Dr. KITILA aliitisha mdahalo wa changamoto ya Elimu na rasilimari za nchi

BAPUPEGHE

JF-Expert Member
Dec 14, 2012
220
38
Wanabodi jana dr. KITILA aliitisha mdahalo wa changamoto ya Elimu na rasilimari za nchi.

Na matangazo yalitolewa wiki nzima ktk vyuo vikuu vyote Dodoma, lakn cha kushangaza kulikuwa na watu 46 ukijumlisha na meza kuu walikuwa jumla 53.
 
Sasa anataka tutafakari elimu ya wanao wakati ye anayo sasa ukikataa kwenda nani umemkomoa
 
Na kitila naye alikosa vyuo vikuu hadi aende vya Dodoma? Alitegemea kupata wasomi wa St John na UDOM?
Kama aliona chuo kikuu cha Dar es salaam hakilipi bora angevitafuta Mzumbe na SUA morogoro, angalau huko huwa kuna watu wenye mwelekeo wa mageuzi kuliko Dodoma?
 
Wanabodi jana dr. KITILA aliitisha mdahalo wa changamoto ya Elimu na rasilimari za nchi.

Na matangazo yalitolewa wiki nzima ktk vyuo vikuu vyote Dodoma, lakn cha kushangaza kulikuwa na watu 46 ukijumlisha na meza kuu walikuwa jumla 53.
Hapa vipi wadau, mzee hana uwezo au watu wamewachoka?

chama chako kingefurahia kupata watu 53 kwenye mikutano yao arusha kimandholu
 
Nijuavyo mimi wanachuo wengi karibia vyuo vyote wanafanya test na maandalizi ya UE hivyo hiyo inaweza kuwa sababu mojawapo.Japokuwa pia utafiti usio rasmi unaonesha mwamko wa kuchangamkia masuala ya msingi kitaifa kama elimu ni mdogo sana haswa kwa vyuo vya Dodoma. Labda macho yao yanaona hakuna haja ya kujadili hatma ya elimu kwani yawezekana hawaoni tatizo lolote!
 
Sasa hilo ni tatizo la nani? Vyuo hivyo vimejidhalilisha vyenyewe.Vina leta ushabiki ule ule, mahala pale pale na watu ni wale wale
 
Wanabodi jana dr. KITILA aliitisha mdahalo wa changamoto ya Elimu na rasilimari za nchi.

Na matangazo yalitolewa wiki nzima ktk vyuo vikuu vyote Dodoma, lakn cha kushangaza kulikuwa na watu 46 ukijumlisha na meza kuu walikuwa jumla 53.

Labda utusaidie ili tukuelewe zaidi una maana gani kwenye uzi wako huu kwa kutufafanulia ni kwa nini hasa wewe unaiita hii kuwa ni aibu.
 
Wanabodi jana dr. KITILA aliitisha mdahalo wa changamoto ya Elimu na rasilimari za nchi. Na matangazo yalitolewa wiki nzima ktk vyuo vikuu vyote Dodoma, lakn cha kushangaza kulikuwa na watu 46 ukijumlisha na meza kuu walikuwa jumla 53. Hapa vipi wadau, mzee hana uwezo au watu wamewachoka?
Mimi nafikri wewe unamatatizo au hujui maana ya mdahalo, nilifikiri kaumbuka kwa mada na hoja zake kumbe unasema wahudhuriaji hawakujitokeza, ule si mkutano wa hadhara kwamba utaenda kusikiliza na kuondoka, kwenye mdaharo unatakiwa utoe mawazo yako, kwanza hata hao 50 walikuwa wengi sana.
 
Hakuna iabu katika mambo ya msingi,watanzania wengi waoga sana hasa kwa mambo ya msingi kwa taifa lao.wewe unashangaa kwa hili hebu soma historia ya rais obama alivyoanza saisa.kukosekana kwa watu kunatokana vitisho kutoka viongozi wa chama cha wakoloni weusi,pili kuna mikoa inajulikana kuwa iko nyuma sana katika elimu ya uraia,lakini najua ni kwa muda tu wataelimika.Kwa ushauri tujadili rasimu ya katiba kwa ajili yetu na vizazi vyetu kwa manufaa ya nchi yetu, sio kujadili mtu,huko ni kutokuwa uwezo wa kufikiri sawasawa au unatumia akili ya mtu mwingine kufikiri.Tembo wanaisha ,twiga wanasafirishwa wakiwa hai,madini yanaporwa,mikataba mibovu inazidi kusainiwa ,ardhi inaporwa (loliondo),meremeta,Epa nk. wewe unamjadili Dr.kitila.usitumie akili ya wengine kifikiri tumia yako kijana.Nchemba amefanya nini kuhusu hayo niliyosema hapo juu,usitumiwe tu. tafakali kwa ajili ya vizazi vinavyokuja si kwa angalia tumbo lako tu.
 
University Examination ndiyo sababu kubwa. But hao 46 sio kampeni zile watu wawe 600.
 
Wanabodi jana dr. KITILA aliitisha mdahalo wa changamoto ya Elimu na rasilimari za nchi.

Na matangazo yalitolewa wiki nzima ktk vyuo vikuu vyote Dodoma, lakn cha kushangaza kulikuwa na watu 46 ukijumlisha na meza kuu walikuwa jumla 53.

huyo jamaa alikosea sana, hakupaswa kuupa mdaharo wake hicho kichwa cha habari cha Changamoto ya Elimu na Rasilimali TZ, alipaswa kuuta kama vile kwa mfano Ufisadi wa Bw. Lowasa, au Mwisho wa CCM umefika, wajue walioweka fedha Uswisi, au tunapitia upya orodha ya Mafisadi ya Bw.Slaa, hapo ungeona jinsi ambavyo watu wangejaa mpaka wengine wangerudishwa mlangoni!
 
Hili ndilo tatizo la wanasiasa wanaojipambanua kwa itikadi zao ya kisiasa halafu hapo hapo wanataka wananchi wasijipambanue na itikadi zao ili kuongelea maswala yanayohusu mstakabali wa Taifa.

Kama yeye hawezi kukitenda kile anachokihubiri, anategemea wananchi wengine ndiyo watakitenda.

People are taciturn to a politician like Dr. Kitila Mkumbo, siyo ajabu hakupata watu wengi pamoja maandalizi na promo kubwa.
 
Ukiona magamba wanatoka povu hapa, ujue wamesikilizia makali ya kisu kwenye mfupa. Ujumbe umefika...vinginevyo kwa nini wahangaike/wahangaishwe na CHADEMA!


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


BARAZA LA VIJANA CHADEMA WAANDAA KONGAMANO KUBWA LA ELIMU




KUTOKANA na kutambua kuwa moja ya matatizo makubwa yanayowakabili vijana wa Tanzania kwa muda mrefu sasa ni ukosefu wa elimu bora inayokidhi viwango vya kutoa taaluma na utaalam kwa ajili ya mahitaji halisi ya jamii yetu, Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limeandaa kongamano kubwa la kujadili elimu na mustakabali wataifa la Tanzania litakalofanyika mjini Dodoma siku ya tarehe 9, 2013, Ukumbi wa Kilimani.

Kongamano hilo ambalo litawakutanisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, vyuo vikuu, walimu pamoja na wahadhiri, litajadili hali ya elimu nchini na mstakabali wa nchi yetu kwa miaka 50 hadi 100 ijayo, likijikita katika kuchambua namna mfumo wa uendeshaji na usimamizi unavyosababisha kuporomoka kwa sekta hiyo nyeti na kisha kujadili njia mbadala za kusaidia kuondoka hapa tulipokwama kama taifa.

BAVICHA limeandaa kongamano hilo, wakati ambapo tayari viashiria vya matatizo makubwa katika mfumo wa elimu yetu nchini yameanza kuonekana wazi wazi kupitia matokeo mabovu ya vijana wanaohitimu ngazi mbalimbali za elimu nchini.

Aidha, kongamano hilo linafanyika wakati huu ambapo serikali ya CCM imeweza kuonesha pasi na shaka yoyote, kiwango cha hali ya juu cha kushindwa kusimamia na kuendesha sekta ya elimu ambayo ndiyo injini ya taifa lolote lile linalotaka kupigania ustawi na maendeleo ya watu wake, kwa vizazi na vizazi.

Pia BAVICHA inaandaa kongamano hili baada ya serikali kupitia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kushindwa kuonesha ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili sekta ya elimu na badala yake imeendelea na ubabaishaji ambao umetufikisha hapa kwenye anguko na janga kubwa la kizazi cha leo na kesho kutokana na kuporomoka kwa elimu yetu.

Baada ya uchambuzi wa hoja zitakazoibuliwa wakati wa mjadala wa kongamano hilo, BAVICHA itawasilisha maoni yake kwa chama ikiwa ni sehemu ya mchango wa vijana wa Tanzania, kuboresha sera ya CHADEMA katika elimu.

Maoni hayo yatasaidia CHADEMA kuendelea kusimamia na kusukuma agenda hii muhimu ya elimu katika nchi hii, tukitambua kuwa chama kimeshaazimia kuifanya elimu kuwa ni kipaumbele namba moja, namba mbili, kati ya sera kuu tulizonazo kwa ajili ya mawazo mbadala kwa maendeleo ya taifa letu.

Imetolewa leo tarehe 07.06.2013 Jijini Dar es salaam na;

Deogratias Munishi
Katibu Mkuu BAVICHA
 
Walitangaza kiitikadi, et Bavicha waandaa kongamano la elimu, wangesema tu kuna kongamano la dkt. Cku nyingine asome nyakati. Sahz stdnt a bsy.
 
Sehemu ya Watanzania vijana waliohudhuria kongamano hilo, bila kujali itikadi zozote zile, kujadili mada husika.
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1370848562.331592.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1370848562.331592.jpg
    88.8 KB · Views: 75
  • ImageUploadedByJamiiForums1370848593.996781.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1370848593.996781.jpg
    94.5 KB · Views: 43
  • ImageUploadedByJamiiForums1370848641.488063.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1370848641.488063.jpg
    86.2 KB · Views: 49
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom