Dr. Kitila Mkumbo Anafaa Kugombea Urais wa Tanganyika Kwa Tiketi ya CHADEMA

Exaud Mamuya

Verified Member
Jul 26, 2011
403
195
Maswala ya nani atagombea Urais ndani ya Chadema kwa sasa muda wake bado. Japokuwa na yeye anazo sifa zote kikatiba japo hana umaarufu kama Dr Slaa ila kwa sasa Chadema kimejikita katika ujenzi wake mijini na vijijini na wala sio kuangalia nani atapeperusha bendera yake kipindi cha uchaguzi mkuu wa Rais.

Nachokiona hapa ni kwamba unajaribu kuleta hoja ambazo kwa upeo wako mdogo unadhani zitaleta mtafaruku na mpasuko ndani ya Chadema kwa kuwagawa viongozi wa juu wa Chadema kupitia swala hili la Urais kama mlivyofanya propaganda hii kwa kumpitia Zitto.

Ushauri wangu kwako ni kwamba kajipange tena upya ili uje na plan B maana plan A imegonga mwamba

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,891
2,000
Ndugu wana JF,
Kwa vyovyote vile, kuundwa kwa serikali ya Tanganyika/Tanzania Bara haizuiliki tena. Kwa kuwa kutakuwa na Rais/kiongozi wa Tanganyika kama alivyo Rais wa Zanzibar, nadhani ni muda muafaka tuanze kufikiria ni nani anafaa kushika bendera ya CHADEMA kwa Urais wa Tanganyika.

Nikipepesa macho, namwona kijana msomi, mwenye uwezo mkubwa wa kiuongozi, mwenye hoja nzito, mnyenyekevu, asiyependa makuu, asiye na majivuno, asiye na doa, anayekubalika kwa watu wa rika zote, mchapa kazi na mzalendo wa kweli, huyu si mwingine ni Dr Kitila Mkumbo.

Kwa wale wanaomfahamu vizuri watakubaliana nami kuwa CHADEMA wakimsimamisha kwa urais wa Tanganyika, watakuwa wamemweka mtu ambaye si tu kuwa atatoa ushindani mkubwa bali anauwezekano mkubwa wa kushinda.

Toa maoni yako mwana JF.
Sasa ushasema anakubalika na watu wa rika zote, unahitaji maoni ya nini?! Halafu bado unasema ana uwezekano mkubwa wa kushinda?! Uwezekano kwa mtu anayekubalika na rika zote, sijui huu uchunguzi uliufanya kwa muda gani?!
 

Lugano5

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
4,358
1,250
Wana ccm wenzangu nashangaa tunapigizana kelele na hawa waropokaji sababu hawana hoja za msingi kweli mtu mwenye akili timamu anaweza sema dr. Kitila awe rais wa tanganyika .....duuhh kweli kizazi cha chadema ni janga la taifa....yaani hawafikirii kabisa sisi mpaka sasa hatujajua rais ni nani kwani tunawasomi wengi na watu wenye kujua uongozi waliopikika kiukweli....nasubiri kifo cha chadema 2014 na 2015"together we conquer"

"kidumu chama tawala"
 

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,891
2,000
Huku ni kutaka kutuaminisha kile ambacho wewe unajua! Anakubalika na watu wa rika zote, wapi? Akina nani hao wanaomkubali dr.kitila kama si wewe na wenzako wachache? hivi kweli leo hii kitila agombee urais wa nchi?!
 

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,508
0
Kwao tu hakubaliki, tena kijijini alikozaliwa.
Sio hakubali! Noo...kule Iramba watu wenye vingamuzi ni wakuhesabika......so hata tiviii kuangalia ni sikukuu.....So ukiwaambia watu kuhusu Dr Kitila Mkumbo hawamjui......kwa sababu hata Habari kwenye TV hawapati....pili kwa sababu Magamba wanahonga na yeye hakuwa na pesa za kuohonga ndio maana kazi ikawa ngumu.....si unajua MIGULU chemba alitumia umaskini wa wana Iramba kuwahonga ndio akashinda! afu anajisifia!!!
 

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,508
0
Wana ccm wenzangu nashangaa tunapigizana kelele na hawa waropokaji sababu hawana hoja za msingi kweli mtu mwenye akili timamu anaweza sema dr. Kitila awe rais wa tanganyika .....duuhh kweli kizazi cha chadema ni janga la taifa....yaani hawafikirii kabisa sisi mpaka sasa hatujajua rais ni nani kwani tunawasomi wengi na watu wenye kujua uongozi waliopikika kiukweli....nasubiri kifo cha chadema 2014 na 2015"together we conquer"

"kidumu chama tawala"
Unasubiri kifo cha chademaaaa? Kwa hiyo umepanga mikakati ya kukiua? BAsi wewe Gaidi
 
Top Bottom