Dr Linda anafukuza wanachuo kwenye majengo ya umma!

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,978
5,025
Yule daktari aliyeandikwa kwenye magazeti miezi michache iliyopita kwa tuhuma za kuhamishia vifaa vya dialysis vya mnh kwenye centre yake amekuja na stail mpya ya kuwafukuza wanachuo clinic. Wanachuo wa Md5 Muhas wanaorotate internal medicine wanatakiwa kuhudhuria wodini na clinic kwa kila kitengo ili kujifunza zaidi ikiwa ni sehemu ya patient oriented medicine. Lakini imejitokeza kwamba dr linda wa nephrology anawafukuza wanachuo hao kila anapowakuta clinic husika. Hali hii imesababisha kukosa mafunzo ya wagonjwa wa nje tofauti na wale waliolazwa wodini. Hili tukio hulifanya hata akiwakuta wanafundishwa na specialist mwingine japokuwa yeye huwa hafundishi kwani kuna group aliikuta ikifundishwa na dr Kisanga yeye akawaambia waondoke wanabana nafasi. Swala la kujiuliza ni, yale si majengo yanayojengwa na kodi zetu? Kwa nini mtu mmoja awanyanya madaktari watarajiwa wa watanzania maskini? Au analipiza kwa uhuni wao walioufanya na nyoni ukagundulika? Intern wanaporudi kufanya kazi huwa wanatukana kwamba hamjui kitu,sasa watajuaje huku wanafukuzwa? Au wamembania kuwa promoted kielimu na hasira zake amamalizia kwa md5? Kama hataki kuwafundisha si awaache wafundishwe na wenye nia na moyo wa kusaidia? Hata kama kuna msuguano wa muda mrefu kati ya mnh na muhas,mbona vitengo vingine hawafukuzi na wanafundisha wanachuo?
 
Kila kitengo kina mfalme mnyonyaji, kutokana na kukosekana kwa utu na ubinadamu. poleni ndugu zangu, msiache kupambana
 
poleni nawashauri mchukue hatua muafaka badala ya kusemea pembeni. 40 yake itafika tu asijifanye yuko juu ya sheria.
 
naomba msiwe mnaenda group kubwa, watu watatu tu mkifundishwa pamoja itakuwa vizuri. Drs wengine huwa hawapendi wanafunzi na mbaya zaidi mkiwa wengi.
 
poleni nawashauri mchukue hatua muafaka badala ya kusemea pembeni. 40 yake itafika tu asijifanye yuko juu ya sheria.

unajua kila sehemu kumeoza nchi hii. Watu wanapelekewa taarifa lakini wanachukua muda mrefu kufanyia kazi na vitu ndo vinapita.
 
naomba msiwe mnaenda group kubwa, watu watatu tu mkifundishwa pamoja itakuwa vizuri. Drs wengine huwa hawapendi wanafunzi na mbaya zaidi mkiwa wengi.

yeye anasema hapendi kuona wanachuo! Wanadai amewaambia wanamtia kichefuchefu
 
yeye anasema hapendi kuona wanachuo! Wanadai amewaambia wanamtia kichefuchefu
Kwani yeye kabla ya kuwa specialist hakuwai kuwa mwanachuo?kama anasikia kichefuchefu mwambieni akafanye UPT labda ni +ve,MD5 wakaze buti tu shule imeshaisha
 
Poleni wadogo zangu MD5, kwanini msimripoti kwa Prof. Karim? Nasikia ndio Dean of students anaweza kuwasaidia.
 
Yeye pia alikuwa mwanafunzi!! huyo ni mmoja wa wale walikuwa na tabia ya kufelisha watu sana naomba alaaniwe kwa nguvu zote mnh sio nymbani kwake lazima ajue walikuwepo akina Swai(hematology&micro) walifikiri hapo watakaa milele , MMEKARIBIA KUMALIZA VIJANA MSIIGE CHEMBE YA TABIA YA HUYO MTU!!!!
 
Back
Top Bottom