Dr. Kikwete mtaalam wetu, tutatulie na hili kwa hotuba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Kikwete mtaalam wetu, tutatulie na hili kwa hotuba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bumpkin Billionare, Mar 17, 2012.

 1. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Inakwenda wiki ya pili sasa mgao bubu wa umeme umeshika kasi na sasa umefikia kuhatarisha mitaji ya watu na usalama wa nyumba zao. Mhishimiwa Mkuu wa Kaya amezua tabia ya kukusanya wacheza bao wa mwembe Yanga na kufanya hotuba ya kujibaraguza kila mambo yanapokuwa magumu na hotuba hizi hushangiliwa na kila aliyekosa ufahamu na kuziita suluhisho.

  Ombi langu kwa Rais: Wakusanye the called wazee wa daresalamu ufanye nao hotuba tupate umeme. Nikukumbushe mhishimiwa, mmoja kati ya mawaziri wako alituambia mwisho ni mwa mwaka jana kuwa ifikapo desemba 2011, mgao wa umeme Tanzania utakuwa historia. Je, mgao huu mpya ndio maandishi ya hiyo historia?

  Nchi hii inaharibiwa na CCM na siasa zake za mdomo na tumbo. Kila kitu longo longo bin blah blah na ndio maana likitokea tatizo, badala ya mkuu wa kaya kuongea na wasomi wenye vision zao, anakimbilia kuzungumza na wacheza bao wasio na kazi wala mtazamo.

  Hapo zamani kuwa Mtanzania lilikuwa jambo la kujivunia, sasa ni jambo la kuvumilia.
   
Loading...