Dr. Kitla Mkumbo ataka vijana wapiganie Demokrasia katika vyama vyao

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284
Yanayoendelea Uganda na sehemu zingine katika bara letu, ikiwemo Zanzibar, itukumbushe tena kwamba Waafrika tuliupokea utamaduni wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kwa shinngo upande. Kuanzia tunavyoendesha mambo ndani ya vyama vyetu hadi katika ngazi ya taifa ni utani unaogeuka kuwa mateso kwa wanachama na wananchi. Bahati mbaya ni kwamba tumeiga mambo yetu karibu yote kutoka hukohuko tulikoiga demokrasia, ikiwemo maana ya maendeleo!! Sasa yatupasa tutambue kwamba hayo maendeleo ya kizungu tunayopigana kuyapata, ikiwemo dhana mpya ya uchumi wa kati, msingi wake ni demokrasia. Madamu tumeamua kuchezea demokrasia ya kimagharibi tusahau kabisa maendeleo ya kimagharibi. Hii ni Kwa sababu pasipo demokrasia ya magharibi haiwezekani kupata maendeleo ya kimagharibi. Kama hatutaki hii demokrasia tuachane kabisa na dhana yao ya maendeleo ya kimagharibi na tuanze kujenga dhana ya kiafrika isiyotegemea demokrasia hii tuliyoiga kishingo upande ili tuendelee kupata nidsaada yao.

Lakini nawaona vijana wetu walivyojipanga kupata maendeleo ya kimagharibi na siamini kwamba inawezekana kuwashawishi waachana na hii dhana ya maendeleo. Basi Nawakumbusha hawa vijana kwamba hawatafanikiwa sana kupata maendeleo ya kimagharibi kama hawatapigania demokrasia ya kweli ya kimagharibi. Hivyo basi nawasihi vijana popote mlipo, wakati mkiendelea kupigania maendeleo ya kimagharibi msiache kamwe kupigania demokrasia yake Kwa sababu ndiyo msingi wa hayo maendeleo myatakayo. Na tena muanze kupigania demokrasia kuanzia katika vyama vyenu. Amini nawaambieni hatuwezi kamwe kujenga demokrasia ya kimagharibi katika nchi bila kwanza kueneza utamaduni wa kidemokrasia ndani ya vyama vyetu. Msingi wa demokrasia katika taifa ni demokrasia katika vyama vya siasa. wanachama wanaokumbatia vyama visivyo vya kidemokrasia hawana uhalali wa kiroho wa kudai demokrasia katika nchi. Huu ndiyo ujumbe wangu wa leo.
 
Back
Top Bottom