Dr. Kitila Mkumbo akizungumzia Ubunge wa Afrika ya Mashariki (Video ITV)

Luushu

JF-Expert Member
Apr 8, 2012
812
468
[video=youtube_share;APKDf5SZAX8]http://youtu.be/APKDf5SZAX8[/video]

Mbunge mtarajiwa wa Iramba magharibi Kitila Mkumbo yupo studio ITV saa hii pongezi kwa kuelimisha jamii
 
Huyu aendelee tu kishika chaki!!
Sidhani kama ana quality za kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi!!
 
Mkuu angeshuka nondo kama Dr. Kessy angeweza kubadili matokeo. Hivi unadhani CCM woooote hawaipendi CDM? Kuna watu wamo CCM lakini wana mahaba na CDM.

ccm WANA BIFU NA CDM. NDO MAANA HAWAINGII KWENYE UCHAGUZI, MPAKA WAPANGE WAMCHAGUE NANI
 
[video=youtube_share;apkdf5szax8]http://youtu.be/apkdf5szax8[/video]

mbunge mtarajiwa wa iramba magharibi kitila mkumbo yupo studio itv saa hii pongezi kwa kuelimisha jamii

ubunge wa afrika mashariki kwani ni miaka mingapi?
 
Dr. Kitila amezungumza point ya maana sana.. Wabunge wa Africa Mashariki hawapaswi kutoka katika mikumbo hii ya kisiasa hapa kwetu.. Hawa wanaenda kuwakilisha Tanzania na ukiangalia kwa mfumo wa hawa wa juzi utagundua tunaweza kuwapeleka bogus kule..
 
Leo nimemsikiliza Dr Kitila Mkumbo akihojiwa na kituo cha televisheni cha ITV, kwa kweli amenigusa sana!!

Kati ya mambo mengi aliyoyazungumza ambayo mengi yake yana faida kubwa kwa watanzania, pia alizungumzia suala la Rushwa katika Tanzania na suala la Tanzania kujiunga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kitila amesema kwamba rushwa kuendelea kutolewa wakati wa uchaguzi imedhihirika siyo suala la umaskini tena wa watanzania bali imeshakuwa ni sehehmu ya maisha ya watanzania.

Kitila amejenga hoja kwamba kama imefikia wabunge ambao kwa viwango vya kawaida vya watanzania wanaonekana ni watu wenye kipato cha kutosha, nao pia wanapokea rushwa ili wawachague watu kuingia kwenye Bunge la Afrika Mashariki, basi kuzungumzia kwamba watu wanapokea rushwa kwa sababu ya umaskini itakuwa si sahihi.

Kwenye maelezo yake amebainisha kwamba tukichukulia rushwa iko kwa sababu ya umaskini tutakuwa tunakosea kwani inavyoonekana rushwa ni tatizo kubwa zaidi ya vile watu wanavyolichukulia. Pia anaamini TAKUKURU imeshashindwa kazi ya kupambana na rushwa za wanasiasa badala yake inajishughulisha na kukamata watu wanaopokea rushwa ndogondogo na kushindwa kufanya chochote kwenye rushwa za wanasiasa.Kuhusu Afrika Mashariki amewataka watanzania waachane na hofu ya kujiunga na jumuiya hiyo kwani nchi nyingine hazitawasubiri wawe tayari.

Nimependa jinsi alivyokuwa anawasilisha hoja zake kwani ni aina ya watu tunaotaka wawe wengi ili tuweze kuwa na mabadiliko ya kweli yenye tija!!

Big UP Kitila Mkumbo!!
 
Back
Top Bottom