Dr. Lilian Mbowe: Interview alofanya na Kipindi Cha Wanawake Live Eatv Jumanne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Lilian Mbowe: Interview alofanya na Kipindi Cha Wanawake Live Eatv Jumanne

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nicole, Sep 26, 2012.

 1. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Majibu ya interview alofanyiwa na kipindi cha wanawake live cha EATV.

  Aliulizwa yeye ni mke wa mtu mwenye nafasi kubwa katika jamii (kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ndugu Aikael Mbowe), wana mali na maisha mazuri inakuwaje anachapa kazi kwa bidii?

  Mimi ni mwanamke msomi wa degree na masters ya udaktari, nimelelewa katika mantiki ya kujijenga mimi kama mimi na nisitegemee mtu mwingine. Mimi kuolewa na mwanaume mwenye fursa ktk jamii siyo tija na kuna kitu ktk roho yangu kinachoniambia lazima nifanye kazi.Siamini katika mantiki ya kula kulala, hata kama pesa ipo lazima mtu ufanye kazi fulani kusudi uweze kuijenga ile pesa, kuingiza kipato na kujua kinachotokea.Kama ningekuwa amelala nyumbani sifanyi kitu chochote,tatizo laweza tokea, kuna leo na kesho.Leo niko na mume wangu kesho na kesho kutwa siko naye .Sasa baada ya hapo nitakwenda wapi? Au baada ya hapo nitafanya nini?

  Je wanawake tegemezi wapo?

  Kadri siku zinavyo kwenda kina mama nao wanaanza kujipatia kipato. Kuna kupewa lakini kupewa huko kuna mwisho wake.Kadri siku zinavyo kwenda zana ya mama wa nyumbani inatoweka, /inapungua kwa kina mama wengi.Lakini bado wako wengine wanapenda maisha ya kufurahia mali na position /kazi za waume zao na kutake advantage.

  Unawaambia nini wanawake wategemezi?
  Wawe waangalifu,kazi za watu zinapanda na kushuka, biashara nazo zinacollapse zinaisha,kuna kuchukuliwa na mwenyezi Mungu ghafla tu,sasa mama kama hujasimama na miguu yako miwili unaweza kupata shida sana.

  Ushauri kwa wanaume wanaodekeza wake zao;
  Sidhani kama ni vizuri kudekeza mwanamke,kuna dini na mila zisemazo kwamba mwanaume ndo anatunza mwanamke lakini kwa karne hii ya 21 sidhani kama twaweza kuendelea kushikilia mila za zamani za kusema mwanamke tu atunzwe.Kwajinsi maisha yanavyokwenda na baadhi ya mambo kubadilika, wanaume wengi wanaona nikiondoka leo, au nikimpa talaka huyu mwanamke anaweza akapata shida, hivyo kama unampenda mwenzio, nashauri kinababa wajaribu kusukuma kina mama wajaribu kufanya kitu chochote cha kujiendeleza, badala ya kuwadekeza sana na wao kubakia wanashughulikia kila kitu.

  Anasema ana bahati mumewe siyo wa aina ile ya wanaume kudekeza wanawake na kuwaacha wakae tu idle, while wao wakiprovide kila kitu.Ana mume ambaye naye ndiye anayemsukuma na anamwambia kwamba lazima uwe na maisha yako lazima uwe na vitu vyako, lazima ujijenge. Anasema Kama siku hizi huwa wanagombana maana anamwambia lazima aende akasomee MBA, ukizingatia she is a doctor by profession, lakini sasa anashughulika na family business so mumewe anamsukuma asome zaidi hataki abaki hapo alipo anamshawishi achukue MBA ili aweze kufanya biashara vizuri.

  My take:
  Binafsi nilikuwa sijawahi kumwona Dr. Lilian Mbowe kabla, nimemwona kwa mara ya kwanza kwenye interview hii. Appearance yake natural and simpe, classy, msomi, even the way she speak amedisplay hilo.Sasa nimeamini wanawake wengi wenye uwezo na wachapa kazi, ni very discreet, hawacomplicate wala kufake appearances, they know how to speak and even to behave. Tofauti na manungayembe, kichwani hamna kitu, lakini atajishaua kila mtu amjue yeye ni mke wa nani.

  Big up Dr. Lilian Mbowe, umeniinspire and am adding you to the list of my role models!!
   
 2. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Ukiwa na elimu yako inayoeleweka na ya kukupa kipato k yako inahifadhiwa kwa ufasaha. Haiwezi kuwa ya kila mtu.
   
 3. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sikubahatika kuona kipindi,but
  big up to her
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sasa wangemhoji yule wa magogoni ndo ungechoka na roho yako...
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  wa magogoni yupo New York sa hivi na shavu lake dododo
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  yule wa magogoni siku moja nilimsikia akihutubia yaani ni vituko......
   
 7. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  jamani mbona dr lilian mbowe na yule wamagogoni hawaendani kabisaaaaaa
  elimu-dr ana masters medicine=magogoni ana cheti cha ualimu daraja la tatu
  vyeo-daktari=mjumbe wa nec lindi
  malezi-daktari ana watoto 2=magogoni kama saba hivi
   
 8. C

  CAY JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwani hujasikia kuwa anasisitiza wanawake wasome lakini yeye hasomi!
   
 9. C

  CAY JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi saba=7
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  JF kazi kweli kweli
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Inategemea na mtu mwenyewe, mbona wapo wasomi wanagawa K kama pipi...??
   
 12. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  " Mimi kuolewa na mwanaume mwenye fursa ktk jamii siyo tija"

  Ha ha ha, nimecheeeka! hivi dada mbona anatudanganya mchana kweupe! wakati anaolewa na huyu bwana miaka ya tisini enzi hizo tupo shule sisi, huyu alikuwa na fursa gani ZAIDI YA MCHEZO DISCO A.K.A DISCO JOKER .. jamani acheni kuongopea wenzenu nyie loh! bila ya ukabila wa mzee mtei kutaka mkwe akae katika hicho kiti saa hizi huyu angekuwa kama baba yake banana zoro ! na nawaza je akikuacha itakuwaje?
   
 13. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  parhaps ! we chezea wa mjomba wa magogoni wewe!
   
 14. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ukiwa mke wa rais hauna haja ya kusoma, unaanzisha NGO (Nothing's Going On)! maan muhimu ni mshiko.
   
 15. T

  Teko JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kipindi huwa kinarudiwa tena jumapili mchana,ingawa sijajua ni saa ngapi.Kama utakuwa na nafasi unaweza ukaangalia.
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Hivi naye anaitwa mama nani tena......manake huyu Mama Mwanaasha mmmmmh
   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Wewe bure kabisa........umesoma thread juujuu unakuja na utumbo wako....Mbowe kacheza disco lini? Kawa Disco joker lini?
   
 18. Lovebird

  Lovebird JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 27, 2012
  Messages: 2,197
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145


  She really made my day, there is a need for changing our way of thinking: MEN and WOMEN. The way she was talking I thought Mbowe has also been natured by her.
   
Loading...