ESPRESSO COFFEE
JF-Expert Member
- Sep 6, 2014
- 6,170
- 7,662
Dr.Kitila Mkumbo akizungumza na kitua ha East Africa Radio amefafanua kuhusu Elimu bure katika kipindi cha Super Mix kipengele cha darasa huru!
Akiongea katika kipindi hicho amesema kuwa Elimu bure inahusisha vitu viwili kwanza ni ada kufutwa pili ni michango ambayo mzazi alikuwa anatoa hapo ndo Elimu bure huwa
Kaendelea kusema kuwa kwa wanafunzi wa bweni Majukumu huwa kwa serikali kwa kufuta michango na Ada! Na kwa wanafunzi wa kutwa ambapo jukumu la chakula na mahitaji ya muhimu hubaki kuwa majukumu ya wazazi
Kitila amesema kuwa Suala la elimu bure haimanishi bure kabisa kama wazazi walivyo elewa na kuna baadhi ya Majukumu wazazi watakuwa nayo kama yalivyo ainishwa na serikali ikiwapo usimamizi wa wanafunzi wa kutwa
Dr.Kitila ameongeza kuwa Shule ni za jamii na Elimu ni Nyumbani na shule Hivyo wazazi na jamii kwa ujumla ni lazima isaidiane na Serikali katika kutimiza suala la Elimu bure ikiwa ni pamoja na kutekeleza Majuku ambayo wazazi wamepewa katika kutimiza suala la Elimu bure
Dr Kitila Mkumbo amesisitiza kwamba katika hatua hizi za Awali katika utekelezwaji wa Sera ya Elimu bure ni lazima Kutokee mkanganyiko kati ya serikali na Wazazi au walezi na nijambo lisilo kwepeka! Amesisitiza mkanganyiko huu ni kutokana na uelewa wa wazazi kuhusu Elimu bure na wao kujiona kuwa hawana majukumu,majukumu wa nayo na ni kwa wanafunzi wa kutwa na mahitaji Muhimu kwa wanafunzi ila suala lakuwa Wazazi hawana majukumu kabisa amepinga na halipo kabisa katika suala la elimu bure!
Dr.Kitila Mkumbo amesema katika kutatua mkanganyiko huo ni lazima Serikali iendelee Kutoa Elimu endelevu kwa jamii kuhusu elimu bure Ili Jamii ipate uelewa kuhusu Elimu bure!
Katika suala la pesa zilizo tolewa Dr Kitila Mkumbo amesema Kuwa serikali imetoa kiwango cha chini lakini sababu ni Mwanzo tuipe serikali mda kidogo!
Alipo Ulizwa kuhusu Faida ya sera Bure alisema sera hii imeondoa usumbufu kwa wazazi kwa swala la ada na michango!
Alipo ulizwa kuhusu Madhara ya hii sera Dr.Kitila Mkumbo amesema kuwa Duniani kote Madhara ya sera ya Elimu bure ni KUSHUKA KWA KIWANGO CHA ELIMU! Amesema kuwa sera ya Elimu bure kamwe haiwezi kuboresha elimu! Sababu wazazi wengi watapeleka watoto shule huku miundo mbinu shuleni italemewa
Alipo ulizwa nini kifanyike alisema kuwa ni lazima serikali iwekeze pesa nyingi sana katika Elimu ikiwa ni kuboresha maslahi ya walimu na miundo mbinu Ya shule
Dr.Kitila Mkumbo amesema kuwa kuboresha elimu ni suala la muda mrefu na umuhimu wa sera ya Elimu bure huenda usionekane katika utawala huu wa Magufuli ukaja kuonekana baadae sana na katika kuboresha elimu kuna machungu makubwa na sio kama wanasiasa wengi wanavyo sema ili wapigiwe Makofi
Mwisho akahitimisha kwa kusema kuwa wazazi serikali na jamii lazima zishirikiane