Dr. Kitila Mkumbo asimamishwa Uongozi DUCE kwa kushiriki siasa akiwa Mtumishi wa Umma!

Status
Not open for further replies.
Kesho kutwa ataitisha Press conference na kuushambulia Uongozi wa Chuo kwa kumtengenezea tuhuma, na kudai sababu walizotangaza kuwa ndiyo zilizompelekea kumvua uongozi hapo chuoni, siyo zilizojadiliwa ndani ya kikao cha kumsimamisha, na ataulaumu kuwa uongozi hautaki mabadiriko. Pia anatarajiwa kujitetea kuwa yeye hajawahi kuwa mwana CHADEMA kwa dhati bali ni sehemu yake ya kazi maalum ndiyo ilisababisha aingie ili aonekana ni mwanachama.
Tayari nimewaona jamaa fulani pale Serena Hotel wakiulizia ghalama za Ukumbi
 
Kama ni kweli basi hizi taratibu zetu zingine ni UPUUZI kabisa.

Mwalimu hata akiwa kiongozi wa chama hakuna madhara kabisa kwa wanafunzi.
 
Akafanye kazi private sheria zetu za kazi haziruhusu kujihusisha na siasa at the sametime ni mtumishi wa umma.

Msaidieni mwenzenu, kwani mlikuwa hamjui siku zote kuwa alikuwa Chadema na ni Mjumbe wa Kamati kuu! CCM mnang'ata na kupuliza!
 
CCM hawana rafiki wa kudumu

chadema ni majizi sana. Kwenye kuunda kambi ya upinzani bungeni waliwatenga wenzao, wakawaita cuf mashoga walipobanwa wakaishiwa nguvu kwenye katiba wakajidai kuwakumbatia na kuwaona wapenzi wao wa kufa na kuzikana. Shame kwenu
 
heeh,yamekuwa hayo tena,yaani ni kweli CCM wanafiki.

Unafiki gani wakati nimezungumzia sheria ilivyo? Ukitaka kuwa mwanasiasa lazima uache kazi ofisi za umma/mtumishi wa umma. Simple unaweza kuomba likizo isiyo na malipo na ukichoka na siasa unaweza rudia kazi yako.
 
Unafiki gani wakati nimezungumzia sheria ilivyo? Ukitaka kuwa mwanasiasa lazima uache kazi ofisi za umma/mtumishi wa umma. Simple unaweza kuomba likizo isiyo na malipo na ukichoka na siasa unaweza rudia kazi yako.

Mkuu CHAMVIGA
sheria zipo wazi huwezi kuwatumikia mabwana wawili; hili la Kitila Mkumbo nina uhakika ni uvunjaji wa sheria za utumishi wa umma zimefanywa kwa makusudi; ni bora aachane DUCE ili aitumikie Chadema vizuri!
 
Last edited by a moderator:
Aah ccm wakikupa kazi ukashindwa kukamilisha mission, lazima wakufanyizie, nafiliri ccm wamechukia kwa kuwa jamaa kakiri
 
Kama ni kweli basi hizi taratibu zetu zingine ni UPUUZI kabisa.

Mwalimu hata akiwa kiongozi wa chama hakuna madhara kabisa kwa wanafunzi.

Mtanzania

Mie nafikiri ni tactic ya Mwalimu Kitila kujitoa kabisa kwenye Siasa za CHADEMA. Sifikiri kama hao DUCE walikuwa hawajui kwamba jamaa ni kiongozi chadema. Nafikiri ni move ya mwenyewe tu, kaona siasa ama alichokuwa anafikiria kinawezekana chadema kumbe hakiwezekani.
 
Taarifa zinasema kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umemvua kwa muda Mhadhiwa Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo madaraka ya kuongoza Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE).

Hatua hiyo inatajwa kuchukuliwa baada ya uongozi wa UDSM kupata taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa Dk Kitila Mkumbo alikuwa kiongozi wa chama cha siasa, CHADEMA wakati angali ni mtumishi wa umma, jambo ambalo Uongozi wa chuo hicho umekariri kuwa ni kinyume cha sheria ya nchi na Serikali kwa mfanyakazi wa umma kushika wadhifa katika chama cha siasa.

Chanzo habari

Vipi kuhusu ajira yake? Je, anameet vigezo?
 
Niweke sawa mambo fulani hapa. Kugombea ubunge ndani ya chama (mchakato wa kumpata mgombea) haikatazwi wala haihitaji kujiondoa katika utumishi wa umma, ila ukishapitishwa na chama chako kusimama katika uchaguzi wa kitaifa, hapo unatakiwa ujiondoe katika utumishi wa umma
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom