Dr. Kitila Mkumbo Anafaa Kugombea Urais wa Tanganyika Kwa Tiketi ya CHADEMA

matasha

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
378
0
Ndugu wana JF,
Kwa vyovyote vile, kuundwa kwa serikali ya Tanganyika/Tanzania Bara haizuiliki tena. Kwa kuwa kutakuwa na Rais/kiongozi wa Tanganyika kama alivyo Rais wa Zanzibar, nadhani ni muda muafaka tuanze kufikiria ni nani anafaa kushika bendera ya CHADEMA kwa Urais wa Tanganyika.

Nikipepesa macho, namwona kijana msomi, mwenye uwezo mkubwa wa kiuongozi, mwenye hoja nzito, mnyenyekevu, asiyependa makuu, asiye na majivuno, asiye na doa, anayekubalika kwa watu wa rika zote, mchapa kazi na mzalendo wa kweli, huyu si mwingine ni Dr Kitila Mkumbo.

Kwa wale wanaomfahamu vizuri watakubaliana nami kuwa CHADEMA wakimsimamisha kwa urais wa Tanganyika, watakuwa wamemweka mtu ambaye si tu kuwa atatoa ushindani mkubwa bali anauwezekano mkubwa wa kushinda.

Toa maoni yako mwana JF.
 
ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
0
Dr Mkumbo ni jembe sana na CCM wanamwogopa sana. Chadema wakimsimamisha kwa Tanganyika na Dr Slaa urais wa Muungano itakuwa ni sawa na timu yenye Messi na Ronaldo.
 
Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,649
2,000
Alikuwa Rais wa DARUSO UDSM wakati nasoma pale.

Kwa kweli aliongoza vizuri sana. Ana msimamo mzuri, hata Uongozi wa Chuo wakati huo (Prof. Luhanga na Prof. Mkude) walimheshimu sana. Alikuwa mteteaji mkubwa sana wa haki za wanafunzi lakini wakati huo huo alikuwa anakemea upuuzi wa wanafunzi pale ilipokuwa lazima.

Nakumbuka wakati wa mgomo mmoja, baada ya FFU kutawanya maandamano ya wanafunzi Ubungo mataa, wanafunzi wa Engineering walikuwa wako tayari kutengeneza mabomu ya Petroli kupambana na FFU, lakini Kitila aliwazuia, na wakati huo huo akafanikiwa kuishawishi serikali kutatua tatizo la wanafunzi mara moja, wakamsikiliza na mgomo ukaisha.

Ni kiongozi mzuri na muadilifu
 
Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,509
2,000
Dr Mkumbo ni jembe sana na CCM wanamwogopa sana.
Kwa lipi hasa? Hizo konsoltansi za kampuni ya familia ya Mtei? Hata chaguzi za ndani ya CDM Kitila hana uwezo wa kushinda kiti chochote cha kugombea.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
18,470
2,000
sasa mbona 6 anasema hawezi kujiunga chama ambacho kina kiongozi mmoja tu, hawa hajawaona pia
 
HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
6,955
2,000
Alikuwa Rais wa DARUSO UDSM wakati nasoma pale.

Kwa kweli aliongoza vizuri sana. Ana msimamo mzuri, hata Uongozi wa Chuo wakati huo (Prof. Luhanga na Prof. Mkude) walimheshimu sana. Alikuwa mteteaji mkubwa sana wa haki za wanafunzi lakini wakati huo huo alikuwa anakemea upuuzi wa wanafunzi pale ilipokuwa lazima.

Nakumbuka wakati wa mgomo mmoja, baada ya FFU kutawanya maandamano ya wanafunzi Ubungo mataa, wanafunzi wa Engineering walikuwa wako tayari kutengeneza mabomu ya Petroli kupambana na FFU, lakini Kitila aliwazuia, na wakati huo huo akafanikiwa kuishawishi serikali kutatua tatizo la wanafunzi mara moja, wakamsikiliza na mgomo ukaisha.

Ni kiongozi mzuri na muadilifu
Kijijini kwao hawayajui haya, ndio maana wamempiga za uso kwenye uchaguzi wa vijiji na vitongoji. Kwa umbea wako wa kuandika vitu visivyo kuwepo, wenda ungefanikiwa kuwalaghai wanakijiji na wangeipa CHADEMA kwa mwamvuli wa Mkumbo.
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,258
2,000
Mtu hajawahi hata kuwa katibu kata watu wakampima uwezo wake katika masuala ya kisiasa utawezaje kumpa nafasi kubwa ya urais wa Tanganyika.

Mpaka leo hajaweza kusema alitumia vigezo gani katika kuchaguwa wabunge wa viti maalum Chadema.

Nadhani angeanza kwanza kugombea ubunge huko Singida.
 
ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
0
Kwa lipi hasa? Hizo konsoltansi za kampuni ya familia ya Mtei? Hata chaguzi za ndani ya CDM Kitila hana uwezo wa kushinda kiti chochote cha kugombea.
Jadili hoja badala ya kuingiza mambo ambayo hayana uhusiano na hoja iliyopo mezani
 
Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,649
2,000
Kwao tu hakubaliki, tena kijijini alikozaliwa.
Ama humfahamu Mkumbo au unapiga propaganda.

Nakwambia, tukiacha chaguzi za wabunge na Rais, hakuna uchaguzi ulio mgumu kama wa Rais wa wanafunzi wa Chuo Kikuu, na hili Kitila alifanikiwa vizuri sana katika kujenga mvuto na kuchaguliwa. Lakini pia aliongoza vizuri.

Ukimsikia Mkumbo anaelezea Vision yake ya kukabiliana na changamoto zilizo mbele yake katika jukumu analotaka kulichukua, utamkubali tu!!!
 
ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
0
Vijiji vya iramba tu vimemshinda leo unatuletea story za kwenye kahawa hapa tena
Kwani yeye aligombea au alienda kupiga kampeni? Sidhani kama hicho ni kigezo. Dr Shein hakuwa kwenye siasa lakini alianzia umakamu wa Rais na sasa Rais wa Zanzibar na anafanya vizuri sana. Kwamba mtu ameshawahi kuwa mbunge si issue, issue ni uwezo wa kuongoza. Dr Mkumbo ana uwezo mkubwa sana na huo ndio ukweli.
 
utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,198

Kama alishindwa kuwashawishi ndugu zake kijijini alikozaliwa wachague wagombea wa chama chake, atawezaje kutushawishi watanzania tumchague yeye??? Shein alikuwa mbunge ktk baraza la wawakishi, mind you.
 
ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
0
Ivi ile kesi ya mauwaji inayomkabili kule singida imefikia wapi???
Inaonekana kabisa kuwa CCM mnamwogopa sana ndio maana mnatoa kauli za mfa maji. Sisi wanachadema tunajua jamaa ni jembe, kama wewe huoni shauri yako
 
utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,198
2,000
Ama humfahamu Mkumbo au unapiga propaganda.

Nakwambia, tukiacha chaguzi za wabunge na Rais, hakuna uchaguzi ulio mgumu kama wa Rais wa wanafunzi wa Chuo Kikuu, na hili Kitila alifanikiwa vizuri sana katika kujenga mvuto na kuchaguliwa. Lakini pia aliongoza vizuri.

Ukimsikia Mkumbo anaelezea Vision yake ya kukabiliana na changamoto zilizo mbele yake katika jukumu analotaka kulichukua, utamkubali tu!!!
Namjua vzr na najua vzr changamoto za uchaguzi wa daruso..lakini kwann alishinndwa kuwashawishi wana kijiji alikozaliwa wachague wenyeviti wa vijiji wa chadema huko kwao iramba??? Daruso is history now, talk on real politics
 
Top Bottom