Dr. Louis Shika asisitiza nia ya kuzinunua nyumba za Lugumi, atoa ujumbe mzito kwa TRA na Yono wasimbeze

Aisee in short huyu jamaa yetu kichwani zimeyumba.

Au anajua anachokifanya.
Usicheze na urusi baba.
Been there 8 years.

Jamaa wengi nimeona wakifa kizembe na wengine wakiwa mentor kindezibsana wanakupigisha mastori ya billions dollars.


In short nitaanzishs uzi wa life la wanafunzi wa .ru na dramma zao.

Na kitu gani kinasababisha.
Na huwa wakiondoka hapa wanakuwa na expectation gani, familia zinaexpect nini kwa mtoto wao aliyepo ulaya.
Na sasa wanachokikuta kule, na wanachowaambia ndugu zao.

Na akirudi huku ana akirudishwa huku ni aibu. Anarudi na pum** tu, ndugu wanategemea urudi kutoa msaada.

Sasa wengi wao anamua kujifanya kuwa chizi.


( kama hutoelewa concept yangu fuatilia thread nitakayoanzisha)
Cc Inna Maserati
Aisee in short huyu jamaa yetu kichwani zimeyumba.

Au anajua anachokifanya.
Usicheze na urusi baba.
Been there 8 years.

Jamaa wengi nimeona wakifa kizembe na wengine wakiwa mentor kindezibsana wanakupigisha mastori ya billions dollars.


In short nitaanzishs uzi wa life la wanafunzi wa .ru na dramma zao.

Na kitu gani kinasababisha.
Na huwa wakiondoka hapa wanakuwa na expectation gani, familia zinaexpect nini kwa mtoto wao aliyepo ulaya.
Na sasa wanachokikuta kule, na wanachowaambia ndugu zao.

Na akirudi huku ana akirudishwa huku ni aibu. Anarudi na pum** tu, ndugu wanategemea urudi kutoa msaada.

Sasa wengi wao anamua kujifanya kuwa chizi.


( kama hutoelewa concept yangu fuatilia thread nitakayoanzisha)
Cc Inna Maserati
Nitaomba tag ya nguvuuuuuu
 



Dar es Salaam.
'Bilionea' wa nyumba za Lugumi, Dk Louis Shika ameachiwa na kwenda kupanda daladala kuelekea nyumbani huku akisema mpango wake wa kununua nyumba za Lugumi uko palepale.

Baada ya kuachiwa na polisi leo Jumanne jioni amesema kwamba bado mpango wake wa kununua nyumba hizo uko palepale.

Amesema anachosubiri sasa ni fedha kuingizwa kwenye akaunti yake na kulipa asilimia 25 anayodaiwa.

"Siku nikipeleka fedha nataka Yono na TRA waite waandishi wa habari waone na wautangazie umma," amesema.

Amesema vyombo vya habari vimetoa taarifa zake lakini vitaumbuka siku akienda kupeleka fedha hizo.

Ameendelea kusisitiza kwamba nyumba hizo zinahitajiwa na kampuni yake ambayo hakuitaja.

Njiani wakati akielekea kwenye kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja, Dk Shika alikuwa kivutio kwa watu aliokuwa akipishana nao.

Alipopanda daladala la Tabata Mawenzi, kondakta alimkaribisha kwa kumweleza karibu mzee Shika.

Kauli hiyo iliwaamsha abiria ambao walikuwa na hamu ya kumwona.

Dk Shika alipanda daladala na kusimama huku akionyesha tabasamu lisiloisha

*R.I.P DR. SHIKA😭*

Dr.Shika alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri lakini bahati mbaya elimu yake haijaweza kusaidia taifa hili achilia mbali kumsaidia yeye binafsi.

Wengi walimchukulia kimzaha tangu alipoonekana kwenye tukio la mnada wa nyumba za Lugumi (mia tisa itapendeza). Makampuni ya kibiashara yalitumia umaarufu wake kama fursa ya matangazo lakini yakamuacha hohehahe asiye hata na mahali rasmi pa kuishi. Aliwahi kuripotiwa na kituo kimoja cha TV kufukuzwa kwenye nyumba aliyokua akiishi huko Tabata baada ya kushindwa kulipia kodi.

Vyombo vingi vya habari vilikuwa vikimdhihaki na vingine kumuita Kalubandika. Lakini bila shaka vilifanya hivyo pasipo kumjua kiundani *Dr.Shika.*

Ni mzaliwa wa kijiji cha Kalemela wilaya ya Busega, mkoani Simiyu. Majina yake halisi ni Louis Shika Kidola. Yeye na ndugu yake Jeremiah Shika Kidola *(marehemu pia)* walikuwa wanafunzi wenye akili sana na waliofaulu vizuri masomo yao ya sekondari kwa alama za juu na kupata ufadhili wa kusoma udaktari nchini Urusi mwaka 1984 hadi 1991 waliporejea na kuanza kutibu hospitali ya taifa Muhimbili.

Mwaka 1994 Louis Shika alirejea Urusi kujiendeleza kimasomo. Alisomea shahada ya uzamili katika magonjwa ya kuambukiza (MSc in Infectious Diseases) na udaktari bingwa wa magonjwa ya akili Master of Medicine (Psychiatry). Akiwa huko alishirikiana na wenzake kuanzisha kampuni ya usambazaji wa kemikali viwandani iitwayo Lancefort Ltd.

Kwa sasa ni moja ya makampuni makubwa ya usambazaji wa kemikali nchini Urusi, na jina la Dr.Shika lipo kwenye website yao kama Muasisi na Rais wa kwanza wa kampuni.

Inadaiwa shirika la ujasusi la Urusi (KGB) liligundua kwamba akina Shika walipata fedha za kuanzisha kampuni kutoka Marekani kama mkakati wa Marekani kudukua taarifa za Urusi. Kwahiyo baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo walikamatwa. Dr.Shika alitekwa na watu waliodhaniwa kuwa majambazi kupewa mateso makali sana ikiwemo kukatwa vidole.

Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Urusi, Patrick Chokala mwaka 2017 alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba ilibidi kutumia mbinu za "kijasusi" kumnasua Dr.Shika na kumrudisha nchini kwa dharura. Tangu aliporejea alijiingiza kwenye ulevi wa kupindukia kutokana na msongo wa mawazo.

Kwahiyo ukifuatilia historia ya *Marehemu Dr.Shika* utagundua hakuwa "kalubandika" kama ilivyodhaniwa. Ni mtu aliyekua na maono makubwa. Kama si mipango yake kuvurugika huenda angekuwa daktari bingwa na mfanyabiashara mkubwa wa kemikali duniani.

Ni kwamba tu alijikwaa, akadondoka na hakuweza kusimama tena. Serikali ilipaswa kumsaidia kusimama lakini nayo ilimtelekeza. Kwahiyo ameishi maisha ya upweke, masononeko na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.

Kampuni aliyoanzisha ya Lancefort Ltd ambayo kwa sasa inamilikiwa na serikali ya Urusi (ilitaifishwa) ina thamani ya $27Bil sawa na TZS 60Trilioni (Bajeti ya nchi kwa miaka miwili).
_
Kwa hiyo Dr.Shika alikuwa anajiita "Bilionea" si kwamba alikuwa anaota. He used to have money. Na hiki ndicho kilichokuwa kinamtesa maana alishindwa kukubaliana na hali yake ya sasa. Hakutaka kuamini kama aliwahi kuwa na pesa.

Kujikwaa na kuanguka ni kawaida katika maisha lakini jambo la msingi ni uwezo wa kusimama tena baada ya kuanguka. Whinston Churchil aliwahi kusema "Success is not final and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"
_
Mtu kama huyo hakuwa mtu wa "kumchukulia poa" hata kidogo. Serikali haikutakiwa kumtelekeza. Alipaswa kupewa nafasi nyingine. Either angerudishwa Muhimbili kutibu au angetafutiwa fursa mahali pengine ambapo taifa lingeweza kufaidi ujuzi wake na pia ingekua njia ya kumsaidia kuondokana na msongo wa mawazo na kusahau "mabilioni" yake kule Urusi.

*Pumzika kwa amani Mr. mia tisa itapendeza*

C&P from WhatsApp group.

RIP Dr. Louis Shika.

P
 
*R.I.P DR. SHIKA😭*

Lancefort Ltd.

Kwa sasa ni moja ya makampuni makubwa ya usambazaji wa kemikali nchini Urusi, na jina la Dr.Shika lipo kwenye website yao kama Muasisi na Rais wa kwanza wa kampuni.



*Pumzika kwa amani Mr. mia tisa itapendeza*

C&P from WhatsApp group.

RIP Dr. Louis Shika.

P

Screenshot_20200825-132315_Samsung Internet.jpg

Daaahhhh, Aiseeeee, Maisha haya hakuna ajuaye Kesho
 
Back
Top Bottom