
Kamanda punguza mzuka, NAPE kichwa kinamuma, anashindwa awaambie nini watz, swala la mafisadi, rushwa, kujivua gamba, na watoto wa wakubwa ndani ya chama chake inamchanganya, anatamani hata leo ajiachie, ila ataelekea wapi na chama gani?

Ameamua kufa na tai ..., anangojea makosa na vurugu ndani ya chadema huenda akapata la kusema, na lile tego halijanasa(divide and rule through money roundry, weak political parties) hapo alipo anajuta kwa kuishambulia chadema na sasa ana kesi ya kujibu, Muhurumieni MAPE
 
Nilifikiri kazungumzia kujivua gamba!
Anyway, giving the devil his due, Nape ni lulu iliyozama kwenye tope. Kwa kuendelea kukaa na kuxingirwa na matope zaidi yaweza kujikuta na yenyewe ishakuwa tope.
 
kwa kweli Nape amekubali kwa thati kabisa wazo la Dk.Lwaitama kuwa CCM aisadie iwe chama cha upinzani cha mfano.hakumjibu Dokta,badala yake amesema dk ni mzee mwenye busara na huwa anamshauri mambo mengi.mimi nape nimefanya naye kazi Masasi.Ana akili sana na mchapa kazi.ni mwadilifu vile vile.kwa namna alivyozungumza leo na ukimya wake tangu kikao cha NEC amaanza kuwa na mawazo tofauti juu ya CCM.
Mungu ampe nape ujasiri wa kuishtukia ccm na kuanza kuichukia ccm
 
Back
Top Bottom