Dr. Kitila Mkumbo Anafaa Kugombea Urais wa Tanganyika Kwa Tiketi ya CHADEMA

Eti Slaa Muungano kitila Tanganyika! Unakurupuka tu, who is Kitila? Hatutaki watu wa kujifunzia kuongoza. Huyo Dk. wenu kazeeka hatutaki wazee sisi. Bora mtuwekee yule Mkigoma tumchague.
 
Ama humfahamu Mkumbo au unapiga propaganda.

Nakwambia, tukiacha chaguzi za wabunge na Rais, hakuna uchaguzi ulio mgumu kama wa Rais wa wanafunzi wa Chuo Kikuu, na hili Kitila alifanikiwa vizuri sana katika kujenga mvuto na kuchaguliwa. Lakini pia aliongoza vizuri.

Ukimsikia Mkumbo anaelezea Vision yake ya kukabiliana na changamoto zilizo mbele yake katika jukumu analotaka kulichukua, utamkubali tu!!!

Unapoteza muda kubishana na jitu ambalo halijui hata maana ya DARUSO!
 
Hata mimi napata wasiwasi na ufahamu wako, hivi kazi za Rais wa Tanganyika zinafanana na kazi za Rais wa Chuo Kikuu.

Umeishajiuliza kwa nini ajawahi kugombea nafasi yoyote ndani ya chama kama ana uwezo.

Julius Mtatiro na John Mnyika nani mwenye uwezo?

Kwani Mtatiro alikuwa Rais wa Daruso?yeye alikuwa ni Waziri Mkuu,nafasi ya kuteuliwa!
 
Tatizo lako kwa sababu akili yako tayari imeisha kuwa poisoned by negative comtemplative basi kila kikitajwa kijiji unafikiria ukabila.

Swali la kwanza kwa mtu anayegombea Urais huwa ni WHO'S THIS?. Sasa kama hata watu wa kijijini kwake hawamfahamu, unategemea watanzania wengine ndiyo watamfahamu kwa undani zaidi.

He's just floating without political foundation.
Mbona tunamfahamu
 
Umejaa fitina tu wewe huna lolote, Profesa Safari ndio alipaswa kuwa Mufti mkuu wa Waislamu baada ya kifo cha Mufti Sheikh Juma Bin Hemed, ila kwa fitina za wapenda ubwabwa kama wewe mkamchaguwa darasa la saba Mufti Simba.

Matokeo yake mtaendelea kuimba nyimbo ya mfumo kristo mpaka mwisho wa Dunia hii. Profesa Safari ni msomi nisiye na shaka naye na asiyependa makuu, yuko simple siku zote.
Mkuu Matola nakuunga mkono kwa hili, hivi vijiwe vyetu vya kahawa huwa tunadanganya sana na kueneza sumu mbaya ya udini ndio maana muda wote tunaona tunaonewa kumbe tatizo letu kubwa ni shule
 
Last edited by a moderator:
Kijijini kwao hawayajui haya, ndio maana wamempiga za uso kwenye uchaguzi wa vijiji na vitongoji. Kwa umbea wako wa kuandika vitu visivyo kuwepo, wenda ungefanikiwa kuwalaghai wanakijiji na wangeipa CHADEMA kwa mwamvuli wa Mkumbo.
Mambo ya kijijini kwao hayana uhusiano na uwezo wake wa uonhozi. After all, hajawahi kujitangaza kule maana,anabanwa na sheria kwa kuwa yeye ni mfanyakazi wa serikali
 
wanamwogopa sana kwa sababu ni muuaji..kumbuka walipoenda singida wakaua kijana wa watu asiyekuwa na hatia
Moderators, tusimamie sheria za jamvi letu.

Msiruhusu watu kuandika mambo ambayo hayajathibitishwa. Kesi ziko mahakamani na kadiri ya sheria mtu hana hatia mpaka pale ambapo mahakama imejiridhisha bila kuacha wingu la mashaka kuwa ana hatia.

Nadhani pia kuna sheria ya name calling!

Cc. Paw, Fang, Invisible
 
Last edited by a moderator:
Jitihada zako za kumtetea Mkumbo kuwa yeye ni jembe haziwezi kuzaa matunda kwani humu JF tuna mfahamu kuwa Mkumbo ni mweupe tu.

Umeeleza kwenye maelezo yako ya awali kuwa alifanikisha kuwatuliza wana-COET kwa ushawishi wake, huu ndio uongo mkuu. Kuhusu kuwa rais wa DARUSO hilo sipingi.

Pia umemtetea kuwa yeye hakuwa kwenye timu ya kampeni iliyo ongozwa na zezeta Ally Bananga, ni kweli, ila labda hukuwa makini katika kuisoma post yangu.

Nimesema, kama wanakijiji wangemjua kuwa Kitila ni jembe, wangeichagua CHADEMA kwa mwamvuli wake, maana hata sababu ya Kitila kufunguliwa kesi na Mwigulu ni kwa sababu ya kusimama kwake majukwaani na kukashifu watu badala ya kufanya siasa safi.

Mtu wa namna hii asie kuwa na maadili wala staha nani ampe urais?
Kumbe tunabishana na mtu mwenye chuki binafsi unawaita watu mazezeta bwana acha hizo
 
Tatizo lako kwa sababu akili yako tayari imeisha kuwa poisoned by negative comtemplative basi kila kikitajwa kijiji unafikiria ukabila.

Swali la kwanza kwa mtu anayegombea Urais huwa ni WHO'S THIS?. Sasa kama hata watu wa kijijini kwake hawamfahamu, unategemea watanzania wengine ndiyo watamfahamu kwa undani zaidi.

He's just floating without political foundation.
unashughulika na hoja ambayo haina maana. Nani amekuambia nyumbani kwake hawamjui? Yeye hajawahi kugombea kule iramba. Kumbuka hata Mbowe na Prof Lipumba mwaka 2005 majimbo yao yalichukuliwa na ccm. Mbona hatukuwahukumu kwa hili? Hadi leo hata kitongoji cha mahali alipozaliwa Lipumba kipo chini ya CCM mbona hamsemi Lipumba hafai? Kwa hiyo hicho si kipimo cha uongozi
 
dr kitila anafaa kwa asilimia zote bila kuangalia itikadi,ukanda wa kabila nakumbuka sana msaada huyu jamaa kwa wanafunzi UDSM.
 
Hata Mwigulu ni jembe,anafaa kuwa presdaa.Ni mtu mwenye kujiamini,ni mchumi nambari 1 tz,ni mbunifu,ni mzalendo,n.k
Toa uthibitisho. Amefanya machapisho mangapi? Amefanya kitengo gani cha uchumi kwa mafanikio? Kuna tofauti ya kusoma na kuelimika, Nchema amesoma ila hajaelimika kutokana na matendo yake ambayo hayafananii mtu aliyesoma
 
Eti Slaa Muungano kitila Tanganyika! Unakurupuka tu, who is Kitila? Hatutaki watu wa kujifunzia kuongoza. Huyo Dk. wenu kazeeka hatutaki wazee sisi. Bora mtuwekee yule Mkigoma tumchague.
ungesema sitaki ingeeleweka zaidi haliko kusema hatutaki, wewe na nani?
 
Alikuwa Rais wa DARUSO UDSM wakati nasoma pale.

Kwa kweli aliongoza vizuri sana. Ana msimamo mzuri, hata Uongozi wa Chuo wakati huo (Prof. Luhanga na Prof. Mkude) walimheshimu sana. Alikuwa mteteaji mkubwa sana wa haki za wanafunzi lakini wakati huo huo alikuwa anakemea upuuzi wa wanafunzi pale ilipokuwa lazima.

Nakumbuka wakati wa mgomo mmoja, baada ya FFU kutawanya maandamano ya wanafunzi Ubungo mataa, wanafunzi wa Engineering walikuwa wako tayari kutengeneza mabomu ya Petroli kupambana na FFU, lakini Kitila aliwazuia, na wakati huo huo akafanikiwa kuishawishi serikali kutatua tatizo la wanafunzi mara moja, wakamsikiliza na mgomo ukaisha.

Ni kiongozi mzuri na muadilifu
Kama aliweza kushawishi hilo hapo kwenye wekundu lisitokee basi si haba kijana ana uwezo. Huenda hao wahitimu wengine wako Mtwara nini, kwani mabomu kama hayo ndiyo yaliyokuwa yantumika Masasi kuunguza majengo wakati wa vurugu
 
Ndugu wana JF,
Kwa vyovyote vile, kuundwa kwa serikali ya Tanganyika/Tanzania Bara haizuiliki tena. Kwa kuwa kutakuwa na Rais/kiongozi wa Tanganyika kama alivyo Rais wa Zanzibar, nadhani ni muda muafaka tuanze kufikiria ni nani anafaa kushika bendera ya CHADEMA kwa Urais wa Tanganyika.

Nikipepesa macho, namwona kijana msomi, mwenye uwezo mkubwa wa kiuongozi, mwenye hoja nzito, mnyenyekevu, asiyependa makuu, asiye na majivuno, asiye na doa, anayekubalika kwa watu wa rika zote, mchapa kazi na mzalendo wa kweli, huyu si mwingine ni Dr Kitila Mkumbo.

Kwa wale wanaomfahamu vizuri watakubaliana nami kuwa CHADEMA wakimsimamisha kwa urais wa Tanganyika, watakuwa wamemweka mtu ambaye si tu kuwa atatoa ushindani mkubwa bali anauwezekano mkubwa wa kushinda.

Toa maoni yako mwana JF.

Umetumia hivyo vigezo tu?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom