Dr. Levy arudi kivingine, sasa awavaa wale waunga juhudi

sawa

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,750
2,000
Maandiko ninayoyaamini mimi, wewe na viongozi wa dini walioenda Ikulu hivi karibuni yanatutaka tumsujudie Mungu mmoja muumba mbingu na ardhi. Na tusiabudu miungu mingine.

Zaidi tunajulishwa kuwa Mungu ni mwenye wivu. Anapenda kuabudiwa na kusifiwa yeye tu. Tusitaje bure jina lake. Na usisahau neno ‘’heshimu mamlaka mlizopewa duniani. Na pia Mungu wetu tumeelezwa ni mkali.

Kwa kufupi Mungu hapendi upinzani kabisa. Sasa kama kuna kiongozi hapa duniani ambaye hataki upinzani, ujue anataka ‘umungu’.

Yaani yeye ndiye mpinzani rasmi wa Mungu kwa kutaka ‘umungu’. Kiongozi asiyetaka mawazo mbadala, maana yake anataka asujudiwe, asifiwe na kuogopwa yeye tu. Kutotaka upinzani maana yake hataki tuabudu ‘miungu’ mingine.

Unakuta kiongozi anataka asifiwe tu. Kama ambavyo Mungu anatueleza tumuabudu na kumsifu. Kiongozi asiyetaka upinzani hukerwa na wanasiasa au wanahabari wanaothubutu kumkosoa au kusifia wapinzani wake. Anataka asikilizwe na asifiwe yeye tu. Wapo wanaowaita majina mengi mabaya ila mimi viongozi wa hivi nawaita wapinzani wakuu wa Mungu.

Ni wapinzani wa Mungu kwa kutaka ‘umungu’ wakati Mungu katuonya tusiabudu na kusujudia miungu mingine. Ni ‘miungu’ wanaotaka kupindua mamlaka ya Mungu duniani. Wanapenda kuwapa mamlaka na nguvu kubwa wasaidizi wao. Kwa maana ileile ya heshimuni serikali mlizopewa duniani. Basi nao wanatulazimisha tuheshimu na kuwaogopa wasaidizi wao kiserikali.

Mungu anatuasa kuwa usitaje bure jina la bwana Mungu wako. Sasa viongozi wasiopenda upinzani, wanakasirika sana kutajwa majina yao bure au kwa jambo ambalo siyo rafiki masikioni mwake au kwa wafuasi wake.

Kwa mfano kiongozi akikosea hataki akosolewe au kuelekezwa. Kwa sababu hataki kutajwa bure jina lake bila kulipamba na kulisifu kwa nyimbo na pambio za kutosha.

Ndiyo maana viongozi wasiopenda upinzani au kukosolewa na kutaka kusifiwa kila hatua, huishia pabaya. Kwa kuwa laana wanayopata haitoki kwa wapinzani wao, bali kwa Mungu ambaye hapendi uwepo wa ‘miungu’ wengine.

Kiongozi anayetaka kusujudiwa tu, kupambwa tu, kusifiwa tu, na kutopingwa, huyo anataka ‘umungu’ na Mungu ni mkali. Lazima atamnyoosha tu.
 

sawa

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,750
2,000
Wale wote wanaopiga kelele flani asulubiwe waje kusoma hii, watakimbia na hakika
 

sawa

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,750
2,000
1551177422983.png
 

sawa

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,750
2,000
Kutoka 20:1-
Mungu akanena maneno haya yote akasema,

2Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 3Usiwe na miungu mingine ila mimi. 4Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 7Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. 8Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. 12Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. 13Usiue. 14Usizini. 15Usiibe. 16Usimshuhudie jirani yako uongo. 17Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako. 18Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali. 19Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa. 20Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
6,998
2,000
Shetani kapewa za uso ,mulemule anapopita ,sifa zake ndio hizo hizo zilizotajwa .Sifa zote zilizotajwa shetani anazo .
 

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,332
2,000
duuu ngoja niikopi hii elimu nikae nayo nianze kuitafakari!! ila nimeelewa sehem moja tuu! mtu asiyetaka wapinzani huyo anataka kuchukua nafasi ya Mungu. koz Mungu hatak wapinzani kule mbingun kwake ndio maana shetan alitimuliwa. asante Dr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom